Eti kuna njama za kumdhuru wakili mwale

Kowakdengo

Member
Mar 20, 2012
21
12
Kuna tetesi kuwa baada ya upande wa mashtaka katika kesi ya kupatikana na fedha inayosadikiwa kupatikana kwa njia isiyo halali (uhujumu uchumi), linalomkabili wakili Median Mwale kujitahidi kukusanya ushahidi na kushindwa kupata taarifa zinazojitosheleza, sasa kuna njama zinaandaliwa na watu wasiojulikana wakishirikiana na baadhi ya askari polisi kutoka makao makuu Jijini Dar pamoja na mawakili wa serikali wanaohusika na shauri hilo wanafanya njama za kumtoa mahabusu ya gereza la Kisongo mtuhumiwa huyo na kumpeleka kusikojulikana kwa madai ya kutaka kumhoji zaidi.

Watu hao wamekuwa mara kadhaa wakienda magereza wakiwa na hati ya kumtoa mshakiwa huyo mahabusu lakini mara zote wameshindwa kufanikiwa njama zao kutokana na Mwale kuwa na uelewa wa kisheria na hivyo kukataa akishinikiza mwenye kutaka kumhoji atumie njia ya kisheria kwa kuwasilisha maombi mbele ya mahakama na kupewa kibali au wamhoji hapo hapo gerezani.

Leo hii Mwale ameieleza mahakama kuwa anahofia usalama wake kwa sababu wanaokwenda gerezaji kutaka kumchukua hawatoi ombi la kuitaji kumhoji zaidi kila kesi hiyo inapokuja mahakamani kwa ajili ya kutajwa.

Hakimu Msofe aliyehairisha shauri hilo kwa niaba ya hakimu Charles Magesa alipanga machi 28, mwaka huu kwa ajili ya malalamiko ya Mwale kusikilizwa mbele ya Magesa ambaye leo hakuwepo mahakamani.
 
Bwana atakulinda, kumbuka kusali mara kwa mara na haki yako itatendeka
 
Back
Top Bottom