Elections 2010 Eti Kumbe ni Mbowe Ndiye Aliyetisha Kumwaga Damu Chadema Isipochaguliwa!

Nani kasema Habari Leo ni gazeti? Hicho ni kipeperushi cha Chama Cha Majini AKA CCM.Achana nacho , wanasoma wale mandondocha wa JK

Bwana Douglass Sallu,

Maneno yako siyo sahihi. Hata kama unaichukia CCM siyo vizuri kusema maneno hayo.
 
Baada ya kuona hii thread nimeenda kulisoma hili gazeti na nakukuu "Iwapo hatutatangazwa washindi katika uchaguzi mkuu ujao, Tanzania hapatatosha na tuko tayari kumwaga damu," alinukuliwa akisema kwa msisitizo Mwenyekiti Freeman Mbowe, huku akiungwa mkono na Dk Slaa. Na imeandikwa aliyazungumza September 28 mwaka huu. Kama ni kweli Mbowe alizungumza haya maneno ni vizur akemewe. Sheria ni msumeno na tunaipenda aman ya nchi yetu ndio maana hata Generali Shimbo tulimlalamikia. Kama ni uongo basi akanushe. Au mwenye maelezo alikuwa anamaanisha nini atuweke sawa.

Kwa nini HAKUKAMATWA?
Mtu anayetishia Usalama wa TAIFA SI ANATAKIWA KUKAMATWA NA KUSHITAKIWA?
 
Huyo mwandishi alitaka kuuza gazeti tu, ila hakuna ukweli wowote. Ni kuichafulia hadhi CHADEMA tu, kwani wameona wao ndio mwiba ktk uchaguzi huu so matumbo yao lazima yawe joto na kuanza kuzusha mambo kwa kutumia media kama ilivyotokea kwa mwandishi huyo.
 
Nikienda TRA nikadai kiasi fulani cha kodi zangu kule nitakuwa nimekosea!?

Haya ni maajabu!!!! Utaendaje TRA kudai kodi zako? wewe utakuwa ni mtu wa kwanza duniani. Tatizo la Wana-Chadema wala hamjui taratibu za nchi zinaendeshwaje.
 
Harooo Wakuu Tafajali.....Mkishashindwa kwenye uchaguzi....nendeni pale chini ya mwembe
chinjeni mbuzi,mle nyama yake,vimiminika kwa pembeni....Halafu damu yake,msiinywe,bali imwageni,ili mtimize adhima yenu ya kumwaga damu ! kuna ubaya gani mkishangilia...hakuna kulia......Halafu siku inayofuata kafanyeni kazi kwa bidii,Tanzania ni watu Bwana.
Tupunguze hasira wazeeeee.
 
Nimesoma Habari leo! Mwandishi Steven Peter ameanika wazi kuwa Mbowe ndiye aliyetangaza kumwaga damu kama Chadema isingechaguliwa. Nakumbuka Mh Dr Slaa akiwapa changamoto mjeshi amkamate aliyetoa kauli hio lakini Shimbo na wenzie wamejimumunya tu mdomo. Kumbe wanajua nini kilichotokea, najiuliza kwa nini hawakumsikiliza Slaa wakamkamata!?

Lakini jana Mbowe alnusura apate shida kubwa huko kwake Hai, Green Guards walimfanyia vurugu. Sasa nielewe vipi. Steven analalamika kwamba Chadema wamezidi kulalamika.

Ah someni hapa HabariLeo | Chadema uzushi, malalamiko havina tija

Habari Leo ni Tafsiri ya Daily news na wamiliki wao ni TSN, Kampuni ya Serikali. Sasa kama hukushtuliwa na tahariri ya Daily News kuhusu Dk Slaa, huna sababu ya kushtuka kuhusu gazeti dada la Habari Leo. Baada ya Maoni ya Mhariri wa Daily News kuhusu Dk Slaa umeshasikia Serikali imemwondoa Mhariri wake. Magazeti ya Serikali D/ News na H/ Leo yana mission maalumu ambayo kwa bahati mbaya ni uchochezi na damu za Watanzania zikimwagika kwa ajili ta upuuzi wao basi ICC inawangoja kule Holland.
 
Zimebaki siku chache, walishasahau ethics za uandishi wa habari. The day is coming very soon.......
 
Back
Top Bottom