Elections 2010 Eti Kumbe ni Mbowe Ndiye Aliyetisha Kumwaga Damu Chadema Isipochaguliwa!

Njilembera

JF-Expert Member
May 10, 2008
1,496
607
Nimesoma Habari leo! Mwandishi Steven Peter ameanika wazi kuwa Mbowe ndiye aliyetangaza kumwaga damu kama Chadema isingechaguliwa. Nakumbuka Mh Dr Slaa akiwapa changamoto mjeshi amkamate aliyetoa kauli hio lakini Shimbo na wenzie wamejimumunya tu mdomo. Kumbe wanajua nini kilichotokea, najiuliza kwa nini hawakumsikiliza Slaa wakamkamata!?

Lakini jana Mbowe alnusura apate shida kubwa huko kwake Hai, Green Guards walimfanyia vurugu. Sasa nielewe vipi. Steven analalamika kwamba Chadema wamezidi kulalamika.

Ah someni hapa HabariLeo | Chadema uzushi, malalamiko havina tija
 
Duh, mkuu bado unasomaga gazeti la Habarileo? Hili gazeti ni la CCM, (CCMleo) halafu waandishi wake taaluma zao zinachechemea, bora hata usome Uwazi, Ijumaa, Sani au lete raha utapata kitu cha maana kuliko gazeti hili. Huwa halina hoja zaidi ya kuandika udaku na kusifia upuuzi wa CCM. Ni wachumia tumbo hao!!!
 
Lukolo, leo nilisoma pia taarifa za Synovate, wakawa wametaja Habari Leo kama ni gazeti linalotoa taarifa za uchaguzi bila ubaguzi. Nikavutiwa kwenda kule kusoma, kumbe! Sasa Synovate ni CCM? Kama kweli huyu Steven anaamini Chadema ni wazushi tu, wanalalamika bila sababu na anaandika kwenye gazeti la walipa kodi mimi nikiwemo niwaeleweje hawa jamani? Nikienda TRA nikadai kiasi fulani cha kodi zangu kule nitakuwa nimekosea!?
 
na mda si mrefu watakuwa wanaligawa hilo gazeti bure, nani atanunua huo upupu?????
 
Nimesoma Habari leo! Mwandishi Steven Peter ameanika wazi kuwa Mbowe ndiye aliyetangaza kumwaga damu kama Chadema isingechaguliwa. Nakumbuka Mh Dr Slaa akiwapa changamoto mjeshi amkamate aliyetoa kauli hio lakini Shimbo na wenzie wamejimumunya tu mdomo. Kumbe wanajua nini kilichotokea, najiuliza kwa nini hawakumsikiliza Slaa wakamkamata!?

Lakini jana Mbowe alnusura apate shida kubwa huko kwake Hai, Green Guards walimfanyia vurugu. Sasa nielewe vipi. Steven analalamika kwamba Chadema wamezidi kulalamika.

Ah someni hapa HabariLeo | Chadema uzushi, malalamiko havina tija

Waandishi wa Habari Leo na Daily News huwa hawavai *h**i. Wala usiumize kichwa kuwafikiria.
 
Waandishi wa Habari Leo na Daily News huwa hawavai *h**i. Wala usiumize kichwa kuwafikiria.
ha!ha!ha!... ulijuaje?uliwachungulia?dahh wana hatari kweli kweli sasa kwanin hawavai jaman?wadudu wakiwauma?mmh jaman ntalia mie yan hawavai .......???heeeeee mistaki jaman!!!!
kuwa makin na magazeti.
 
Habari leo ni gazeti la mafisadi. Hapo kuna kila aina ya uongo. CCM aibu TUPU!
 
Nani kasema Habari Leo ni gazeti? Hicho ni kipeperushi cha Chama Cha Majini AKA CCM.Achana nacho , wanasoma wale mandondocha wa JK
 
Baada ya kuona hii thread nimeenda kulisoma hili gazeti na nakukuu "Iwapo hatutatangazwa washindi katika uchaguzi mkuu ujao, Tanzania hapatatosha na tuko tayari kumwaga damu," alinukuliwa akisema kwa msisitizo Mwenyekiti Freeman Mbowe, huku akiungwa mkono na Dk Slaa. Na imeandikwa aliyazungumza September 28 mwaka huu. Kama ni kweli Mbowe alizungumza haya maneno ni vizur akemewe. Sheria ni msumeno na tunaipenda aman ya nchi yetu ndio maana hata Generali Shimbo tulimlalamikia. Kama ni uongo basi akanushe. Au mwenye maelezo alikuwa anamaanisha nini atuweke sawa.
 
Nimesoma Habari leo! Mwandishi Steven Peter ameanika wazi kuwa Mbowe ndiye aliyetangaza kumwaga damu kama Chadema isingechaguliwa. Nakumbuka Mh Dr Slaa akiwapa changamoto mjeshi amkamate aliyetoa kauli hio lakini Shimbo na wenzie wamejimumunya tu mdomo. Kumbe wanajua nini kilichotokea, najiuliza kwa nini hawakumsikiliza Slaa wakamkamata!?

Lakini jana Mbowe alnusura apate shida kubwa huko kwake Hai, Green Guards walimfanyia vurugu. Sasa nielewe vipi. Steven analalamika kwamba Chadema wamezidi kulalamika.

Ah someni hapa HabariLeo | Chadema uzushi, malalamiko havina tija

HabariLeo na Daily News ni dugu moja. Pia lilianzishwa na JK mwenyewe!
 
siku si nyingi watajua kuwa magari yao mazuri, nyumba zao za fahari, mavazi yao ya hariri na hata sigara zao wanazo vuta hazitufai sisi wananchi wenye kutaabika na lindi la umaskini ulo letelezwa na CCM - mafisadi, wahujumu uchumi na wauaji ... sometime soon...
 
Jana hawa HL walipost habari ya Artumas na walipoona mkuu kajikanyaga wakai-unpost.....mkuu kaahidi kuikwamua Artumas kutokana na mtikisiko wa kiuchumi...atawapa hela kama vyama vya ushirika
 
"Iwapo hatutatangazwa washindi katika uchaguzi mkuu ujao, Tanzania hapatatosha na tuko tayari kumwaga damu,"
Aisee hiii kauli kweli aliitoa Mbowe!! Huyu hafai kabisa,,, aje atoe ufafanuzi wa kauli yake hii.
 
Habari ndo hiyo!!! Mimi nilikuwa napenda kusoma habari Leo wakati natafuta kazi serikalini. Siku hizi sitaki hata kulichungulia kabisa, sitanii hata baada ya uchaguzi sitaki kuliona kwani linaniharaibia siku zangu kila nikilisoma. Huwa nashindwa kuamini kama wanaoandika wana taaluma sawa au ni Vihiyo tu ambao hawapewa mafuzo sawa.

Jaribu tu kuchua gazeti moja la habari leo, linganisha na la wakenya kuna tofauti kubwa mno. Huwezi kutoka na kitu ndani ya habariLeo lakini ukisoma la kenya utaona tofauti kubwa, utajifunza vitu vingi sana na hujutii kununua gazeti.
 
"Iwapo hatutatangazwa washindi katika uchaguzi mkuu ujao, Tanzania hapatatosha na tuko tayari kumwaga damu,"
Ukipata maneno yake ya kabla ya kauli hiyo au baada utapata ukweli watakuwa wameyachakachua....Siamini kama kuna kiongozi hapa tanzania anaweza kutoa kauli kama hiyo awe Chadema, CCM, CUF
 
Kila Anayesoma uchuro huo Habari Leo, (pamoja na nduguze yaani UHURU, MZALENDO, nk yote haya ya Chama Cha Majini) ajue anashirikiana na wenyewe - wenye Majini, ujiandae kudondoka-dondoka kama wenyewe, ukianzia na kwenye hadhara hadi majukwaani, utadondoka tu...Ukitaka kuvuka mto ujue kwanza wewe mwogeleaji...!
Tupilia mbali uchuro huo...!
 
Ni upuuzi mkubwa kutumia maneno kumwaga damu kama mtaji wa kisiasa.
Hata hivyo maneno hayo yanatumika kama vitisho kwa wananchi na hayana ukweli wowote.
Hayo maneno hayatakiwi kutajwa mara kwa mara na badala yake hali yoyote inayoashiria kumwaga damu idhibitiwe na vyombo vinavyohusika.
Damu za watanzania zimemwagika Musoma, Tarime etc kwa sababu tu ya umasikini wa akili na mali wa wafuasi wa vyama, Zinamwagika mara kwa mara barabarani kwa sababu ya ajali, zinamwagika sehemu mbali mbali kwa sababu ya ujambazi, mambo haya yote yadhibitiwe badala ya kufanya ngonjera kwenye majukwaa ya kisiasa na mikutano na waandishi wa habari.
Tunachohitaji ni sera na muelekeo wa kututoa katika hali duni tuliyo nayo kwa sasa kwenda kwenye hali bora kihalisia.
Tunatakiwa tukubaliane na kuziunga mkono hoja za msingi za kutuletea maendeleo zinazotolewa na mtanzania yeyote yule bila kujali itikadi yake na kupuuza hoja za kipuuzi zinazotolewa na yeyote yule bila kujali chama na ushabiki kama wa Simba na Yanga uachwe!
Hii itawezekana tu kwa wewe ambaye unaelewa kuanza kuwaelimisha watu wote wanaokuzunguka ili hatimaye mawazo hayo yaenee nchi nzima.
 
kataa iyo
hiv uwa wanauza nakala ngapi kwa siku adi Synovate wasems kuwa ndo linaloongoza?? duh tumeshitukaaa
 
Back
Top Bottom