Eti kimasai sio kibantu?

Wamaasai ni nilotic ukiunganisha makabila kama wakaramojong wa uganda, Dinka of southern sudan, including, pokot of kenya
 
Yeah, kimasai, kimbulu nafikiri na kisandawe si vibantu, kwasababu maneno ya kwenye lugha hizi hayashabihiani, hayafanani hata kidogo na yale yaliyopo kwenye lugha za kibantu zilizozaa kiswahili, kwenye lugha za kibantu kuna maneno yanafanana fanana kidogo ndani ya lugha zao na ile ya kiswahili, lugha za kibantu na kiarabu ndizo zimeleta lugha ya kiswahili, but kiarabu si kibantu, ni kiarabu tu, kwa sababu wabantu wametokea, ni watu wa eneo nafikiri la pwani, kati na karibu kusini kidogo mwa afrika, ninachojua si wakazi wote wa afrika ni wabantu, wabantu ni wale ambao kugha za ni za kibantu, baadhi ya maneno kwenye vilugha vyao yamefanana vyenyewe kwa vyenyewe pamoja na yale yaliyomo kwenye kiswahili, baadhi ya maneno ya kiswahili ambayo ni mengi, asili yake imetoka kwenye vilugha hivyo, vilugha hivyo vimesaidia kukizalisha kiswahili, mfano neno Mtu kwenye kiswahili limetoka kwenye baadhi ya lugha za kibantu kama kimakonde, Ntu, kikongo nafikiri ni Mutu, pamoja na kichaga, kama cha kwetu ni Mndu, maneno hayo yanayotoka kwenye vilugha vilivyotambuliwa kuwa ni vibantu baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kina, maneno hayo ambayo yana maana moja ya kumaanisha binadamu, yanarekebishwa kidogo na tunapata neno Mtu kwenye kiswahili, ambalo linamaanisha pia binadamu kwenye kiswahili, asilimia ya mchango wa vilugha hivi kwenye kiswahili zinatofautiana, vingine vimechangia maneno yake kwenye lugha ya kiswahili kwa asilimia 20, vingine kwa asilimia 35 n.k, kiswahili pia kimeundwa na maneno kutoka kwenye lugha ya kiarabu kama nilivyosema, pia kutoka kwenye lugha kama kiingereza, kihindi, kijerumani na kichina nafikiri, maneno kama Laki ni kihindi, peni, mashine ni kiingereza, shukrani, Dar es Salaam ni kiarabu, nafikiri pia neno, nanasi asili yake inatoka kwenye lugha ya kijerumani, nafikiri wao ndio walileta mananasi Afrika Mashariki, kimasai, kisandawe na kimbulu si vibantu kwasababu maneno ya lugha hizo, hayafanani na ya lugha nyingine za kibantu.
 
Back
Top Bottom