Eti Katibu wa CCM anadai Dar imekuwa ya mwisho kuzalisha mazao ya kilimo, ikiwemo Arusha na Mbeya. Hivi viazi, ndizi vinatoka Dodoma?

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Katibu Mkuu wa CCM ameshangaa sana kwanini mkoa wa Dar es Salaam umekuwa wa mwisho kitaifa ktk uzalishaji wa mazao ya kilimo. Nikajiuliza hivi kweli alitegemea Dar iwe ya kwanza? Hivi Kinondoni, Sinza, Buguruni, Mbezi, Oysterbay, kuna mashamba?
Hivi huyu jamaa si PhD huyu? 🤣🤣🤣

Ivi viazi, mchele, ndizi vinatoka dodoma au mbeya?

======

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Bashiru Ally ametaja mikoa minne inayofanya vizuri na mingine inayofanya vibaya katika suala zima la ushirikiano kati ya viongozi wa serikali na wa chama kutekeleza ilani ya chama.

Ametoa tathimini hiyo jana wakati akitoa salamu zake katika sherehe za kufunga Maonesho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane iliyofanyika kitaifa katika Kanda ya Ziwa Mashariki, kwenye viwanja vya Nyakabindi wilayani Bariadi katika mkoa wa Simiyu.

Ameitaja mkoa wa Simiyu kuwa unaongoza kwa kufanya vizuri kutokana na kuwapo ushirikiano kati ya viongozi wa serikali na chama ukifuatiwa na Singida, Dodoma na Pwani.

Mikoa inayofanya vibaya na imetakiwa kujiangalia ni Mara, Arusha, Mbeya na Dar es Salaam.
“Sasa matarajio yangu ni kwamba wakati tunawapongeza hawa, wanaoshika mkia wajiangalie. Mimi nasimamia ilani na naamini katika mambo ya nidhamu ya utendaji na uadilifu, dhana ya kujitegemea na ushirikiano,” amesema Ally.

“Tuko katika kufanya tathimini ya utekelezaji wa ilani ya chama kwa sababu tumefika nusu ya utekelezaji. Tathimini ya haraka inaonesha serikali inafanya vizuri na mfano wa mafanikio hayo ni hadhara hii,” alisema.

Akisifu mshikamano uliopo, mtendaji huyo wa chama ambaye aliwasimamisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka na Mwenyekiti wa CCM wa mkoa, Enock Jacob na kuwapongeza.

“Na matokeo mnayoyaona, yanayofurahisha chanzo chake ni mshikamano baina ya uongozi wa chama na serikali katika mkoa,” amesema na kutaja mikoa hiyo mitatu inayofuatia kwa kufanya vizuri.

Amesema ukitembelea mikoa hii, utakuta viongozi wa CCM na watendaji ndani ya serikali wameshikamana kwa shida na raha.

Alisisitiza kuwa kwa chama, mshikamano ndiyo msingi mkubwa wa utekelezaji wa ilani. Alisema chama kinapata tabu pale panapokosekana mshikamano na umoja.

“Tumeumizwa sana na makundi ndani ya chama na ndani ya serikali. Nawataka mikoa hii muendelee …,”. Akielezea mikoa inayofanya vibaya, Dk Bashiru alisema, “Lakini shilingi ina pande mbili. Iko mikoa isiyofanya vizuri. Unaoongoza ni mkoa wa Mara.

Akimuelekeza Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima aliyekuwapo jana kwenye sherhe hizo, Bashiru amesema Mkuu wa Mkoa na Mwenyekiti wa mkoa ni kama paka na panya.

Amesema Kamati ya siasa ya mkoa haiwezi ikakaa kuteleleza ilani ya chama. Amesisitiza kuwa alishawaeleza wajirekebishe.

Alisema mikoa hiyo inayofanya vibaya ilitarajiwa iwe kinara kwa sababu ya ukongwe wake lakini imekuwa tofauti.
 
Katibu Mkuu wa CCM ameshangaa sana kwanini mkoa wa Dar es Salaam umekuwa wa mwisho kitaifa ktk uzalishaji wa mazao ya kilimo. Nikajiuliza hivi kweli alitegemea Dar iwe ya kwanza? Hivi Kinondoni, Sinza, Buguruni, Mbezi, Oysterbay, kuna mashamba?
Hivi huyu jamaa si PhD huyu? 🤣🤣🤣

Ivi viazi, mchele, ndizi vinatoka dodoma au mbeya?
ukiingia ccm akili unaacha mlangoni
 
Back
Top Bottom