Ester Matiko: Kama Chama kikiona kuna mwingine anafaa zaidi ya Ester Matiko, niko tayari

Hahahaa hakuna Muha anakataa hela wewe eti kisa siasa, siasa kitu gani wewe.. hao wanaotangaza wenzao wasiende wamevimba mashavu kama paka maana wao wanapiga ruzuku acha na wanawake wenzako wapige posho za bunge.
Miongoni mwa Waha wachache wapumbavu niliowahi kuwashuhudia.
 
Haya ngoja tusubiri hiyo tarehe 27 pindi watakapofukuzwa uanachama
Mbowe na Makamu wake wamebariki mchakato mzima kwa mujibu wa maelezo ya Mdee na wenzake Matiko na Bulaya..sasa nani wa kumfukuza mwenzake hapo!!
Nawapa hongera sana kwa maamuzi waliyoyafanya,
Sasa huu ndio upinzani, upinzani sio kununiana wala kuchukiana
 
Mbowe na Makamu wake wamebariki mchakato mzima kwa mujibu wa maelezo ya Mdee na wenzake matiko na Bulaya..sasa nani wa kumfukuza mwenzake hapo!!
nawapa hongera sana kwa maamuzi waliyo yafanya,
sasa huu ndio upinzani, uponzani sio kununiana wala kuchukiana
Tarehe 27 ni keshokutwa tu mkuu. Tusubiri tuone wanavyofukuzwa uanachama.
 
Kwa maoni yangu, wananchi tunahitaji watu wa kutusemea Bungeni hata kama ni wachache. Wale wengi wapo upande wa serikali hivyo hawatakuwa upande wetu sana; hawa 20 ni bora waachwe tuu kwani wachache hupewa nafasi kubwa ya kusikilizwa naamini tutawakilishwa vyema.

Hayo mengine yaliyotokea kwa kuwa wanasiasa wengi huubiri suala la KUJIAJIRI ni vizuri NAO wakajiajiri hii miaka mitano.
Kukusemea kwa nani ili akusikilize kama huyo anayepaswa kukusikiliza huwa hakusikilizi?
 
Tarehe 27 ni keshokutwa tu mkuu.Tusubiri tuone wanavyofukuzwa uanachama.
Tatizo sio kufukuzwa tatizo hapo hakuna chama tena, watu wanagawana mbao hapo. Kila kiongozi anachukua chake ndio ujue kuwa CHADEMA hakikuwa chama chenye mfumo unaoeleweka. Sasa ni dhahiri kilikuwa chama cha mtu au kikundi cha baadhi ya watu walio jijengea umaarufu.
 
She is also very dissapointed. Dada kaibiwa kura asubuhi saa mbili na akatupwa selo. Wewe Nifah na wenzio badala ya kuandamana kumtetea, ukaja huku JF. Hii ni payback time!

Sasa mnataka aishije wakati hajawahi hata kujaribu kufungua genge la kuuza nyanya? 10M+ per month sio mchezo ninyi. Hawa Ubunge ndio ajira zao
Mimi Hawa ndiyo mwarubani wa CHADEMA. Hawa ndiyo wataweka ndiyo wameweka overdrive hadi 2025.
 
Baada ya jana wabunge wa viti maalum kuapishwa, waandishi wa habari walifanikiwa kufanya mahojiano madogo na mbunge mmojawapo, Ester Matiko huku wengine wakigoma. Yafuatayo ni maswali kutoka kwa waandishi na majibu kutoka kwa Ester Matiko.

MWANDISHI: Mmepata baraka za Chama?

MATIKO: Nadhani wote tunajua taratibu za viti maalum mpaka kuweza kufika wabunge kuteuliwa, kuna utaratibu ambao unaendelea ndani ya chama kupitia wings mbalimbali na baadae chama kinabariki na majina yanaenda kwenye tume ya Taifa ya uchaguzi, binafsi nilitaarifiwa nimeteuliwa ndio maana nimefika hapa kuja kuapa.

MWANDISHI: Ulitaarifiwa na katibu?

MATIKO: Na mamlaka husika

MWANDISHI: Lakini katibu wa chama anasema hana taarifa na hilo na watachukua hatua kali dhidi yenu, hili unalizungumziaje?

MATIKO: Sijui zaidi ya hapo, kwa uchache wetu ambao tumekuja hapa, nipende tu kuwaambia watanzania, wategemee makubwa kwetu pamoja na kwamba tuko 19. Tunajua yote yaliyojiri kwenye uchaguzi mkuu ulioisha hadi tukapata hiki kidogo katika ushindi wetu mkubwa tuliokuwa nao.

MWANDISHI: Endapo chama kikiwafuta uanachama, mmejiandaa kuchukua hatua?

MATIKO: Tupo hapa kwa sababu ya chama kwa hiyo kikiona kuna mwingine anafaa zaidi ya Ester Matiko, niko tayari.

MWANDISHI: Awali msimamo wa chama chenu ilionekana haukubaliani kuweza nyie kushiriki hapa

MATIKO: Nadhani leo jukumu kubwa ni kuapa na tumetimiza hilo, yanayojiri mengine yote yanawezwa kuzungumzwa kwa wakati muafaka. Katika neno letu la shukrani tumesema dhahiri kabisa tunakishkuru chama cha demokrasia na maendeleo kututeua sisi watu 19 kukiwakilisha katika bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania kuweza kuwasemea watanzania na chama chetu sasa mengine kama yalijiri yakaenda yakarudi, yatazungumzwa kwa wakati muafaka. Asante.

MWANDISHI: Ndio kusema mmesalimu amri

MATIKO: Sio msemaji wa chama, mimi ni mbunge mteule, ASANTENI SANA.

Kimsingi sahihi ya mwisho ya uthibitishaji wa hawa wabunge kwa upande wa chama inatoka kwa katibu mkuu na sii mwenyekiti.
Sasa katibu mkuu wa chama ndie huyo amejitokeza kukana kuwa hajawahi kupeleka majina NEC.
Hakuna tena shaka juu ya hawa viti maalumu chadema ni wasaliti wanaoshirikiana na mtesi wao ccm wakiishirikisha dola kuhujumu chama.
Binafsi napendekeza msaliti ahukumiwe kama msaliti na taratibu zote za kisheria zichukuliwe ikiwa ni pamoja na kuwasikiliza kwanza mbele ya baraza.
Huenda nao kuna baadhi yao wameingizwa mkenge bila kujua hili wala lile
Haya yote yatajulikana baada ya utetezi wao na hukumu itatolewa kulingana na utetezi wa kila mmoja.
 
Matiko Yuko vizuri yeye kaambiwa kateuliwa na mamlaka husika inatosha mamlaka husika ni Mweyekiti wa Chama na NEC katibu mkuu kazi yake kuandika Minute tu za vikao vikivyoitishwa na mwenyekiti akijisikia kuitisha

Si kila kitu katibu lazima ashirikishwe
Na wewe, kuna muandika minutes na mutasari. Katibu ni mtendaji mkuu wa chama. Ndiye ana kalenda ya vikao vya chama, yeye na secretariyeti yake ndiyo inandaa agenda . Fedha zote za chama ziko chinI ya milki yake. Kwa maana nyingine ni mtawala
 
Kwa maoni yangu, wananchi tunahitaji watu wa kutusemea Bungeni hata kama ni wachache. Wale wengi wapo upande wa serikali hivyo hawatakuwa upande wetu sana; hawa 20 ni bora waachwe tuu kwani wachache hupewa nafasi kubwa ya kusikilizwa naamini tutawakilishwa vyema.

Hayo mengine yaliyotokea kwa kuwa wanasiasa wengi huubiri suala la KUJIAJIRI ni vizuri NAO wakajiajiri hii miaka mitano.
Pumbavu,kwanini hukuwachagua kwa kura kama unawahitaji wakakusemee,au ndo unakiri kuwa kura za chadema ziliibiwa?
 
Mimi hao wengine wote sina muda nao, nalia na Halima tu mimi.
Halima amekivunja chama kabisa, Halima tulimuamini na kumpa jeshi letu la wanawake na nilitegemea pasi na shaka Mbowe akistaafu uwenyekiti basi kama sio Lissu, Heche basi ni yeye!
I’m disappointed
Tuliza mshono dada wenzako wako kazini unafikiri wanapiga domo bure kama wewe?
 
Baada ya jana wabunge wa viti maalum kuapishwa, waandishi wa habari walifanikiwa kufanya mahojiano madogo na mbunge mmojawapo, Ester Matiko huku wengine wakigoma. Yafuatayo ni maswali kutoka kwa waandishi na majibu kutoka kwa Ester Matiko.

MWANDISHI: Mmepata baraka za Chama?

MATIKO: Nadhani wote tunajua taratibu za viti maalum mpaka kuweza kufika wabunge kuteuliwa, kuna utaratibu ambao unaendelea ndani ya chama kupitia wings mbalimbali na baadae chama kinabariki na majina yanaenda kwenye tume ya Taifa ya uchaguzi, binafsi nilitaarifiwa nimeteuliwa ndio maana nimefika hapa kuja kuapa.

MWANDISHI: Ulitaarifiwa na katibu?

MATIKO: Na mamlaka husika

MWANDISHI: Lakini katibu wa chama anasema hana taarifa na hilo na watachukua hatua kali dhidi yenu, hili unalizungumziaje?

MATIKO: Sijui zaidi ya hapo, kwa uchache wetu ambao tumekuja hapa, nipende tu kuwaambia watanzania, wategemee makubwa kwetu pamoja na kwamba tuko 19. Tunajua yote yaliyojiri kwenye uchaguzi mkuu ulioisha hadi tukapata hiki kidogo katika ushindi wetu mkubwa tuliokuwa nao.

MWANDISHI: Endapo chama kikiwafuta uanachama, mmejiandaa kuchukua hatua?

MATIKO: Tupo hapa kwa sababu ya chama kwa hiyo kikiona kuna mwingine anafaa zaidi ya Ester Matiko, niko tayari.

MWANDISHI: Awali msimamo wa chama chenu ilionekana haukubaliani kuweza nyie kushiriki hapa

MATIKO: Nadhani leo jukumu kubwa ni kuapa na tumetimiza hilo, yanayojiri mengine yote yanawezwa kuzungumzwa kwa wakati muafaka. Katika neno letu la shukrani tumesema dhahiri kabisa tunakishkuru chama cha demokrasia na maendeleo kututeua sisi watu 19 kukiwakilisha katika bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania kuweza kuwasemea watanzania na chama chetu sasa mengine kama yalijiri yakaenda yakarudi, yatazungumzwa kwa wakati muafaka. Asante.

MWANDISHI: Ndio kusema mmesalimu amri

MATIKO: Sio msemaji wa chama, mimi ni mbunge mteule, ASANTENI SANA.

Kwa sisi tunaojua kuunga dot hili changa limetoka CCM ili kuidhalilisha chadema kupitia spika .NEC na jiwe

Yaan apo ata CHADEMA iwafukuze uanachama kaz bure tu watatetewa na spika katiba imeekwa kapuni nanukuu tu
"Mm ni kichaa ma ndio maana nimechagua vichaa wenzangu "
 
Back
Top Bottom