Eng. Stella Manyanya aanza kwa kasi ya Magufuli, afanya ziara ya kushtukiza TEA, atatimua waalimu!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,503
113,612
16/12/2015 By Pasco wa JF. Walimu Wakuu
Kufukuzwa Kazi.

Katika kuendena na kasi ya Magufuli, Naibu Waziri wa Elimu, Ufundi, Sayansi na Technolojia, Eng. Stella Manyanya, afanya ziara ya kushtukiza Mamlaka ya Elimu, TEA, akuta mambo safi!, Atishia Kutimua Kazi Walimu Wakuu wote, ambao wanafunzi wao, wataingia darasa la tatu bila kujua kusoma na Kuandika!.

Naibu Waziri Manyanya, aliyasema hayo, wakati wa ziara ya kushtukiza aliyoifanya kutembelea Mamlaka ya Elimu Tanzania, TEA ambapo alikuta mambo safi.

Kuhusu timua timua ya waalimu wakuu wa shule za Msingi za Umma, Eng. Manyanya amesema, emeshuhudia wanafunzi wa shule za awali, yaani chekechea, ambao wanajua kusoma na kuandika, hivyo haiwezekani, mwanafunzi wa darasa la tatu shule za umma, asijue kusoma na kuandika!, huu utakuwa ni uzembe wa waalimu.

Hivyo, watafanya ukaguzi kwa shule zote za umma, na wakikuta kuna wanafunzi wa darasa la tatu hawajui kusoma na kuandika!, ni bora waalimu wakuu wa shule hizo, waandike baua za kuachia ngazi kwa kushindwa kazi, kabla hawafikiwa, maana wakifikiwa , watafukuzwa kazi!.

Ziara hiyo ilifutiwa na tukio la kukabidhiwa madawati 1000, na kampuni ya mafuta ya Total, iliyokwenda sambamba na ufunguzi wa kituo kipya cha mafuta cha Ukuni, kilichopo wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani.

Akikabidhi madawati hayo, Mwenyekiti wa Total kwa Bara la Afika, na Arabuni, Jean ?Christian Begeron aliahidi Total kuendelea kuchangia mipango mbalimbali ya kijamii na kueleza kuwa kampuni ya Totali, sio tuu ipo kwa ajili ya kufanya biashara, bali ni sehemu ya Jamii, hivyo inaguswa na matatizo ya jamii husika, na kuchangia katika utatuzi wa matatizo ya kijamii kama wajibu na sio hisani.

Uzinduzi wa kituo hicho ni katika juhudi za Kampuni ya Total kupanua wigo wake wa kibiashara, kuwafikia wateja wengi zaidi, na kutoa huduma bora n aza kisasa zaidi, ndio maana Total Tanzania, imezindua kituo kipya cha Mafuta, chenye muonekano mpya, kwa ajili ya kuuizia bidhaa za Total, na huduma za kisasa, kiitwacho Ukuni Service Station, kilichopo Barabara ya Msata, Wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani.

Uzinduzi wa kituo hicho kipya, umekwenda sambamba na utoaji wa madawati 1000 kwa shule 9 za Dar es Salaam na moja ya Bagamoyo. ambapo zoezi hili la utoaji wa madawati, limefanikishwa kwa kampuni ya Total Tanzania ikishirikiana na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) pamoja na Kampuni ya Katson LTD,

Total Tanzania, inawashukuru wateja wake wa mikoa ya Dar esalaam na Bagamoyo kwa kutoa madawati kwa shule 9 za Dar es Salaam na shule moja Bagamoyo. Kila shule itapata madawati 100 na kufanya idadi ya madawati 1000. Total imekuwa ikitoa madawati kuanzia mwaka 2013 mpaka mwaka huu 2015 Total imekwisha toa jumla ya madawati 3000 katika shule za msingi, yenye thamani ya ???

Mkurugenzi wa Total Tanzania, Bwana Tarik Moufaddal amesema Total Tanzania, ,itaendelea kutoa ushirikiano na serikali ya Awamu ya Tano, inayoongozwa na Mhe. Dr. John Pombe Magufuli, katika miradi mbalimbali ya kijamii ili kuisaidia serikali yetu kuboresha hali ya elimu nchini?. Bwana Moufaddal alizitaja shule zinazopokea madawati kuwa ni BUYUNI II, MJIMPYA, PUGU KAJIUNGENI, NZASA, SANDALI, KIZINGA, MTONI NIANJEMA, MAGOMENI, MSHIKAMANO.

Akipokea msaada huo, Naibu waziri wa Elimu, Eng. Stella Manyanya ? Aliishukuru kampuni ya Total Tanzania, kwa misaada yake na kuyahimiza makampuni megine ya umma na binafsi kuiga mfano wa Total Tanzania na kuipa jukumu la ziada TEA kuhakikisha inafanya kampeni maalum ya uhamasishaji ili mashiika, makapuni na watu binafsi wachangie ili madawati ya kutosha yapatikane, hakuna tena mwanafunzi kukaa chini!.

Total Tanzania kampuni ambayo imekuwa nchini kwa miaka 46, inajikita katika kutoa huduma bora na za uhakika kwa wateja wake. Inawahakikishia wateja wake bidhaa zilizo na viwango vya hali ya juu kuanzia Mafuta ya gari, Vilainishi, Taa za sola za Awango, Kadi za mafuta za Total na huduma zingine zinazopatikana vituoni kama kuosha magari na duka. Kampuni inalenga kufanya vituo vyake ni sehemu ambayo mteja wake anapata huduma zote muhimu ikiwa utengenezaji wa magari, chakula na bidhaa za nyumbani kwenye maduka yake .
Mwisho.
 
Attachments

  • DSC_1275.JPG
    DSC_1275.JPG
    488.3 KB · Views: 2,169
  • DSC_1279.JPG
    DSC_1279.JPG
    487.7 KB · Views: 1,861
  • DSC_1281.JPG
    DSC_1281.JPG
    364.8 KB · Views: 1,945
  • DSC_1300.JPG
    DSC_1300.JPG
    497.3 KB · Views: 1,733
  • DSC_1295.JPG
    DSC_1295.JPG
    427.7 KB · Views: 1,548
  • DSC_1274.JPG
    DSC_1274.JPG
    512 KB · Views: 1,426
  • DSC_1277.JPG
    DSC_1277.JPG
    515.9 KB · Views: 1,393
  • DSC_1270.JPG
    DSC_1270.JPG
    468.7 KB · Views: 1,333
  • DSC_1299.JPG
    DSC_1299.JPG
    475.6 KB · Views: 1,285
Hii ndiyo dalili ya kwanza ya kushindwa kwa huyu mheshimiwa. Ahadi kama hizi zilishatoka nyingi huko nyuma na hatujawahi kuona hatua ikuchukuliwa.

Why set the bar too high?
 
Sasa hivi tunapoelekea mpk madiwani watawatishia watendaji wa kata
 
kwa hiyo kwako wewe, hiyo ndio ziara ya kushtukiza?
huo ufunguzi nao ulikuwa wa kushtukiza?

vipi tukio la kukabidhiwa madawati nalo lilikuwa la kushtukiza?..

mnatufanya watoto,sio?
 
Naomba kufahamu, hao walimu wakuu alikutana nao TEA?

kuna shule za mazingira magumu vijijini,mtoto anaanza la kwanza bila kupitia awali mpaka ajue kusoma yuko la nne! Du sijui itakuaje huko vijijini.
 
Wewe #Pasco tangu Lowassa ashindwe uchaguzi hata uandishi wako wa Kiswahili umetetereka kwa kasi ya ajabu. Sikutaka kukusahihisha mbele ya umma, lakini hebu pitia tena makala yako na utagundua kwamba umeandika kama vile umekurupushwa. Ni hayo tu.
 
Mnajuwa kudanganya watu sana. eti kakuta mambo safi kwenye ziara ya kushtukizia, hapo hapo anakabizi madawati. haingii akilini kabisa
 
azingatie capacity ya darasa na shule, kama kwenye chumba kutakuwa wanafunzi 200 nikifukuzwa naua mtu, walimu 4 je shule ya watoto 700? ukimuajili kocha kama mourinho atakwambia namtaka mchezaji yule, yule na yule ili nikupe ubingwa, mama manyanya tuhurumie wenzio changamoto za ufundishaji ni nyingi sana, kila mtu anapenda mavuno bora
 
kwa hiyo kwako wewe, hiyo ndio ziara ya kushtukiza?
huo ufunguzi nao ulikuwa wa kushtukiza?

vipi tukio la kukabidhiwa madawati nalo lilikuwa la kushtukiza?..

mnatufanya watoto,sio?
Mkuu Naibu Waziri alialikwa Bagamoyo kupokea madawati!, akaamua kabla ya kwenda Bagamoyo akaanzia TEA!.

Hivyo kushtukiza ni TEA tuu, uzinduzi ulipangwa, madawati yalipangwa!.

Pasco
 
16/12/2015 By Pasco wa JF. Walimu Wakuu
Kufukuzwa Kazi.

Katika kuendena na kasi ya Magufuli, Naibu Waziri wa Elimu, Ufundi, Sayansi na Technolojia, Eng. Stella Manyanya, afanya ziara ya kushtukiza Mamlaka ya Elimu, TEA, akuta mambo safi!, Atishia Kutimua Kazi Walimu Wakuu wote, ambao wanafunzi wao, wataingia darasa la tatu bila kujua kusoma na Kuandika!.

Naibu Waziri Manyanya, aliyasema hayo, wakati wa ziara ya kushtukiza aliyoifanya kutembelea Mamlaka ya Elimu Tanzania, TEA ambapo alikuta mambo safi.

Kuhusu timua timua ya waalimu wakuu wa shule za Msingi za Umma, Eng. Manyanya amesema, emeshuhudia wanafunzi wa shule za awali, yaani chekechea, ambao wanajua kusoma na kuandika, hivyo haiwezekani, mwanafunzi wa darasa la tatu shule za umma, asijue kusoma na kuandika!, huu utakuwa ni uzembe wa waalimu.

Hivyo, watafanya ukaguzi kwa shule zote za umma, na wakikuta kuna wanafunzi wa darasa la tatu hawajui kusoma na kuandika!, ni bora waalimu wakuu wa shule hizo, waandike baua za kuachia ngazi kwa kushindwa kazi, kabla hawafikiwa, maana wakifikiwa , watafukuzwa kazi!.

Ziara hiyo ilifutiwa na tukio la kukabidhiwa madawati 1000, na kampuni ya mafuta ya Total, iliyokwenda sambamba na ufunguzi wa kituo kipya cha mafuta cha Ukuni, kilichopo wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani.

Akikabidhi madawati hayo, Mwenyekiti wa Total kwa Bara la Afika, na Arabuni, Jean ?Christian Begeron aliahidi Total kuendelea kuchangia mipango mbalimbali ya kijamii na kueleza kuwa kampuni ya Totali, sio tuu ipo kwa ajili ya kufanya biashara, bali ni sehemu ya Jamii, hivyo inaguswa na matatizo ya jamii husika, na kuchangia katika utatuzi wa matatizo ya kijamii kama wajibu na sio hisani.

Uzinduzi wa kituo hicho ni katika juhudi za Kampuni ya Total kupanua wigo wake wa kibiashara, kuwafikia wateja wengi zaidi, na kutoa huduma bora n aza kisasa zaidi, ndio maana Total Tanzania, imezindua kituo kipya cha Mafuta, chenye muonekano mpya, kwa ajili ya kuuizia bidhaa za Total, na huduma za kisasa, kiitwacho Ukuni Service Station, kilichopo Barabara ya Msata, Wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani.

Uzinduzi wa kituo hicho kipya, umekwenda sambamba na utoaji wa madawati 1000 kwa shule 9 za Dar es Salaam na moja ya Bagamoyo. ambapo zoezi hili la utoaji wa madawati, limefanikishwa kwa kampuni ya Total Tanzania ikishirikiana na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) pamoja na Kampuni ya Katson LTD,

Total Tanzania, inawashukuru wateja wake wa mikoa ya Dar esalaam na Bagamoyo kwa kutoa madawati kwa shule 9 za Dar es Salaam na shule moja Bagamoyo. Kila shule itapata madawati 100 na kufanya idadi ya madawati 1000. Total imekuwa ikitoa madawati kuanzia mwaka 2013 mpaka mwaka huu 2015 Total imekwisha toa jumla ya madawati 3000 katika shule za msingi, yenye thamani ya ???

Mkurugenzi wa Total Tanzania, Bwana Tarik Moufaddal amesema Total Tanzania, ,itaendelea kutoa ushirikiano na serikali ya Awamu ya Tano, inayoongozwa na Mhe. Dr. John Pombe Magufuli, katika miradi mbalimbali ya kijamii ili kuisaidia serikali yetu kuboresha hali ya elimu nchini?. Bwana Moufaddal alizitaja shule zinazopokea madawati kuwa ni BUYUNI II, MJIMPYA, PUGU KAJIUNGENI, NZASA, SANDALI, KIZINGA, MTONI NIANJEMA, MAGOMENI, MSHIKAMANO.

Akipokea msaada huo, Naibu waziri wa Elimu, Eng. Stella Manyanya ? Aliishukuru kampuni ya Total Tanzania, kwa misaada yake na kuyahimiza makampuni megine ya umma na binafsi kuiga mfano wa Total Tanzania na kuipa jukumu la ziada TEA kuhakikisha inafanya kampeni maalum ya uhamasishaji ili mashiika, makapuni na watu binafsi wachangie ili madawati ya kutosha yapatikane, hakuna tena mwanafunzi kukaa chini!.

Total Tanzania kampuni ambayo imekuwa nchini kwa miaka 46, inajikita katika kutoa huduma bora na za uhakika kwa wateja wake. Inawahakikishia wateja wake bidhaa zilizo na viwango vya hali ya juu kuanzia Mafuta ya gari, Vilainishi, Taa za sola za Awango, Kadi za mafuta za Total na huduma zingine zinazopatikana vituoni kama kuosha magari na duka. Kampuni inalenga kufanya vituo vyake ni sehemu ambayo mteja wake anapata huduma zote muhimu ikiwa utengenezaji wa magari, chakula na bidhaa za nyumbani kwenye maduka yake .
Mwisho.

Mdau,haya mambo bwana yasiwe ya kishabiki,huko mashuleni wamewapelekea vitendea kazi?shule zina vitabu?hivi miundombinu ya shule binafs na govt owned ipo sawa?idad ya wanafunzi darasani ipoje?mkuu wa shule hapo anawajibikaje?halafu mkuu wa shule mwajiri wake ni TAMISEMI/UTUMISHI si waziri wa elimu
 
Back
Top Bottom