Elections 2010 Endapo Hakutakuwa na Mshindi ktk Uchaguzi wa Rais Katiba Inasemaje?

Teko

JF-Expert Member
Jul 3, 2010
230
61
Waungwana naomba mnijuvye, kutokana na hali ya ushindani inayoonekana katika Uchaguzi wa Rais mwaka huu, endapo ikitokea hakuna aliyepata angalau asilimia 50% ya kura au zaidi kuweza kuunda serikali, je katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaruhusu kuundwa kwa serikali ya mseto itakayojumuisha vyama zaidi ya kimoja? Endapo katiba hairuhusu nini kitafanyika?

Nauliza hivi kwasababu Zanzibar walifanya 'referundum' kuwauliza wananchi endapo wangependa kuwe na serikali ya mseto ama la, na baada ya kukubaliana iwe hivyo Baraza la wawakilishi lilikaa likabadili katiba yao ili kuruhusu serikali ya mseto baada ya uchaguzi wa mwaka huu. Hivi sasa bunge limevunjwa nani atabadili katiba endapo italazimika kuwa hivyo? Au kwanini basi watungasheria hawakuiona hatari hiyo mapema ili kushinikiza mabadiliko ya katiba yenye kipengele hicho? Au inaaminika tu kuwa ni lazima chama kimoja kishinde kwa kishindo?

Nisaidieni kuelewa tafadhali.
 
Mshindi ni mshindi tu hata kama kapata asilimia 40 ya kura zote. Kwa TZ rais kushinda hahitaji asilimia 50 ya kura. Hakuna kurudia uchaguzi, yeyote anayeshinda ndio rais wetu.

Kama mgombea urais hana mpinzani basi hapo lazima apate kura za NDIYO zaidi ya asilimia 50.
 
Back
Top Bottom