Elimu yetu hii sijui tutafika?

Mwana va Mutwa

JF-Expert Member
Jun 9, 2009
459
53
wanafunzikuni.jpg

Wanafunzi wa Shule ya msingi Ihanga wilayani Mufindi, mkoa wa Iringa wakiwa wamebeka kuni kupelekea kwa mteja aliyenunua kuni hizo kutoka katika Shule yao kama walivyokutwa na mwandishi wetu, Waalimu hutumia muda wa masomo kufanya biashara hiyo. Picha na Hakumu Mwafongo
 
Du...wananikumbusha enzi hawa...nimefanya kazi hizo sana huko sweka!
Sisi ilikuwa tunaenda msituni kukata fito za kusimamishia miche ya nyanya.
 
dah!! tuna long way to go!!hii ni ya miaka ya tisini, sasa tuko 21st century!!kasheshe!
 
Duu! Tusifanye mchezo...per diems za wakurugenzi wa wizara ya elimu kwa mwaka inaweza kubadili hii hali....something must be done.
 
Jamani hao waalimu inabidi mtu awaonyeshe hii picha kwamba ipo kwnye mtandao na kuwapiga mkwara wa ki aina badala ya kusubiria waziri ndiyo aseme maana inatia uchungu sana
 
na kuna mengi zaidi ya haya yanayofanyika shule za vijijini kama kuchota maji ya walimu waki wa muda wa masomo.Inauma sana
 
Tunayaona na kuyajadiri matokeo, vyanzo tunavivalia miwani ya mbao viendelee kuharibu mambo ili kesho matokeo yawe mabaya zaidi.
Hapa tulipo tumefikaje?
 
wanafunzikuni.jpg

Wanafunzi wa Shule ya msingi Ihanga wilayani Mufindi, mkoa wa Iringa wakiwa wamebeka kuni kupelekea kwa mteja aliyenunua kuni hizo kutoka katika Shule yao kama walivyokutwa na mwandishi wetu, Waalimu hutumia muda wa masomo kufanya biashara hiyo. Picha na Hakumu Mwafongo

Duh, kichwa ni kwa ajili ya kuweka material lakini umri wa mtoto huyo, na ukubwa wa mzigo vinafanya kichwa kifanye kazi below capacity. Huyu ni mtaalamu wa miaka ijayo.Tutafika kweli??
 
Ngambo Ngali uko sahihi kabisaa! Hivi hawa watoto ndani ya picha hii wanapata stadi zipi? Za ujasiriamali (kama sera za sasa zinavyosisitiza) au za kujitegemea (kama sera za Baba wa Taifa)? Walimu wao wanakazia maarifa kwa kuwafunza uharibifu wa mazingira kwa vitendo halisi! Tena wa hali ya juu!
 
Ndugu yangu kwani ni stadi basi, ukiona hivyo ujue mwalimu hajalipwa mshahara na hana EPA wala Richmond, ponea yake ni kutumia wanafunzi kukata kuni, kuzibeba na kuzipeleka kwenye gulio la karibu ili ziuzwe na mwalimu apate angalau chakula na wanawe. Hii ndio Jerusalemu waliyoahidiwa walimu na wanafunzi. Asubuhi labda walienda kwenye bustani ya mwalimu mwingine au kufyatua tofali za mwalimu hii ndo Elimu ya Tanzania. Akimaliza darasa la saba hajui kitu ukimwambia hesabu kwa kiingererza akifika kumi badala ya kumi na moja anasema ten one.Akija huku uraiani, Kumuiya ya africa Mashariki, akitaka kazi anenda interview na mwanafunzi wa kigali English, French Swahili na Computer literacy ile mbaya. Inatisha jamani tuipende nchi yetu wajukuu wetu watakuwa wageni wa nani.
 
wanafunzikuni.jpg

Wanafunzi wa Shule ya msingi Ihanga wilayani Mufindi, mkoa wa Iringa wakiwa wamebeka kuni kupelekea kwa mteja aliyenunua kuni hizo kutoka katika Shule yao kama walivyokutwa na mwandishi wetu, Waalimu hutumia muda wa masomo kufanya biashara hiyo. Picha na Hakumu Mwafongo

Na Wazazi wanakimya huku wakiangalia jinsi watoto wao wanavyo fanywa watumwa katika nchi huru. Inashangaza kweli kweli.
 
wanafunzikuni.jpg

Wanafunzi wa Shule ya msingi Ihanga wilayani Mufindi, mkoa wa Iringa wakiwa wamebeka kuni kupelekea kwa mteja aliyenunua kuni hizo kutoka katika Shule yao kama walivyokutwa na mwandishi wetu, Waalimu hutumia muda wa masomo kufanya biashara hiyo. Picha na Hakumu Mwafongo

Dear Nd. Mwana va Mutwa,

Kwa hii picha unatukata matumbo wengine!!!
Natumai Mzee Mwanakijiji sasa anajua kwanini sisi tutabakia kuwa maskini maishi.
 
Si ndiyo child abuse disguised as "Elimu ni Kazi" ya fikra sahihi za mwalimu Nyerere hiyo?
 
Unategemea mtoto atafaulu hapo kweli?

Akifika nyumbani anaenda kuchota Maji 10km, then apike, afanye usafi wa mifugo kama wanayo..........ATASOMA saa ngapi

Giza likiingia hawezi kusoma ,hakuna Umeme, Kachoka vibaya mno

Hii ndio Tanzania bwana alaaaaaaaaaaaha, kesho naenda kugombea Ubunge jimbo hilo.........Mguu juu bungeni
 
Un-believable!

Hujaona hata robo ya maisha ya Watanzania wa kawaida vijijini, usiambiwe, unashangaa hii. Wa mijini umeme wa mgao, maji yakikatika, foleni za magari, nakadhalika ni issue, wa vijijini haielezeki. Wahenga walisema tembea uone sisi hatutembei, Tukienda Kempiski, Ngurudoto na lodge ya Arusha ya US $ 3000 hoooo Tanzania Tambarare, nani kasema????
 
Back
Top Bottom