KIMOMWEMOTORS
JF-Expert Member
- May 17, 2018
- 358
- 670
Salam kutoka Kimomwe Motors waagizaji wa magari kutoka Japan na Ulaya!
Watanzania tulio wengi tumekua tukiamini na kuaminishana kua gari zenye Cc ndogo kama vile Pajero Mini na Terious Kid hutumia mafuta kidogo zaidi ikilinganishwa na gari zenye Cc zaidi ya 1000. Kwa uzoefu tulio nao katika tasnia hii ya uagizaji wa magari, sehemu kubwa inaonesha kua watanzania wengi wamekua wakizitaka gari hizi kwa kwa maelezo kua zina injini ndogo ambazo hupelekea utumiaji mdogo wa mafuta.
Ukweli ni kua baadhi ya gari hizi kama nilivyozitaja hapo juu hutumia mafuta zaidi ya gari zenye Cc kubwa zaidi. Kwa wastani gari kama Terious Kid na Pajero Mini hutumia mafuta kati ya km14-16 kwa lita, wakati magari mengine kama IST ya Cc 1300, Toyota Tercel, Toyota Cami, Toyota Passo au Toyota Raum hutumia mafuta chini zaidi kiasi cha lita 1 kwa km 15-17.
Ukubwa au udogo wa injini kwa Cc sio kigezo pekee kinachosababisha utumiaji mkubwa au mdogo wa mafuta.
Sababu ya kwanza ya gari kama Pajero Mini na Terious Kid kutumia mafuta mengi zaidi ukilinganisha na gari nyingine nilizotaja haswa kutoka Toyota ni teknolojia. Teknolojia ya mfumo wa mafuta iliyotuika kwenye Mini au Terious Kidi ni ya kizamani ambayo gari hutumia mafuta zaidi katika kujiendesha, wakati hizi gari nyingine hutumia nguvu ya umeme zaidi katika uendeshaji wa gari. Mfano, Toyota Tercel ya mwaka 1996 yenye Cc 1330 huweza kuzalisha kilowati 66 ambayo huweza kuzungusha injini kwa mzunguko wa 5500 rpm, hivyo utaona kua tercel imetumia umeme mwingi zaidi katika kutengeneza mzunguko wa injini wakati Mini au Terious Kid ambazo nyingi zina mfumo wa zamani wa mafuta ujulikanao kama caburator huzalisha 37 kilowati ambayo huzungusha injini kwa mzunguko wa 7500 rpm.
pamoja na hilo la teknolojia, mambo mengine yanayochangia utumiaji mkubwa wa mafuta kwa gari hizi zenye Cc ndogo ni uwepo wa 4while drive ambayo huweka uzito kwenye injini na kufanya matumizi ya mafuta kua juu zaidi. Pia gari nilizotaja hapo juu, nyingi zina Turbo ambayo pia huchangia utumiaji wa mafuta zaidi ingawa pia turbo inapokufa injini hupoteza nguvu yake hali ambayo humuingiza gharama zisizo za lazima mmiliki wa gari hii kwa kutakiwa kufunga turbo nyingine ambapo fundi mzuri atashauri injini nzima ifanyiwe marekebisho ili nguvu yake iendane na turbo mpya.
Wengine hukimbilia gari hizi kwa sababu ya unafuu wa kuziagiza. Ni kweli kuagiza gari hizi Mini na Terious kid kwa wastani ni 7.5m mpaka 8m, lakini gari hizi huja kuwaumiza zaidi kwenye spea na mafuta bila wao wenyewe kufahamu, na wakati utakapotaka kuuza gari ya aina hii kwa wastani sio rahisi kupata mteja aliye tayari kulipa zaidi ya 5m bila kujali imetembea kiasi gani.
Kuna gari nzuri zenye injini za kisasa ambazo hutumia mafuta kidogo japo injini ni zaidi ya Cc 1000, pia spea zake ni nyingi na bei nafuu, na utakapotaka kuuza kwa wastani utaiuza kwa bei nzuri zaidi hivyo pesa yako kutopoteza thamani yake. Gari hizo kwa wastani kuagiza kwake huanzia 8m mpaka 10m.