DustBin
JF-Expert Member
- Jun 3, 2021
- 544
- 558
Nawasalimu kwa jina la JMT
Kazi iendelee.....
Nikiwa kama mdau wa Elimu nimebaini haya yafuatayo hasa baada ya kupitia maoni ya baadhi ya watu ambao wengi wao ni walimu juu ya utekelezaji wa kalenda mpya ya mtaala inayowataka walimu wote Tanzania kuwa sawa ktk ufundishaji. Kwa maana kama leo jumatatu ya tarehe 7/2/2022 Mwalimu wa Feza Boys akifundisha mada ya simultaneous equation na Mwalimu wa huko Maundo Tandahimba afundishe mada hiyo hiyo, wasitifautiane.
Bila shaka serikali ina nia njema juu ya hili; lakini hata hivyo sisi wadau tunalo la kuchangia huenda tukaisaidia serikali kufanya maboresho.
Changamoto hizo ni kama ifuatavyo;-
(1) Kutofautiana kwa idadi ya vipindi kati ya syllabus na kalenda katika baadhi ya masomo. Maeneo mengi yameonesha kwenye syllabus kuwa na vipindi vingi katika mada husika wakati kwenye kalenda mada hizo hizo zimewekewa vipindi vichache na hali muda wa vipindi ni ule ule
(2) Kalenda imechukua muda wote wa mwaka mzima kwa ajili ya kusoma darasani na siku chache kwa ajili ya upimaji na likizo. Hivyo kumfanya mwalimu akose muda wa kuwa na upimaji wa wiki (weekly test), upimaji wa mwezi (monthly test) na hata muda wa kufanya mtihani wa utimilifu (Mock exams). Kubwa zaidi mwalimu huyu huyu hakuwekewa muda wa kusahisha hiyo mitihani na kufanya marudio kama somo halikufahamika vizuri kwa wanafunzi
(3) Kalenda haikuzingatia uwepo wa shuguli za kitaifa zinazowahusisha walimu na wanafunzi pia kama vile Mwenge, Umiseta na Umitashunta, kazi maalumu nk.
(4) Kwa mujibu wa kalenda mitihani ya robo muhula imetengewa siku tatu tu jambo ambalo ni changamoto kwa shule zenye masomo zaidi ya 10 kumtahini mwanafunzi ndani ya siku tatu tu kwa mtihani wenye vigezo stahili/timilifu. Kwa kawaida shule hutumia siku 7 hadi 12 kwa ajili ya mitihani hiyo ya robo muhula.
(5) Kalenda haikuzingatia dharura mbalimbali zitakazomfanya mwalimu asiingie darasani siku husika kama vile maradhi, matatizo/shuguli za kijamii au za kiserikali nk. Ukizingatia baadhi ya shule (ambazo ni nyingi) zina uhaba wa walimu.
MAPENDEKEZO
Kwa kuwa huu mpango wa kalenda unaonyesha kuwa na mafanikio, na kwa sababu ndio kwa mara ya kwanza unaingizwa kwenye field kufanyiwa kazi ili kuwa na ufanisi mdau mimi ningependekeza, hii kalenda ingeanza na kidato cha kwanza wa mwaka huu wa 2022, ili madarasa mengine waendelee na utaratibu wa kawaida uliozoeleka. Kupitia hao wanafunzi wa kidato cha kwanza tungefanya tathimini mwisho wa mwaka na kubaini kama tuendelee nao au la.!! Na kama utaonekana hauna tija hasara ingekua kidogo. Lakini kwa hali ya sasa ya majaribio alafu tunafanya majaribio hayo na hata kwa madarasa ya mitihani nina hofu kama usipoleta ma