EDWARD wa 1 na EDWARD wa 2, wanatofautiana sura, lakini wanafanana jina, kabila na uchapakazi

Status
Not open for further replies.

Jumakidogo

R I P
Jul 16, 2009
1,851
417
Hayati Moringe alikuwa halali, kila siku alihakikisha anapambana vikali na walanguzi pamoja na wahujumu uchumi. Alikuwa ni kati ya mawaziri wakuu bora kabisa. Ngoyae naye akiwa na wadhifa huohuo alihakikisha anapambana na viongozi wazembe kwa nguvu zake pamoja na kuhimiza bidii katika kulijenga taifa.

Moringe alifariki kwa ajali ya gari kabla ya kutimiza ndoto yake ya kuwafyeka wahujumu, Ngoyae yeye alijiuzulu kwa kutwishwa zigo la dhambi za watu wengine ili kupitia yeye waokoke na kuingia katika ufalme wa milele.

Wajuvi wa mambo walitabiri kuwa Moringe ndiye angekuwa mrithi wa Julius wakati wadadisi wa mambo wanaamini kuwa Ngoyae ndiye atakuwa mrithi wa kiti cha Mrisho.

Haya ni maoni, watukanaji watukane! Wenye akili timamu wanakaribishwa sana.
 
EDWARD MORINGE SOKOINE hakuwah kuwa na kashfa yoyote ya uhujumu uchumi lkn EDWARD LOWASSA ana kashfa nzito za kuhujumu uchumi na kuwaweka watanzania kwenye maisha magumu HATA KAMA mnadai kasingiziwa swali langu ni kwanini akubali kusingiziwa? iwe ni kweli au c kweli lakini tayari LOWASSA anamadoadoa kama kenge.
 
Mkuu heshima, nimechungulia ulivyojaribu bila mafanikio kuwalandanisha waliopata kuwa mawaziri wakuu wenye jina la Edward, Hawafanani, wewe unalazimisha kuwafananisha, Moringe hakuwa na mvi ngoyai ana mvi kibao.

Moringe alihamasisha kusukuma gurudumu la maendeleo kwenda mbele, hakujilimbikizia mali, ngoyai ni mtu wa kupiga madili, ni mtu wa kujilimbikizia mali, Moringe alikuwa muadilifu, ngoyai hana chembe ya uadilifu. UNATAKA KUUFICHA UOVU WA NGOYAI KWENYE UADILIFU WA MORINGE.
 
Hayati Moringe alikuwa halali, kila siku alihakikisha anapambana vikali na walanguzi pamoja na wahujumu uchumi. Alikuwa ni kati ya mawaziri wakuu bora kabisa. Ngoyae naye akiwa na wadhifa huohuo alihakikisha anapambana na viongozi wazembe kwa nguvu zake pamoja na kuhimiza bidii katika kulijenga taifa. Moringe alifariki kwa ajali ya gari kabla ya kutimiza ndoto yake ya kuwafyeka wahujumu, Ngoyae yeye alijiuzulu kwa kutwishwa zigo la dhambi za watu wengine ili kupitia yeye waokoke na kuingia katika ufalme wa milele. Wajuvi wa mambo walitabiri kuwa Moringe ndiye angekuwa mrithi wa Julius wakati wadadisi wa mambo wanaamini kuwa Ngoyae ndiye atakuwa mrithi wa kiti cha Mrisho. Haya ni maoni, watukanaji watukane! Wenye akili timamu wanakaribishwa sana.

Edwardi wa pili ni mmeru! Kamulize??
 
Naunga mkono hoja.Wenye fikra finyu walete madhambi ya EL
mnasema alisingiziwa kashfa ya richmond? swali kma yeye ni mwadilifu kama mnavyomnadi kwanini alikubali kusingiziwa na kujiuzulu uwaziri mkuu? Ni kwanini hakuthubutu kukana tuhuma hizo kwa kuwataja wahusika wa richmond? Hauoni tayari yeye ni zaid ya jambazi kwa kuficha majambazi?? JE LOWASA YK TAYARI KUFA KWA KUSIMAMIA HAKI NA UKWELI KM SOKOINE??
 
Naamini Lowassa angepewa muda angemwacha mbali sana Moringe katika kuchapa kazi.
 
TUESDAY, APRIL 12, 2011

ALIYOYASEMA EDWARD MORINGE SOKOINE




Ndugu Edward Moringe Sokoine (01/08/1938-12/04/1984) alikuwa Waziri Mkuu wa aina yake nchini Tanzania. Aliongoza katika kipindi ambacho nchi ilikuwa katika hali ngumu sana ya kiuchumi. Leo ni miaka 27 toka Taifa limpoteze shujaa huyu. Katika kuenzi fikra zake ambazo bado zinahitajika sana leo, Udadisi inakuletea nukuu zifuatazo kama ilivyozipata kutoka kwenye Kitabu cha Edward Moringe Sokoine: Kiongozi wa Watu Aliyejitolea kilichoandikwa na Luteni Kanali Albert N. Kigadye mnamo mwaka 1984:

"Ole wake kiongozi mzembe na asiye na nidhamu nitakayemkuta: Kiongozi wa siasa hana usalama wa aina yoyote. Usalama wake ni kudra ya Mungu na Wananchi peke yake. Viongozi wazembe na wabadhirifu wahesabu siku zao. Labda tusiwajue. Hawa hatuna sababu ya kuwapa imani, kuwa tutawalinda kama vitendo vyao viovu" - Edward Moringe Sokoine, 26 Machi 1983

"Juu ya suala hili la mapato kutolingana na matumizi ni kwamba tungependa kupunguza uongezaji wa wataalam wasiohitajika katika Serikali na katika mashirika ya umma mpaka hapo hali yetu ya uchumi itakapokuwa katika hali nzuri" - Edward Moringe Sokoine, 23 Oktoba 1982

"Serikali inasimamia bei, lakini Serikali yetu itakwenda mpaka itasimamia bei ya mhogo, dagaa na bei ya kila kitu? Haiwezekani, vitu vingine ni lazima vizalishwe kwa wingi ili bei yenyewe iweze kujirekebisha" - Edward Moringe Sokoine, 24 Septemba 1983

"Wajibu wa kila Mtanzania, kila familia na kila anayekula ni kujilisha mwenyewe. Si wajibu wa Taifa kumlisha mtu. Unaweza ukasaidiwa unapopatikana na janga. Lakini kama hakuna janga ni wajibu wa kila mtu aweze kujitosheleza kwa chakula na atoe ziada kwa Taifa" - Edward Moringe Sokoine, 4 Oktoba 1983

"Vijana leo wengi wana mali zaidi kuliko wazee waliofanya kazi miaka thelathini hadi arobaini. Lakini wanaitaka Serikali ndiyo iwaulize mali hiyo wameipata wapi. Hivi kwa nini mzazi asimuulize mwanae, 'mali hii umeipata wapi?'" - Edward Moringe Sokoine, 23 Oktoba 1983

"Katika nchi inayojali haki na usawa, majeshi hayana budi yawe ni chombo cha kulinda haki na maslahi ya walio wengi. Na kamwe hayaruhusiwi kuwa ni chombo cha wachache wenye kujali nafsi zao na kusahau maslahi ya walio wengi" - Edward Moringe Sokoine, 1 Februari 1977

UDADISI: Rethinking in Action: ALIYOYASEMA EDWARD MORINGE SOKOINE




 
Mkapa alifungua kampuni ANBEM akiwa ikulu,kuna uchafu,ufisadi zaidi ya huo?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom