EDWARD wa 1 na EDWARD wa 2, wanatofautiana sura, lakini wanafanana jina, kabila na uchapakazi

Status
Not open for further replies.
Kule kwetu wanasema " i kya ighali ne kya njenga"
Yaani umefaninisha spare ya gari na ya baiskeli
 
hawafanani kabisaa, huyu tuliyenaye ni mpenda mali, wakati aliyeagishwa dunia alikuwa mpenda watu na mkombozi
 
Naunga mkono hoja.Wenye fikra finyu walete madhambi ya EL

SItaki kuamini kuwa kkuna watu ni vihiyo namna hiyo! yaani kuna watu bado wanataka kila siku watajiwe madhambi ya Lowassa wakati almost every Tanzanian knows ufisadi wa in-fact kama sio fisadi alitakiwa alipojiuzulu azitake mamlaka husika kumsafisha.............
 
Wote mnaishia kushutumu tu. Sasa bila ushadi tutaamini vipi. Kama kila mwenye mali ni fisadi, basi wanasiasa wote ni mafisadi mpaka wale wa upinzani kwani nao wana mali pia. Tunataka ushahidi wa kumtia mtu hatiani wala sio kufuata mkumbo wa maneno ya vijiweni.
 
Inawezekana kabisa EL ni fisadi ,,ninachoamini asilimia kubwa ya wa TZ ni washabiki na si watafuta ukweli,,wengi huwa tunajua kushabikia hasa jambo likitokea bungeni maana tunaamini habari za muhimili huo,,lkn tunashindwa kufikiria kuwa kunawatu wanamaslahi binafsi ,,kama EL hafai kuwa rais JK HANA UHALALI WA KULIONGOZA TAIFA HILI MAANA NAE NI FISADI,,,,KAMA SHERIA INATUKATAZA TUSIHUKUMU BILA USHAHIDI BASI TUTAFUTE USHAHIDI WA TUHUMA ZA JK NA EL ,,,nchi hii imeoza inanuka,inatiakinyaa,,,RAIS FEKI,WATENDAJI WAKE FEKI,CCM FEKI WAANDISHI WENGI FEKI,,WANASIASA WENGI FEKI....UCHUMI UMEDORORA ,FALSAFA YA HALI ZAID,KASI ZAID NA NGUVU ZAID IMEFELI .........POOR TANZANIA

Wenzetu walioendelea hawampimi mtu kwa mali alizo nazo, kwanza utajiri ni dalili za uchapakazi, tatizo letu watanzania wavivu, wakufikiri na wakufanya kazi! Edward is a hard working fellow, to me ni afadahli mwizi anayefanya kazi kuliko mtu mvivu!!!
 
Apia Mkuu!
 
EDWARD MORINGE SOKOINE hakuwah kuwa na kashfa yoyote ya uhujumu uchumi lkn EDWARD LOWASSA ana kashfa nzito za kuhujumu uchumi na kuwaweka watanzania kwenye maisha magumu HATA KAMA mnadai kasingiziwa swali langu ni kwanini akubali kusingiziwa? iwe ni kweli au c kweli lakini tayari LOWASSA anamadoadoa kama kenge.

Hivi Lowasa ndio Rais wa JMT? Anawezaje akawaweka Watanzania kwenye maisha magumu wakati hana cheo chochote? Au unataka kutuambia Richmond ndio imeleta maisha magumu mpaka gharama za maisha zimepanda, mishahara ya watumishi wa UMMA inatoka mwezi unaofuata? Hivi ufisadi ni richmond tu? Vipi kuhusu MEREMETA, IPTL, SONGAS nk ? Funguka mzee. Tatizo sio Lowasa, Tatizo ni CCM. Hata mtu awe msafi wa aina gani lakini achaguliwe toka CCM ili awe Rais wa JMT, tatizo litakuwa pale pale. Kinachosumbua CCM na serikali yake ni mfumo wa kulindana kwa sababu sio wasafi kama alivyowahi sema Sofia Simba.
 
Wenzetu walioendelea hawampimi mtu kwa mali alizo nazo, kwanza utajiri ni dalili za uchapakazi, tatizo letu watanzania wavivu, wakufikiri na wakufanya kazi! Edward is a hard working fellow, to me ni afadahli mwizi anayefanya kazi kuliko mtu mvivu!!!

Ndo tatizo lililopo hapa kwa watu wenye akili finyu amba wameshindwa kufikiria kuwa mtu anaweza kutajirika kutokana na bidii yake. Kuwa na utajiri si maana ya ufisadi. Hata hao mnaowapigia debe kuwa wapinga ufisadi nao ni matajiri pia. Hoja ya msingi, kama mtu anao ushahidi wa wizi, ama ufisadi wa EL. Auweke hadharani ili ashitakiwe kwa mujibu wa sheria. Hao maadui zake wachache walioteka akili zenu kwa kuwadanganya kuhusu wizi wa EL mbona wako kimya.
 
SItaki kuamini kuwa kkuna watu ni vihiyo namna hiyo! yaani kuna watu bado wanataka kila siku watajiwe madhambi ya Lowassa wakati almost every Tanzanian knows ufisadi wa in-fact kama sio fisadi alitakiwa alipojiuzulu azitake mamlaka husika kumsafisha.............

Hatutaki kubwata bwata hapa, leteni ushahidi wa madai yenu. Mtu akishindwa kuthibitisha tuhuma anatakiw apate adhabu. Naona mnajua jinsi kibao kinavyotaka kumgeukia Nape, mbona sasa kakaa kimya? Ni ujinga kung'ania jambo ambalo huna ushahidi nalo.
 
Hayati Moringe alikuwa halali, kila siku alihakikisha anapambana vikali na walanguzi pamoja na wahujumu uchumi. Alikuwa ni kati ya mawaziri wakuu bora kabisa. Ngoyae naye akiwa na wadhifa huohuo alihakikisha anapambana na viongozi wazembe kwa nguvu zake pamoja na kuhimiza bidii katika kulijenga taifa.

Moringe alifariki kwa ajali ya gari kabla ya kutimiza ndoto yake ya kuwafyeka wahujumu, Ngoyae yeye alijiuzulu kwa kutwishwa zigo la dhambi za watu wengine ili kupitia yeye waokoke na kuingia katika ufalme wa milele.

Wajuvi wa mambo walitabiri kuwa Moringe ndiye angekuwa mrithi wa Julius wakati wadadisi wa mambo wanaamini kuwa Ngoyae ndiye atakuwa mrithi wa kiti cha Mrisho.

Haya ni maoni, watukanaji watukane! Wenye akili timamu wanakaribishwa sana.

Baba yangu Lowassa naomba nikueleze kuwa hii kampen yako ya kujisafisha hakika haitofanikiwa zaidi ya kuongeza chuki kwetu!leo watanzania tumeamka vya kutosha,tunauelewa wa kutosha,tumehamasika vya kutosha.Raisi wa 2015 lazima awe mwadilifu,asiye na makundi asiye na doa wala shaka mbele ya jamii ambako mzee wangu sifa hz huna acha kupoteza pesa,nguvu na muda wako
 
kama lowasa sio fisadi kwann alikubali kubeba mzigo wa ufisadi ambao haumhusu.kwann mpaka leo hajawataja wahusika wa richmond.ushahidi wa kimazingira unaonesa lowasa ni mwizi na hawezi kuaminika tena kwa urais wa nchi.
 
tatzo unapandikizwa chuki,embu ushahidi aliwahi kumfisid mzaz wako
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom