Edward Lowassa ahojiwa Makao Makuu ya Polisi kuhusu uchochezi, aachiliwa kwa Dhamana

Mjumbe wa kamati kuu na mgombea urais mwaka 2015 ndugu Edward Lowassa, amewasili makao makuu ya Polisi saa nne kama alivyoambiwa na DCI.

Lowassa alikuwa amefuatana na Magari manne ya kwake pamoja na magari mawili ya polisi wenye Siraha.

Kabla ya kuwasili kwa Lowassa, aliyetangulia mapema leo alikuwa katibu mkuu wa CHADEMA Dr. Mashinji. Aliwasili kuhakikisha anaweka sawa maswala ya kisheria na msaada wowote utakaohitajika.

Waandishi wa habari hawakuruhusiwa kusogea eneo la tukio kwani ulinzi umeimalishwa.

Kwa lolote litakalotokea tutazidi kujuzana.

Jana Edward Lowassa alipokea wito wa kumtaka aonane na DCI leo saa nne bila kukosa.

Sasa kama ameitikia wito, hayo magari mawili ya polisi wenye silaha ni ya nini tena?!
 
Ndugai alisema kuwa wote tuwe tayari kwani msumeno utakata kote, na tuelewe kuwa msumeno sio magufuli bali ni sheria ya haki, magufuli kawapa ruhusa tu mafundi seremala wafanye kazi waliyokuwa wamezuiwa!
Mm nipo tayari yeyote atakaepatikana na hatia afungwe na kufilisiwa kwa kuwa najua walivyoishi kama malaika kwa jasho la watanzania, ile ni kufuru, huku watanzania wa kawaida wanawaza wale nn na watoto wao, hao na watoto wao wanaruka na ndege kama daladala, wengine mpaka wanapokea 400milioni kwa siku! Za jasho la watanzania, halafu wanataka kujificha kwenye kichaka cha kututetea watz , hao wote wachunguzwe NA ATAKAEPONA APONE KWA HAKI TU!
 
Mjumbe wa kamati kuu na mgombea urais mwaka 2015 ndugu Edward Lowassa, amewasili makao makuu ya Polisi saa nne kama alivyoambiwa na DCI.

Lowassa alikuwa amefuatana na Magari manne ya kwake pamoja na magari mawili ya polisi wenye Siraha.

Kabla ya kuwasili kwa Lowassa, aliyetangulia mapema leo alikuwa katibu mkuu wa CHADEMA Dr. Mashinji. Aliwasili kuhakikisha anaweka sawa maswala ya kisheria na msaada wowote utakaohitajika.

Waandishi wa habari hawakuruhusiwa kusogea eneo la tukio kwani ulinzi umeimalishwa.

Kwa lolote litakalotokea tutazidi kujuzana.

Jana Edward Lowassa alipokea wito wa kumtaka aonane na DCI leo saa nne bila kukosa.
Kabla hujaongea fikilia
 
Back
Top Bottom