Edo Kumwembe: Yannick Bangala, kutoka Avic Town hadi Mbagala

Oldmantz

JF-Expert Member
Jan 24, 2023
430
996
KAMA kuna mchezaji ambaye alikuwa anapendwa na Wanayanga miezi 12 iliyopita mmojawapo alikuwa Yannick Bangala. Watangazaji wa Azam TV walimuita Mzee wa Kazi Chafu. Kuna wachezaji walionekana kufanya kazi nyingi ambazo zingeonekana kiurahisi. Yeye alikuwa anafanya kazi nyuma ya pazia.

Usingeweza kuamini kwamba miezi 12 mingine, Bangala angekuwa anasaini mkataba wa kuichezea Azam FC katika ofisi za klabu hiyo zilizopo Mzizima pale karibu na Chang’ombe. Imewezekana vipi? Inashangaza kidogo, lakini mambo mengi yamepita hapa katikati.

Ni ngumu kwa mchezaji staa kuvuka boda la kucheza katika klabu za Simba, Yanga na Azam ukiwa katika ubora wako. Ilianzia kwa Mrisho Ngassa alipouzwa kwenda Azam akitokea Yanga katika utawala wa Mwenyekiti, Iman Madega.

Ikaja tena pale Azam walipokosea baada ya kuja na sera ya kijinga ambayo iliwapoteza kwa pamoja John Bocco, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni na Aishi Manula waliokwenda Simba kwa mkupuo na kuiimarisha klabu hiyo. Walikwenda bure kabisa.

Majuzi ilitokea tena wakati Ibrahim Ajibu alipotoka Simba kwenda Azam lakini zaidi ni hii ya Fei Toto kutoka Yanga kwa kulazimisha na kisha kujiunga Azam. Na sasa mkononi tuna sakata la Bangala ambaye anatoka Yanga kwenda Azam. Haikutazamiwa.

Yanga wamepata bahati kubwa. Wiki iliyopita walitambulisha kikosi chao na majina ya Bangala, Djuma Shaaban na Fiston Mayele hayakuwepo. Inaeleweka kwanini Mayele hakuwepo. Anakaribia kuuzwa Yanga.
Djuma na Bangala walikuwa na matatizo na Yanga. Yanga ni kama wamepata bahati kumuuza Bangala kwa kile kiasi kinachodaiwa kuwa ni zaidi ya Shilingi 100 milioni za Kitanzania. Ni mchezaji ambaye hawakumhitaji kikosini, ingawa walikuwa na mkataba naye.

Wakati wakijiuliza wangeweza vipi kuondoka na Bangala huku wakiwa wametambulisha kikosi chao ghafla Azam wakaja mezani kumtaka Bangala. Wakaamua kumuuza bila ya vurugu kama ilivyotokea kwa Fei Toto. Ilikuwa ni kama kumpiga teke chura.

Pale tu ambapo Azam walimtaka Bangala, basi kila upande ulitaka jambo hili litokee. Bangala hakuhitajika Yanga kwa sababu ya kile kinachotajwa kuwa ni utovu wa nidhamu. Yeye na Djuma ‘walinuka’ Yanga kwa kile kinachodaiwa kuendekeza migogoro katika masuala yaliyohusu pesa.

Lakini hapo hapo Bangala, alikuwa katika kiwango duni katika msimu ulioisha. Kama angekuwa katika kile kile cha msimu wa kwanza kilichomfanya awe mchezaji bora wa msimu, nadhani Azam wangemsikia redioni tu na sasa hivi Yanga wangekuwa katika mchakato wa kumuongezea mkataba mwingine.

Ukichanganya kiwango chake na tuhuma zake basi yalikuwa maamuzi rahisi kwa Yanga kutomtambulisha katika ile wiki yao. Lakini imekuwa rahisi pia kumuuza kwenda Azam na kupata kiasi kikubwa cha pesa ambacho katika soka letu kimeanza kuwa jambo la kawaida siku hizi.

Hii ina maana gani? Yanga wamepata walichokitaka. Lakini Bangala pia amekitaka alichokipata. Hapo katikati alikuwa na kiwewe, kwa sababu hakujua hatima yake. Hakujua angecheza wapi msimu ujao baada ya kufungiwa milango na Yanga.

Lakini sasa anaendelea kubakia Dar es Salaam. Amehama tu kutoka Avic Town, Kigamboni katika kambi ya Yanga kwenda Mbagala katika makazi ya Azam. Ni bahati kwake. Hawa wachezaji wa Kicongo wamefurahia maisha ya Dar es salaam. Usidhani kama Djuma amependa kurudi Congo. Tanzania ina utamu wake. Dar es salaam ina utamu wake.

Lakini Azam ni kama wamecheza kamari ile ile ambayo Yanga wameichukua kwa Jonas Mkude. Wamemchukua mchezaji ambaye msimu mmoja uliopita alikuwa mchezaji bora wa msimu, huku akionyesha uwezo wa kushangaza.

Bangala alikuwa na uwezo mkubwa wa kucheza kama beki wa kati lakini hapo hapo alikuwa na uwezo mkubwa wa kucheza kama kiungo akicheza sambamba na mtaalamu mwenzake Khalid Aucho. Hapa Azam inakuwa imesajili wachezaji wawili kwa kutumia mchezaji mmoja.

Kinachotakiwa kwa sasa ni kumrudisha Bangala katika uwezo wale ule. Ni kama ambavyo nafahamu kwamba Yanga watapambana kumrudisha Mkude katika uwezo wake wa miezi 36 nyuma ambapo alikuwa panga pangua katika kikosi cha Simba.

Msimu huu ulioisha, Bangala alikosekana katika mechi muhimu za Yanga na mashabiki wa timu hii walikuwa wanaona ni sawa tu kwa sababu hakuonyesha ukali katika mechi ambazo alikuwa anacheza. Azam wanaamini kwamba watakuwa wameokota dodo chini ya mwembe kwa kuinasa saini yake.

Kwa upande wa Bangala mwenyewe nadhani atakuwa amedhamiria kurudisha heshima yake katika soka letu. Heshima iliyopotea ambayo kwa kiasi kikubwa nusura impoteze katika ramani ya soka letu kama sio Azam kumnunua kutoka Yanga. Fikiria Bangala huyu alikuwa anahusishwa kwenda Singida Fontaine Gate.

Kazi yake kubwa itakuwa kupata nafasi katika kikosi cha Azam ambacho kinaonekana kimekamilika. Fikiria kwanza kupata nafasi ya kucheza katika kikosi ambacho kina Sospeter Bajana, Fei Toto na James Akaminko. Baada ya hapo ni kuendelea kuishikilia namba yake kwa muda mrefu.

CREDIT: MWANANCHI
 
Uandishi mzuri lakini ifahamike kutokea katika maficho ya Avic town nyota wapya wamezaliwa na Yanga mpya imezaliwa kizazi cha wachezaji wenye uchu na hasira wanaotaka kuonesha kuwa huu ni wakati wao.

Yes yanga itaimbwa Kila Kona ya Tanzania Maxwell Nzengeli ni nyota mpya
 
Sipendagi uandishi wake maana inaonyesha huwa ana agenda. Eti alikuwa na kiwewe? Bangala angeachwa mapema na Yanga angepata timu ndani ya masaa 24. Utasemaje pia "alikosekana katika mechi muhimu za Yanga", kama zipi? Maana fainali ya CAF shirikisho amecheza, fainali ya FA amecheza, derby amecheza. Mechi zipi muhimu kuliko hizo?
 
Huyu mnazi wa yanga maneno ya kujifariji na kufariji Wapenzi wa yanga . Bangala asikwambie mtu hakuna kiungo nchi hii tuko hapa
 
Back
Top Bottom