Kichankuli
JF-Expert Member
- Dec 18, 2008
- 887
- 189
Mimi huwa napenda kuangalia kipindi cha michezo cha Runinga ya Star Tv kwani kwa maoni yangu huwa wana habari za kina kuliko Runinga nyingine za Bongo. Jana kwenye kipindi hicho ambacho hurushwa baada ya taarifa ya habari ya saa 2 usiku Bw. Edmund Ruta ambaye alikuwa mtangazaji wa michezo alituhabarisha kuhusu Meneja wa Arsenal alivyojibu utabiri wa mshambuliaji wa Man. United Nani. Naamini habari hii aliisoma kwenye mtandao. Katika habari hiyo kulikuwa na kipengele hiki ambacho wenga alinukuliwa na vyombo vya habari:
I personally dont know who will win the league and I have managed 1,600 games. If Nani knows he must be 1,600 times more intelligent than I am.
Sasa Bw. Ruta kwasababu habari yake aliiandaa kwa lunga ya kiswahili, neno "intelligent" alilitafsiri kwa maana ya Mpelelezi. Kwa kweli nilicheka sana. Ila kilichonishangaza zaidi sijui hivi vipindi huwa havina wahariri.