Duru za siasa - Mgongano wa mawazo

Nguruvi,

..Bajeti yetu inategemea nchi wahisani kwa asilimia 26.

..je, Iran wanaweza kubeba mzigo huo peke yao??

..mimi ningekuwa ktk uongozi ningewaambia Iran wapande dau ndipo tuwasaidie kukwepa vikwazo.

..sasa hivi nina hakika hata US wakituuliza "what r u getting frm Iran??", tutabaki tumebun'gaa.

..Hata Kenya na Uganda hawawezi kujiingiza kwenye michezo hii bila kuhakikisha wanafaidika kwelikweli.

..nakumbuka Mchina "alipanda dau" kwa kutujengea reli ya TAZARA baada ya nchi za magharibi kutuwekea longolongo.

..nchi za magharibi zilikuwa zinapinga uanachama wa China UN wakiipendelea Taiwan. Watanzania tulipambana kwelikweli ndani ya UN na "kufunga goli la kidiplomasia" pale kura yetu ilipowezesha China kurudishwa UN.

NB:

..naomba mnirekebishe hapo juu kama nimekosea kuhusu suala la China ktk UN.

..pia muwahabarishe wasomaji kuhusu kisa cha Salim Salim vs George Bush ndani ya UN.
 
Nguruvi,

..Bajeti yetu inategemea nchi wahisani kwa asilimia 26.

..je, Iran wanaweza kubeba mzigo huo peke yao??

..mimi ningekuwa ktk uongozi ningewaambia Iran wapande dau ndipo tuwasaidie kukwepa vikwazo.

..sasa hivi nina hakika hata US wakituuliza "what r u getting frm Iran??", tutabaki tumebun'gaa.

..Hata Kenya na Uganda hawawezi kujiingiza kwenye michezo hii bila kuhakikisha wanafaidika kwelikweli.

..nakumbuka Mchina "alipanda dau" kwa kutujengea reli ya TAZARA baada ya nchi za magharibi kutuwekea longolongo.

..nchi za magharibi zilikuwa zinapinga uanachama wa China UN wakiipendelea Taiwan. Watanzania tulipambana kwelikweli ndani ya UN na "kufunga goli la kidiplomasia" pale kura yetu ilipowezesha China kurudishwa UN.

NB:

..naomba mnirekebishe hapo juu kama nimekosea kuhusu suala la China ktk UN.

..pia muwahabarishe wasomaji kuhusu kisa cha Salim Salim vs George Bush ndani ya UN.


Jokakuu,

Kuhusu mchina na reli ya uhuru, kuna ukweli na yale unayoyasema. Ujenzi wa TAZARA ulikuwa ni grand scheme of Chinese foreign policies.

Na matatizo yake ni kuwa wakati wa vita vya baridi tulikuwa stadi to use our own foreign policies as a bargain chip to acquire foreign aid.

Kwa maoni yangu binafsi, we should start living within our own means.
 
Nguruvi,..nakumbuka Mchina "alipanda dau" kwa kutujengea reli ya TAZARA baada ya nchi za magharibi kutuwekea longolongo.
..nchi za magharibi zilikuwa zinapinga uanachama wa China UN wakiipendelea Taiwan. Watanzania tulipambana kwelikweli ndani ya UN na "kufunga goli la kidiplomasia" pale kura yetu ilipowezesha China kurudishwa UN.
NB:..naomba mnirekebishe hapo juu kama nimekosea kuhusu suala la China ktk UN
Mkuu Joka kuu, ni kweli kisa cha UN wakati wa mgogoro wa People republic of China (PRC) na Republic of China (ROC).
Marekani ilileta mswada wa kupinga ulioshindwa. China ilitumia sana ushiriki wake katika NAM na South south cooperation ambako Nyerere alikuwa na ushawishi mkubwa sana.
 
BENDERA ZA TANZANIA: MZOZO WA KIDIPLOMASIA, IRAN & MAREKANI

Inaendelea........

Taarifa za uhakika za meli za Iran kubeba bendera ya Tanzania ni za kushtua. Ni taarifa za kushtua kwasababu;
Zimepataikana katika vyombo vya habari kama Reuter na dunia inajua nini kinaendelea.
Hili limefanywa makusudi na mwenyekiti wa kamati ya bunge la Marekani na wala si kuvuja kwa habari.
Barua nyeti kama ile isingeweza kuvuja tu bila kuwa na kusudio ambalo nimelitaja.

Pili, ujumbe mzito kama huu una njia za kidiplomasia za kuufikisha kunakohusika.
Hizi ni dalili za awali za hasira ambayo inaenezwa kwa makusudi ili jumuiya ya Kimataifa itambue nini Tanzania inakifanya.
Barua ile imeandikwa kiufundi sana bila kuonyesha chuki au kumnyooshea kidole mtu bali bendera za Tanzania.

Kiitifaki Tanzania ni nchi moja na yenye kiti kimoja UN. Bendera ya Tanzania ndiyo utambulisho wa nchi katika maeneo mbali mbali ikiwa ni pamoja na vyombo vinavyosafiri duniani kama vya majini. Kwa mtazamo huo kama meli zimeonekana zikiwa na bendera yetu basi hizo ni meli zetu. Marekani wana haki ya kutuuliza kuhusu utata wa meli zinazofahamika ni za Iran lakini zimebeba bendera yetu kama ambavyo tungewauliza kama kuna kombora kutoka katika meli yenye bendera ya USA.

Nikumbushe tu kuwa wale makomandoo wa Israel waliomfuatilia na kumuua kiongozi wa Hamas kule Dubai walikuwa na Passport za nchi mbali mbali. Ingawa nchi hizo hazikuhusika lakini matumizi ya Passport zao yalileta mgogoro wa kidiplomasia na nyingi kukiri kuwa Isarel ilikiuka taratibu za Kimataifa.
Zote zililaani na Dubai kufuta ile imani 'trust' ya Pasport ya Malikia jambo liloidhalilisha Uingereza na hata kufikia wasafiri kuwa na wakati mgumu.

Kwa taarifa tu za vyombo vya habari hakuna anayeweza kusema meli hizo zilikuwa za nchi au ni za watu binafsi.
Hata kama ni za watu binafsi bado wana haki ya kutumia bendera ya nchi yao, swali linakuja je, bendera zimetumika kwa kufuata misingi na taratibu za kisheria na kiitafaki?

Kuna tetesi zisizothibitishwa kuwa wapo wafanyabiashara wenye mahusiano na ofisi kubwa za nchi wanaotumia mwanya wa vikwazo vya Iran kufanya biashara zao kwa mgongo na bendera ya nchi.

Kuna habari pia ya kuwa mfanyabiashara mmoja anayejulikana kama Abdulla ndiye anahusika.
Mkanganyiko ni kuwa inasemekeana meli hizo zimesajiliwa Zanzibar katika mazingira tatanishi.

Hili linathibitishwa na ukweli kuwa yupo mjumbe wa BLW aliyetoa tuhuma kuwa bendera ni suala la muungano na hizi ni njama za Tanzania bara kuzuia Zanzibar isifanye biashara. Kama ilivyo ada Zbar ni wepesi wa kutumia muungano pale penye mafao yao na ni wepesi wa kulaumu muungano hata pasipohitajika.

Aliyelalamika si Tanganyika ni Marekani, na ukweli ni kuwa bendera yetu UN ndiyo inayopepea katia meli hizo.
Hakika hatujui meli hizo zimebeba nini na ni ujinga uliokubuhu kukurupuka na kusema ni suala la biashara.
Lakini muhimu ni kuwa ZBAR ina bendera yake sasa ya muungano ni ya nini? Kwanini hao watu kama si seriakali ya muungano wasiitumie katika shughuli zao.

Ni Zbar hiyo hiyo isiyo na waziri wa mambo ya nje haijawahi kujitokeza kudai sehemu ya madeni ya nje ya nchi kuwa ni ya muungano nao wanapaswa kulipia-'Joka kuu' na wala hawajawahi kusema wanachangia nini katika kupeperusha bendera hiyo zaidi ya kuzusha tuhuma ambazo zipo nje ya itifaki za kidiplomasia!

Zanzibar haijawahi kusimama na kusema gaidi wa kimataifa aliyeua Watanzania ubalozini Mohamed Ghailan ni wao.
Najaribu tu kugusia haya kuonyesha jinsi gani suala hili lilivyo zito kisiasa na kidiplomasia na wala si nia yangu kuongelea ZNZ na tuhuma zisizo na mashiko wala kuhitaji ceritficate kutambua chele na pumba.

Kwa hali yoyote iwayo serikali yetu ipo katika wakati mgumu sana wa kuieleza si Marekani bali jumuiya ya kimataifa nini kinaendelea juu ya sakata hili. Pamoja na ukweli kuwa matumizi ya bendera yetu ni haki yetu na ukweli kuwa hatuchaguliwi adui au rafiki bado tukiwa kama sehemu ya jumuiya ya kimataifa tuna dhima ya kueleza nini kilichotokea.

Tunaweza kuchagua kuwa na jeuri au kiburi, kwa bahati mbaya hii si Tanzania iliyowahi kugomea Olympic, kupinga ujio wa Henry Kissinger wa Marekani, kusimama na kumwambia Malikia Rhodesia si Uingereza, kulaani na kuvunja uhusiano na Israel, kusimama na kutetea Biafra,kusimamia China UN,kuunga mkono Sahar au kuiambia Magharibi mnatunyonya!

Hii ni Tanzania iliyopoteza thamani kama taifa na kile inachokisimamia, ni Tanzania inayoendeshwa kama klabu ya simba au Yangu kupitisha bakuli la bajeti, ni Tanzania iliyoshindwa kusimama dhidi ya wahalifu wa ndani achilia wale wa nje.

Mgogoro huu wa bendera unaweza kutupelekea nchi kuwa katika wakati mgumu.
Mathalani, Iran inajulikana kama nchi yenye kuunga mkono ugaidi kwa tafsiri za Magharibi. Kunasibishwa na sifa hiyo ni kuiweka nchi katika wakati mgumu sana kidiplomasia, kisiasa na kiuchumi.

Hatari kubwa ziaidi ni ile ya usalama. Nchi za Magharibi na Marekani zina nguvu sana na uwezo wa juu wa ku-distabilize vinchi masikini kama vyetu. Kazi ya CIA kuishinda KGB na kuangauka kwa Urusi ni mfano tu, achilia mbali mapinduzi na mauaji kama ya akina Patric Lumbumba n.k.

Ni dhima ya serikali kuueleza umma ukweli kuhusu bendera na meli zinazotuhumiwa.
Siyo vibaya kama mahusiano ya meli hizo ni ya mataifa mawili lakini basi serikali iweke msimamo wazi na si kujificha.
Endapo kuna wafanyabiashara wamezitumia meli hizo tunahitaji kujua, wamezitumia kwa utaratibu gani na bendera zimetumika kwa utaratibu gani.

Mgogoro huu ni wa kidiplomasia utakaoigusa nchi kwa namna nyingi, kiusalama, uchumi na kisiasa. Umeshavuka mipaka ya kidiplomasia na sasa ni 'Public story'. Hakuna njia ya mkato ni sisi wananchi kujua ukweli wa tuhuma hizi nzito.

Tusemezane
 
EAC : NCHI ZETU ZA AFRIKA MASHARIKI ZINAJIFUNZA NINI KUTOKA ULAYA?

Hebu tuziangalie duru za siasa za Marekani na Ulaya halafu tujikite katika ushirikiano unaokua wa Afrika mashariki.
Kampeni za Uchaguzi Marekani zinaendelea huku ikiwa ni dhahiri kuwa Mitt Romney ndiye mbeba bendera ya Republican dhidi ya Rais Obama wa Democrat.

Mahakama ya rufaa ya Marekani imetupilia mbali hoja ya wanachama wa Repulican iliyotaka kuondoa ulazima wa wananchi kuwa na bima ya afya kwa madai kuwa hilo ni kuingilia uhuru wa watu na maisha yao.

Zipo sura mbili za matokeo haya. Sura ya kwanza ni ushindi kwa Rais Obama kwa kujihakikishia kuwa mpango wake wa bima za afya (Obamacare) utaendelea kama ulivyopangwa japo kupita November ya mwaka huu.
Hii inampa nafasi nzuri kwa kundi la walala hoi ambalo ni sehemu ya wapiga kura.

Kuna wanao ona mpango huo ni mzuri na wapo wanaouona si mzuri na kundi la mwisho lakini muhimu ni lile lisiloegemea upande wowote 'independent voters'. Katika wakati huu nchi ikiwa imegawanyika nusu kwa nusu Independent voters huamua nani mshindi.

Sura ya pili ya suala hili ni kusinyaa kwa Republican. Wao walidhani kuwa utenguzi wa Obamacare ungewapa mahali pa kujenga hoja kuwa Rais ametumia muda mwingi na pesa nyingi kwa takribani miaka 2 bila kuwa na kitu cha maana kuhusu mpango wake wa afya.

Hoja nyingine ilikuwa iwe kuwa Rais ameingilia uhuru wa Wamarekani ni hiyo siyo 'America way'.
Hoja hizi zingeunganishwa na ile ya uchumi kuwa Obama anashughulikia mambo yasiyo na uhusiano na tatizo la wananchi ambalo ni uchumi.

Kwasasa hoja zote zimefutika na yamebaki malumbano kati ya Conservative(wahafidhina) wa Republican na Mitt Romney.
Inaonekana Mitt anahukumiwa na historia kwasababu alipokuwa Gavana wa Massachussets alikuwa na mpango wa afya unaoshabihiana sana na wa Obama, sasa kuukana hawezi na wakati huo huo wahafidhina wakimlazimisha aukosoe wa Obama. Kwa Mitt Romney huu ni upanga wenye makali sehemu nyuma na mbele.

Tatizo na mada kuu ni uchumi. Kwa siku za karibuni uchumi umeonekana kudorora ukilinganisha na miezi ya nyuma.
Ingawa takwimu zinaonyesha ukuaji katika uzalishaji viwandani na ajira kwa sekta binafasi, kuna tishio kubwa linalotoka nchi za Ulaya linalowatisha wawekezaji. Hili linamuumiza kichwa Obama kwasababu anaweza kujikuta akiliomba bunge litoe kichochoe cha uchumi 'stimulus package' katika wakati huu wa uchaguzi na huenda akazama nalo.

Mdororo wa Uchumi wa nchi za Ulaya unasukumwa sana na nchi za Italy, Greece, Spain na Portugal.
Greece imekuwa ikiomba udhamini kutokana na hali yake kuwa mbaya. Katika nchi zote Ujerumani ndiye anaonekana Baba wa kuwalea hao wote kwa kutoa dhamana au fedha.

Kuna swali linaulizwa kwanini Ulaya isiiache Greece izame kivyake? Yapo majibu mengi lakini moja ni kuwa Greece ni mteja mzuri wa bidhaa za Ujerumani na kwingineko. Wao wamekuwa wanakopa na hawakusanyi kodi.

Sasa kuanguka kwa Greece kuna maana ya kuzama kwa pesa za mabenki ya nchi kama Ujerumani na hilo litaitikisa Ulaya.
Litaitikisa ulaya kama ilivyotokea Marekani baada ya kuzama kwa sekta ya ujenzi (Housing Market collapse) kulikozamisha benki na hivyo kuvuta kila kitu kwenda chini.

Imefikia mahali kuna mtafaruku mkubwa Ulaya. Wajerumani wanataka pesa yao ya (Dochi mak-kiswahili) irejee waachane na Euro. Hilo lilitokea Ufaransa na kuna manung'uniko mengi tu kuwa wapo wanaobebwa na hawabebeki.
Sheria za uanachama wa EU zinabadilika kidogo kidogo na pengine baada ya mwaka kuna watakaojikuta nje ya Ukanda.

Matatizo ya kiuchumi yanaingiliana sana na ya kisiasa na kijamii na ile EU tunayoijua hakika ina mtafaruku.
Jambo zuri ni kuwa wenzetu hukaa na kuongea wakiongozwa na ukweli (facts).
Sasa hivi baada ya kuwabana wahamiaji kutoka nchi masikini sasa wanaanza kubanana wao kwa wao kwa njia za kimya kimya.

Ukitafakari jinsi na kasi ya ushirikiano wa Afrika mashariki utaona kuna kufanana na pengine kutofoautina kwa namna fulani na Ulaya. Ushirikiano wetu unaonekana kuwa umeagizwa 'imoprted' na si kitu tunachodhani ni chetu kulingana na mazingira yetu.

Hata kama kiuchumi hatukaribiani na wenzetu lakini tunajitahidi kutengeneza kitu cha mfano wa EU ambao umeanza mwaka 1957 ukiwa EEC kama ule wetu wa 1967 na mambo mengi tu tunayofanya kwa mfano wa 'template ya EU'

Afrika mashariki inaweza kuingia katika matatizo makubwa zaidi ya tunayoyaona Ulaya.

Hebu tuangalie ushirikiano tunaotaka kuunda (EAC) kwa wepesi tu kijamii, kisiasa na kiuchumi.

Itaendelea.........
 
SERIKALI: MBINU CHAFU ZA KISIASA, MCHEZO NA MAISHA YA WANANCHI

Takribani miezi miwili serikali ya Tanzania imekuwa katika wakati mgumu kufuatia matukio mbali mbali.
Yapo mengi lakini yanayotingisha zaidi ni haya;
1. Vurugu za Zanzibar, hata kama ni za ZNZ Rais na serikali ya muungano bado inawajibika
2. Jaribio la kutaka kumuua Dr Ulimboka ambalo linaihusisha serikali moja kwa moja
3. Sakata la Chadema kutaja wanaokusudiwa kudhuriwa huku ikiweka wazi majina ya wahusika.
4. Mgomo wa madaktari ambao hauonekani kuwa na mwisho katika siku za usoni huku mamia ya wananchi wakiumia
5. Likazuka suala la mabilioni ya sh takribani 300 yaliyofichwa Uswiss na watu wachache viongozi wa nchi wakitajwa

Katika hayo, tukio namba 1,2,3 tunaweza kuyaweka pamoja kama itakavyojiri.

Jumuiya ya kimataifa imeshtushwa na tukio la uchomaji moto makanisa bila hatua kwa wahusika, na wakati huo huo ikionekana kukandamiza uhuru wa kutoa maoni kwa kuwatawanya wana UAMSHO. Kwa hili serikali haikuonekanekana kuwa na nguvu ya dola wala hekima kulikabili zaidi ya woga wa kisiasa. Ikumbukwe tatizo ni la nchi ya Tanzania hata kama limetokea ZNZ.

Jaribio la kumdhuru Dr Ulimboka likazidi kutoa kivuli kibaya 'cast shadow on' rekodi ya Tanzania kuhusiana na haki za binadamu na utawala bora na wa kisheria. Jaribio hilo limeelezewa duniani kote.

Mgogoro wa madaktari umeifanya dunia ifikiri nchi masikini kama Tanzania hali ni mbaya hata bila mgomo, inakuwaje kukiwa na mgomo! Dunia inajiuliza kuna jitihada gani mezani za kulimaliza tatizo hili.

Hayo yakitokea chama cha upinzani kimetoa madai mazito kuhusu njama za mauaji ya viongozi wake.
Yote yakikusanywa yanatia shaka zaidi kuliko wasi wasi.

Yanatia shaka kwasababu si mara ya kwanza mauaji yametokea bila maelezo na kuisha bila watuhumiwa kuchukuliwa sheria kama ilivyotokea kwa Kubenea, Mbwambo, shambulizi la wabunge, mauaji Igunga na sasa Dr Uliomboka.
Si mara ya kwanza madai ya njama za mauaji yametolewa na wana CCM kama Samueli Sitta, Mwakyembe nk.
Hakuna hata siku moja watoa tuhuma walifikishwa mbele ya sheria, ushahidi kuwa huo ni ukweli

Kibaya zaidi CDM wametaja hadi wahusika, huku serikali ikishindwa kutoa maelezo juu ya shambulizi la Uliomboka.
Ujanja wa kubambikia kesi vibaka ili kuziba watu midomo kwa kauli ya suala lipo mahakamani imeshindikana.
Kwa Dr Uliomboka ushahidi upo wazi kiasi kwamba serikali haina pa kutokea bali kuchanganyikiwa.

Wakati serikali ikishindwa kuinua hali za sekta ya afya kama inavyodaiwa na Madkatari, hoja namba 4 inaingia. Mgomo hauonekani kuwa na mwisho na suluhu ya serikali ni kuwafukuza madaktari. Ni wazi kuwa madakatari bingwa hawatahimili vishindo vya wingi wa kazi na wao watajiunga kama hawajajiunga.

Wakati huo bunge linalowakilisha wananchi limejificha nyuma ya kisingizio cha suala lipo mahakamani.
Sijui sauti ya masikini wanaoteseka na mgogoro huu inasemwa na nani?
Spika na wenyeviti wa bunge wamekazana kutoa miongozo ya kuwatoa nje watu badala ya kushughulikia mambo ya kitaifa.

Habari kwa upande wa serikali zinakuwa mbaya pale hoja namba 5 inapoingia.
Wakati hakuna fedha za kuimarisha huduma ya afya imebainika kuwa kikundi cha watu wasiozidi 10 kwa ushirikiano na wafanyabiashara wahalifu kimewekeza kiasi cha sh bilioni 300 Uswis.
Hayo yametokea kukiwa na usalama wa taifa TISS, Police, Takukuru nk.

Eti serikali inasubiri taarifa kutoka Uswis. Ni usanii ule ule wa Rada ambayo ilimgharimu Clair shot kazi yake na mwisho kuwaona akina Membe wakienda kubeba pesa. Hakuna mhalifu aliyekamatwa kana kwamba pesa zilikuwa na miguu.

Kashfa ya Uswis kama ilivyo ya Rada, Richmond, Meremeta nk. zitafunikwa chini ya kapeti na vyombo vya dola kushughulika na mtu mmoja kule Mabwepande!

Nimeeleza mambo haya kwasababu wiki hii taarifa iliyotawala vyombo vya habari, mablog nk. ni kuhusu Kamili aliyemfkisha Dr Slaa mahakamani kwa mambo ya kifamilia.

Ukiangalia kwa makini hii ilikuwa 'calculated move' baada ya Dr Slaa kueleza mbinu za kumdhuru Josephine ili shindwe majukumu yake kikazi na kumnyamazisha kuhusu masuala ya kitaifa.
Sina ushahidi lakini ushahidi wa kimazingira hauna shaka kuwa hii ni moja ya mbinu za serikali kuondoa 'attention' ya umma kutoka kwenye masuala nyeti ya kitaifa na yanayohusu maisha ya Watanzania moja kwa moja.

Tutafafanua kwa undani kuhusu mbinu hii chafu ya serikali, kushindwa kazi kwa vyombo vya dola ambavyo sasa ni kama vijibwa 'puppet' vya kupewa maagizo bila kufikiri au kutafakuri na udhalimu unaoendekeza utamaduni wa mauaji

Itaendelea.....
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Mkuu Nguruvi:
Huo ndio mfumo wa siasa tuliouchagua, ni kupoteza muda tu kuhoji mbona kimetokea hiki na hiki! Kwani ukifuga manyigu utalina asali? Itoke wapi?
Tutapiga kelele, lakini ukweli hauwezi kupingwa "Mfumo mbovu wa Siasa, ni chanzo cha matatizo yote katika taifa lolote la Kiafrika"
Ubepari ni "pigania kunyonya kwa njia yoyote ile" na umegawanyika katika sehemu kuu mbili "no more"
1. Internal Capitalism-unyonyaji ndani ya taifa moja baina ya mtu na mtu. Kwanini sasa tumshangae Lowassa, Rostam, Mbowe, Ndesamburo, Nkono, Sumaye, Mkapa, Riz 1 na babaye? Mfumo umeruhusu!
2. External Capitalism-taifa kunyonya taifa...tunawaona migodini, mbugani, majini, wanajiita wawekezaji. Kipi cha kushangaa?
Nchi nying za ng'ambo zipo katika daraja la pili, ndio maana hakuna kero nyingi kama zitokeazo kwetu. Sasa, ni lini tunadhani tunaweza kufikia hatua ya juu?
Ukifuga manyigu usililie asali, tena usishangae kung'atwa nao! Fuga nyuki. UBUNIFU HAUJAWAI KUFIKA MWISHO.
Mungu wetu anaita!
 
Nguruvi3,

Hakika umeyaweka maswala haya yote vizuri sana na ktk mtiririko ambao binafsi yangu kwa muda wote nimekuwa tofauti sana na Watanzania wenzangu ktk maswala haya yote japokuwa sababu zipo za maana kabisa..Nisichokubaliana nacho mimi ktk yote haya ni maandaliazi na maamuzi mabaya ambayo badala ya kuujenga yanaubomoa Umma wenyewe.


1. Kwanza swala la vurugu za Zanzibar,
Swala hili limetokana na baadhi ya watu kuitumia dini ktk siasa japokuwa ktk Uislaam tumeamrishwa kuwa ndio mfumo wa Maisha yetu kwa maana ya kwamba Uislaam kiutawala unapigania vitu vitatu vikubwa kwa Umati wake navyo ni UHURU (Freedom), HAKI (Justice) na USAWA (Equality). Hakuna sura hata moja inayozungumzia mipaka ya nchi na watu wake wala hakuna hata sura moja nayozungumzia wadhifa ama ushirikisho wa Waislaam ktk utawala isipokuwa kinachotakiwa ni kuhakikisha binadamu wote wanapata Uhuru, haki na usawa.

Lakini pia ndani ya Uislaam hakuna Liberty isipokuwa ile tulomrishwa na Mwenyezi Mungu, yaani hakuna uhuru wa kuchagua (Freedom of choice) ya kwamba naweza chagua kuabudu kitu kingine chochote zaidi ya Mwenyezi Mungu. Sasa hapa ndipo utata unapoingia na hasa kwa jamaa zetu wa Zanzibar na Waislaam wengi wenye siasa kali ambao kwa fikra zao wanafikiri kwamba wanayo haki ya Kuimpose na kulazimisha sheria kwa kila mtu kuabudu Mwenyezi Mungu ktk kufanya Ibada.

Nimeandika sana kuhusu Dini Islaam ya kwamba hii ni dini inayojitegemea. Ni dini ya Mwenyezi Mungu na hakuna binadamu anayeweza kuilinda isipokuwa Subhana wataallah yaani Mungu mwenyewe ambaye ndiye kaileta dini hiyo kwetu sisi. Hivyo tunachoweza tu sisi kufanya ni kuwalinda watu walioamini ktk Uislaam pale Waislaam wanapokatazwa kuabudu na kufanya Ibada zao lakini sii kulazimisha wengine waabudu tunacho abudu sisi. Hivyo hatutakiwi kuwalazimisha watu kuabudu Uislaam na wala wao hawatakiwi kutulazimisha sisi kuabudu wanacho kiabudu wao. Huu ndio UHURU tulopewa kiimani na ulozungumziwa ktk Uislaam.

Hivyo napomwona Muislaam akijaribu kulazimisha Mkristu afuate imani yake kwa lazima au kumfukuza hapo alipo wakati Historia ya dini hii ya Kiislaam imekuja wakati Mecca na Madina kote walikuwa Makafir lakini mtume Muhammad (SAW) aliweza kuwageuza hawa watu imani zao na wakaifuata dini na kutetea uhuru wao kuchagua dini hii na hata kupigana vita pale dini ilipokatazwa ama watu kunyimwa Uhuru wa kuabudu ktk misingi ya Kiislaam. Leo Waislaam wamesahau historia ya dini yao wanataka wao kulazimisha watu wengine kuwa Waislaam tena kwa shahada ya kupata jina la Kiarabu wakati ushenzi wote unafanyika nyuma ya pazia....nini hii jamani maana ktk Uislaam tumeamrishwa kukatazana mabaya (Law) na kufundishana yaliyo mema (Knowledge).. Nabaki kushangaa Elimu ya dini ya hawa Masheikh wetu, maana unapochoma Makanisa moto ni ktk kulazimisha watu wawe waislaam.

2. Swala la Madkatari,
Hapa tena nimekutana na utata mkubwa zaidi pengine labda mimi hufikiria tofauti sana na watu wengine kwa sababu sikubaliani kabisa na maandalizi au maamuzi ambayo kwamba yanalenga kumuumiza mtu mwingine ili kufikisha Ujumbe. Sikubaliani na Hijackers wa ndege, Olimpiki na sijui shule ili kufikisha ujumbe na kutafuta attetion ya serikali au vyombo vinavyowanyanyasa. Sikubaliani na maandalizi na maamuzi ya nchi za mgharibi kuwawekea vikwazo Zimbabwe au Iran ili kuziangusha nchi hizo kiuchumi ilihali wanaokufa ni raiwa wananchi wasiokuwa na hatia wakati Mugabe, Ahmadnajad na Familia zao wanakula kuku kwa mvinyo..Sikubalianani na maandalizi yoyote yenye maamuzi ya kupambana na wadhalimu kwa kutumia Vifo vya watu kama ujumbe wa kuonyesha haki na umuhimu wa madai yako iwe 9/11, Dikteta au kunyimwa HAKI unayodai.

Ila nitakubaliana na maandalizi yenye maamuzi ya kuweka madai moja kwa moja kwa mhusika.. Kama unateka ndege, teka ndege ya rais, kama unaweka vikwazo mwekee vikwazo rais, kama una tatizo lolote na serikali iliyopo madarakani iadhibu serikali yenyewe kwa sababu ukiadhibu wananchi ktk nchi zetu hizi hakuna kiongozi atajali hilo mana haathiriki yeye na familia yake kwa lolote.

Ni jana tu nimesikia Historia ya Kongo wakisema hadi sasa inakadiriwa wameisha kufa watu mil 5, jamani watu Millioni 5 na dunia tumekaa kimyaa tukitazama ati hao ni - Casualties of war!..Hawa wenzetu wanagombania Biriani walowekewa ktk mkeka, wapishi wenyewe Marekani na China wakiiba rasilimali zao toka jikoni na hawajui kinachoendelea huko jikoni, na wengine kina sisi kwa Ujinga wetu tunamsifia Kagame kwa kupora Utajiri wa Kongo kuiendeleza Rwanda vile vile. Yaani mwizi ndiye anasifika maadam kafanikiwa kuiba bila kushikwa. Na wala simlaumu sana Kagame kwa sababu sisi wenyewe mijitu mijinga sana tuko radhi kutothamini UTU na uhai wetu kwa utajiri hivyo ukiwa na Mtu kama Kagame - Sindbad wa Afrika kwa nini usimpe sifa zote..

Mwisho wa yote, Ya Zanzibar, Madaktari, Ulimboka na sakata la Chadema naweza kusema tu ya kwamba sisi Watanzania tuna matatizo sana ktk maandalizi na maamuzi gani tunatakiwa kuchukua. Most of the time tunafanya maamuzi mabaya sana na yanatugharimu iwe kutuingiza ktk utumwa kiuchumi au hata kimaisha na ndio maana sisi bado maskini. Mara nyingi tunataka kuitazama Tanzania kama Amerika au UK kwa msingi huu kila mtu anataka kuishi kama wao..Hapo ndipo tunapo putana viganja ktk sinia la biriani maana sisi maskini tunaokula ktk sinia na siii mezani wala jikoni.. Ni muhimu sana sisi Watanzania tuelewe ya kwamba sasa hivi hatugawani keki ya Taifa isipokuwa tunanyang'anyana keki hiyo. Til siku mfumo huu utakapogeuzwa tukaacha kuweka mduara na sinia la biriani mkekani.. Tukaacha kuchugua wapishi (viongozi) kutokana na umaarufu wao bali wapishi wanajua kupika sii hawa viongozi wetu wanaokaa jikoni kwa sababu ndiko wanakowahi biriani na nyama za kutosha..basi nchi hii tutaendelea kuadhibiana wenyewe kama Jinsi Marekani wanavyofikiria kwa kumuadhibu Mugabe kiuchumi atakuja achia utawala siku moja... Hii akili kweli?..

Labda niulize hivi kuna Mfalme, rais au Waziri mkuu gani aliyewahi kuachia uongozi kutokana na vikwazo vya kiuchumi? Simple as that, ni kwamba hakuna mtu wala serikali iliyowahi kupiga magoti kwa Terrorist...Iwe wananchi wa Zanzibar, Madaktari au serikali yenyewe kutumia vitisho haiwezi kubadilisha mwamko wa wananchi Kifikra.. The most powerful thing than MONEY is KNOWLEDGE.. Ikiweza kumfundisha mtu knowledge akaujua thamani ya UTU wake basi sii rahisi fedha kumnunua, thriugh Knowledge ndio Mapinduzi ya kweli hutokea.
 
Mkuu Mkandara,
Bandiko lako #167 nimelisoma vema nashukuru kwa maoni yako yenye kina.
Ninachokiona mimi ni kile ulichokihitimishia kuwa kitu cha muhimu katika kumkomboa mtu ni knowlege.
Ukisoma bandiko langu #164 nilisema ukombozi wa kweli unatoka kwa mtu mwenyewe kwanza kabla ya mkusanyiko.
Hili litawezekana nikishadidia hoja yako ya knowledge kwanza.

Tatizo la ZNZ ukiliangalia ni kundi la watu wenye dhamira za kisiasa na kwa bahati mbaya wamejificha katika mgongo wa dini.Hakuna mtu anayeweza kutenga imani na siasa kwa ukweli wa maisha.
Wanasiasa wana mwingiliano mkubwa sana kikazi na dini kama ilivyo kinyume chake
Kinachotokea sasa hivi nchini si msuguano wa dini na siasa, bali msuguano wa viongozi wa dini wanaotaka masilahi ya kisiasa na viongozi wa kisiasa wanaotaka kuungwa mkono na dini.

Ikifika hapo ndipo unakuta viongozi wa dini wakichipuka kama uyoga na wengine wakidandia hoja ili mradi tu kila mmoja aonekane na huenda apate anachokitaka si kile dini inachokitaka.

Hili limefanya kauli za viongozi wa dini zionekane kelele tu kinyume na huko nyuma ambapo kauli zao zilichukuliwa kwa uzito mkubwa. Kwa hili ningeomba unafahamishe hivi inakuwaje kila kiongozi hasa Waislam anaibuka na kusema 'sisi waislam' au waislam wanasema. Hapa kuna utaratibu gani wa kuongoza jamii.
Na pia unifahamishe hivi madaraja katika uislam yanapatikanaje ili umma uweze kutofautisha kati ya sheikh na shekha!


Kuhusu madaktari natofoatiana na wewe kwa jambo moja.
Kwa serikali isiyosikia kama ya Tanzania kuna wakati hatua chungu ni lazima si kwa kupenda bali kwa ulazima.
Suala la huduma mbovu hospitali limeshazungumzwa sana katika migomo iliyotangulia, makongamano na warsha.
Hakuna hatua yoyote ile ya maana inayochukuliwa ku-adress the issue.

Kwanini tuwalaumu madakatari wanaohitaji MRI machine ili waweze kutibu masikini kwa ufanisi!
Inakuwaje hospitali kubwa ya rufaa inakosa vitu muhimu kama MRI katika dunia ya sasa.
Huko wilayani hakuna X-ray katika wilaya zaidi ya 110. Kwa maneno mengine Madaktari wetu wanafanya kazi kwa 'ramli' na siyo utaalamu.
Kwa mantiki hiyo watu wanaokufa kwa kukosa vifaa au misdiagnosis kutokana na uhaba wa vifaa ni wengi kuliko inavyodhaniwa.

Lakini pia lazima tuanagalie suala hili kwa kiwango cha kawaida tu. Hivi unajisikiaje mgonjwa wako akiwa amelazwa hopsitali kwa tatizo la uti wa mgongo unaouma halafu akatoka hospitali akiwa na TB kwasababu alikuwa katika kitanda kimoja na wagonjwa 2, mmoja wa kuhara na mwingine wa TB!
Hapo kweli kuna tiba na utatibu au kuambukiziana na kuuana.
Kwanini hili tusione kama mauaji tuone mgomo wa madaktari unaolenga kuimarisha hali ya afya kama tatizo kubwa zaidi. Hapa kwanini tunakuwa na makengeza kuangalia tulipoangukia na siyo tulipojikwaa.

Wakati hayo yakitokea na kuwalaumu madaktari, sisi wananchi hatujawahi kulaumu mamilioni ya dollar yanayotumika kutibu watu wachache sana nchini.

Siku hizi kila kiongozi anayeumwa anapelekwa Appolo! haya hayakuwepo miaka ya nyuma sasa tatizo limeanza vipi.
Je, ni haki kuwalaumu viongozi wanokwenda India kupatiwa MRI ambayo haipo muhimbili? Kwanini tusifikiriea kutumia pesa kununua na kuimarisha sekta ya afya ihudumie kila mmoja wetu tunadhani kwenda India ndio suluhisho!

Najua upo utetezi kuwa hatuna uwezo! hiki ni kichekesho na kuonyesha jinsi gani viongozi wanadharau umma wa Watanzania. Bajeti ya mwaka huu ina bilioni 16 za vitafunio vya chai tu.

Kumtibu mbunge mmoja tu India ni zaidi ya milioni 50 kwa safari na kutegemeana na tatizo.
Wapo wabunge wamekaa India miezi 6 achilia mbali wale wanaokwenda kupima malaria na BP. Pesa zinatoka wapi?

Bajeti ya mwaka huu imetenga bilioni 7 kwa ajili ya JK, BWMkapa, AHMwinyi, JSMalecela, CDMsuya, ENLowasa, FTSumaye, JSWarioba. Hizo ni lazima zitumike waumwe wasiumwe! Kwa wastani ni bilioni moja kwa kila kiongozi.
Kwanini visinuliliwe vifaa ili wao pamoja na wananchi wengine wafaidike kwa pamoja?

Huko serikalini ndiko usiseme, kila siku kama si mkurugenzi ni katibu mkuu au mkuu wa Idara anakwenda India kupima mafua yasiyoisha kwa wiki mbili sasa. Pesa zinatoka wapi?

Sasa ikifika mahali ambapo mtu na familia yake wanauhakika wa kutibiwa India, South Afrika nk. nani atajali kuwa kuna wazazi hospitali ya Temeke wanapanga foleni kuingia katika chumba cha kuzalishia kwasababu kitanda ni kimoja!

Mimi nadhani ni makosa kuwalaumu madaktari kwasababu wao wanauwezo wa kwenda kazini na kila mgonjwa anaandikiwa kwenda India. Hadi hapo watakuwa hawajagoma na wametimiza kiapo chao cha udaktari.
Je, masikini wangapi waliobeba mgonjwa katika baiskeli wanaweza kununu tiketi tu ya India achilia mbali matibabu!

Kwanini tuangalie tulipoangukia na siyo tulipojikwaa!
Kuna njia gani Kiongozi wa Tanzania na mtumishi wa umma mwenye akaunti ya dola 700,000 benki anaweza kuelewa kilio cha Watanzania?
Nadhani mgomo wa madaktari si ujumbe kwa serikali ni ujumbe muhimu sana kwa wananchi wanaolipa kodi.
 
JokaKuu, hili la nchi za kiarabu zenye utajiri wa mafuta kushinikiza Wapestina wapewe haki yao limeathiriwa sana na vita ya Iraq. Pengine hali ya Palestine ingekuwa na nafuu kuliko ilivyo sasa kama hii vita haikuwepo. Sadam Hussein alikuwa rafiki wa marekani kabla hajawa hasimu wao mkubwa. Vita ya Iraq na kifo chake Sadam Hussein kwanza kilitoa mwanya kwa shia majority ndani ya Iraq kushika madaraka makubwa, lakini kubwa IRAN iliibuka kama big brother fulani wa ukanda huu wa Middle East. Iran watu wake wengi ni Shia, na jirani sasa nako wengi ni shia.

Looser number moja wa huu mtafaruku anakuwa Saudi Arabia (na hata UAE). Hawa ni sunni, na kwa muda walikuwa juu (dominance), sasa wanakuwa challenged na Iran ambayo iko kwenye mkakati wake wa Nuclear. Hili la nuclear linazidi kupandisha mashetani wasaudia na marafiki zake marekani. Na hapa ndipo urafiki wa Saudia na mmarekani unazidi kuimarika kwa sababu wote wana common enemy - Iran. Marekani kwa upande mwingine na muisraeli ni kitu kimoja. Na hapa ndipo tunakuja kwa looser number mbili Palestine.

Saudia ina nafasi kubwa sana kuongoza nchi nyingine middle east ili kuisaidia palestina. Lakini vile vile Saudia na wenzake wanamuhitaji sana mmarekani kupambana na Iran. Mmarekani yuko na Israel na kuna fununu kwamba nyuma za pazia Saudia anakubaliana mambo mengi tu na Israel kupitia kwa middle man - marekani.
Mkuu wangu hizi ni siasa za kwenye luninga, siasa ambazo nchi za magharibi zinataka sisi tuamini lakini ukweli upo wazi kabisa ya kwamba vita kuu ya sasa hivi kidunia ni UKOLONI MAMBOLEO... Hakuna siasa (Uhuru na UTU wa watu) kutangulia Uchumi bali uchumi ndio unaojenga uhuru wa watu wenyewe..

Labda nikueleze tu kwa kifupi, Miaka yote ya Ubepoari Marekani na nchi za magharibi ilikuwa kutawala nchi kiuchumi na hapakuwa na nia rahisi zaidi ya kukamata makoloni..Mataifa mengi yalipojikuta yanaathirika kiuchumi kwa kukoloniwa yalifikiri kufanya mageuzi ya utawla ndio njia pekee ya kuboresha maisha yao kiuchumi wakiwa huru na ndio maana hatua ya kwanza ktk ukombozi wa nchi zetu ilikuwa Uhuru wa Bendera.

Sasa katika mahesabu ya nchi magharibi wakakubali kutoa Uhuru lakini kwa sababu walikuwa wameisha weka mitego yao ktk investment zao wanatafuta njia ya kuzilinda mali zao ndio kina Saadam Hussein, Shah, Mobutu, na wengine wengi tu wakipachikwa kwa maandalizi maalum. Hata Nyerere alikuwa ktk kundi hilo japokuiwa hawakujua undani wake.. yeye alikuwa na mahesabu yake tayari maana alizungukwa na wajamaa kina Abrahaman Babu, Nassor Moyo, Hanga na wengine wengi tu wasomi.

Ndio tukaona Uhuru ukitolewa kama karanga lakini bado nchi nyingi hazikuwa na viwanda isipokuwa utoaji wa mali ghafi - wanasema dhahabu sii dhahabu until imetengenezwa kito kwa maana kwamba Pamba haina thamani kama zao isipokuwa kile kinachotokana na zao hilo ndio thaminisho la Pamba..

Tukapewa Uhuru wetu lakini baadhi ya viongozi wa nchi hizi wakaanza kushtuka na kukoloniwa Kiuchumi, kumbe muda wote wakoloni walikuja nchi hizi kufuata rasilimali zetu na sio kututawala sisi kama watumwa!!!. Maana historia inatuambia Wakoloni walikuja Afrika kuchukua watumwa kama cheap labours, wakafunga utumwa wenyewe lakinni bado wakabakia Afrika kututawala, haya wametupa Uhuru lakini bado maisha ya wananchi hayajabadilika ndio kujua kwamba hawa watu walikuja kuchuma na sii kututawala. Kina Nyerere wakapiga sana kelele ktk vikao vya UN lakini hakuna aliyewasikia..

Likaja vuguvugu la kifikra, viongozi na wanasiasa wetu kuzitazama upya fikra za kina Karl Max na Stalin ambazo muda wote walielewa asili ya kupe ni kunyonya damu na sii kutafuta makazi au usafiri wa bure..Ndio mageuzi yakaanza kuiva kina Nyerere wakatokea na kupigwa vita vikali sana maana waligusa interest zao. Japokuwa imechukua muda mrefu sana kwa wananchi wa nchi mbali mbali kugundua kwamba tumetawaliwa kiuchumi, nguvu ya fikra hizi sasa hivi ni kubwa zaidi kuliko wakati wowote ule hata kupita wakati wa vita baridi..

Nirudi kwa Saadam HUssein, huyu mkuu wangu tatizo lake alitangaza kubadilisha mauzo yake na kutumia Euro badala ya dollar, alianza kuweka mikataba na Wachina badala ya Marekani. hana Tofauti na Ghadaffi ambaye aliweka mkataba na Wachina tena baada ya kutaka kuwatosa Wafaransa kwa mara ya pili. Maana ktk makubaliano ya kuondoa vikwazo Libya walikubali kurudisha mashirika ya mafuta ya Shell na yale ya Ufaransa na kwa muda wa miaka minne waliweza kujua ngome zote za Ghadaffi..Hivyo kuondolewa watu hawa ilikuwa Lazima na sii swala la vita na Israel au urafiki na Palestine.

Saudi Arabia on the other hand wanatawaliwa kiuchumi, kwa miaka 35 walikuwa hawapati kitu toka machimbo ya mafuta hadi mkataba ulipokwisha ndio mali ile imerudi kwa Sultan. Kuna tatizo kubwa la uhasama baina ya Sunni na Shia na huu ndio mtaji mkubwa wa Marekani.. The more Shia becomes a threat to Saudia the more they depends on western world ambao wamewahakikishia usalama lakini wakati huo huo hawa west wanahakikisha Saudia inazungukwa na Shias hivyo bado Marekani na nchi za magharibi wana investment zao nyingi sana na kubwa Saudia. Jiulize ikiwa baba yake Osama ni mmoja wa matajiri wakuba Saudia lakini kibiashara ni mbia wa familia ya Bush, unategemea kuna kina Bush wangapi Saudia?.

Nchi ya pili duniani kwa kutoa mafuta ni Iran, toka mapinduzi ya Khomein, nchi za magharibi wamepoteza utajiri mkubwa sana toka nchi hiyo, na nakuhakikishia sio swala la Nuclear hata kidogo isipokuwa ni flash tulotupiwa machoni ghafla limetupumbaza hatuoni mbali. Wanachotaka ni Utajiri wa Iran na watafanya kila hila kuhakiisha anaingia kibaraka wao kama walivyofanya Afghanstan, Pakistan, Misri pengine na kwetu vile vile who knows maana dalili zote zipo. Palestine is another catch 22. Jiulize kwani Palestine wakipewa Uhuru wao kutatokea nini?..As a fact, Israel kuwepo ndio tishio kubwa la Waarabu kuliko kutokuwepo na hivyo wanahitaji ulinzi na Technologia zaidi kujilinda wao. Where will they get all this - Western Countries!.. More money more power to the west!..Palestine wakiupata Uhuru wao kuna sababu gani ya waarabu kujilinda tena maana hakuna mgonvi kila mtu kapata alichokitaka. Nchi za magharibi hawatauza vifaa vya kivita na ndio walipowekeza zaidi na kupiga mabillioni ya fedha - Fear is the Key!

Kama kweli Marekani na nchi za magharibi wanaogopa Iran kuwa na Nuclear head bomb mbona wanashirikiana na Pakistan nchi ambayo haina kabisa muamana kutengeneza nuclear bomb. Ebu tufikiri kwa undani zaidi, ikiwa Iran ina utajiri mkubwa hivyo na kumetokea vita unafikiri wanashindwa kununua nuclear head missile lililokwisha tengenezwa toka nchi hizo hizo kama wanavyonunua vifaa vingine vya kivita? maana silaha zote hizi zinatengenezwa ili viuzwe na sii kusubiri vita kaa itatokea. Iran walipokuwa wakipigana na Iraq, Marekani aliwauzia Iraq mabomu ambayo hayaruhusiwi vitani wakati Iraq walikuwa hawawezi kutengeneza mabomu hayo. Sisi hatutengenezi vifaa vya kivita lakini tunaweza kununua vifaa vyovyote na technologia tuitakayo kama fedha ipo..

So if they can sale all war machine of distruction what makes us think Russia, Pakistan, India, UK, USA wont sale nuclear head missle if the price is right ---They have used it before why care now! kwa hiyo kama kweli wanaogopa Nuclear bomb inatakiwa zote ziteketezwe pasiwepo na nuclear bombs..Again nitasisitiza sana ndugu zangu mkumbuke hili moja.. Marekani are not inerested in anything other than your Resources...

Uranium yetu haina bei hadi itengeneze bomu au nguvu za umeme na hapo ndipo utajiri ulipo..Kama sisi Afrika tusingekuwa na Utajiri huu, ninakuhakikishieni no single Western country would have been interest in us, Iran or Saudia. Economic power rules the world today na sio mabavu au ushujaa wa kina Umsolopagas - You can buy them..
 
Hospitali-Tanzania.jpg


Picha hii ni kwa hisani ya mtandao wa Bongocelebrity.com (Ninawashukuru)

Katika bandiko #173 hapo juu tumeelezea kwa maneno tu juu ya hali za sekta ya afya nchini.
Tumeeleza kuwa mgomo wa madaktari si ujumbe kwa serikali ni ujumbe kwa walipa kodi.
Wakati akina mama hao wamebanana sawa sawa kuna haya yamejiri Dodoma;
1. Bajeti ya vitafunio Bilioni 16 Shs
2. Bajeti ya viongozi wastaafu Biloni 7 Tshs
3. Bajeti ya mashangingi (Bilioni mia kadha)
4. Bajeti ya ofisi ya makamu wa Rais kwa ajili ya mambo ya ZNZ (Bilioni 32)
5. Misamaha ya kodi (Trilioni 1.2)
nk.nk.

Wakati tunashangaa mkusanyiko huo wa wagonjwa bila hewa ya kutosha achilia mbali kuambukizana maradhi, tusisahau kuwa kuna mtu mmoja anaitwa Gavana wa BoT anaishi katika jumba lililojengwa na serikali hii isiyo na pesa kwa gharama ya Bilioni 2.5.

Muhimu kujiuliza ni kuwa huyu Daktari anayepita hapo kwa ''ward round '' kujua hali za wagonjwa anapitia wapi?
Hivi huyu Daktari anafanya kazi katika 'risk' ya namna gani?
Hivi kiapo cha udaktari maana yake ni kutibu au ni kufa kwa maambukizi.

Katika hao unawaona hapo nani anaweza kukodi teksi ya kumpeleka Airport hata kama amepewa tiketi ya bure na malazi,matibabu bure India!!

Kwanini tunaliangalia suala la mgomo kwa jicho pembe na si kwa macho mawili. Katika mazingira hayo hapo juu nani atasimama kuwasemea kama si madaktari. Kwanini tuchague hoja ya mafao ya madaktari na tuache kujadili tatizo hili linalowakabili mamilioni ya Watanzania?

Ni nani katika wale wabunge 320 anaweza kulala usiku mmoja tu katika hiyo wodi.
Nani katika baraza la mawaziri anaweza kukubali mtoto wake alale hapo usiku mmoja.!
Nani katika makatibu wakuu, wakurugenzi nk anaweza kukubali mkewe alale hapo kwa masaa 6!

Je, hivi ndivyo wanavyotibiwa Appolo India!
 
Nguruvi3,

Mkuu wangu kama umewahi kunisoma nyuma utagundua kwamba nilikuwa siko pamoja na madaktari ktk mgomo wao ambao sielewi kwa nini walikosea maandalizi yake na hata hatua walizochukua toka ule mgomo wa kwanza..

Binafsi yangu niseme haki lillah hakuna kitu kinachoniudhi hapa duniani kama mtu anayetaka kulinganisha umuhimu baina ya mtu na mtu ama kazi na kazi. Na sintowatetea viongozi wala wabunge lakini Madaktari wanapoweka madai yao kwa sababu wanafikiria wao ni muhimu kuliko Wabunge au mfanyakzi mwingine yeyote hapo ndipo huchoka na uwezo wa wasomi wetu kufikiri na nitasema kwa nini..

Kwanza kabisa daktari ni mtu anayeponya yaani walikwisha atharika kupewa tiba na daktari, umuhimu wake ni mkubwa sana lakini unatanguliwa pia na serikali ambayo ndio inatunga policies na hata bunge maana hawa ndio wanaopitisha matumizi ya serikali ktk kuzuia maradhi na hata kupunguza hesabu ya wagonjwa. Hawa ndio miungu watu wa dunia hii ya leo wanaoweza kusema Be and it shall be!..hakuna sababu ya kudharau kazi yao hata kidogo.

Afya yetu sote hapa inategemea serikali, hospitalini ni baada ya... Kama serikali itashindwa kuweka mikakati bora ya kuteketeza mbu wa malaria, basi madaktari watakuwa na kazi kubwa zaidi kuponyesha na pengine vifo kuongezeka pamoja na jitihada zao kubwa zinazotambuliwa. Hivyo umuhimu wa wabunge na serikali uko palepale kwamba wao ndio ngao yetu, wao ndio wanaweza kutuahidi maisha bora na yakawezekana na wao ndio WALOTUFIKISHA hapa tulipo leo..ni wao na umuhimu wao unajionyesha tunapopiga makelele haya yote..

Hivyo jamani, sii vizuri kusema Daktari ni mbora kuliko Mbunge au Polisi au mkandarasi au mbeba taka...Kwa kutazama nchi za magharibi ambao kwa makusudi kabisa huzalisha magonjwa ili biashara ya AFYA ifanikiwe. Daktari anathaminika sii kwa kuponya wagonjwa wengi au mtaalam wa magonjwa wa isipokuwa kwa uwezo wake kuliingizia shirika faida kubwa kwa mwaka. Hospital it's a huge business kuliko biashara nyingi sana na kazi yake ngumu lakini yenye mapato makubwa sana.. Wenzetu wanajua fika kwamba sigara zinaambukiza Cancer, lakini uliona wapi wakipiga marufuku kutengenezwa sigara? Vyakula vyote vya Maabara vina side effects zake na wanazijua lakini uliona wapi mbegu za MF zikipigwa marufuku. Vyakula vya makopo vina atahari zake lakini uliona wapi wakipiga marufuku uwekaji wa vyakula ktk makopo na kusisitiza fresh food to ndio viuzwe?.

Kina sisi jamani hatujafika huko! bado swala la maradhi ni adui wa maendeleo yetu wakati wenzetu maradhi ni sehemu ya mapato yao..lazima tutakuwa tofauti ktk mbinu za kufanikiwa..Haya yote ni baadhi ya mambo machache yanazozinufaisha investment za Big Corporates zilizowekeza mabillions ya fedha zao ktk kitengo cha AFYA kibiashara na hakika siku zote ukinunua share zako ktk mashirika ya madawa hutapoteza uwekezaji huo - It's a win win situation. Sisi kwetu ndio kwanza tunauziwa madawa feki maana hakuna biashara ki hivyo, tupo vitani kupambana na maradhi an expensive expenditure. Why Marekani wanatumia billions ktk fungu la Jeshi? kwa sababu wanatengeneza silaha na wanaziuza kwa faida kubwa, sisi tunao nunua silaha hizo hatuwezi kutenga fungu sawa na nchi hizo ama kuwalipa wanajeshi wetu kama Ulaya kwa kununua silaha ili kupigana vita..Ni expenses juu ya expenses. Hivyo sisi tunaogopa vita wakati wenzetu wanavikaribisha kila mwaa ili wauze silaha zao.

Inaendelea....
 
Sasa narudi ktk mada yetu, swali zuri sana umeweza kuwauliza Wabunge lakini unachoshindwa kuelewa hawa ni watu wasiotakiwa kuwepo pale lakini sisi wenyewe ndio tumewachagua. Tulishindwa vipi kuwachagua Wabunge wanaowekea maanani swala la AFYA?.

Ni chama gani kilichoweka sera zake wazi kuhusu AFYA na sisi tukakichagua kwa sababu hiyo?..Why tulikataa kuchagua Chadema wakati imetoa ahadi zinazowahusu madaktari na wananchi kwa ujumla. Chama kilichoweka wazi mapambano yake kuhusu maadui wetu watatu yaani Ujinga, Umaskini na Maradhi kakam kipaumbele kinachotangulia yote badala yuake wakaitwa wahuni, magaidi na wakristu?.

Ni rahisi sana watu kuwanyooshea kidole wabunge wetu lakini ajabu ni kwamba hawa wabunge wenyewe baadhi yao ni Madaktari! na wanaoitengeneza bajeti ya AFYA ni Madaktari, na kati ya vijana wetu waliosomea Udaktari ni makada wa CCM halafu hawa hawa leo wamekuja tuadhibu wananchi kwa ghiriba walowadanganya wananchi kutowachagua wabunge wenye nia njema na Taifa hili..

Halafu basi, katika mgomo wa kwanza walionishangaza sana pale walipokataa ushirika wa Tucta wala Chadema kwa madai kwamba hili halikuwa swala la SIASA, jamani hivi siasa ni kitu gani?.. Kama unadai mishahara mikubwa, vifaa vya kutendea kazi na mazingira bora ukiyaelekeza kwa serikali itakuwaje isiwe siasa maana haya mambo au madai ndio huzungumzwa bungeni la wala sii mitaani..Nakumbuka vizuri sana jinsi walivyomwacha Mnyika Uchi akaonekana anataka kujipendekeza ktk jambo lisilomhusu japokuwa maswala mengi ni kwa maslahi yao wenyewe.

Haya wakadai siju hawataki kukutana na Waziri mkuu hadi Waziri wa Afya na Naibu wake wafukuzwe kazi? Jamani nikawashauri sana waache mgomo wakutane na Waziri mkuu maana hawa ni wateule wa serikali ile ile mnayoweka madai yenu, jibu lolote mnalopewa linatoka juu. Hawakuchukua ushauri wetu wakaenda hadi Ikulu wakapozwa na juice. Maana kufukuzwa kwa mawaziri hao haitawezesha madai yoyote ya awali isipokuwa serikali itanunua muda maana hawana fedha, bajeti hadi July..Wakasubiri..

Bajeti ilipotoka wakakuta wamepigwa changa la macho tena, I mean guyz hii ndio serikali ilowaahidi wananchi wa Kigoma kujengewa Dubai, kupewa meli mpya za usafiri, Flyover all of Dar, Umeme kutokuwa adha ya kitaifa ifikapo 2008... leo tumefanikisha lipi? Kwa hiyo hasira zao kama hasira za wananchi na raia wengine wote ilikuwa tuziweke ktk ujumla wa utawala uliopo ili tupate mwongozo mpya. hatuwezi kufanikiwa kwa lolote ktk madai haya ikiwa serikali imepoteza dira maana zamani tulisema maadui wetu ni watatu na tukaweka nguvu yote pale.

Kama madaktari hawataweza kusoma alama za nyakati na wakaendelea kumlaumu JK wakati sisi wenyewe tumechagua kuachana na sera zinazoelekeza nguvu ktk kufuta Umaskini, UJinga na Maradhi tukakumbatioa sera zinazokinga mbu wasituume wakati tumelala tukagawiwa vyandarua ili kuponya malaria, sijui huu udaktari tumeusomea wapi kama sio biashara?. Na, I hate to say kila napowasoma madaktari wangu naiona picha ya wafanyabiashara zaidi ya wahudumu - sorry to say that!..maana ni hawa hawa waliokuwepo wizarani, idara na asasi za kiafya kote wamejaa madaktari lakini kila mmoja wao anatafuta ULAJI wake.

Mwisho nitamalizia kwa kusema, ukombozi wa kweli hautaletwa kwa mtu mmoja mmoja wala kitengo kimoja kimoja maaa sisi hatujafika ktk utajiri bado ni maskini ambao kwa pamoja nguvu yetu ndio inaweza kutondoa hapa tulipokwama laa sivyo tutabakia kama Kaa wa bahari waliwekwa ktk kapu wakisubiri mafuta vya moto kukaangwa. Doctors, Walimu, Polisi na watumishi woote wa Umma mnapolalamikia serikali fahamuni mnailalamikia CCM na CCM wanayo haki kabisa ya kusema hili ni swala la kisiasa na pengine Madaktari mnachombezwa na wanansiasa wa vyama vya Upinzani..Kubalini swala hili liende kisiasa, Union zenu zishiriki kikamilifu ktk kuchagua viongozi mnaowataka, viuongozi watakao waonyesheni sera za mabadiliko ktk sekta nzima ya Afya na hata mishahara na posho zenu lakini sii kusema nyie ni wabora kuliko wabunge ilihali hawa wabunge ndio mawaziri wetu mnaowaomba wapitishe ongezeko la mishahara yenu.
 
Well said mkuu Mkandara:
Hivyo ndivyo inavyotakiwa iwe! Ni mpumbavu anayeyapa thamani zaidi maisha yake kuliko ya "majority"
Uzungumziacho mkuu ni "UTU", yaani madaktari wangejali UTU kwanza kabla ya masilahi yao binafsi-ni kweli.
Lakini nani anaishi hivyo kwa sasa? Kwani wao watangulize UTU hali wengine hawana? Labda wangejali, lakini wametengenezwa kutokuja, nani alaumiwe sasa? Wao? Wewe na mimi? Au nani? Kwangu ni mimi na wewe...ndio wakwanza kulaumiwa! Tena hasa nafsi yangu na yako!
Wanachofanya madaktari kwa sasa, ni kupigania kile MUHIMU nacho ni KITU, si UTU! Wametengenezwa kuwa hivyo! Kwa sasa kuonekana una busara ni lazima uwe tajiri, hekima ni utajiri kwa sasa, utu ni ujinga, haki ni johari! Muhimu ni KITU, ndio maana madaktari wanakipigania hicho! KITU na SI UTU! Mimi na wewe ndio tumewatengeneza!
Kwanini tuwapigie kelele wao peke yao hali kuna Mengi amejilimbikizia utajiri unaoweza kununua CT Scan wilaya zote Tanzania? Mnaita utajiri wa halali! Sasa kwanini Dr. kwake isiwe halali?
Mbowe, anajenga club za starehe hali Muhimbili kina watoto wetu wanazaliwa sakafuni, mnaita HAKI, tena ni wakombozi. Kwanini madaktari nao wasiitwe hivyo?
Lowasa na Sumaye, wanaweza kujenga Muhimbili mpya Mtwara au Kigoma, lakini wamezilalia pesa, watu wanakufa mahospitalini eti mwezi huu daktari hana zamu ya huku leo. Kwanini tusiaanze nao hawa? UHALALI GANI MNAOUTETEA!? Wewe sio mzalendo, kwanini unishangae mimi kutokuwa mzalendo?
Wenyewe wanajipandishia mishahara kila leo, wanapeana magari ya kifahari, wanajengeana majumba makubwa ya ajabu ajabu. Kwanini tusianze kukemea hayo mimi na wewe kwa vitendo sio porojo za midomo!
Tulishauzika uzalendo na Zanzibar Resolution, tulishaacha kufuga nyuki huko, tukawageukia manyigu, hata tukiwapondaponda wao wenyewe kwenye kinu hawatotoa asali, zaidi ya sumu! FUGA NYUKI, UKIKOSA ASALI UTAKUWA NA HAKI YA KULAUMU.
Hata hivyo, kila mtu amejaliwa UTU nafsini mwake, kwani mantiki ya UTU i nafsini mwa kila mtu, kutoiishi ni sawa na kujinafiki na kujisaliti. Nawalaumu madaktari kwa kuzisaliti nafsi zao, lakini pia kwetu si raia kwa kutoipigania mantiki hiyo!
Mungu wetu anaita sasa!
 
Well said mkuu Mkandara:
Hivyo ndivyo inavyotakiwa iwe! Ni mpumbavu anayeyapa thamani zaidi maisha yake kuliko ya "majority"
Uzungumziacho mkuu ni "UTU", yaani madaktari wangejali UTU kwanza kabla ya masilahi yao binafsi-ni kweli.
Lakini nani anaishi hivyo kwa sasa? Kwani wao watangulize UTU hali wengine hawana? Labda wangejali, lakini wametengenezwa kutokuja, nani alaumiwe sasa? Wao? Wewe na mimi? Au nani? Kwangu ni mimi na wewe...ndio wakwanza kulaumiwa! Tena hasa nafsi yangu na yako!
Wanachofanya madaktari kwa sasa, ni kupigania kile MUHIMU nacho ni KITU, si UTU! Wametengenezwa kuwa hivyo! Kwa sasa kuonekana una busara ni lazima uwe tajiri, hekima ni utajiri kwa sasa, utu ni ujinga, haki ni johari! Muhimu ni KITU, ndio maana madaktari wanakipigania hicho! KITU na SI UTU! Mimi na wewe ndio tumewatengeneza!
Kwanini tuwapigie kelele wao peke yao hali kuna Mengi amejilimbikizia utajiri unaoweza kununua CT Scan wilaya zote Tanzania? Mnaita utajiri wa halali! Sasa kwanini Dr. kwake isiwe halali?
Mbowe, anajenga club za starehe hali Muhimbili kina watoto wetu wanazaliwa sakafuni, mnaita HAKI, tena ni wakombozi. Kwanini madaktari nao wasiitwe hivyo?
Lowasa na Sumaye, wanaweza kujenga Muhimbili mpya Mtwara au Kigoma, lakini wamezilalia pesa, watu wanakufa mahospitalini eti mwezi huu daktari hana zamu ya huku leo. Kwanini tusiaanze nao hawa? UHALALI GANI MNAOUTETEA!? Wewe sio mzalendo, kwanini unishangae mimi kutokuwa mzalendo?
Wenyewe wanajipandishia mishahara kila leo, wanapeana magari ya kifahari, wanajengeana majumba makubwa ya ajabu ajabu. Kwanini tusianze kukemea hayo mimi na wewe kwa vitendo sio porojo za midomo!
Tulishauzika uzalendo na Zanzibar Resolution, tulishaacha kufuga nyuki huko, tukawageukia manyigu, hata tukiwapondaponda wao wenyewe kwenye kinu hawatotoa asali, zaidi ya sumu! FUGA NYUKI, UKIKOSA ASALI UTAKUWA NA HAKI YA KULAUMU.
Hata hivyo, kila mtu amejaliwa UTU nafsini mwake, kwani mantiki ya UTU i nafsini mwa kila mtu, kutoiishi ni sawa na kujinafiki na kujisaliti. Nawalaumu madaktari kwa kuzisaliti nafsi zao, lakini pia kwetu si raia kwa kutoipigania mantiki hiyo!
Mungu wetu anaita sasa!
Maneno mazito sana haya mkuu wangu na hasa kipande hiki kimeniacha hoi bin taaban - Kwa sasa kuonekana una busara ni lazima uwe tajiri, hekima ni utajiri kwa sasa, utu ni ujinga, haki ni johari! Muhimu ni KITU, ndio maana madaktari wanakipigania hicho! KITU na SI UTU! Mimi na wewe ndio tumewatengeneza!

 
Sasa tunaanza kuona flexibility na dalili za kubadili sera za US huko Egypt na Mashariki ya kati.Tayari Waziri wa Mambo ya Nje amefanya ziara ya haraka kuonana na Morsi.Upande Mwingine Israel imechukizwa sana na kitendo hicho na Hilary Clinton ameelekea tel Aviv.Kwa wale wanaofutalia evolution ya US Foreign Policy kunazia Utawala wa Rais wa pili kuhusu engagement and disengagement wanaelewa kinachoendelea
 
Wakuu Mkandara na JingalaFalsafa,
Kwanza nikubaliane nanyi kuwa hakuna kazi muhimu kuliko nyingine, lakini nitofautiane nanyi kuwa kuna kazi ambazo ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku.

Mimi binafsi sipendezwi na mgomo wa madaktari kwasababu ya athari zake kwa maisha ya kila mmoja wetu.
Sikubaliani kuwa kazi ya Ualimu au Udaktari ni za wito na zinapaswa kufanywa na wazalendo.
Kazi ya ulinzi wa nchi ndani na nje ni ya uzalendo kama ilivyo ya mhasaibu , Injia na bwana shamba nk!
Linapofika suala la masilahi hapa uzalendo wa Madaktari unatakiwa zaidi kuliko tena kwa kauli mbiu ya wito!!

Tuanchokiona sasa hivi ni kitu kinaitwa 'classwarfare' mvutano wa madaraja nchini.
Tumeona Wabunge wakidai posho za laki mbili kwa kwenda kazini na kukaa katika sehemu za kazi zao hata kama wanabaki kucheka siku nzima.

Mbunge ndiye mtu aliyechaguliwa hasa kwa uzalendo wake, hakuchukua mkopo popote wala hahitaji qualification yoyote.
Kazi yake haina sheria wala ethics ukiachilia zile za ndani ya bunge tu au risk zitokanazo ukiacha za siasa chafu . Huyu ndiye role model wa Uzalendo kama tutataka iwe hivyo.Tuache hilo kwanza

Tumefikaje katika 'classwarfare'?
Hakuna aliyeshtuka marupu rupu ya Nyerere alipokuwa kazini hata alipostaafu.
Nakumbuka ilifika mahali watu wakahoji hivi Rais Mwinyi alijengaje nyumba ya ghorofa! licha ya ukweli kuwa alikuwa madarakani miaka 10.

Rais Mkapa kwa ushirika na Sumaye walipeleka mswada wa masilahi yao licha ya ukweli kuwa kazi zao tu ziliwahahkikishia maisha mazuri. Mswada ulipokwama wakatoa hongo za kuongeza posho za wabunge.

Baada ya hapo kila kundi kuanzia wabunge, makatibu wakuu, wakurugenzi likaanza kupigania masilahi yake.
Tumeshuhudia mgomo wa Walimu nk. Yote haya yalikuwa si kwa uzalendo bali kulinda masilahi yao kile kitu ' KITU' na si 'UTU' kama alivyonena JingalaFalsafa.

Ni hiyo classwarfare ya akina Mkapa na Sumaye sasa imeshika moto hadi madiwani wanadai magari n.k.
Sasa ni zamu ya Madaktari, la haula!! nchi nzima inalilia uzalendo na kuwalaani kwa kujiona ni bora! mbona haya yameanza siku nyingi na uzalendo haukusemwa! kwanini madaktari kama kundi jamii wao wasiwe na haki ya kugombea mkate wao ikiwa Mkapa, Sumaye, Wabunge n.k waliweka uzalendo pembeni? Why Madaktari

Tukitumia theory ya elimination, basi tufikirie kuwa madaktari wana makosa na hilo tuliondoe katika madai yao.
Linabaki suala la vitendea kazi na hali za sekta nzima ya afya.

Hivi unamfikiriaje Daktari anayefanya operesheni bila gloves na kisha mgonjwa wa operesheni alazwe kitanda kimoja na mgojwa wa majeraha ya ajali! Hapo kuna medicine kweli! kuna tofauti gani kati ya Daktari na ngariba anayetumia wembe mmoja kutahiri vijana kumi na saba!
Je,huyo mgonjwa ametendewa haki kwa kupelekwa kaburini kwasababu ya 'infection' aliyopita kupitia majeraha ya mtu mwingine.

Hivi Daktari anapomwacha mgonjwa theatre ili akimbie famasi kununu kifaa cha sh 1500 kuna heri gani kwake na kwa mgonjwa?

Hayo yakitokea Bunge limekaa kimya na kuzuia mijadala. Bunge halijadili vifaa vya hospitali bali magari gani watumie wao na wenzao wa serikali. Hapa uzalendo upo wapi ambao madaktari wameukosa? Kwa mlango wa nyuma Rais JK alisaini ongezeko la marupu rupu kwa kificho! why kificho! anaogopa nini kama wao ni sehemu muhimu ya jamii kama wengine

Katika classwarfare hiyo wao wamejiwekea utaratibu wa kucheki afya Appolo India, wakiwa na uhakika wa wake zao kutopanga foleni ya kujifungua.

Nikifika hapo nahitimisha kuwa tunachokiona kwa madaktari ni 'classwarfare' iliyoanzishwa siku nyingi, kwa vile haina impact ya ghafla katika maisha yetu hiyo tunaiona kawaida. Hii ya madaktari inaonekana ni ukosefu wa uzalendo na kujali kitu badala ya utu kwa vile inatugusa moja kwa moja.

Hatupaswi kuwalaumu madaktari kwa kuendeleza utaratibu uliopo, tunatakiwa tuelezane na kuwaeleza watu wetu kuwa anayewaumiza ni serikali ambaye ni mtoto wa mzee Bunge. Hasira zetu tuzielekeze huko kwanza.

Wenzetu duniani kwingine bei ya mkate ikipanda hawamshambulii muuzaji au mchuuzi wanashambulia wale waliowatuma na wale walioajiriwa kulinda masilahi ya wananchi. Imetokea Poland, India, Georgia, Columbia n.k. Inashindikanaje hapa kwetu?
 
Ritz,
Nasser alikuwa na mtazamo mpana sana. Yeye ni mmoja wa waanzilishi wa NAM ambayo magwiji walikuwa akina Jose Bros Tito, Nyerere, Nkrumah, KK n.k.

Siasa za Nasser zilitawala sana Arab world. Yeye aliunda kitu kinaitwa Pan-Arab na wafuasi wa siasa zake walijulikana kama Nasserist na siasa zake Nasserism. Alisaidia sana Uhuru wa Ageria, na Yemen na hakika aliiachia Cairo iwe kituo cha harakati kwa Wayemen dhidi ya Saudia.

Vita aliyoshindwa na Israel ya siku sita na hata alipojaribu tena haikuwa baina yake na Israel tu bali France na Uingereza kwa kile kinalichojulikana kama Suez Canal crisis. Ni wakati wa Nasser ndipo Suez Canal ilikuwa na Wabia kitendo kilichowaudhi sana Waingereza na nchi za Magharibi.

Lengo lake kubwa lilikuwa kuwakomboa Wamisri. Ukiangalia vema Tahariri square haikuanza leo ilianza wakati wa mwingereza na hasa alipoua askari wa Misiri kule Ismailia.

Kilichomsadia sana kuielewa Misir ni jinsi alivyokuwa anahama shule na kusafiri sana. Nasser ni mwanajeshi hata hivyo na hili libeneke la akina Tantawi ni sehemu tu ya mazoea kuwa jeshi ni chombo cha kipekee nchini Misri na kwamba dollar billion kadhaa kutoka magharibi wao ndio wanastahiki.

Ben, Kama umesoma vema awali niliwahi kusema haya mabadiliko hakika USA haikuyapenda. USA ilitaka mambo yaende taratibu ili kumpata mrithi wa Mubarak. CIA ilikuwa na taarifa za hali tete ya Mubarak na walikuwa katika process za kutafuta mrithi. Bahati nzuri au mbaya gharika ikatimia.

Wanachokifanya sasa ni ku-buy the time. Kwao wanaona ni vema waka engage kuliko kuleta confrontation. Tatizo ni kuwa wao si ma-champion wa demokrasi!! sasa uchaguzi wa Misri wata ukataaje na ili hali ulikuwa halali.
Matarajio yao ya kwanza ilikuwa Al Baradei na wa pili Amour Mousa wa Arab League.
Ni wao walifanya njama za kumwengua mgombea wa Brotherhood kwa kutoa siri za uraia wa wazazi wake.

Kama wao walivyokuwa na plan A na B ndivyo ilivyokuwa kwa brotherhood pia na sasa plan B ya Morsi imefanya kazi.
Israel haitafurahia na inataka kuwapeleka puta Marekani kwa hofu tu ya Brotherhood. Lakini wana genuine concern kwasababu brotherhood is unpredictable political movement.

Hali ya Misri bado ni tete na hili ni homa kwa nchi za magharibi hasa Marekani.
 
Mkuu Nguruvi:
Nadhani hatujatofautiana.
Raia kupitia siasa zao husimika viongozi wao madarakani, lengo WARATIBU MAENDELEO/USTAWI WAO KWA UJUMLA, hiyo ndio kazi pekee ya kiongozi. Uratibu huo ni katika nyanja zote, ikiwemo ya AFYA na ELIMU. Raia kupitia serikali yao wanatakiwa kuhakikisha ufanisi mahospitalini na mashuleni mwetu, kwani uozo wowote humo wao raia ndio wahanga wakubwa!
Tujiulize, mara ngapi tunalala sakafuni mahospitalini mwetu, shule ngapi hazina maktaba wala walimu, hospitali ngapi hazina madawa wala wahudumu? Vijiji vingapi havina hospitali? Acha barabara, umeme na maji. Kwanini ifikie hatua ya watumishi wetu kuigomea serikali(kama wametugomea sisi vile)? Sisi raia tupo wapi? Kwanini raia wasiwe wa kwanza kuishinikiza serikali yao kuwatengenezea walimu na madaktari mazingira sahihi ya kazi? Kwanza nguvu yetu ni kubwa kuliko ya madaktari na walimu, pili tungeepusha makovu mengi kutokana migomo yao!
Swali muhimu ni kwanini raia hawaichezi nafasi yao katika kulinda ustawi wao? "Mental Enslavement" Tumewatengeneza viongozi wetu kuwaona kama miungu watu...tunawaogopa. Pia tumetengenezwa kujiona duni, si chochote katika chochote! Tupo tupo tu! Bora liende! Ni MITEGO, na tumeshanaswa! Huna KITU, huna CHOCHOTE-kaa chini wenye KITU waongee! (mama yangu anayeshindwa kuninulia japo bukta ya kuficha utupu wangu, atamkemea vipi kiongozi wake aliyekuja na shangingi, jeuri ni pesa, hana-kaa chini) Na hiyo ndio Demokrasia katika falsafa na misingi yake mikuu kabisa!
Tunapaswa kujilaumu wenyewe kukubali kulaghaiwa kufuga manyigu hali tunachotaka asali. Haukuna world realistic duniani zaidi ya UTU, vingene vyote ni vya kugushi. Mbaya zaidi bado tu tunaendelea kumezeshana dozi za usingizi kila leo!
Tulishazikwa hai, tusiache watoto wetu nao kuzikwa hai. Hizi HESABU, kuzipangua ni lazima nasi tutumie HESABU YA JUU KABISA.
UBUNIFU HAUJAWAI KUFIKA MWISHO. TUNAWEZA. Nguvu yetu ni UMOJA na KUTHUBUTU.
Mungu wetu anaita!
 
Wakuu Mkandara na JingalaFalsafa,
Kwanza nikubaliane nanyi kuwa hakuna kazi muhimu kuliko nyingine, lakini nitofautiane nanyi kuwa kuna kazi ambazo ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku.

Mimi binafsi sipendezwi na mgomo wa madaktari kwasababu ya athari zake kwa maisha ya kila mmoja wetu.
Sikubaliani kuwa kazi ya Ualimu au Udaktari ni za wito na zinapaswa kufanywa na wazalendo.
Kazi ya ulinzi wa nchi ndani na nje ni ya uzalendo kama ilivyo ya mhasaibu , Injia na bwana shamba nk!
Linapofika suala la masilahi hapa uzalendo wa Madaktari unatakiwa zaidi kuliko tena kwa kauli mbiu ya wito!!

Tuanchokiona sasa hivi ni kitu kinaitwa 'classwarfare' mvutano wa madaraja nchini.
Tumeona Wabunge wakidai posho za laki mbili kwa kwenda kazini na kukaa katika sehemu za kazi zao hata kama wanabaki kucheka siku nzima.

Mbunge ndiye mtu aliyechaguliwa hasa kwa uzalendo wake, hakuchukua mkopo popote wala hahitaji qualification yoyote.
Kazi yake haina sheria wala ethics ukiachilia zile za ndani ya bunge tu au risk zitokanazo ukiacha za siasa chafu . Huyu ndiye role model wa Uzalendo kama tutataka iwe hivyo.Tuache hilo kwanza

Tumefikaje katika 'classwarfare'?
Hakuna aliyeshtuka marupu rupu ya Nyerere alipokuwa kazini hata alipostaafu.
Nakumbuka ilifika mahali watu wakahoji hivi Rais Mwinyi alijengaje nyumba ya ghorofa! licha ya ukweli kuwa alikuwa madarakani miaka 10.

Rais Mkapa kwa ushirika na Sumaye walipeleka mswada wa masilahi yao licha ya ukweli kuwa kazi zao tu ziliwahahkikishia maisha mazuri. Mswada ulipokwama wakatoa hongo za kuongeza posho za wabunge.

Baada ya hapo kila kundi kuanzia wabunge, makatibu wakuu, wakurugenzi likaanza kupigania masilahi yake.
Tumeshuhudia mgomo wa Walimu nk. Yote haya yalikuwa si kwa uzalendo bali kulinda masilahi yao kile kitu ' KITU' na si 'UTU' kama alivyonena JingalaFalsafa.

Ni hiyo classwarfare ya akina Mkapa na Sumaye sasa imeshika moto hadi madiwani wanadai magari n.k.
Sasa ni zamu ya Madaktari, la haula!! nchi nzima inalilia uzalendo na kuwalaani kwa kujiona ni bora! mbona haya yameanza siku nyingi na uzalendo haukusemwa! kwanini madaktari kama kundi jamii wao wasiwe na haki ya kugombea mkate wao ikiwa Mkapa, Sumaye, Wabunge n.k waliweka uzalendo pembeni? Why Madaktari

Tukitumia theory ya elimination, basi tufikirie kuwa madaktari wana makosa na hilo tuliondoe katika madai yao.
Linabaki suala la vitendea kazi na hali za sekta nzima ya afya.

Hivi unamfikiriaje Daktari anayefanya operesheni bila gloves na kisha mgonjwa wa operesheni alazwe kitanda kimoja na mgojwa wa majeraha ya ajali! Hapo kuna medicine kweli! kuna tofauti gani kati ya Daktari na ngariba anayetumia wembe mmoja kutahiri vijana kumi na saba!
Je,huyo mgonjwa ametendewa haki kwa kupelekwa kaburini kwasababu ya 'infection' aliyopita kupitia majeraha ya mtu mwingine.

Hivi Daktari anapomwacha mgonjwa theatre ili akimbie famasi kununu kifaa cha sh 1500 kuna heri gani kwake na kwa mgonjwa?

Hayo yakitokea Bunge limekaa kimya na kuzuia mijadala. Bunge halijadili vifaa vya hospitali bali magari gani watumie wao na wenzao wa serikali. Hapa uzalendo upo wapi ambao madaktari wameukosa? Kwa mlango wa nyuma Rais JK alisaini ongezeko la marupu rupu kwa kificho! why kificho! anaogopa nini kama wao ni sehemu muhimu ya jamii kama wengine

Katika classwarfare hiyo wao wamejiwekea utaratibu wa kucheki afya Appolo India, wakiwa na uhakika wa wake zao kutopanga foleni ya kujifungua.

Nikifika hapo nahitimisha kuwa tunachokiona kwa madaktari ni 'classwarfare' iliyoanzishwa siku nyingi, kwa vile haina impact ya ghafla katika maisha yetu hiyo tunaiona kawaida. Hii ya madaktari inaonekana ni ukosefu wa uzalendo na kujali kitu badala ya utu kwa vile inatugusa moja kwa moja.

Hatupaswi kuwalaumu madaktari kwa kuendeleza utaratibu uliopo, tunatakiwa tuelezane na kuwaeleza watu wetu kuwa anayewaumiza ni serikali ambaye ni mtoto wa mzee Bunge. Hasira zetu tuzielekeze huko kwanza.

Wenzetu duniani kwingine bei ya mkate ikipanda hawamshambulii muuzaji au mchuuzi wanashambulia wale waliowatuma na wale walioajiriwa kulinda masilahi ya wananchi. Imetokea Poland, India, Georgia, Columbia n.k. Inashindikanaje hapa kwetu?
Mkuu wangu pengine tukubaliane kutokubaliana ktk hili la UZALENDO, lakini Kazi ya Udaktari inatakiwa Uzalendo mkubwa pengine kuliko kazi zote ulizozitaja hapo na inaweza tu kulinganishwa na kazi nyingine zenye kiapo kama hicho iwe Bungeni, Urais, Hakimu, Mwanajeshi vitani, wana Usalama wa Taifa na kadhalika maana ndio tunawakabidhi maisha yetu. Na hawa ndio watu tunaowalalamikia hapa JF muda wote kwa kupoteza Uzalendo iweje iwe nafuu kwa Daktari.

Hivi leo tunamlalamikia JK kwa sababu gani? sii kwa sababu tunampa mshahara mkubwa, Tunawalalamikia Wabunge wetu kwa sababu gani? sidhani ni kwa sababu tunategemea wafanye vizuri kutokana na mishahara na posho tunazowapa. Isipokuwa Uzalendo wao walioapa kulitumikia Taifa na hata wanapofikia wao kudai mishahara mikubwa zaidi lazima bado iendane na kiapo chao..

Kitu kimoja ambacho mimi napenda kusema hapa ni kwamba sisi tuliunda mfumo wetu wa AFYA na ELIMU kwa sababu maalum ya kupambana na maadui wetu hawa. Na gharama yake tumeilipia wananchi wote kuwasomesha hawa madaktari bure ili tuweze kupunguza vifo na maradhi nchini. Sasa wanapokuja na madai sawa na nchi za Kibepari, nchi ambazo mtoto aliyefikia Udaktari amelipa zaidi ya dollar laki 2, leo umpe mshahara mdogo kama wetu wakati mfumo mzima wa Hospital zao ni biashara zinazoendeshwa kwa faida hawezi kukubali wala haiwezekani. Hapa ndipo madaktari wetu wameshindwa kutofautisha kati ya Daktari aliyeko Tanzania na yule wa Botswana au Namibia na kwa nini tuna tofauti kubwa.

Hawa wenzetu walisoma kwa fedha zao toka mfukoni au walikopeshwa na ndio maana wana upungufu mkubwa wa madaktari tofauti na sisi, na pia ndio maana wanalipwa mishahara mikubwa sana kutokana na gharama walizoingia wao na pia AFYA kwao ni biashara, hivyo Hospital can pay big salary maana wanatoza kulingana na gharama za tiba, vifaa na mishahara ya Daktari na kubakia na faida kubwa. Sisi kifupi tuliandaa vijana wetu kufanyakazi ya kanisa isipokuwa ujio wa Azimio la Zanzibar ndipo kila kitu kikabadilika..

Wabunge wakaanza kudai mishahara mikubwa, tukalalamika, Rais, mawaziri, Manaibu, Makatibu wakuu wote wakataka mishahara mikubwa kwa sababu hakuna tena kazi ya kanisa. Wizara za AFYA na ELIMU zikakabidhiwa wadau wapya wenye mtazamo huo huo wa kibiashara zaidi na sii huduma bure kwa wananchi walio jitolea kodi na nguvu zao kwa miaka. Hii ndio sababu na sii kwamba nawapinga madaktari isipokuwa mfumo uliopo ndio sababu ya ushawishi kwa madaktari na ilijitokeza wazi kabisa kuwa mishahara na posho kubwa za wabunge ndizo sababu kubwa za madai ya madaktari na kupima kujiona wao muhimu kuliko Wabunge..

Leo viapo vyao vyote hawa vimekuwa void kiaina, ndio Watawala tulokuwa nao leo hii ambao mimi nawapinga muda wote wa mijadala ktk hoja zangu. Sasa leo wanapokuja madaktari kwa haki ile ile ya viongozi hawa waliokiuka viapo vyao na kuanzisha utawala mpya unaojali fedha kwa huduma halafu mimi nigeuke na kuwaunga madaktari kwa makosa yale yale nayowalalamikia viongozi wangu kila siku hapa JF? hapana nitakuwa na sura mbili kuchagua upande badala ya idea nzima ya kupoteza Uzalendo.

Kwa hiyo hoja yangu bado ipo palepale, Uzalendo kwa viongozi na wananchi umepotea na hili linatugharimu sana iwe kwa Viongozi, Madaktari, walimu na hata mitaani kwa sababu hatukuwandaa watu ktk misingi ya kibiashara. Kutoka Ujamaa kuingia Ubepari ni sawa na mtu alokwenda kubadilisha dini kutoka Uislaam kuingia Ukristu au kinyume lazima atakuwa na tafsiri mbovu za faradhi na sunna za imani aloingia. Kwa hiyo nitaendelea kupinga mfumo huu wa Afya nchini na pengine nitasema Madaktari ni victims wa mfumo huu uloanzishwa na Mwinyi na Lowassa in 1992 and we are paying for that.
 
Back
Top Bottom