Duru za siasa - Mgongano wa mawazo

Ni kweli kabisa naunga mkono wazo lako.

Poa kinachonitatiza na JF siku hizi ni kwamba inakuwa vigumu sana kumfuatilia mtu pengine tuanzishe mpango wa ku Tag mtu mjadala inapopaswa. Mada ni nyingi sana huwezi kusoma zote hadi unategea kuona wakali wako wamechangia wapi zaidi ndio unajiunga. Kuna watu natafuta michango yao huwa siwapati japokuwa huwaona wame log in..
 
Poa kinachonitatiza na JF siku hizi ni kwamba inakuwa vigumu sana kumfuatilia mtu pengine tuanzishe mpango wa ku Tag mtu mjadala inapopaswa. Mada ni nyingi sana huwezi kusoma zote hadi unategea kuona wakali wako wamechangia wapi zaidi ndio unajiunga. Kuna watu natafuta michango yao huwa siwapati japokuwa huwaona wame log in..
Absolutely! Na nadhani JF wameona hili jambo ndipo wakaweka Tag.
Hii ya ku-tag inafanya kazi kwa namna fulani.

Tatizo la wingi wa mada inachangiwa pia na matumizi mabaya ya majukwaa. Mtu anaweka mada, Siasa: Nasikia kuna mkutano wa chama X, mwenye habari atujuze. Labda angeweka kwenye tetesi wasomaji wangeelewa ni tetesi na uzito wake unakuwa kama ulivyo. Ningeomba sana wakuu wa JF waliangalie hili.

Tatizo jingine ni kujirudia rudia kwa mada, mfano: Siasa; Hatutaki muungano halafu siasa: Muungano kwishnei na siku hiyo hiyo siasa; muungano wa nini? Sasa ukichunguza si mada bali ni baadhi tu wanapoza machungu kwa mistari miwili

Mahali ninapoweza kusema japo mada zinaweza kufuatiliwa ni MMU. Unaweza kukuta mada inakaa wiki 2 au 3.
Kuna mada nyingi sana zinapelekwa MMU lakini wana utaratibu usio rasimi wao wanasema 'potezea' kwaniyo mada hafifu zinakufa within hours. Jukwaa la siasa wanaendekeza mada hafifu na hilo ni chanzo cha kupoteza mada nzito.
 
Duru za siasa
Tukianza na CCM tumeiona ikiyumba ama kuelekea kukosa ubunifu tumeona mkutano wake wa hivi karibuni kwenye viwanja vya Jangwani umeacha somo kwa wale wapendao kujifunza.

Kuna CCM tatu ndani ya chama kimoja, CCM inapaswa kurudisha uhai wa chama ili watu waione CCM iliyo hai na pia waone faida ya CCM kwenye maisha yao, watu wanataka wasikie CCM inasema nini badala ya watu wanasema nini, kwenye mkutano wa pale Jangwani CCM haikuwa moja na pia CCM haikusema chochote badala yake watu binafsi ndio waliosema kwa kutumia nyadhifa zao na na nafasi zao.

Ninapozungumzia kauli ya cha nina maana pana, kwanza kuna mengi ambayo CCM inapaswa kuyatolea kauli ama kuyatolea ufafanuzi ili watu wasikie chama kimesema nini. Kitendo cha kuwaalika Wawaziri ili waje wawaeleze Wananchi mazuri yanayofanywa na Serikali ya CCM ni kujikanyaga, chama ndicho kinapaswa kuitetea serikali na sio serikali kujitetea mbele ya Wananchi ili kukisafisha ama kukinufaisha chama tawala.

Mawaziri wanalo jukwaa lao ambalo wananchi huwasubiri na kuwasikiliza ni bungeni wakati wa kuwasilisha makadirio ya matumizi ya wizara zao.Tutaendelea na Duru za siasa.
Ritz, Suala la kuyumba kwa CCM ni dhairi kabisa.
Ona jinsi ambavyo Nape alivyosusiwa kampeni. Amebaki anazunguka mikoani kueneza uhai wa chama peke yake.
Wakati anafanya hayo wazee wa chama akina Makamba wanasubiri kumsulubu katika vikao kama kilichokwisha cha NEC

Uenezi wa chama siyo one man show ni kazi ya pamoja (team work). Katika kufanya hivyo Nape anakosa timu ya mkakati na matokeo yake ni ima kutoa matusi au kujibu tuhuma na wala si kueleza sera za chama.

Chama tawala sasa hakiongozi bali kinaongozwa kwasababu CDM wakitoa hoja CCM haielezi kwa ufaha hoja husika bali kujibu hoja. CCM imebaki na sera za kueneza udini na ukabila na wala siyo zile sera za chama au ilani ya uchaguzi

Kuna kundi linalosubiri chama kidhoofike ili litumie mbinu zao kukirudishia uhai. Hili ndilo lililowatuma wazee wamkaange Nape kuwa anaua chama na Mkama si kiongozi mzuri. Kundi hili linaloundwa na mafisadi linasubiri wakati muafaka na nakuhakikishia kuanzia mwakani utaliona likiibuka kwa kasi. Sasa hivi linafanya kazi ya kuhamasisha na kuchochea chuki
dhidi ya wenzao ndani ya chama linatafuta kuungwa mkono na hasa taasisi za kidini.

Wale uliowaona Jangwani si kwamba walikuwa wanaeneza chama, ni kundi la pili linalojitutumua kukipa uhai chama kwa kutambua kuwa Watanzania wengi wamechoshwa na ulaghai na kwamba kwa kujipambanua kuwa linapigania haki za wanyonge katika misingi ya chama lina nafasi ya kutoa mgombea.

Kwa vile lengo ni mgombea ndiyo maana hakuna aliyekuwa 'anahubiri' sera za chama bali kila mmoja anajitafutia ka nafasi.
Na wala kundi hili haliwezi kuitetea serikali kwakuwa serikali yenyewe ni mzigo tosha na kujinasibisha nayo ni kujipalia makaa.

Pia tuelewe kuwa hakuna kundi linaloweza kukitetea chama kwasababu chama kimekosa uongozi.
Hivi fisadi anawezaje kusimama na kukitetea chama au serikali kwa hasira zilizopo za wananchi?
Hivi wapambanaji wa ufisadi wanawezaje kukitetea chama au serikali ili hali wameshindwa kuwatia nidhamu mafisadi?

Mfano mzuri wa jinsi wanachama wasivyoweza kukitetea chama, ni wa waziri mwanadamizi Membe anayenyemelea nafasi ya kuongoza nchi. Membe anajinasibu kuwa mtetezi wa rasilimali za nchi kama tulivyoona akishupalia suala la Rada.
Ni membe huyo huyo hawezi kutaja hata mhusika mmoja na kila akiulizwa anasema yeye hahusiki.
Sasa kama yeye hahusiki kujua nani mwizi anawezaje kuitetea serikali yake yenye mkono ndani ya kashafa ya Rada?

Hivi Membe anawezaje kusimama na kutetea sera za chama za kupinga ubadhirifu na ufisadi tukijua kuwa hawezi kumtaja achilia mbali kuchukua hatua dhidi ya wahusika!
Hapa ni wazi Membe amepoteza 'moral authority' ya kutetea serikali yake au kukemea ufisadi.
Sasa katika mkanganyiko wa wanamna hiyo Membe anawezaje kusimama na kurudisha uhai wa chama.

Kwa ufupi ni kuwa CCM imetekwa nyara na wahuni wachache na uongozi uliopo una ombwe kubwa la kiuongozi, ni uongozi dhaifu ambao sidhani kama unaweza kurudisha uhai wa chama tena.
Vyovyote vile wavyo muda wa CCM kutawala iwe bungeni au serikalini hauna ashirio la mwisho mzuri.
 
HOJA YA MUUNGANO: ZANZIBAR INACHEZA KARATA MBOVU

Katika mabadiko # 98 na 99 tumeongelea vugu vugu linaloendelea la muungano. Tulisema nia kubwa ya Zanzibar si kuvunja muungano kama wanavyotaka baadhi yao iwe. Wao wanataka kuwepo na serikali 3, mkataba au uhusiano maalum.Kwa hakika wameshindwa kuwashawishi Watanzania bara kwanini tuwe na vitu hivyo kama tulivyoeleza huko myuma.

Katika siku za karibuni kumebuniwa mbinu mpya ambayo haina tofauti na zilizopita.
Lakini Kwanza, vikao vya BLW na Bunge vinaendelea na tunaona cheche hasa BLW.
Hadi sasa ni mwakilishi mmoja au wawili walisema hawataki muungano hadharani.
Kikubwa tunachosubiri ni kusikia wabunge kutoka Zanzibar wakiukataa muungano.

Hilo halitatokea kwasababu Zanzibar inautaka muungano kuliko inavyodhaniwa. Wao wanataka nchi yao na baadhi ya huduma, gharama na shughuli za kijamii zihudumiwe na Tanganyika. Ni kwa mantiki hiyo baada ya kuambiwa LET ZNZ GO! Joto la kisiasa linashuka na wametambua kuwa ni kweli LET ZNZ GO!

Turudi kwenye hoja yao mpya ambayo ni kutaka Serikali ya Tanganyika irudi kwanza ili Zanzibar ikae na Tanganyika kama washirika wa muungano.

Wanachotaka ni mambo yale matatu kwa maana kuwa uwepo wa Tanganyika na Zanzibar kama nchi mbili utazaa serikali ya muungano. Hapa tayari ni serikali 3 kama wanavyotaka kila mara. Mambo yatakyokuwemo katika serikali ya shirikisho ndio mkataba wanaoutaka, na uwepo wa mkataba ndio ushirikiano maalumu wanaousema.
Kurudi kwa Tanganyika kwao ni sawa na hoja ya serikali 3.

Wasichoelewa Wazanzibar ni kuwa uwepo wa Tanganyika ndio kifo cha muungano na hata kile wanachodhani watakipata hawatakipata! Ni kwa vipi?

Tanganyika itakuwa serikali huru yenye mamlaka yake kama ilivyo Zanzibar. Itakuwa na mihimili ya dola kamili. Zaidi ya hapo itakuwa na Vyombo vya usalama na ulinzi na hakika kiuchumi na kijamii itakuwa mbali sana ya Zanzibar.
Kwahiyo serikali ya Tanganyika haitaihitaji ZNZ na itakuwa kinyume chake.

Serikali ya muungano haitakuwa na nguvu ndiyo maana nasema utakuwa mwisho wa muungano.
Haitakuwa na nguvu kwasababu serikali ya Tanganyika itadai ushiriki sawa na mbia mwenza Zanzibar.
Mathalani ikiamuliwa kuwa Jeshi liwe la pamoja kama sehemu ya muungano, Tanganyika itauliza Mchango wa Zbar ni nini katika kuliendesha hilo jeshi? na kukosekana kwa wazanzibar katika jeshi kutaathiri vipi jeshi la Tanganyika?
Mchango wa ZNZ ni nini katika kuhudumia serikali ya muungano kama mbia?

Kwa maneno mengine kwa vile Tanganyika itakuwa nchi huru kama Zanzibar na zimeungana kila moja itataka kulinda masilahi ya wananchi wake na haitakubali kuhudumia serikali nyingine bila sababu.
Hoja hapa ni kuwa hakuna mdogo wala mkubwa,sasa kuleana kutaanzia wapi?

Zanzibar ikitaka mkataba, serikali 3 au mahusiano Tanganyika itatanguliza mwaswali yafuatayo;
1. Kwanini tunaihitaji kuwa na mahusiano ya aina yoyote na Zanzibar?
2. Tunafaidika na nini katika mahusiano hayo
3. Nini mchango wa Zanzibar katika mahusiano
4. Tanganyika itaathirika nini bila uwepo wa Zanzibar au mahusiano

Hadi hapo hakuna muungano kwasababu Tanganyika haitakuwa tayari kuumia kwasababu ya mbia mwenza.
Ikitokea Zanzibar na Tanganyika zikaamua kuwa na mahusiano mengine nje ya serikali 3, hicho kitakuwa kitanzi kwa Wazanzibar. Mathalani, wakiamua kuweka mkataba wa ajira, Tanganyika itadai haki ya ajira ZNZ kama ZNZ inavyofanya.
Zanzibar ikiweka sheria za ardhi, Tanganyika itakuwa na haki ya kuweka zake n.k.

Huko nyuma ZNZ walikuwa na sheria za Mtangayika kwenda na Passport. Tanganyika ilipodai nao waje na passport ilichukua wiki mbili ZNZ wakafuta passport na ikawa ndio mwisho na wala hilo hulisikii tena. Wamedai bendera, wimbo n.j lakini husikii wakidai passport, bado wanatumia ya kijani kwasababu kinyume chake ni maumivu makali.
Huu ndio mfano mzuri wa kuashiria nini kitatokea. Itakuwa ni nipe nikupe na siyo nikupe.

Kwa mantiki hiyo uwepo wa Tanganyika utafuta matumaini ya serikali 3, mkataba, au mahusiano maalumu kwasababu moja muhimu, Tanganyika itakuwa na dola isiyoyohitaji Zanzibar na kila hoja itakapokuja itakumbuna na swali moja'
'' Ili iweje na iwe nini na kwa faida gani''

Hapa ndipo nasema ZNZ iendelee na harakati za kujitoa katika muungano ambazo zinaungwa mkono na Watanganyika.
Kinyume chake mbinu zinazofikiriwa zitaiwezesha Zanzibar kunufaika kama ilivyo sasa hazifai na hazitakubalika.

Vurugu za Zanzibar zimewafungua macho sana Watanganyika na kuona jinsi gani ukarimu na fadhila zao kwa ndugu zao unavyokuwa shuburi.

Ni kwa muktadha huo, serikali 3, mahusiano, mkataba au kurudi kwanza kwa Tanganyika hakutaisadia ZNZ kwa namna yoyote. Wenye lugha zao wanasema ZNZ imefungua 'can of worms' sasa tusiburi tu.
Nami nasema hii ni karata mbovu sana na inazidi kuiweka znz katika wakati mzuri wa kujitoa na si vinginevyo


Tusemezane
 
Duru za siasa.
Inabidi viongozi wa kitaifa wa CCM warudishe imani ya wananchi kwa chama chao, tatizo liliopo sasa ni kwamba CCM kimejiweka mbali na watu ndio maana imefikia hali hii ya kustukiziwa na makombora ya Chadema...CCM kwakuwa hakijashindwa kwenye uchaguzi wowote kinafanana na timu ya mpira inayoshinda ubingwa mfulilizo hufikia hatua hujisahau na kudhani ushindi unaweza kupatikana hata pasipo kujituma.

Fikiri kwa jiji la Dar es Salaam ambalo linakabiliwa na tatizo la maji kwa mwezi sasa kisha watu wanamwalika Waziri wa Maji Prof Jumanne Maghembe awahutubie wananchi, sijui awaeleze juu ya nini wakati maji hakuna kama sio kumsimamisha 'kizimbani' na kumlazimisha kujibu shitaka la bomba liliharibika na ambalo halitoi maji...naye Nape akiwa Mufindi alipobanwa kwamba watoto wanasoma wanakaa chini wakati Mufindi ndio yenye msitu wa mbao, Nape badala ya kujibu kichama akajifanya Waziri na kujibu kuna chenji yetu ya Rada, tumekubaliana kwamba fedha hizo ziingizwe kwenye elimu.

Waziri wa Mawasiliano Dr Mwakyembe kawaeleza wananchi madudu aliyoyakuta kwenye wizara yake hapo alikuwa anakiri kwamba serikali ya CCM ina madudu..Inabidi wajumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM waamke na kufanya kazi za chama badala ya kukaa mijini tu na kusubiri wakati wa kampeni ufike, Siasa za namna hiyo zimepitwa na wakati.
 
Ritz CCM imeacha misingi yake ya kuwasemea wanyonge ukipenda tabaka la wakulima na wafanyakazi bahati mbaya baadhi ya wanachama na viongozi wa CCM wanajaribu kumtwisha zigo la lawama Rais Kikwete wanajifanya hawakumbuki /hawajui azimio la Zanzibar lilipitishwa lini na madhumuni yake yalikuwa yapi.

Leo hii ukitaka nafasi ya uongozi kupitia CCM kama unatoka tabaka la wakulima na wafanyakazi hakika nafasi yako itakuwa finyu na uwezekano wa kupenya ni mdogo mno CCM ya leo ni CCM ya wafanyabiashara,madalali wa kuuza nchi ndiyo maana wasomi wengi baada ya kubaini muelekeo wa CCM wamekikimbia.Tabaka la wafanyakazi na wakulima limebaini halina nafasi ndani ya CCM.Ikatokea bahati mfanyakazi au mkulima kupata nafasi ya uongozi katika ngazi yoyote atajikuta anatumikia mfumo wa wafanyabishara wakubwa na kuliacha tabaka la wafanyakazi bila uwakilishi wa maana.Mfano mzuri ni mgogoro wa madaktari,waalimu na wanafunzi wa elimu ya juu wamejikuta hawana mtetezi wala mwakilishi toka chama tawala chenye wabunge wengi.Tabaka la wafanyakazi wa sekta mbali mbali linaona wenzao wanavyonyanyaswa,wanavyopigwa,wanavyotishwa usifikiri wote watakuwa manyumbu wanaoliwa na mamba wa mto Grumeti hapana wataiadhibu CCM katika sanduku la kura.

Mwl Nyerere aliwahi kuionya CCM ubaya kuacha misingi yake bahati mbaya viongozi wa chama na serekali wakati huu hawakuliona hilo walidhani waTanzania wataendelea kuwachagua bila kujali wanachowafanyia.
 
Last edited by a moderator:
Ngongo,
Kwa kuongezea juu ya tabaka la wakulima na wafanyakazi walivyotengwa, hata watu wenye mtizamo tofauti na wakibiashara nao wametengwa. Ingawa watu hao wapo CCM lakini hawana imani na uongozi na kinachoendelea. Kundi hili huwa linaumia sana kwa kuona ile CCM wanaoijua wao siyo ya sasa, CCM-biashara.

Unakumbuka jinsi MNF ya akina Butiku ilivyoshambuliwa pale walipotaka kutoa maoni.
Sasa hivi wameanzisha baraza la wazee ambalo si sehemu ya CC, NEC au mkutano mkuu. Ni club ya chai inayoweza kuongelea chama kama tunavyoongelea Simba na Yanga na baada ya hapo kila mtu anaenda kulala. Wametengwa tayari

Wafanyabiashara wamekiteka chama kila sehemu muhimu moja kwa moja na kupitia mawakala wao.
Lakini Mwenyekiti naye anasehemu yake ya lawama kwasababu ni yeye aliyeanza kutekwa na wafanyabiashara, na ni yeye anayecheza kara mbili, ya wema na ya kuuma (Double standard) matokeo yake hata wenye uthubutu sasa wamerudi nyuma kwasababu Mwenyekiti anaweza kuwatosa au kuwatoa kafara.

Utakumbuka mzozo wa posho na sakata la Pinda. Msimamo wa chama tawala haukuwepo. Mwenyekiti anadhalilisha watendaji wake sasa hapo nani atasimama na kukemea uovu. Mwenyekiti amekumbatia wahalifu sasa nani atakayepambana nao.

Anguko la CCM ni mchanganyiko wa 'factors' na hakika kurudi tena ulingoni zinahitajika jitihada zailizokithiri.
Kwa upande wangu, nadhani ni vema wana CCM wakaanza kujadili msiba na arobani maana mgonjwa aliye ICU ni mahututi
 
Nguruvi3,
Katika swala la Muungano bnafsi yangu nimekuwa mkweli zaidi kuwafahamisha ndugu zangu wa Zanzibar kuhusu hali halisi ya Muungano wenyewe na jinsi gani Zanizibar inauhitaji kuliko hizi hadithi za baadhi viongozi wanaotafuta kura ili wapate kuingizwa ktk system.

Kuna jambo moja muhimu sana lazima ulifahamu. Kama navyosisitiza siku zote ni lazima tuwasome WATU tujue wanafikria nini na kitu gani kinafanyika ktk MAZINGIRA tuliyopo ili kufanya maamuzi mazito dhidi ya tatizo linalojitokeza. Kwa mfano sasa hivi wanasiasa wote wanajua ya kwamba huwezi kuhesabika ikiwa hutaleta hoja yenye mgogoro naukaonekana mwiba kwa serikali. Ukionekana mwiba ytavutwa ktk system na ndipo ulaji wako utakapo anza na utahesabiwa.

Kwa hiyo vurugu nyingi sana za kisiasa zinavyofanywa na wanansiasa sii kwa lengo la kuboresha system yenyewe maana huwezi kuipinga system wakati ukiwa mwajiriwa wa system ile ile unayopingana nayo. Siku zote kisiasa tumeona watu wanaopingana na system iliyopo madarakani kwa kuingia msituni ama kuuunda chama pinzani dhidi ya utawala uliopo lakini hii ya Kibongo mtu anaweka muafaka na CCM halafu wakati huo huo anadai Kuvunja muungano au serikali tatu hakika ni upotoshaji ambao lengo lake ni kutafuta sababu ili wahesabiwe.

Madai ya Wazanaibar kwa mwenye kuelewa hayana mantiki kabisa..Tunapozungumzia serikali TATU ina maana kinachotakiwa ni kuundwa serikali ya Tanganyika! Sasa nashindwa kuelewa serikali ya Tanganyika ikiundwa itawafaidisha nini Wazanzibar ambao tayari wapo ktk mfumo wa serikali tatu kiaina. Wao tayari wanayo serikali ya Jimbo (state or Province) wakiwa na viongozi wao pia wamo ktk serikali ya muungano kikamilifu, hivyo ujio wa serikali tatu hautabadilisha kitu isipokuwa Bara ndio itaunda serikali na uongozi kama waliokuwa nao wao mbali na serikali ya Muungano. Kwa nini wanataka Bara nayo iwe na serikali kama wao hapo ndipo napokwama kuelewa itawafaidisha nini maana halikuwa dai lao bali tulotakiwa kudai ni bara.

Haya wengine wanadai tuuvunje muungano wa nchi zetu na kuunda Jumuiya ya Ushirikiano mpya kama wa EAC ambao sii muungano wa nchi bali ushirikiano ktk kuboresha mahusiano ya nchi na nchi kibiashara na movement za wananchi wake. Tana bila aibu wanataka kufananisha na Umoja wa nchi za Ulaya!.. Jamani hao wenzetu wamefika stage tofauti kabisa ya maendeleo, wao wanachotazama ni UCHUMI wa nchi zao ambao hauwezi kukuia zaidi pasipo kupanua wigo la ushirikiano. Kutoa ruksa zaidi ya uwekezaji kwa lengo la kukuza chumi ya nchi husika, lakini panapokuwa na Ubepari ni lazima kila nchi itazame advantage za mahusiano hayo. Huku North America waliunda kitu kama hicho kiitwa FREE TRADE zone lakini kwa kutazama mazingira ya hapa wameondoa free movement ya watu tofauti na jumuiya ya Ulaya. Hawa wenzetu matajiri wameunda Jumuiya ya matajiri ili kukuza pato lao zaidi na zaidi, leo nasi maskini tunaunda jumuiya kwa kufuata misingi ya Matajiri badala ya kufikiria kama maskini waloungana na jinsi gani watajilinda kuwa na kauli moja.

Sasa maadam hili la EAC linatushinda kutokana na fikra za vitabu kutaka kuunda jumuiya kama ile ya Ulaya, ushirika kama ule wa Ulaya ilihali sisi maskini ndio maana tumejikuta tatizo kubwa la Tanzania ni ardhi yetu maana sisi ardhi ni mali ya serikali wakati wenzetu walishagawana toka mkoloni. Maskini utajiri wake ni ardhi na hii atailinda kuliko hata mwanaye mwenyewe wa kumzaa..

Nashindwa kuelewa hawa Wazanzibara ambao leo wamesha pata uraia na makazi yao Bara hawa watahesabika vipi au ndio ktk makubaliano mapya. Na hayo makubaliano yatakuwa ya upande mmoja? maana tatizo kubwa la Wazanzibar ni wabara wanaohamia visiwani kibiashara. Wabara wanaitwa bomba la Mavi kwa dhana ya kwamba wabara sii Wastaarabu, wao ndio wanapeleka haramu zote mbaya visiwani. Kweli watu wanaofikiria hivi unaweza vipi fikia muafaka hata kama tutauvunja muungano? maana tayari mgogoro unao jitokeza ni wa kiimani (fikra) kuwa wao ni wabora zaidi ya wabara tutashirikaniana vipi kati yetu..

Nategenmea sana mada ya - Let's Zanzibar GO itawaamsha walolala kwa sababu wengi ya watu hawa wanaodai Uhuru na haki ya Wazanzibar hawajawahi kuishi nchi zilizokuwa na Muungano kama wetu. Binafsi yangu naamini kabisa kama tutaunda serikali tatu basi Zanzibar itakufa kabisa kama zilivyokufa states za Marekani au Province za Canada na inajulikana nchi ya Marekani (USA au Canada). Binafsi yangu naamini kabisa kuna tatizo la kimfumo ktk uongozi na hili ndio sababu kubwa ya makundi haya ya watu kujitokeza. Wengine wanataka kuhesabiwa, wakipiga kelele wataingizwa ktk payroll ya serikali ama kujiunga ktk system. wakisha pata malengo yao basi hutawasikia tena wakizungumzia haki za wananchi wake.

Huu ni mchezo wa kisiasa tu, lazima wananchi wa Zanzibar watambue kwamba hawawezi kutumiwa na kundi la watu ktk kujitafutia umaarufu. Kama hao viongozi wao ni wakweli na wameunda serikali ya mseto kwa manufaa ya Wazanzibar watueleze wazi ni wapi wanapokwamishwa na serikali ya Muungano ikiwa ndani ya serikali hiyo wamo Wazanzibar? Hivi wamewahi kujiuliza kwa nini TANU ilipovunjika iliitwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) hili neno Mapinduzi limetokana na nini na kwa nini liemchukua uzito mkubwa ktk ujenzi wa CCM.
 
Mkuu Mkandara,
Umeeleza mengi sana kwa mantiki na kama ulivyosema kama wanauelewa basi ule uzi wa LET ZNZ GO! ungewasadia sana.

Hili la viongozi kutafuta mahali pa kutokea ili waonekane naliafiki kabisa. Najaribu kufikiri mjumbe mmoja wa tume ya katiba ambaye ni msemaji sana katika redio tena za nje. Huyu bw. sikutegemea kusikia amekubali kuwa mjumbe wa tume kwa jinsi anavyouchukia muungano. Leo kakaa kimya anasema yupo kutetea ZNZ, sijui anaitetea vipi akiwa meza moja na maadui. Kwanini asingesusa kabisa! Pengine keshaonekana baada ya kuzua mgogoro na ulaji tayari!!

Ukiwasikiliza vizuri WZNZ hawasemi tuachane, wanasema tuwe na mkataba au serikali 3 au mahusiano ya EU.
Kila hoja moja iliposhindwa waliibua nyingine kwasababu tu hawawezi kutoka katika muungano wanaouhitaji lakini wanataka wawe na sehemu yao isiyowahusu wenzao.

Baada ya hoja zote tatu kugonga mwamba sasa wanakuja na hoja ya Tanganyika irudi kwanza.
Wasichokijua ni kuwa kurudi kwa Tanganyika kama nilivyosema na ulivyosema ndio watamezwa kabisa au muungano utakufa.Sasa hivi wanasauti sana kwasababu wapo ndani ya serikali ya muungano wanayosema ni yetu sote halafu wanayo ya kwao wanayosema ya ZNZ.

Wasichokijua ni kuwa uwepo wa Tanganyika utaleta tatizo kwao. Tanganyika itaingia kama mbia hapo kila kitu ni jino kwa jino. Sasa hivi wakija bara wanasema ni sehemu ya muungano lakini wao wanaserikali na sheria zao tena makusudi kumbagua mbara. Tanganyika ikirudi itakuwa ni jino kwa jino. Hutaki ajira hakuna ajira, hutaki ardhi hakuna ardhi n.k.

Kwa Zanzibar kuingia EAC ni lazima watahitajika kuwa sawa na wanachama wengine.
katika nchi zote hakuna atakayesema yeye ana eneo dogo au idadi chache ya watu.
Rwanda na Burundi ni ndogo lakini bado zinawajibika kama wanachama wengine, itashangaza kama Mzanzibar ataweka sheria za kuwazuia raia wa nchi nyingine ili hali yeye anafaidika na ushirikiano.
Hapo tena si wabara kila atakayetaka kwenda ZNZ atakwenda!

Kuhusu ukazi, itakapotokea ZNZ ikajitenga nakuhakikishia kuwa wapo watakaoikana na kubaki raia wa bara.
Lakini kwa mwendo wa chuki walioijenga sidhani kama ukaazi wao utakuwa na heri.

Ikitokea hivyo, ZNZ itajikuta katika wakati mgumu sana hasa katika biashara na ajira.
Sidhani kisiwa kile kinaweza kuhimili WZNZ wote walioko bara, na hapo zitaanza fitna za urangi, nywele, nani mzalendo na nani mamluki.

Tutasikia HIZBU na Mapinduzi Daima. Hayo ni katika kugombea kamkate kadogo!
Kinachonisikitisha zaidi ni watu wa chini ambao ndani ya muungano hawaoni kilicho mbele yao. Wavuvi watabaki kugombea soko la Hoteli za waitaliano n.k. tofauti na ilivyo sasa.

Tukijiuliza katika yote hayo Tanganyika itakosa nini kiasi cha kuihitaji Zanzibar, jibu ni hakuna.
Mkandara, kama ulivyogusia ni ngumu sana kuelewa wanataka nini haswa! Hoja zote ni dhifu sana kama ile ya mambo ya muungano yaliyoongezwa. Nimeuliza swali na kila mara topic inaishia hapo kwasababu hawana jibu.

Swali ninalouliza ni kuwa katika mambo 11 yaliyoongezwa ili kuiumiza Zanzibar ni yapi hayo? Mmoja ameniletea orodha na kushindwa kutetea hoja ya kuwa yanamuumizaje MZNZ zaidi ya kumnufaisha.

Mathalani, elimu ya juu imeongezwa na hakika anyefaidika ni MZNZ kwasababu gharama za elimu hiyo kwake ni bure! halipi. Pili, nafasi ya kupata elimu hiyo ni ya upendeleo kwa gharama za Mtanganyika.
Sasa hili linamsaidiaje Mtanganyika kama ameliongeza katika yale 11 ?

Kwasababu ya hasira wameamua kuunda baraza lao la mitihani kwa vile wanaonewa.
Hiyo ni haki yao kabisa. Wasichokijua ni kuwa itabidi wahitimu wao wafikie kiwango cha elimu ya vyuo vya bara.
Hapo tayari watakuwa wameshajitoa katika elimu ya bure achilia mbali nafasi. Nina uhakika kuanzia mwakani kamisheni ya elimu ya juu itaanza kutathimini Watahiniwa wa ZNZ kama wanakidhi vigezo kama mtahiniwa wa NECTA.

Binafsi nawaombea heri wazanzibar katika jitihada za kujitoa katika muungano. Nawatakia heri kwasababu hakuna siku Mtanganyika anaweza kusema kukosekana kwa ZNZ ni tatizo kwake.
Kwa vyovyote iwavyo ZNZ inaihitaji Tanganyika na wala si kinyume chake.
LET ZNZ GO! There is nothing to lose iota.
 
Tatizo ni aina ya huu mnaoita "Muungano". Hata sielewi ni wa namna gani, yaani sioni vigezo vya kuitwa hivyo. Uwepo wa Union Affairs na Non-Union Affairs ndio chanzo cha kila kitu!

Mfano mzuri ni muungano wa "mke na mume" hawa hawaungani kwa "tendo la ndoa tu", bali ni pamoja na fikra, mitazamo, functions na hata imani! Kwa kuungana hivi, inakuwa rahisi kwa kila mmoja kuwa huru kumrekebisha mwenzake pale anapoonesha kulega.

Uwepo wa Non- and Union Affairs umeondoa kabisa uhalali wa "Muungano", kwangu ni "Ushirikiano tu". Ni sawa kwa mwanaume na mwanamke kukutana mtaani wakala na kulala pamoja, asubuhi kila mmoja anaweza kushawishika kumsahau mwenzake!

Kwani ni nani hasa anayeratibu Non Union affairs za bara? Si ndio huyo wa Union affairs? Je atakuwa na hekima gani ya kuwa fair?
Tuachane na hilo: Hivi, si tunajua kuwa aina yoyote ya umoja, Afrika...ni kero kwa adui zetu? Mbona tumewapa mianya ya kutuvuruga? Kupitia kile tunachotofautiana, kitatumika kuua kile tunachofanana!

Huwezi kuulinda huo "muungano" kwa kuwatisha waznzbr kuwa wataathirika kwa kutukimbia, kwanza wapo wanaowaongoza, wamewashikia akili, nao wameziba masikio ila kwao tu! Wachache mno wenye kujua mambo Znz, nguvu yao ni ndogo, ndio maana swala hili halipatiwi ufumbuzi kwao! Wachache wanaona faida yake, hali wengi hawaoni!

Hakuna jambo jema dunian kwa wanyonge kama UMOJA! Lakini Muungano wa kinafiki unaleta rafiki mnafiki, unafiki, unafiki, unafiki, unafiki.

ACHA WAENDE, tumekutana nao tu mtaani tukaenda geust house!
Tafsiri ya Muungano au umoja sio lazima iwe imetolewa na mzungu, ndio maana tunaburuzwa!
Mungu wetu anaita!
 
Ritz CCM imeacha misingi yake ya kuwasemea wanyonge ukipenda tabaka la wakulima na wafanyakazi bahati mbaya baadhi ya wanachama na viongozi wa CCM wanajaribu kumtwisha zigo la lawama Rais Kikwete wanajifanya hawakumbuki /hawajui azimio la Zanzibar lilipitishwa lini na madhumuni yake yalikuwa yapi...

Ngongo.
CCM uzinduka wakati wa kampeni tu na baada za kampeni kupita wahusika hawaoni tena ulazima wa kufanya mikutano ya kuonana na wananchi na pia mikutano ya kupima uhai wa chama chao.
 
Wakuu Mkandara, Nguruvi3, Barubaru..
Siku za karibuni pamekuwepo kauli za kukumbushana historia za kikoloni kwamba maili kumi za pwani ya Tanganyika ni sehemu ya Zanzibar.

Kauli hiyo inamaanisha kwamba eneo kubwa la majiji ya Dar es Salaam na Tanga na miji ya Bagamoyo, Kilwa, Mtwara na Lindi pamoja na visiwa vya Mafia ni mali ya Zanzibar hii historia ina ukweli wowote.
 
Last edited by a moderator:
Ritz Umesahau Mombasa ya Kenya.


Wakuu Mkandara, Nguruvi3, Barubaru..
Siku za karibuni pamekuwepo kauli za kukumbushana historia za kikoloni kwamba maili kumi za pwani ya Tanganyika ni sehemu ya Zanzibar.

Kauli hiyo inamaanisha kwamba eneo kubwa la majiji ya Dar es Salaam na Tanga na miji ya Bagamoyo, Kilwa, Mtwara na Lindi pamoja na visiwa vya Mafia ni mali ya Zanzibar hii historia ina ukweli wowote.
 
Last edited by a moderator:
Ritz Umesahau Mombasa ya Kenya.


Mkuu Ngongo.
Historia ya huo mgawanyo wa maili kumi unaanzia katika mkutano wa Berlin ulikamalika mwaka 1885 ambapo kwa maslahi yake Uingereza ilishindikiza eneo la pwani ya Afrika Mashariki litolewe kwa usultani wa Zanzibar kwa upande wa Kenya historia hiyo inaonyesha mpaka mto Tana ambako kwa sasa ni nchini Kenya.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Ngongo.
Historia ya huo mgawanyo wa maili kumi unaanzia katika mkutano wa Berlin ulikamalika mwaka 1885 ambapo kwa maslahi yake Uingereza ilishindikiza eneo la pwani ya Afrika Mashariki litolewe kwa usultani wa Zanzibar kwa upande wa Kenya historia hiyo inaonyesha mpaka mto Tana ambako kwa sasa ni nchini Kenya.
Inategemea unataka kurudi nyuma miaka mingapi maana kama tutasema hivyo mbona Mjarumani alipotawala Tanganyika makao yake yalikuwa Dar? na Muingereza vile vile. Ujenzi wa Tanganyika toka Dar hadi Kigoma mbona huyo Sultan hakuhusishwa kama ilivyokuwa Zanzibar?. Nachoelewa mimi Rwanda na Burundi zilikuwa sehemu ya Tanganyika wakati wa Mjarumani baada ya vita zikawa sehemu ya Kongo (Mbelgiji) na kisha zikaundiwa mipaka yake lakini hili la Dar na pwani zetu kuwa milki ya Sultan zinarudi nyuma sana kabla ya historia kubadilika. Je, na sisi tunaweza kuzidai Rwanda na Burundi?

Lakini tukirudi nyuma zaidi tunakuta Sultan alitawala sehemu kubwa ya Pwani wakati makao yake yakiwa Mombasa kabla ya kuhamia Zanzibar. Na kama sii kulindwa na Muingereza bila shaka Zanzibar ingekuwa koloni la Mreno, hatujui mipaka yake ingekuwaje tofauti na iliyopo leo. Hivyo nasi tutumie akili zetu wenyewe. Hii mipaka iliwekwa na wakoloni wakigawana ardhi yetu kama tunavyokatikana viwanja, sasa mzee wako anapouza sehemu ya kiwanja huwezi kuendelea kudai kilikuwa chetu mzee alikosea kwa kutumia haki yake ya kumiliki ardhi ile kabla hajakimegua kipande na kukiuza. Kibaya zaidi huyo Sultan mwenyewe hakuwa na uhalali wowote wa kuitawala visiwa vya Zanzibar, Mombasa wala Kilwa na ndio maana alipinduliwa na kuondolewa.

Nachoweza kusema kati ya wote waliokaa Mkutano wa Berlim mwaka 1885 hakuna hata mmoja wao mwenye mamalka ya kuzungumzia Ardhi ya Zanzibar wala bara, sii Sultan, Mjarumani wala Muingereza isipokuwa kuna mazungumzo ya ukombozi wa Afrika Pan African na yale ya kuunda Afrika moja ndio yaliyoshinikiza Mapinduzi ya UHURU wa mwafrika ktk nchi yake. Mazungumzo haya yalishirikishwa wajumbe toka Zanzibar kina Karume na Abrahman Babu ktk maandalizi ya uhuru wetu sisi na ndio kilichopelekea kuwepo Muungano wetu..Huyo Sultan hayajui haya! Lakini Upande wa Pili kina Shamte walikuwa na mawazo mengine ya kumrudisha Sultan wakafanya mazungumzo na Kenyatta kuhusu Mombasa Lamu na Malindi yaani Unafiki wa mtu mweusi haukuanza jana. Tuna tatizo kubwa sana la Utwana kifikra pengine tumeumbwa kuwa watumwa tuu miaka yote.

Watu wengi wanapenda sana kumtetea Sultan kwa sababu ya uchaguzi ulofanyika na Shamte akashinda kuwa ndio Uhuru kamili wa Zanzibar, mimi nishawaambia wala sii mara moja ya kwamba imefanyika hivyo Rhodesia na South Afrika wala sii swala la kutambuliwa na UN bali wananchi wenyewe kuitambua kutambua Uhuru wao. Palestine ilikuwa nchi na ikitambuliwa na UN leo wako wapi? imemegwa taratibu hadi kimebakia vipande vidogo sana na yawezekana kabisa Palestine ikaondoka ktk historia wajukuu zetu wasijue kulikuwa na nchi ikiitwa Palestine.

Kwa hiyo mbali na mkutano wa Berlin hata sisi waasisi wa Uhuru wetu walikuwa na mikuttano yao ambayo haitambuliwi na wakoloni lakini tulifikia maamuzi ambayo leo baadhi ya watu hawayatambui kwa sababu walokubaliana ni waafrika weusi wasiokuwa na ustaarabu.
 
Mkuu Mkandara,
'Umeninyang'anya maneno' nakushukuru sana kwa hilo.
Mfano wa Burundi na Rwanda tu unatosha.

Unajua kinachofanyika ni kutapa tapa baada ya hoja za serikali 3, mkataba n.k kutokuwa na majibu.
Ili kujenga uhalali wa madai yasiyo na mashiko zinatumika mbinu za kutaka kuungwa mkono na watu wa pwani, lakini kibaya zaidi ni kuitisha Tanganyika kuwa tukikataa mkataba, serikali 3 au mahusiano ZNZ itadai sehemu ya maili 10. Huu ni ukosefu wa mbinu na fikra wa hali ya juu sana kwa Wazanzibar.

Wao wanaamini kuwa Sultan kutoka Oman aliyekuja kuwafanya watwana ndiye mwenye haki ya kuweka mipaka.
Halafu wanajichanganya sana wanaposema ZNZ ilikuwepo kabla ya Tanganyika miaka 500, sasa ilikuwepo vipi na hiyo maili 10 iliyokuwa haipo? Wanasema ZNZ ilikuwa huru 1963 na kiti UN, well! uhuru huo ulipatikana vipi bila ya maili 10?
Je waliwahi kuonyesha concern juu ya suala hilo

Wanazidi kujichanganya kwasababu Pemba wanamadai UN kuwa si sehemu ya ZNZ na znz inaundwa na Unguja na Pemba,
sasa kwanini waSijadili tatizo lao wanataka maili 10 zisizokuwepo!

Wanaamini mipaka iliyowekwa na wakoloni ni muhimu sana kuliko Uafrika wao.
Tunachosema LET ZNZ GO! Hatutishwi nyau tumeamua LET ZNZ GO!
 
Inaendelea ........ [Kutoka bandiko #103]

BAJETI: UDHAIFU WA SERIKALI
Tumesemakubana matumizi au kupata vyanzo vya mapato njia mojawapo ni kupunguza ukubwa wa serikali.
Ninasikia kuwa Wabunge wameahidiwa kupewa ofisi na wafanyakazi takribani 4.

Sote tunajua kuwa mbunge ni mwakilishi na wala si mtendaji. Ofisi ya kila mbunge ni ofisi za wananchi. Mbunge ambaye anafanya kazi kama sehemu ya halmashauri au jiji haihitaji ofisi kubwa, anaweza kuwa na ofisi katika ofisi ya mkuu wa Wilaya au Halmashauri

Kwa wabunge wetu muda mwingi wanautumia safarini Dodoma na Dar es Salaam kwenye kamati zao! hakuna sababu ya kutenga fedha za ofisi majimboni. Huku ni kumwongezea mlipa kodi gharama za anasa kwasababu Ofisi ya mbunge si muhimu, cha muhimu ni Mbunge mwenyewe.

akati hayo yakiendelea tunasikia wanajengewa Hosteli, sasa tunajiuliza za nini wakati wapo Dodoma kwa muda tu! Na pia wana mfuko wa mbunge ambao hatujui nani anaukagua! Haya yote ndiyo mambo yanayo ongeza gharama zisizo za lazima na mlipa kodi anabeba mzigo huo.

Tumewahi kusema sehemu ya jamii inayoumia sana na kodi ni Wafanyakazi ambao hawana chaguo.
Wakati huo huo misamaha ya kodi kwa wafanyabiashara ni lukuki.
Imeshasemwa sana kuwa serikali dhaifu ni ile isiyoweza kukusanya kodi kama ilivyo Greece leo
Hii kodi tunayoiona ni matokeo ya kukamuliwa wafanyakazi na wanunua vocha za simu huku kodi kubwa sana ikiwa imefichwa katika bidhaa za walaji 'consumers' na misamaha ya kodi ya kifisadi

Haiingii akilini kuwa kampuni za vinywaji mathalani bia zinakuwa miongoni mwa walipa kodi 10 bora nchini.
Nchi yenye madini kama yetu inasikitisha kuona sekta hiyo inachangia kidogo sana katika uchumi.
Hapa kuna walakini na Rais alipounda tume ya kuchunguza sekta hiyo hakumaanisha kutafuta suluhu, ilikuwa ni kuficha maovu yaliyotendwa na pengine yaliyo mbioni.

Tunasema hivi kwa sababu taarifa za tume hiyo zimefungiwa Ikulu huku wachimbaji wakituachia mashimo na serikali ikitafuta namna ya kukamua kodi za vocha za simu! Hii kama si aibu, aje ajaye aniambie ni nini.

Tumesema kuna eneo la biashara ambalo ni muhimu sana. Serikali haiwezi kufanya biashara lakini inawajibu wa kujenga mazingira mazuri ya biashara. Hakuna sababu yoyote ya sisi kutofaidika na fursa ya ushirikiano wa EAC. Hakika tumejaaliwa sana kijiografia na rasilimali.

Endapo tungekuwa makini tungeweza kuvuna sana kodi kwa kutumia bandari zetu za Tanga, Dar na Mtwara.
Inashangaza Zambia sasa wantumia bandari ya Beira ili hali tayari tuna miundo mbinu nao. Kuna Congo, Rwanda na Burundi ikiwa ni pamoja na Uganda ambazo zingeweza kutumia bandari zetu tu na kuwa chanzo kizuri cha mapato.
Kilichopo ni urasimu na ubadhirifu bila kuwa na mipango ya kuendeleza bandari hizo.
Tutafafanua hoja hii tutakapoijadili EAC na mstakabali wa kiuchumi, kisiasa na kijamii kama alivyoshauri Mkuu Ngongo

Leo kuna habari kuwa Precision air imeanza safari za Zambia mara 3 kwa wiki.Wazambia wamefahia sana huduma hiyo.
Hii maana yake ni kuwa Tanzania ipo katika kitu kinaitwa 'strategic geo position'. Na kwamba miundo mbinu ni sehemu muhimu sana kwa maendeleo na uchumi.

Wenzetu kama Ethiopia, Egypt na hata Kenya huduma za jamii kama miundo mbinu ya usafiri wa anga ni kiungo muhimu sana cha uchumi. Mathalani, hawezi kusafiri na Ethipoia Airline bila kufika Adis ambako utaacha dollar ima katika ticket au matumizi ya kawaida.

Mnaokumba enzi hizo tulikuwa na mashirika mbali mbali yakija hapa kwetu. Nakumbuka France, Lufthansa, Scandinavia, PIA, KLM, Russia, BA n.k. Kwa sehemu kubwa sana Dar es Salaam ilikuwa 'HUB' au Gateway kwa nchi majirani.

Leo mashirika mengi yamejitoa na kuendeleza huduma Kenya. Hakuna anayejiuliza ni kwanini.
Utashangaa bodi ya utalii ikitoa takwimu za ongezeko la Watalii, wasichojiuliza ni kuwa wanafikia wapi?
Kwanini tuwahesabu wakiingia mbugani na kwenye fukwe na si kuanzia pale wanapotua uwanja wa ndege? wanapotumia usafiri wetu na wanapoingia mbugani? Tunapoteza mapato kiasi gani? Je kile kidogo kinachpatikana kinafika hazina?

Miundo mbinu ni sehemu ya huduma kwa jamii lakini ni sehemu muhimu ya uchumi. Mataifa yenye miundo mbinu bora kama Marekani na nchi zingine ikiwemo south Africa kila siku kuna shughuli za ujenzi wa miundo mbinu.
Siku ya leo bunge la marekani limepitisha mswada wa ujenzi wa miundo mbinu kwa sababu za kiuchumi ikiwa ni pamoja na kuendeleza uchumi.

Sisi tumeshindwa kuweka mabehewa katika reli ili tukusanye mapato yatokanayo. Lakini si mapato tu hii ni sehemu ya kuimarisha uchumi na kupunguza gharama zisizo za lazima. Ukinunua mahindi ya mkulima wa Sumbawanga kwa bei nzuri na kuyahifadhi ghala la taifa hatutumia dollar kuagiza unga! Hii pia ni motisha kwa wakulima na kwa Tanzania ya leo watu wangeacha kazi na kwenda kulima kilimo cha kisasa na kitaalamu. Jinsi jamii inavyopanda kimaisha ndivyo uwezo wa serikli unavyoongezeka.

Na eneo la mwisho ni uvuvi. Hili linaonekana kama sehemu tu ya maisha na wala si uchumi. Hutujiulizi kwanini iwepo mei kutoka japan kuvua samaki katika fukwe zetu! hadi hapo hatujaona umuhimu tu.
Kwa nchi za wenzetu laiti wangekuwa na mito, maziwa na bahari kamatuliyonayo pengine wasingehitaji hata kujua vocha inauzwaje.Kodi ya vocha za simu ni sehemu ndogo sana ya sekta ya uvuvi kama itapewa mtiizamo halisi na wenye maono.Bajeti nzima uvuvi unatajwa tu kwavile kuna samaki baasi!

Kwa hayo machache tu bado hatujaangalia viwanda kwa maana ya vile tunavyoweza kuwa navyo na si viwanda kama vya mataifa makbwa.

Tutaendelea kuangangalia maenao mengine ili tujirishe kweli kuwa vocha za simu ni chanzo muhimu sana kwa mapato ya taifa au la!

Itaendelea.....
 
Inaendelea.......

Tumeshaongelea kwa uchcahe umuhimu wa miundo mbinu kama sehemu muhimu ya maendeleo ya kiuchumi.
Ni ukweli kuwa tumeshindwa kutumia nafasi tuliyo nayo kuimarisha miundo mbinu na ile ya kijiografia kutafuta vyanzo vya mapato.

Hakuna mwerevu anayeelewa kifo cha huduma za Reli kama Tazara na TRC. Nchi za dunia zilizopiga hatua bado zinatumia miundo mbinu ya reli, ni ajabu sisi tumeshindwa na akili zetu tumezielekeza kwenye kodi za bia na sigara.

Reli kama ya kati ilitosha kabisa kuwa sehemu muhimu ya mapato ya ndani na ya nje. Bandari zetu hazifanyi kazi kwa viwango kwasababu tunalinda masilahi ya mafisadi halafu tunatafuta vyanzo vya kodi!

Tukiangalia upande wa viwanda tulivyokuwa navyo, sioni sababu ya viwanda hivyo kufa.
Hata kama serikali ilijitoa katika kuendesha bado ilipaswa kuhakikisha kuwa viwanda hivyo vinapewa wawekezaji kwa malengo ya kuviboresha na si kugeuza maghala.

Bado nakumbuka Tanganyika Packers na kujiuliza hivi ng'ombe hakuna tena kiasi cha kuagiza nyama za makopo kutoka Saudia au Brazili! Bado najiuliza kwanini Mwatex, Urafiki, Polyster n.k. vilikufa!

Nakumbuka Morogoro ilikuwa ni mji wa viwanda kama Moproco, Polyster maturubai,Tumbaku n.k.
Ajira ziliwasadia sana wananchi na kuongeza huduma kwa jamii. Mji ulikuwa moto moto kama ilivyokuwa Mwanza na Mwatex, Tanbond n.k.

Kule Arusha nakumbuka Sunflag na vingenevyo. Mji wa Tanga ulikuwa na shughuli nyingi za viwanda kama Mbole, chuma n.k.
Ilikuwa ni rahisi kukutana na Mtanzania akisema anafanya kazi shift ya jioni au usiku.
Ilikuwa ni rahisi kusikia wanafunzi wanfanya Tempo wakati wa likizo.
Hayo sasa ni hadithi baada ya saa 12 jioni ni kwenye viti virefu kama wanavyoviita

Hoja yangu ni kuwa uwepo wa viwanda unaongeza nguvu za walaji katika kutumia pesa na ni kwa njia hiyo serikali inakuwa na mtiririko wa ukusanyaji wa mapato kuanzia mkulima, kiwanda, mfanyakazi na wale wanaotoa huduma kwa makundi haya kama wasafirishaji, wagawaji, watutoa huduma za elimu, afaya na hata akina mama ntilie.

Mji wa Mang'ula unajulikana kwasababu ya kiwanda kimoja tu, mji wa Korogwe tangu Kiwanda cha Orange squash kife basi umebaki magofu. Ukiangalia popote pale palipokuwa na ka-kiwanda basi kulikuwa na ukuaji wa shughuli za kiuchumi na kijamii. Nina maana uzalishaji uligusa kila sehemu ya mapato ya taifa.

Faida za kuwa na viwanda vidogo (siyo kulinganisha na dunia ya kwanza), ni nyingi sana kiuchumi na kijamii.
Moja ni kuongeza thamani ya bidhaa kabla haijuzwa. Nakumbuka tumbaku ililimwa Tanzania na kulikuwa na sigara zinauzwa nje (mfano, EMbassy export).

Siku hizi mkulima wa machungwa kule nyumbani Muheza anauza chungwa moja kwa sh 50 na chungwa hilo likifka Kenya na kutengenezwa linarudi katika mifuko ya platic likiuzwa kwa zaidi ya sh 500 kwa kutolea mfano.
Hivi kweli hatuna njia za kutuwezesha kusindika machungwa hapa nchini hadi tusubiri ya South Africa!

Hoja hapa ni kuwa badala ya kukusanya kodi kutoka kwa mkulima wa Pamba, kiwanda, wafanyakazi wa kiwanda, watoa huduma kwa jamii inayouzunguka kiwanda hata kama ni vidogo, serikali inasubiri kodi za waagizaji wa juice, mafuta kutoka malaysi, nguo kutoka Taiwan,China na vocha za simu n.k.

Kwa bahati mbaya zaidi hata hiyo kodi ya kuvizia hatuwezi kuipata ukwepaji na misamaha ya kodi kwa kutumia 'vimemo'.
Hiki ndicho kinapelekea kundi dogo sana la wafanyakazi libebe mzigo wa taifa.
Kundi la wafanyakazi halina namna ya kukwepa kodi au kupewa msamaha.
Kundi athirika lingine ni la walaji 'consumers' kwasababu hizo hizo.

Wakati serikali ikikamua kodi kwa wafanyakazi, walaji na watumia vocha za simu, kuna kikundi kidogo sana kinachofuja kodi hizo kwa kisingizio cha ukubwa. Hakuna sababu ya viongozi kuwa na magari ya kifahari!
Nilishangaa siku moja niliokuwa matembezini Uingereza kumuona waziri akiendesha kigari chake cha Ford.
Huyu ni waziri wa nchi inayotupa misaada.

Kwa nchi nyingine ukiacha kada ya uwaziri au nafasi nyingine nyeti, unapoajiriwa iwe mkuu wa idara au mkurugenzi, wajibu wako nikufika ofisini kwa wakati na kuondoka kwa wakati siyo kazi ya serikali kujua umefika vipi.
Gharama za matumizi ya magari ya serikali zinatisha na hakuna anayeliona hilo, wenzetu kule Dodoma wanajadili vocha za simu

Nihitimishe kwa kusema, kwanza ni aibu miaka 50 bado hatuja balance bajeti yetu! ni kwanini tutumie zaidi ya tunachopata?
Pili, kwanini tusibane matumizi ili kuwa na bajeti yenye uhalisia wa maisha yetu kuliko kuwa na tarakimu zisizo na manufaa yoyote
Tatu, Kwanini serikali isiangalie kwa umakini vyanzo vingine vya kodi zaidi ya vocha za simu?
Nne, hivi rasilimali watu, rasilimali za asili, eneo zuri la kijiografia, maji n.k tusizitumie kuzalisha na kuongeza pato la taifa?
Tano, kwanini tusijiulize iweje Sigara iwe chanzo kizuri cha mapato na si madini, utalii na maliasaili pamoja na uvuvi?
Sita, kwanini tusifikirie zaidi katika kupanua wigo wa kupata kodi kwa njia ya 'viwanda' hata kama ni processing tu!
Saba, Kwanini kunakuwepo na misamaha ya kodi ili hali hakuna msamaha kwa mfanyakazi au mlaji (consumer)

Na pia tujiulize, miaka 50 sasa hatuwezi ku-balance bajeti, hivi kweli akili zetu zimeisha katika kufikiri kiasi kwamba tunavizia kodi za wanafunzi wanaotafuta wachumba! real! waziri wa fedha haoni chanzo kingine zaidi ya vocha za simu! 50 years !

Watanzania bado tuna matumaini kuwa baada ya miaka 50 na maendeleo haya ya kodi ya bia na sigara kwamba tunasonga mbele!
Real! serious! I mean bado tunasubiri tu miujiza zaidi ya hii ya kodi za vocha za wanafunzi kwa bajeti ya taifa!!!!

Tusemezane
 
BENDERA ZA TANZANIA: MZOZO WA KIDIPLOMASIA, IRAN & MAREKANI

Kuna taarifa za kidiplomasia kuhusiana na meli za Iran kubeba bendera za Tanzania pengine kukwepa vikwazo vya kiuchumi ilivyowekewa na nchi za magharibi. Barua ya kamati ya bunge la marekani kuionya Tanzania isiendelee na utaratibu huo si ya kubezwa hata kidogo.

Endapo suala hili lingekuwa katika uzani mwepesi, basi balozi wa Marekani nchini angeweza kuwasiliana na Serikali ili kupata ufafanuzi kama ilivyo itifaki ya kimatifa.

Ikumbukwe kuwa tangu mashambulizi ya Nairobi na Dar Es salaam, marekani ilijenga na kuimarisha ubalozi wake na inasemekana kuwa ubalozi wa Tanzania ni moja ya balozi kubwa sub-Sahara kwa sababu maalumu.
Jambo linapovuka hapo na kuingia katika kamati za bunge la Marekani, jambo hilo ni zito

Ili tuweze kuwa na mjadala ongofu ni vema tukaiangalia nchi ya Iran yenyewe, mahusiano yake na Marekani na Tanzania (background) halafu tutaingia katika kuangalia mzozo huu wa kidiplomasia (diplomatic row) unaolinyemelea taifa.

Iran inajulikana kama Islamic Republic of Iran baada ya mageuzi ya April 1979 yaliyomaliza utawala wa kifalme wa karne nyingi sana. Mwaka 1935 ndipo iliojulikana rasmi kama Iran kabla ya hapo ilikuwa inaitwa Persia.
Neno Persia linamaana 'Land of Aryans'. Hata hivyo bado jina la Persia linatumika kama mbadala wa Iran.

Persia ni tofauti kabisa na Arab na mara nyingi watu wanadhani Persian ni waarabu. Historia ya Persia inamchangayiko wa mambo mengi kusema kwa uchache tu.

Iran ina watu takribani milioni 79 na ni nchi ya 18 kwa ukubwa duniani. Ina umiliki mkubwa wa mafuta na gesi ya asili ikikisiwa kuwa na kisima kikuwa cha nne kwa hifadhi ya mafuta.

Pamoja na utajiri huo bado Iran imekuwa mstari wa mbele katika sayansi ya kisasa hasa nishati ya kutumia nishati ya jua na upepo( wind and solar energy). Kisayansi, Iran imepiga hatua kuanzia zama hizo na mtu wa kwanza kuitambua alcohol (ethanol) alitoka huko. Ni wataalamu wazuri wa mambo ya sayansi na sanaa (Art and Science) n.k toka zama

Iran ina majirani wa Uturuki, Afghanistan, Pakistan, Iraq, Turksmenistan, ghuba ya Oman na bahari ya Caspian.
Kabla ya mapinduzi ya mwaka 1979 kiongozi alikuwa mfalme Pahlavi aliyejulikana kama Shah. Ni huyu ndiye aliyemfunga magereza Ayatollah Khomeni na baadaye kumpeleka uhamishoni Uturuki, Iraq na mwisho Ufaransa kabla hajarudi kama kiongozi wa mapinduzi yaliyomuondoa Shah 1979.

Iran ina mwingiliano sana wa tamaduni kuanzia Roma empire hadi kuingia kwa Uislam.Na kwasasa Waislam wa Iran wengi ni wadhehebu la Shia ingawa wapo Sufi. Mwingiliano huo haukuishia hapo kwani nchi za magharibi zimekuwa katika uhasimu na uswahiba kwa nyakati tofauti.

Kijiografia na kisiasa Iran ina ushawishi mkubwa sana wa mashariki ya kati. Shah wa Iran alikuwa kipennzi cha Marekani na kuondoka kwake kulileta mtafaruku wa kuzuiliwa wafanyakazi wa ubalozi wa Marekani kwa siku 444.
Jaribio la kuwakoa wakati wa Jimmy Carter lilishindikana na mateka waliachiwa huru kwa makubaliano.

Ni mtafaruku huo ndio kilikuwa chanzo cha Rais Jimmy Carter kutochaguliwa tena ukichagizwa na hali ya kiuchumi.
Uhusiano na nchi za magharibi haukuwa mbaya sana hadi alipoingia Ahmadinajade. Rais huyu wa sasa alikuwa ni Meya wa mji wa Teheran na katika kipindi chake alileta mageuzi yaliyompelekea kuwa Rais wengi wakimjua kama mtu wa mabadiliko.

Ikumbukwe kuwa Iran alipigana vita na Iraq na hadi sasa Iran ina ushawishi mzuri sana ndani ya Iraq.
Asilimia 95 ni waumini wa dhehebu la Shia na wengine ni Sunni na usijefanya makosa hata Jews na Christian wapo.

Tunachoweza kusema ni kuwa msuguano wa Iran na nchi za Magharibi upo kwa muda mrefu.
Siasa utamaduni na mchanganyiko wa Iran si jambo la kuandikwa kwa kurasa moja au mbili na ni kwa minajadili ya mada iliyopo tunapaswa kupata mtazamo kwa kiasi tu.

Tuwakumbushe tu kuwa katika bunge la Iran linaloitwa majilis kuna viti maalumu kwa Jews, Christian na wengine.
Kama umewahi kutembelea maeneo ya Pwani ya Afrika mashariki kama Zanzibar na Mombasa au Dar es Salaam utaweza kutana na jamii inayojiita Baluch (Baloch) ambao ni tawi la Baloch Sunni. Hawa asili yao ni Iran ingawa wanaitwa Waarabu pengine kwa mazoea tu.

Mfumo wao wa maisha ni kutoa huduma za social security, pensheni huduma za afya n.k kwa kutumia mapato ya taifa na hii ipo katika katiba yao.

Upande wa elimu, Iran imepiga hatua sana hasa kwa viwango vya UNESCO. Wanayuo vyenye wataalamu wazuri tu na aghalabu sayansi ya nuklia inayoleta matatizo si ya kubeza au ya utegemezi bali ni yao kwa elimu yao.

Hebu tuangalie mfumo wao wa kiutawala na kisha tuingie katika mada haswa kama ilivyotajwa

Itaendelea.......
 
BENDERA ZA TANZANIA: MZOZO WA KIDIPLOMASIA, IRAN & MAREKANI

Inaendelea.......
Mfumo wa kiutawala ni mgumu kuuelewa katika uelewa wa kawaida wa tawala na mgawanyo wa madaraka. Kuna kiongozi wa kidini anayejulikana kama Ayatollah. Ayatollah siyo jina la mtu bali ni wadhifa wa msomi wa kidini, mwana falsafa au mwanazuoni. Kwahiyo Ayatollah wapo wengi kama akina Khamenei, Sistan n.k. Anayebeba wadhifa huo ni lazima awe msomi katika Islamic studies.

Kwa taarifa tu hata neno Mullah ambalo ni la kiarabu siyo jina bali ni wadhifa. Tofauti na Ayatollah pengine Mamulla wamebobea katika Islamic theology na sheria. Katika nchi zinazotumia mullah, neno hilo hutumika sana kwa viongozi wa mitaa kama tunavyotumia maneno Imam.

Ayatollah ndiye anayechagua majaji wa mahakama na mahakama kuu. Kuna majaji wanaoshughulikia mambo ya kiroho na wapo wa mambo ya kijamii. Kuna Jeshi lenye mifumo ya kawaida lakini kuna kikosi kinachojulikana kama Revolutonary guard. Hakika nani ni mkubwa ni suala la mjadala lakini wenyewe wanajua mfumo wao unafanyaje kazi.

Tangu alipoingia Ahmadinajade kumekuwa na msuguano mkubwa wa madaraka kati ya Ayatollaj na Rais. Na msuguano huo bado unaendelea kichini chini. Mhafidhina Ahmadinajade anonekana kukiuka misingi ya mapinduzi kwa kumweka pembeni Ayatollah kwenye baadhi ya maamuzi.

Iran imeendelea sana katika sayansi ya medicine, mathematic, astronomy na kijeshi. Wao wanatengeneza silaha zao wenyewe na sasa inasemekana wana kombora (missiles) isiyojulikana umbali inaosafiri. Ina askari wa akiba wapatao milioni moja na jeshi lenye wataalamu na nguvu za silaha

Siasa za Iran ni zile za kutofungamana na upande (NAM) pamoja na mahusiano ya kidiplomasia na nchi zinazoendelea ambazo kwa hakika ni masikini. Kwa kutumia mwamvuli wa NAM Iran imekuwa na mahusiano na Tanzania kwa muda mrefu na kwa kutumia diplomasia na nchi ziznazoendelea Iran imekuwa ikitoa misaada kwa nchi kama Tanzania.

Uhusiano ulipamba moto wakati Tanzania ikiwa mjumbe wa baraza la usalama(kama nipo sahihi na jina) na hivyo kura yake ilikuwa muhimu sana. Hata hivyo wakati wa Mzee Mwinyi mahusiano yalikuwa murua kwasababu ya mafuta na kama sehemu ya fadhila Wairan walikaribishwa katika bonde la Rufiji. Hili halikuwa jambo baya na hakika ndio msimamo wa South South commission.

Kipindi cha Mkapa mahusiano hayakuwa kama yalivyo sasa.
Kuwa na uhusiano na Iran hakuna tatizo na wala Tanzania haipaswi kuchaguliwa nani awe rafiki nani awe adui.
Pamoja na hayo Tanzania imeshindwa kuweka msimamo wake juu ya mzozo wa Nuklia kati ya Magaharibi na Iran.
Miaka miwili iliyopita Tanzania imekuwa kati na kati kwa kusema Iran inahaki ya kuwa na tekbolojia ya Nuklia wakati huo huo ikisema si vyema teknolojia hiyo ikawa ya Silaha.

Historia ya nchi hii inaonyesha kuwa inapinga uwepo wa Silaha za nuklia. Mwalimu Nyerere akiwa na marehemu Indira Gandhi, Olf Plame, Rais wa Mexico, na Greece walichaguliwa na jumuiya ya kimataifa katika kile kilichoitwa 'Disarmament commission' ili kutoa mapendekezo ya kupunguza silaha kali duniani.
Na tangu hapo hakuna kiongozi aliyefuata ima kukosoa au kupinga msimamo huo ikiwa ni ushahdi kuwa huo ndio msimamo wetu.Tunapocheza karata za kati na kati nadhani hiyo ni dalili ya kutokuwa na msimamo kimataifa kama ilivyo kwa mambo mengine mengi tu.

Marekani na Iran zote zimeonyesha interest na Tanzania. Marekani kama nilivyosema ina ubalozi mmoja kati ya mikubwa sub Saharan. Ubalozi huo umekuwa na tabia ya kuleta viongozi wastaafu wa jeshi na hakuna siri kuwa ni sehemu mojawapo ya CIA.

Inapotokea Rais wa Marekani akaja kugawa vyandarua hapo lipo jambo.Na Iran nayo inapokuwa na haja ya kuwekeza Tanzania na kutoa misaada katika mazingira tatanishi inatia shaka.
Tanzania ina madini ya Uranium ambayo ni kichocheo kizuri cha silaha za nuklia.

Iran ina mahusiano na nchi nyingi sana isipokuwa Israel na Marekani. Marekani kwa shinikizo la Israel kama ilivyo kawaida imeshawishi nchi za magharibi kuiwekea vikwazo vya kiuchumi Iran. Vikwazo hivi ni vya kuidumuza Iran kabla ya shambulio lolote. Hivi ndivyo ilivyokuwa kwa Iraq ailiyokuwa katika vikwazo kwa maiaka 12 au Libya kwa miaka zaidi ya hiyo.

Historia inajieleza kuwa vikwazo katika nchi zilizopiga hatua kama Iran haviwezi kuwa na nguvu kama kuna mianya ya kuvikwepa. Israel kwa kuogopa tishio la Iran iliamua kushambulia hata bila msaada wa Marekani.
Hivyo ndivyo ilivyokuwa wakati Israel iliposhambulia mtambo wa Iraq unaoaminika kuwa wa Nyuklia miaka ya nyuma. Tofauti na Iran, Israel ilikuwa na msaada wa Marekani kule Iraq.

Rais Obama anayeelekea katika uchaguzi asingependa kuingia katika vita kwasababu vilivyopo vinatosha kuamua hatima yake katika siasa za mambo ya nje. Ameikataza Israel isichukue hatua peke yake kwani hakuna mzozo wa kimataifa utakaoiacha Marekani nje kwani kila mahali kuna maslahi yake.

Suala la vikwazo ni 'serious' na hakuna mzaha katika hilo. Tena kwa bahati mbaya unapokosana na Marekani utakosana na kila mmoja wa NATO na magharibi. Rungu la marekani litakuwa na matawi yatakayoumiza kama rungu lenyewe.

Kwanini Tanzania imeingia katika mzozo huu na nchi za magharibi?
Ni uhalali gani au uharam upi unaotokana na Tanzania kutumia bendera zake kwa meli za Iran?

Itaendelea..........
 
54 Reactions
Reply
Back
Top Bottom