Duru za Siasa: Matokeo ya Uchaguzi Marekani

prof-Wole-Soyinka.jpg

Soyinka fulfils promise, shreds U.S. residency green card and returns to Nigeria - This Is Africa

That's nice, it is a good thing to be a person of your words.

We are still waiting for a long list of celebrities (citizens) who promised to move to Canada and other places to fullfill their promises as well.
 
Inasemwa, ajira 110 zitabaki Indiana na hilo linaonekama kama ushindi kwa kuanzia

Samahani mkuu, ila ni ajira 1100 na sio 110.

Na hili amelifanikisha hata kabla hajaapishwa kwa kupiga simu na kuzungumza na CEO. Rais Obama yupo na viongozi wengine wa serikali yake wapo ila waweshindwa kushawishi US companies kubaki US.
 
Inaendelea
Wakati akiongea kuna mtu alipingana naye. Trump alkerwa na kusema 'wapo wasioamini kuwa HC amepoteza' Kwa kauli hii, akiwa Rais mtarajiwa haikuwa njema.

Alichotakiwa ni kukaa kimya aendelee na hotuba yake.

Masahili kama hayo yalimkuta Obama North Carolina, tofauti na Trump Obama aliwazuia wafuasi wake akiwataka waheshimu haki ya mtu kujieleza

Trump akazungumzia uchumi na biashara akisema atafuta mkataba wa NAFTA ulioasisiwa na Bill Clinton na kupigiwa Debe na Hillary.
Hapa haikuwa sahihi, angezungumzia mkataba bila kuwataja

Kuwataja ni kuamsha hisia kwa kundi analohitaji

Trump akarejea kauli ya ku repeal and replace Obamacare.
Inaonekana kana kwamba kuna nyakati anataka kufanya na nyakati anarudi nyuma

Trumpa akasema atafuta regulations zinazouia ukuaji wa biashara na kazi.

Akaendele kusisitiza kupunguza kodi kutoka 35 hadi 15% kwa makampuni

Katika hoja hii kuna jambo la kuangalia.
George Bush alifuta sheria zilizokwaza kazi na ajiri, na kupunguza kodi
Matokeo yake ni mdodoro wa uchumi mkubwa sana.

Haina maana kaongea jambo baya, angeangalia historia pengine kauli zingekuwa tofauti

Obama alipoingia madarakani wakati wa mdororo wa uchumi alipunguza kodi, matokeo hayakuwa kama ilivyokusudiwa. Pengine Trump ana mtazamo tofauti wenye tija.

Trump akamshambulia Obama kwa kauli za 'viongozi wasiojua wanafanya nini'

Matamshi yake dhidi ya Obama yalikuwa kauli za kampeni bila kujali ni Rais mtarajiwa

Katika siasa za nje, kasema ataimarisha visa kwa wale wanaokwenda Marekani kwa kazi za kitaalam zenye manufaa. Hadi sasa visa hutolewa kwa mtindo huo

Katika immigration, Trump kasema lengo ni kuzuia watu wasiojulikana wanatoka wapi, na wale wanaotoka maeneo 'unsafe'

Trump akatolea mfano wa mauaji ya st Bernadino, Orlando, Paris na WTC

Akasema shambulio la chuoni Ohio ni kutokana na upuuzi wa viongozi wa sasa

Trump akasema ataimarisha jeshi na kupambana na ISIS na ugadia

Hapa ndipo Trump anapoonyesha udhaifu. Kwanza, hadi leo hakuna shambulio kubwa Marekani kutoka nje. Mashambulio au mauaji ni ya watu walioko Marekani.

Kwa mfano,kijana aliyeshambulia Ohio alikuja mdogo na kuwa radicalized na mafunzo ya Alwaki

Pili, ISISI wana ideology hawana makao makuu.
Huko walipo ni ngom, mashambulizi hasa ya Ulaya yanafanywa na lone wolf kwa ushawishi.

Ili kukabliana na hali hiyo, haieleweki anawezaje kuzuia mashambulizi yanayotokana na waliokuwa radicalized ndani ya Marekani. Na je itakapotokea atasema nijni?

Inaendelea

Kama kuna kitu Liberals, progressives na Democrats hawakipendi kuhusu PE Trump ni kwamba Trump anazungumza ukweli bila kusita.

Kwamba kuna watu hawaamini kuwa Hillary ameshindwa, ndio ni kweli na wengi wao (zaidi ya millioni 4) wamejisainisha kwenye tovuti ya change.org ili kuwashawishi Electors wa Rep wakampigie kura Hillary tarehe 19.

Na wengi wao wanaamini watabadilisha matokeo ya PA, MI na WI ili kumpa Hillary ushindi.

PE Trump sio mtu wa kukaa kimya au kwenda kusemea pembeni, penye ukweli anaongea. Speaking the truth is his virtue.

Kuhusu NAFTA, Trump alisema hakuwa na haja ya kutaja walioanzisha au waliotetea NAFTA anachoweza kusema ni kuwa atai-fix au kujiondoa kwenye huo mkataba.

PEOTUS toka mwanzo amesema ata-repeal na ku-replace Obama Care. Kwahiyo kusema kwamba 'amerejea kauli' ni wrong kwa sababu hakuwahi kukanusha kauli yake ya mwanzo. Alichosema ni kwamba ata-keep 2 provisions za ACA.

Hata alivyomteua Secretary wa HHS Tom Price mimi sikushangaa lakini Liberals walishangaa maana walishapindisha maneno ya Trump kuhusiana na Health care plan yake.

Kuhusiana na mabadiliko ya kodi, PE Trump ameangalia historia kwani Reagan (1981-1989) alipunguza kodi na regulations na uchumi ulikua hadi kukawa na budget surplus.

Rais Obama hakupunguza kodi kwa wanaotengeneza ajira, yeye na Hillary waliamini katika kuongeza kodi kwa matajiri na makapuni makubwa bula kujali kuwa hiyo top 1% inaajiri zaidi ya 80% ya watu.

Matokeo ya sera za kodi za Rais yanategemea na namna, wapi na mda anapoongeza au kupunguza kodi.

Rais Obama na Hillary waliamini katika kuongeza regulations lakini wafanya biashara wa Marekani wamekimbia US kwenda kuwekeza katika nchi zingine kwa sababu ya hizo regulations na Trump ameshaanza kuzungumza nao wasiondoke na walio nje warudi wawekeze nyumbani.

Trump hajawahi kupenda kuwa 'politically correct', kwahiyo namna alivyozungumza Cincinnati, Ohio ame-balance wakati wake wa kampeni na yeye kama Pres Elect.

Kuhusu Visa, Trump alikuwa anazungumzia kuanzisha matumizi ya mfumo wa Biometric Visa Exit Tracking kwani Illegals wengi waliopo US ni wale ambao Visa yao imesha-expire na hawataki kurudi kwenye nchi zao. PEOTUS anataka kama mtu mda wako umeisha wa kukaa US na unataka kuendelea kukaa ukaombe tena na sio unaishi US isivyo halali.

Kuhusu shambulio la OSU, Trump aliponda mfumo mbovu uliokumbatiwa na Rais Obama na kutetewa na Hillary wa kuleta wakimbizi US ambao kati yao wengine ni magaidi au wanaweza kubadilika na kuwa magaidi. Kama Extreme Vetting haiwezi kufanyika then ni kusitisha hizo programs. Trump anahitaji wakimbizi wahudumiwe huko huko walipo bila kuwaleta US.

Maofisa wamesema huyo kijana wa Kisomali aliefanya shambulio alikuwa self-radicalized.

Kuhusu mauaji ya ndani, Trump ni mtu anaeamini katika 'Law and Order' na amesema ataondoa criminal gangs na drug cartels katika mitaa hasa inner-cities ili kupunguza murder rates kwenye States kama Illinois na US kwa ujumla.

Kitu cha kwanza atakachokifanya Trump katika kuzuia radical islamic terrorism ni kuzuia kuingiza wakimbikizi kutoka kwenye hot-beds na hilo amelizungumzia. Hao viongozi waliomtangulia walishatengeneza tatizo na mashabiki wao hawaelewi namna gani Trump atakavyolishughulikia hilo tatizo, cha kushangaza hawalaumu waliotengeneza tatizo.
 
Inaendelea

Kuhusu kupambana na ISIS hili nalo kaonyesha udhaifu.
Hadi sasa ISIS wanashambuliwa katika ngome zao.

Kuna uwezakano katika siku zilizobaki Iraq ikakombolewa.
Hoja ya ISIS itahamia Syria na huo utakuwa mtihani kwake kwasababu ya Russia

Trump hajaelewa kuwa dunia inabadilika kila uchao.

Kwa mfano, Obama alipoingia madarakani challenge ilikuwa Alqaeeda.
Alielekeza nguvu zake huko hadi kumpata Osama.

Bila kutarajia, ikazuka Arab spring iliyokuwa'complicated' ku solve kutokana na interest za America na iliyosambaza ISIS zaidi

Hivyo kutumia ISIS pekee bila kujua nini kinaweza kutokea katika dunia ya leo ni jambo litakalomkwaza mbele ya safari.

Litamkwaza kwasababu amesema hata hangaika kuondoa madikteta , anataka amani

Hapa anamaanisha kuwaondoa akina Saddam na Gaddafi ni chanzo cha matatizo
Lakini asiasahu maeneo kama Iran yanaweza kuleta usumbufu kwa US kwa njia nyingine

Hoja ni kuwa kuongelea 'item' na si ujumla wa matatizo litakuwa tatizo kwake

Na pia aliongelea kuunda kamati ya maadili.
Hili la maadili litakwenda sambamba na shughuli zake litamrudi mbele ya safari

Kwa ufupi, ameongea mengi, hayo ni kwa tafsi yetu unayoweza kuwa si sahihi na maoni binafsi

Tutaendelea na sehemu nyingine baadaye

Kuhusu kupambana na ISIS, Trump alishasema hataweka mpango wake wazi na kwamba yeye anaamini katika 'Element of Surprise' , unashambulia ndipo unaita vyombo vya habari na sio kuita vyombo vya habari kuwaambia namna utakavyoshambulia then unaenda kushambulia.

ISIS ni failure ya Rais Obama na Hillary, waliondoa majeshi yao huko Iraq na kutengeneza vacuum waliochipukia. Mwanzoni Rais Obama aliwadharau sana na kuwaita JV (Junior Varsity)Team, hakufikiria kuwa ipo siku wataenea zaidi ya nchi 28.

Trump alisema US haiwezi kupigana na ISIS huku wakipigana na majeshi ya Assad ambayo nayo yanapigana na ISIS.

Sir, Arab Spring iliundwa na sio kwamba ilizuka bila kutarajia. US walikuwa wanachochea moto kila kona ili kuondoa hizo regimes. Ilipofika kwa Assad, kukawa kugumu, miaka ikawa inakatika na hawafanikiwi hadi waka-finance rebels lakini wapi Assad akawa anasaidiwa na Russia.

Trump anaamini kuwa chanzo cha matatizo Libya na Iraq ni kuwaondoa Gaddafi na Saddam. Rais Obama mwenyewe alishasema kosa analojutia ni kumuondoa Gaddafi huko Libya maana Libya imekuwa ni matatizo matupu ukilinganisha na kipindi cha Gaddafi.

Trump hana nia ya kuondoa regimes duniani na anaamini katika ku-get along with Russia. Kwahiyo usitegemee kuwa approach ya Rais Trump itakuwa sawa na ile ya Rais Obama.
 
CHINA/TAIWAN

Kama tulivyosema, simu ya Trump kwa kiongozi wa Taiwan imeleta mjadala mzito katika media
Ni kawaida Rais mteule kuongea na viongozi wa dunia akiwa kipindi cha mpito 'tranistion'

Simu ya Trump kwa kiongozi wa Taiwan si tatizo, tatizo ni suala zima la kidiplomasia
Hilo limepanuka na mjadala kuelekea maeneo ambayo Trump asingependa yaende

Sera ya USni Taiwan ni sehemu ya China. Marekani ina uhusiano wa kidiplomasia na China si Taiwan. Mara ya mwisho kwa kiongozi wa Marekani kumpigia simu kiongozi wa Taiwan ilikuwa 1978

Kuanzia hapo uhusiano wa Taiwan unatambuliwa kupitia China kama Jimbo na si moja kwa moja

Maongezi yote ya kimataifaat least hjulikana na state dept kwa kuwa yana masilahi na US

Hapa ndipo lilipo tatizo halisi, kwamba, Trump amevunja utaratibu wa kidiplomasia na kuongea na kiongozi wa Taiwan kama 'Taifa' katika hali itakayoudhi China na utaratibu uliokuwa nje ya diplomasia

Maongezi ya Trump na kiongozi huyo ynasemwa kuwa ;private' na hapo kuchochea udadisi zaidi.

China wamefuata Diplomasia, badala ya kuongea na Trump, wametuma ujumbe WH kwa Obama kutaka maelezo ya nini kinaendelea kati ya Trump na Taiwan na China kufuatia simu hiyo

Tatizo la Simu ya Trump kwenda Taiwan

1. Trump amevunja sera za Marekani kwa Taiwan/China uliodumu kwa Marais 4, Republican na Democrat na kwa takribani miaka 40. Hii ndiyo hoja na si kwanini ameongea na kiongozi wa nje

2. Endapo anataka kubadilisha sera (policy) dhidi ya China/Taiwan kuna utaratibu

Hii ni pamoja na kusbiri aapishwe kwa mantiki kuwa kuna Rais mmoja kwa wakati mmoja
Mathalan, mzozo wowote wa kidiplomasia utakaozuka sasa hivi , mwenye mzigo ni Obama

3. Trump hakufanya mawasiliano na state dept wala WH.
Imesemwa, walioandaa ni wafanyabiasharaHapa linazuka suala jingine
Je maongezi yalihusu biashara za Trump au masilahi ya Marekani?

Tayari kuna habari Trump aliwahi kuongea na Meya wa Taiwan kuhusu uwekezaji huko
Ndivyo ilivyokuwa kwa Trump na interest za uwekezaji kule Philippine

Matatizo mbele ya Safari

1. Kwasasa WH inapaswa kuijibu China kuhusiana na maongezi. Ni wazi, lazima wapate details za maongezi hayo. Yawe yenye masilahi au binafsi kuna tatizo kwa tranisition team leo au miaka ijayo

2.China itataka kulipa kasi. Kumbuka huu ni uchumi namba 2 duniani na una influence kubwa
a) Utaanzisha trade war na china wanaweza kuleta madhara makubwa US

b) China itatunisha misuli kwa kuunga mkono North Korea. China ni muhimu kwa mzozo wa Korea
Ikiamua kumuunga mkono dogo Kim Jong Un, US na washirika kama Japan, S.Korea wana tatizo

c)Kuna mzozo wa South China Sea. Hadi sasa Philipine imeungana na China. Katika hali ya kutoelewana US ipo katika nafasi ya kupoteza kimasilahi kuliko ilivyo sasa

d)Mzozo wa Kidiplomasia utaunganisha China , Iran , Russia naTurkey inayoelekea mashariki na kuweka umoja wa NATO katika mazingira tata kuliko ilivyo sasa

3. Itakapobainika vinginevyo, washirika wa US hasa Ulaya watakuwa na misimamo yao na si ya pamoja kama nchi za NATO. Ulaya haiwezi kukubali kuingia katika mzozo wa Kidiplomasia uliosababishwa na Trump na si Marekani bila maongezi

Allie wa Marekani watakwenda 'solo' na hilo ni tatizo kubwa kwa uchumi na usalama

4. Hoja ya Blind Trust inayomhusu Trump itapata mashiko zaidi

Tusemezane
Rais wa Taiwan amempigia simu Trump kumpongeza kwa kushinda Urais tayari liberals na democrats wameshaanza kuzungumza mambo mengi ya kuhisihisi.

Hiki ulichoandika hapa ndicho alichokizungumza Anderson Cooper wa CNN umebeba kama kilivyo umeleta huku.

Rais Obama aliwahi kuwa-support waandamaji wa Hong Kong walipotaka kujitenga na China na aliwahi hadi kumualika Dalai Lama wa Tibet White House, cha kushangaza kelele zilipigwa na China na Liberal media za US zilikuwa kimya.

Trump kuzungumza na Rais wa Taiwan kelele zinapigwa na China kama kawaida lakini wakisaidiwa na Liberal media za US ambazo zimekuwa biased kwa Trump kwa mda mrefu, funny
 
"El Jefe, post: 18728496, member: 387168"]Sir, the following statements you quoted are not contradicting each other
Mkuu kwanza, kabla sijaeleza mengi napenda nikufahimishe hakuna mahali nilisema kauli zako zina ji contradict.

Nilitaka reader wawe na record na tafakuri jadidi.

Hoja yako ya awali ni illegal immigrants waliompa popular vote Hillary.
Hakuna ushahidi uliotolewa na waanzilishi wa madai , Trump transition team, au El Jefe.

Hadi hapo ushaihidi utakapowekwa bado yanabaki kuwa madai tu

Uliokuwa unajadiliana na Mag3 kuhusu popular vote, ghafla ukahamia kwa California kama sababu.

Wasomaji hawana sababu za kutafuta unasimamia wapi kila machweo

Ndiyo maana nilitaka wasomaji watafakari nini na wapi hasa unasimamia?

Niliwataka wasomaji kwasababu niliachana na 'kushindana' badala ya kujadiliana

Hivyo ninaongea na wasomaji na hili la ku react kuhusu 'contradictions' ni hisia zako tu.

Hakuna mahali niliposema ume ji contradict, nilichofanya ni kuweka rekodi vizuri

Hisia zimepelekea jazba na kuvamia kila bandiko nililoweweka.

Ulichokifanya ni kuchukua maneno out of context, spin, mislead au fabricate information hata kutafuta spelling error ili uweze kufanya kitu kwa mfano wa 'critic' ambalo umefanya vema since you've nothing more to offer

Kwa minajili ya kuthibitisha upotofu na mengine nitapitia hoja zako zenye mapungufu makubwa moja baada ya nyingine ambazo zinazoweza kuwasumbua wasomaji .

Hili nitalifanya kwa faida ya wasomaji kwasababu sina interest ya kujibizana nawe bali nina interest ya kujifunza na kuchangia kidogo nilicho nacho na wengine weledi
 
The study that came up with a 3 million illegals figure was a nationwide study, not specific to any state.
The study can be discredited by many but it may not necessarily mean it is wrong.

Pew Research conducted their own study and found out that approximately 24 million (1 in 8) voter registrations in the US are no longer valid or are significantly inaccurate.

Ignoring these irregularities, we have the election results the way it is. The last quote is my statements with regards to the election results in its current form.
Wasomaji , Uchaguzi umekwisha wiki tatu zilizopita

Hoja hii surrogates wa Trump waliulizwa waithibitishe kwa facts na research. Hakuna aliyeweza

Walichoweza kusema ni research za nyuma na moja ikiwa ni ile ya 2005

Kama kuna msomaji mwenye taasisi iliyofanya research au yenye uhakiki wa madai haya katika uchaguzi wa 2016 ili atusaidie jina la taasisi na mwaka au muda utafiti ulipofanyika
 
Samahani mkuu, ila ni ajira 1100 na sio 110.

Na hili amelifanikisha hata kabla hajaapishwa kwa kupiga simu na kuzungumza na CEO. Rais Obama yupo na viongozi wengine wa serikali yake wapo ila waweshindwa kushawishi US companies kubaki US.
Ndugu wasomaji, Rais Reagan alipoingia WH hakuongea na CEO's wa makampuni
Alipoondoka hali ya uchumi ilikuwa nzuri na kufanya kile kinchoitwa Regan Republican

Rais Bush snr akiingia WH hakuzungumza na CEOs wa makampuni. Ha ali ya uchumi ikayumba

Rais Bill Clinton akiingia WH hakuzungumza na CEOs, alipoondoka aliacha ajira takribani 15M
Aliacha US ikiwa na surplus

Bush Jnr hakuongea na CEOs kwa bahati mbaya akiondoka aliacha nchi na recessio tunayojua
Watu walipoteza kazi katika kiwango cha malaki, masoko kupoteza thamani na deni la Taifa

Bush aliacha vita mbili zikiendelea Iraq na iran

Obama alipoingia WH alikuwa na challenge nyingi na hakuongea na CEOs hadharani.
Kwanza, kuzuia 'bleeding' ya jobs, Pili, kufanya jitiihada kama za ku bail makmpuni
Tatu kusimamia majukumu mengi ya vita zilizokuwa zinaendelea alizorithi

Kuokoa makampuni kama GM kulisaidia na kuokoa ajira kwa maelfu.
Obama alikuwa na kazi ya kutoa nchi katika negative growth, akiwa na unemployment takribani 9, na kupoteza ajira kwa kiwango cha laki kwa mwezi

Economy recovery inaonekana arguably slow lakini si negative.
Kwa mieizi 74 kwa mujibu wa Bureau of stat mfululizo serikali yake imentengeneza ajira, haikupoteza

Infalation rate imeshuka na kufikia 4.6% kwa mujibu wa takwimu

Mwezi wa 11 ajira zilizotengenezwa kwa mujibu wa stat ni 178,000

Katika mazingira hayo, hatuwezi kubeza mafanikio na mapungufu ya kila kiongozi.
Ni makosa kuchukulia deal ya Carrier kama mafanikio makubwa ya uchumi katika wiki 3 si sahihi

Ajira 178,000 tukizigawa kwa siku 30 na kwa minajili ya mjadala huu ni sawa na ajira takribani 6,000 kwa siku. Kwa maneno mengine katika siku 7 ni sawa na ajira 42,000!

Mfano huu unaonyesha kila mmoja ana njia za kutawala kama tulivyoona mlolongo wa Marais

Surrogates wa Trump wanadai Obama hakuongea na CEOs, hivi ni lazima kufanya hivyo?

Surrogates hao hawawelezi kingine chochote wakijua wapo watu watabeba tu kama yule mama wa NC aliyeulizwa na bado anaamini Obama hakuzaliwa Marekani.

Watu wa aina hiyo wamesambaa duniani. Watabebe sentensi kama walivyosikia bila kuangalia kingine
 
Kuhusu NAFTA, Trump alisema hakuwa na haja ya kutaja walioanzisha au waliotetea NAFTA anachoweza kusema ni kuwa atai-fix au kujiondoa kwenye huo mkataba..
Wasomaji, katika bandiko la awali tulisema upotoshaji unapita kiwango na kuchukua sura ya upuuzi! samahani kwa kukosa neno mbadala na nilo

Jana nilieleza kuhusu mkutano wa Trump Ohio nikanukuu maneno yake kuhusu NAFTA

Alisema kuwa ' ...sasa haogopi kusema NAFTA ilianzishwa na Bill na kuungwa mkono na Hillary''

Hoja yetu haikuwa NAFTA, tulisema, katika wakati huu kuwataja akina Clinton ni kuamsha hisia za wafuasi wake. Kwa mgawanyiko uliopo haikuwa sahihi, kazi ya kuuunganisha Taifa itakuwa ngumu

Sikiliza video hii chini kuanzia dakika ya 34 hadi 36 Trump akisema maneno, akiwataja akina Clinton na kuita NAFTA disaster. Akasema ataifuta au fix.

Sikiliza dakika hizo halafu usome nukuu hapo juu uone upotosha wa hali ya juu

Nina shaka comprehensions ipo katika mitaala na kama watu wanajua maana yake ni nini.

Kuandika ni jambo moja, kuelewa kilichosemwa ni jambo jingine na kuwakilisha ni kitu kingine.

Kuondoa maneno katika sentensi ni kupoteza maana, kubadili maneno ni kupoteza maana

Inafika mahali mjadala unavurgwa bila sababu za maana.

Mtu anabadili sentensi ili kukidhi haja bila kujali wanaofuatilia na wenye hamu ya kutaka habari zaidi

Inasikitisha
 
ISIS ni failure ya Rais Obama na Hillary, waliondoa majeshi yao huko Iraq na kutengeneza vacuum waliochipukia. Mwanzoni Rais Obama aliwadharau sana na kuwaita JV (Junior Varsity)Team, hakufikiria kuwa ipo siku wataenea zaidi ya nchi 28.
Wasomaji, wengi wanadhani ISIS ilianza kwa Obama na Hillary. ISIS ilikuwepo wakati wa Bush ndipo neno caliphate lilipoanza kusika.

Caliphate kwa kiswahili ni Khalifa, kwahiyo ISIS walitaka'utawala wa Khalifa' na waislam wanaelewa kwa undani historia na maana nzima ya dhana hiyo.

ISIS ilikuwepo katika mtindo wa Alqaeda in Iraq wakati wa AlZakhawi. Kama mnafuatilia mijadala hapa duru za siasa , tulijadili kuhusu Alqaeda in Iraq na jinsi wanavyosigishana na Alqaeda wenyewe
Ndipo wakaijiunga akina Al Alwaki bila kujua wanatokea kundi gani

Arab Spring na kuondolewa kwa akina Saddam na Gaddafi kukatoa mwanya kwa ISIS kustawi na kujiimarisha ikiwa na identity yake. Ndipo ilipofahamika wazi kuwa Alqaeda in Iraq ndiyo ISIS

Kama mtakumbuka kulikuwa na mgogoro kati ya Obama adm na baadhi ya maseneta kwa McCain waliotaka waasi wa Syria wapewa silaha. Intelejensia ya vyombo vyote ilihoji kuhusu kundi hilo la Syria na ilijua wazi si kundi dhidi ya Assad bali mchanganyiko

Ombwe la kuondolewa akina Saddam liliacha Iraq katika 'anarchy' na ISIS wakaweka makao huku wakiendelea na mashmbulio Syria na kwingine

Trump alisema Obama na Hillary ndio waliotengeneza ISIS kwa kuondoa majeshi mapema

Hoja hii ilitua vema kwa baadhi wasiotaka kupata undani kuhusu suala zima

Obama na wachambuzi wote wa habari walitafuta facts kutokana na madai ya Trump
1. Si kweli kuwa ISIS ilianza wakati wa Obama, ilikuwepo kuanzia wakati wa Bush.
2. Si kweli kuwa Obama aliondoa majeshi mapema, majeshi yalianza ondoka wakati wa Bush

Hoja hizo zilipowekwa hadharani si Trump au mwingine aliyepinga, hoja ikafikia mwisho

Trump aliendelea kuitumia kwa njia nyingine kama kuenea kwa ISIS akitambua katika 'watu' wake wapo watakaobaki na utata alioanzisha, na kwa hilo mnaweza ona alivyofanikiwa
 
Rais wa Taiwan amempigia simu Trump kumpongeza kwa kushinda Urais tayari liberals na democrats wameshaanza kuzungumza mambo mengi ya kuhisihisi.

Hiki ulichoandika hapa ndicho alichokizungumza Anderson Cooper wa CNN umebeba kama kilivyo umeleta huku.

Rais Obama aliwahi kuwa-support waandamaji wa Hong Kong walipotaka kujitenga na China na aliwahi hadi kumualika Dalai Lama wa Tibet White House, cha kushangaza kelele zilipigwa na China na Liberal media za US zilikuwa kimya.

Trump kuzungumza na Rais wa Taiwan kelele zinapigwa na China kama kawaida lakini wakisaidiwa na Liberal media za US ambazo zimekuwa biased kwa Trump kwa mda mrefu, funny
Wasomaji, kitu kama hik ni Anachronism!

Tulieleza kwa Rais Mteule hana tatizo kuongea na Marais wa nchi za nje.

Obama na viongozi waliofuata huo ni kama utamaduni wao.

Wiki iliyopita kabla ya hiyo simu tulisema safari hii Trump kavunja mwiko (si sheria kumbuka) kwamba Rais wa US huongea na ally kama UK kwanza

Safari hii May kawa wa 14 akitanguliwa na Nigel Farage.
Hakuna tatizo wala mpangilio bali ni utamaduni tu ambao ni tofauti.

Tukasema kilichotokea si tatizo la simu wala kuongea, ni kinyume na sera ya Marekani ya 'one China policy' tangu China ilipopata kiti UN na Mzee Salim Ahmed Salim analijua hili vema sana

Tatizo la simu ni kuwa US haina uhusiano wa diplomasia wa moja kwa moja na Taiwan kutokana na hali ya kisiasa ambayo China huona Taiwan ni jimbo na si nchi.

Hivyo maongezi hayo yatazua kile tulichosema ni diplomatic row kati ya China na US

Maongezi si lazima yasimamiwe na state dept lakini kwa hali ilivyokuwa ingalikuwa vema state dept ikawa na taarifa kwasababu US wana Rais mmoja kwa wakati na mzozo wowote utaleta taabu kwa serikali iliyopo madarakani. Kama Trump anataka kubadili policy, angesubiri aapishwe

Maneno hayo hayakupita bure, asubuhi na mapema China wakawa wamewasiliana na WH kujua kuhusu suala hilo. China hawakumjibu Trump kwasababu yeye ni mtarajiwa, serikali ipo kwa Obama

Na wala China hawakuzozona na Taiwani hadharani kwasababu mzozo ni wa kidiplomasia

Tukaendelea kusema, mbele ya safari hili litakuwa tatizo kwa Marekani

1. Litazua' trade war' isiyo na ulazima wakati huu recovery ikeiendelea na ku derail focus
2. Itaisukuma China kumuunga mkono N.Korea kama kulipa kisasi na udhibiti wa utakuwa tatizo
3. Kuna mzozo wa South China sea ambao utazidi kupanuka
Kwa hili tukaeleza kuhusu ushiriki wa Philipine na Rais wao alivyobadilika

4. Tukasema nchi za Russia, Turkey, China, Iran n.k. zitaungana dhidi ya US na kuleta matatizo

5. Tukasema washirika wa US ulaya wataamua kwenda 'solo' kwasababu US inakwenda solo

Hivi ndivyo tulivyoliangalia suala hili kwa mtazamo wetu na si suala la simu nani kapiga nani kapigiwa

Ni matatizo yanayoweza kujitokeza kutokana na simu ikiwemo diplomatic row kati ya US, China na mataifa mengine kwa kujua ukubwa na umuhimu wa US katika siasa za dunia

Kwa hayo 5 hapo juu tunaweza kufafanua mjadala na kufikia kurasa 50 kupata uelewa wenzetu wanafikiria nini , wanafanya nini na inaweza kutuathiri vipi.

Ndio mjadala si suala la conservative , liberal wanasema au simu just simple

Kwanini kuna competition ya east na west kuelekea Afrika?

Tunawezaje ku ignore hayo wakati US ni mkubwa wa dunia na mbabe, halafu China ni namba 2?

Chukua mfano, hoja ya 4.

Russia, Turkey, Iran, China zikitengeneza alliance, Europe na NATO itakuwa katika hali gani?

Israel itakuwa katika hali gani wakati huu inapoiangalia Iran kama tishio na wakati Iran ikiwa na washirika? Je, Trump atabadili policy ya US dhidi ya Israel?

Wasomaji, mtuelewe tunaangalia kutoka angle tofauti na ndio utamaduni wa jamvi hili
Tutaulinda tamaduni huu licha ya jitihada za kutaka kuvuruga heshima ya jamvi hili

Tusemezane
 
Wasomaji, katika bandiko la awali tulisema upotoshaji unapita kiwango na kuchukua sura ya upuuzi! samahani kwa kukosa neno mbadala na nilo

Jana nilieleza kuhusu mkutano wa Trump Ohio nikanukuu maneno yake kuhusu NAFTA

Alisema kuwa ' ...sasa haogopi kusema NAFTA ilianzishwa na Bill na kuungwa mkono na Hillary''

Hoja yetu haikuwa NAFTA, tulisema, katika wakati huu kuwataja akina Clinton ni kuamsha hisia za wafuasi wake. Kwa mgawanyiko uliopo haikuwa sahihi, kazi ya kuuunganisha Taifa itakuwa ngumu

Sikiliza video hii chini kuanzia dakika ya 34 hadi 36 Trump akisema maneno, akiwataja akina Clinton na kuita NAFTA disaster. Akasema ataifuta au fix.

Sikiliza dakika hizo halafu usome nukuu hapo juu uone upotosha wa hali ya juu

Nina shaka comprehensions ipo katika mitaala na kama watu wanajua maana yake ni nini.

Kuandika ni jambo moja, kuelewa kilichosemwa ni jambo jingine na kuwakilisha ni kitu kingine.

Kuondoa maneno katika sentensi ni kupoteza maana, kubadili maneno ni kupoteza maana

Inafika mahali mjadala unavurgwa bila sababu za maana.

Mtu anabadili sentensi ili kukidhi haja bila kujali wanaofuatilia na wenye hamu ya kutaka habari zaidi

Inasikitisha

Mkuu, ukimsikiliza PEOTUS katika hizo dakika alisema:

"Now I don't have to say it was started by Bill Clinton and approved by Hillary, who cares? All I can tell you is that NAFTA is a disaster, what difference does it make?. We will fix NAFTA or we'll terminate it and start all over again"

Sasa hiyo "Haogopi kusema" umeitoa wapi mkuu? .Jaribu kuwa makini hapa umekosea.

Kutafsiri nukuu ya kiingereza kwenda Kiswahili inaweza kuwa ni tatizo kwako lakini kama inapelekea kubadilisha maana ya sentensi za mtu ni tatizo kubwa. Labda ndio maana umenukuu kwa kiswahili badala ya lugha iliyotumika.

Kingine, ukisikiliza point yake yote huwezi ku-argue kuwa amekosea kuwataja. Lakini umechukulia kutaja majina kama ndicho kitu kikubwa na ukasahau ujumbe mzima ya PE Trump kwa wananchi.

Ujumbe wenyewe ni kuwa atairekebisha NAFTA au atajitoa na kuanza upya.

Kwa namna alivyowataja Clintons katika kuelezea ujumbe wake kuhusiana na NAFTA haiathiri juhudi zake za kuunganisha watu.
 
Hoja hii surrogates wa Trump waliulizwa waithibitishe kwa facts na research. Hakuna aliyeweza
Nilisema, PE Trump alikuwa anaelezea concerns zake na huu utakuwa mwanzo wa kuangalia namna ya kuhakikisha kuwa hakuna illegals wanaopiga kura US na kwamba wanaopiga kuwa wote wanakuwa valid na accurate.
 
Ndugu wasomaji, Rais Reagan alipoingia WH hakuongea na CEO's wa makampuni
Alipoondoka hali ya uchumi ilikuwa nzuri na kufanya kile kinchoitwa Regan Republican

Rais Bush snr akiingia WH hakuzungumza na CEOs wa makampuni. Ha ali ya uchumi ikayumba

Rais Bill Clinton akiingia WH hakuzungumza na CEOs, alipoondoka aliacha ajira takribani 15M
Aliacha US ikiwa na surplus

Bush Jnr hakuongea na CEOs kwa bahati mbaya akiondoka aliacha nchi na recessio tunayojua
Watu walipoteza kazi katika kiwango cha malaki, masoko kupoteza thamani na deni la Taifa

Bush aliacha vita mbili zikiendelea Iraq na iran

Obama alipoingia WH alikuwa na challenge nyingi na hakuongea na CEOs hadharani.
Kwanza, kuzuia 'bleeding' ya jobs, Pili, kufanya jitiihada kama za ku bail makmpuni
Tatu kusimamia majukumu mengi ya vita zilizokuwa zinaendelea alizorithi

Kuokoa makampuni kama GM kulisaidia na kuokoa ajira kwa maelfu.
Obama alikuwa na kazi ya kutoa nchi katika negative growth, akiwa na unemployment takribani 9, na kupoteza ajira kwa kiwango cha laki kwa mwezi

Economy recovery inaonekana arguably slow lakini si negative.
Kwa mieizi 74 kwa mujibu wa Bureau of stat mfululizo serikali yake imentengeneza ajira, haikupoteza

Infalation rate imeshuka na kufikia 4.6% kwa mujibu wa takwimu

Mwezi wa 11 ajira zilizotengenezwa kwa mujibu wa stat ni 178,000

Katika mazingira hayo, hatuwezi kubeza mafanikio na mapungufu ya kila kiongozi.
Ni makosa kuchukulia deal ya Carrier kama mafanikio makubwa ya uchumi katika wiki 3 si sahihi

Ajira 178,000 tukizigawa kwa siku 30 na kwa minajili ya mjadala huu ni sawa na ajira takribani 6,000 kwa siku. Kwa maneno mengine katika siku 7 ni sawa na ajira 42,000!

Mfano huu unaonyesha kila mmoja ana njia za kutawala kama tulivyoona mlolongo wa Marais

Surrogates wa Trump wanadai Obama hakuongea na CEOs, hivi ni lazima kufanya hivyo?

Surrogates hao hawawelezi kingine chochote wakijua wapo watu watabeba tu kama yule mama wa NC aliyeulizwa na bado anaamini Obama hakuzaliwa Marekani.

Watu wa aina hiyo wamesambaa duniani. Watabebe sentensi kama walivyosikia bila kuangalia kingine

Kama Rais yupo na anashindwa kuokoa ajira 1,100 zinazoenda Mexico, unadhani wafanyakazi na Raia wanamuonaje?

Kwa sababu kuna ajira 178,000 ziliongezeka kwa mwezi Nov 2016, kwahiyo ajira 1,100 ni insignificant!. Unajua kampuni ngapi na ajira ngapi zimeondoka US katika kipindi cha Rais Obama?

PEOTUS aliwapa Carrier Corp. deal ya $7 million (State tax breaks na kupunguzwa kwa regulations kwa kipindi cha miaka 10) na wakakubali kubaki Indianapolis, Indiana. Ila alianza kwa kuinua simu yake na kumpigia CEO wa Carrier Corp.

Hamna aliyechukulia deal ya Carrier kama mafanikio makubwa ya uchumi katika wiki 3, PEOTUS alisema huo ni mwanzo tu.

Hebu angalia hizi indicators katika kipindi cha Rais Obama:

(i)Median Household income: Flat

2009 = $56,746
2015 = $55,775

(ii) Wamarekani walio kwenye food stamps ( Supplemental Nutrition Assistance Program - SNAP):

2009 = 31.90 Million
2016 = 41 Million

(iii) Labour participation rate: 37-year low

Jan 2009 = 65.7%
Nov 2016 = 62.7%
(Watu zaidi ya million 93 hawana ajira au/na wameacha kuzitafuta kwa sababu hazipo)

(iv) Wamarekani maskini:

2009 = 39.82 Million
2016 = 45 Million

(v) Home Ownership rate: Flat

4Q 2008 = 67.5%
3Q 2016 = 63.5%

(vi) US National Debt :

Jan 2009 = $ 10.62 Trillion
Dec 2016 = $ 20 Trillion

Economic recovery chini ya Rais Obama ndio the worst since the Great Depression.

Kampuni za US zina $ 2.1 Trillion nchi za nje na wanashindwa kuzirudisha US kwa sababu ya kodi kubwa.

Rais Obama amefeli kiuchumi, kisiasa na kijamii. Nitaelezea alivyofeli kisiasa na kijamii.
 
Wasomaji, kitu kama hik ni Anachronism!

Tulieleza kwa Rais Mteule hana tatizo kuongea na Marais wa nchi za nje.

Obama na viongozi waliofuata huo ni kama utamaduni wao.

Wiki iliyopita kabla ya hiyo simu tulisema safari hii Trump kavunja mwiko (si sheria kumbuka) kwamba Rais wa US huongea na ally kama UK kwanza

Safari hii May kawa wa 14 akitanguliwa na Nigel Farage.
Hakuna tatizo wala mpangilio bali ni utamaduni tu ambao ni tofauti.

Tukasema kilichotokea si tatizo la simu wala kuongea, ni kinyume na sera ya Marekani ya 'one China policy' tangu China ilipopata kiti UN na Mzee Salim Ahmed Salim analijua hili vema sana

Tatizo la simu ni kuwa US haina uhusiano wa diplomasia wa moja kwa moja na Taiwan kutokana na hali ya kisiasa ambayo China huona Taiwan ni jimbo na si nchi.

Hivyo maongezi hayo yatazua kile tulichosema ni diplomatic row kati ya China na US

Maongezi si lazima yasimamiwe na state dept lakini kwa hali ilivyokuwa ingalikuwa vema state dept ikawa na taarifa kwasababu US wana Rais mmoja kwa wakati na mzozo wowote utaleta taabu kwa serikali iliyopo madarakani. Kama Trump anataka kubadili policy, angesubiri aapishwe

Maneno hayo hayakupita bure, asubuhi na mapema China wakawa wamewasiliana na WH kujua kuhusu suala hilo. China hawakumjibu Trump kwasababu yeye ni mtarajiwa, serikali ipo kwa Obama

Na wala China hawakuzozona na Taiwani hadharani kwasababu mzozo ni wa kidiplomasia

Tukaendelea kusema, mbele ya safari hili litakuwa tatizo kwa Marekani

1. Litazua' trade war' isiyo na ulazima wakati huu recovery ikeiendelea na ku derail focus
2. Itaisukuma China kumuunga mkono N.Korea kama kulipa kisasi na udhibiti wa utakuwa tatizo
3. Kuna mzozo wa South China sea ambao utazidi kupanuka
Kwa hili tukaeleza kuhusu ushiriki wa Philipine na Rais wao alivyobadilika

4. Tukasema nchi za Russia, Turkey, China, Iran n.k. zitaungana dhidi ya US na kuleta matatizo

5. Tukasema washirika wa US ulaya wataamua kwenda 'solo' kwasababu US inakwenda solo

Hivi ndivyo tulivyoliangalia suala hili kwa mtazamo wetu na si suala la simu nani kapiga nani kapigiwa

Ni matatizo yanayoweza kujitokeza kutokana na simu ikiwemo diplomatic row kati ya US, China na mataifa mengine kwa kujua ukubwa na umuhimu wa US katika siasa za dunia

Kwa hayo 5 hapo juu tunaweza kufafanua mjadala na kufikia kurasa 50 kupata uelewa wenzetu wanafikiria nini , wanafanya nini na inaweza kutuathiri vipi.

Ndio mjadala si suala la conservative , liberal wanasema au simu just simple

Kwanini kuna competition ya east na west kuelekea Afrika?

Tunawezaje ku ignore hayo wakati US ni mkubwa wa dunia na mbabe, halafu China ni namba 2?

Chukua mfano, hoja ya 4.

Russia, Turkey, Iran, China zikitengeneza alliance, Europe na NATO itakuwa katika hali gani?

Israel itakuwa katika hali gani wakati huu inapoiangalia Iran kama tishio na wakati Iran ikiwa na washirika? Je, Trump atabadili policy ya US dhidi ya Israel?

Wasomaji, mtuelewe tunaangalia kutoka angle tofauti na ndio utamaduni wa jamvi hili
Tutaulinda tamaduni huu licha ya jitihada za kutaka kuvuruga heshima ya jamvi hili

Tusemezane
Rais Obama alivyomkaribisha Dalai Lama (Tibet's spiritual Leader) White House unaweza kusema alikosea?
 
Obama na wachambuzi wote wa habari walitafuta facts kutokana na madai ya Trump
1. Si kweli kuwa ISIS ilianza wakati wa Obama, ilikuwepo kuanzia wakati wa Bush.
2. Si kweli kuwa Obama aliondoa majeshi mapema, majeshi yalianza ondoka wakati wa Bush

Hoja hizo zilipowekwa hadharani si Trump au mwingine aliyepinga, hoja ikafikia mwisho

Trump aliendelea kuitumia kwa njia nyingine kama kuenea kwa ISIS akitambua katika 'watu' wake wapo watakaobaki na utata alioanzisha, na kwa hilo mnaweza ona alivyofanikiwa

Hebu please tupe reference/ushahidi wa hiyo argument yako kuwa 'hoja ilifika mwisho'

Hoja ambayo haipingwi ni kuwa kuondoa majeshi Iraq kulitengeneza 'vacuum' ambayo ISIS ikaitumia kuchipukia na kuenea nchi zaidi ya 28.

Sio kweli kwamba Rais Obama aliwaita ISIS kuwa ni JV team?

1. Katika kipindi cha Rais Bush, ISIS ilikuwa katika nchi ngapi na leo hii ipo katika nchi ngapi?

2. Kama Rais Bush alikuwa anaondoa majeshi Iraq, Rais Obama angezunguka kwenye Kampeni mwaka 2008 kuwahubiria wananchi kuwa wamchague kwa sababu ataondoa majeshi ya US Iraq?

Mgombea unaemkubali Hillary alidai atapitisha no-fly zone Syria, akaulizwa, iwapo Russia itapitisha ndege zake kwenye anga la Syria (Russia wameruhusiwa na Assad kurusha ndege zake Syria) atazishambulia? Unakumbuka jibu lake?
 
Gen Petreus

Mkuu JokaKuu kuna bandiko ulidokeza kashfa inayomkabili Petreus

Huyu ni mmoja wa wanaofikiriwa katika nafasi ya sec of state

Katika orodha hiyo wapo akina Romney na Rudy.

Kwa taarifa za leo za washauri wa tranistion team orodha imeongezeka, sasa yupo Jon Huntsman aliyekuwa balozi nchini China na mwingine ni Gavana wa Utah

Kwa Gen Pet, anakiri makosa ya kutoa 'sensitive info' za nchi kwa kimada

Uwezekano wa Gen kuwa SoS utapima utengamano wa 'the establishment' na Trump

Confirmation yake katika seneti inayoongozwa na Republican itakuwa na utata .
Kwamba, tofauti ya scandal za Clinton na Petrus ni ipi?

Hapa kuna sura mbili, kwanza, kuonyesha unafiki uliofanyika na pili kuhoji Rep senate

SoS inaonekana kuwa test kubwa kwa Trump

Kumwacha Romney kwa 'feud' ,Trump ataonekana ame surrender kwa loyalist

Litaamsha hisia kwa 'the estab' na watajibu mapigo kupitia congress au Senate

Kumteua Rudy kuna utata kutokana na conflict of interest zake katika business kutamweka Trump katika hali kama ya Gen Petreus mbele ya senate.

Definite Dem wataleta hoja, kumuondoa Rudy ni kupingana na inner circle ya loyalist

Kuleta outsider kama Jon Huntsman kutazua manung'uniko kwa loyalist na kisasi kwa the estb
 
TRUMP AKUTANA NA AL GORE!

Moja ya sifa wasizoelewa wengi ni Trump mfanyabiashara anayekutana na watu wa aina mbali mbali
Ni katika hilo biashara zake zimebeba mafanikio sana, upande mwingine zikiwa na ukungu

Ni mtu anayeweza kucheza na akili za watu, anajua kusoma mawazokwa urahisi
Ndivyo alivyoweza kuwashinda wenzake katika primaries na uchaguzi mkuu

Katika mahojiano na NY post, Trump alieleza nia ya kutoendelea na 'mashtaka' dhidi ya Clinton

Alisema, Clintons wamepita katika wakati mgumu na asingependa kuendeleza jambo hilo

Kauli ya lock her up ilichagiza kampeni zake. Akiwa Ohio wafuasi wake walilipuka jina la Clinton lilipotajwa kwa kauli za Lock her up.

Trump alielewa halikuwa jambo sahihi, na alisema '...by the way many people are outside still coming in....' Hapo akabadili maoengezi.

Wiki mbili zilizopita kulikuwa na taarifa zikihusisha mtafaruku ndani ya timu yake.
Trump akashikilia suala la 'Hamilton' hata VP aliposema hakuona tatizo wala haja ya kujadili.
Trump aliondoa watu na kuwaelekeza anakotaka, akiendelea na tweets za suala hilo bila sababu

Juzi baada ya simu ya Taiwan, imekuwa habari na kwa sehemu kubwa ilivuruga taswira yake

Suala siyo simu bali kukiuka sera ya miaka 40 ya Marekani kuhusu one china Policy
Pili, kwenda kinyume na utaratibu wa Rais mmoja kwa wakati mmoja

Jambo la kwanza alilofanya ni uteuzi wa Ben Carson kama Secretary.
Hilo halikuonekana kupunguza makali ya mjadala wa Taiwan.

Leo kamwalika Democrat Al Gore kujadiliana naye masuala ya mazingira 'environment'

Trump anayeamini mazingira ni hoax ya china, siasa za mazingira zinavyoharibu ajira leo anajadili suala hilo na Al Gore! Uchaguzi wote Trump hakukubali tatizo la mazingira, leo anatambua!

Akiwa Ohio, aliwaambia wafuasi makaa yatachimbwa, na 'fracking' ya mafuta itaendelea

Mkutano na Al Gore ulilenga kuondoa hoja ya Taiwan na kwa kiasi amefanikiwa

Tatizo, njia hizi zina muda. Akiingia oval office kila sentensi itachunguzwa na kuwa rekodi

Akapokutana na vyombo vya habari hasa vya kimataifa kama Rais itakuwa ngumu kuelekeza mjadala

Mapambano na vyombo vya habari yatamweka pabaya na njia za mkato hazina mwisho mzuri. Oval office ni ofisi ya Taifa kubwa lenye nguvu.!!!

Tusemezane
 
Trump aongea

Katika ziara za ''shukrani'' mteule Trump amezungumza leo North Carolina
Hakuna jipya sana kama ulifuatilia hotuba yake ya Ohio, lakini yapo machache yaliyojitokeza

Kwanza, alionekana kuwa makini dhidi ya waliokuwa wapinzani wake.
Ni mara chache tu alipoondoka katika hoja zake akizungumzia alivyoshinda.
Kaondoka katika hoja kwasababu yeye ni mteule

Pili, ameongelea kuleta umoja wa kitaifa na kuna kila dalili mgawanyiko uliopo unamtisha

Kwa mantiki, Trump anaelewa nguvu yake ipo kwa wananchi si house au senate
Na anaanza kuhisi ukubwa wa tatizo la mgawanyiko kutokana na uchaguzi

Kubwa aliloongea ni US kujenga jeshi akisema ni kwa utayari si mashambulizi
Kwa hilo amemteua rasmi Gen Mattis kama Sec of defense akimwacha Gen Flynn

Trump anasema jeshi halitasambaa na hataondoa tawala dhalimu mashariki ya kati
Kauli hizi zinathibitisha zile alizosema ataondoa majeshinje na kuhusu NATO

Trump alipojichanganya ni aliposema, majeshi yatakuwepo maeneo yenye masilahi
Hakuna Rais aliyepeleka majeshi katika eneo lisilo na masilahi na Marekani

Marekani ni Taifa lenye nguvu, na nguvu zinatokana na 'ubabe' wa kulinda masilah

Rais Obama alisema ' katika mambo aliyojifunza akiwa Rais ni kuwa hakufuata au kutafuta matatizo, inatokea matatizo yanakuja mezani hata kama hakupenda''

Trump anaposema hataondoa tawala dhalimu, maana yake ni kutojishughulisha na mambo mengine yanayogusa dunia na Marekani kwa ujumla.

Kwa mfano, Alqaeda wakiweka makazi Mali , muathirika si Tanzania au Uganda.

Bush alikwenda vitani kwa taarifa za vyombo vya usalama, shambulio la 9/11 lilipangwa nje ya Marekani. Huo ulikuwa mwendelezo wa mashambulizi mengine yaliyotangulia

Je, Trump atakaa kimya North Korea akiendelea na mipango ya silaha za Nyuklia?
Atakaa kimya mkataba wa Iran uingie matatani ambapo Israel ina masilahi?
Trump atakuwa wapi Russia ikijitanua na kutishia washirika wa NATO Ulaya?

Trump anasema atawashinda ISIS walipo. Atafikaje huko kama hao ISIS wanahifadhiwa na tawala dhalimu? Mfano wa hili ni Afghanistan na Taliban, au Somalia au Mali n.k.

Na katika kile kinachoonekana kama 'pre preemptive strategy' leo Obama ameongelea maendeleo ya vita dhidi ya ISIS akisema 2/3 ya maeneo walioshikilia yamekombolewa.

Je, Trump atakaposhauriwa na security agencies kuhusu tishio atakataa ushauri huo?
Bill Clinton alishauriwa kuhusu Osama aliyekuwa kwenye radar, akakataa shambulio.

Matokeo yake gharama hizo alizilipa Bush. Obama hakuchukua chance hata ilipoonkena ni hatari kwa kwake kurudi madarakani kama ilivyokuwa kwa Jimmy Carter na Iran

Trump ana mitazamo yake ambayo si lazima iwe sahihi au yenye makosa, kitu kimoja kinachoonekana, siasa za dunia inayobadilika kila uchao ni ngeni kwake.

Challenges alizokutana nazo Reagan sio alizokutana nazo Bush sr au Clinton au Busha na Obama.

Tusemezane
 
'RUSSIA HACKING'

Wiki hii imetawaliwa na habari kadha wa kadha. Kwanza, katika transition ya Trump Rudy Gullian na Chris Christie wameondolewa katika nafasi ya SoS. Guillian hatakuwa katika cabinet kabisa

Ni pigo kwa loyalist wanaoona kusalitiliwa. Rudy anaonekana kama risk katika senate confirmation kutokana na interest zake za kibiashara na Qatar, Venezuela n.k. kama iClinton foundation

Mitt bado yupo ingawa fursa yake inazibwa kwa kuondolewa loyalist.
Kumteua Mitt kutazusha hasira kubwa kwa loyalist ambao tayari wanaona kuwa sidelined

Katika kupeusha mzozo wa SoS Trump anamfikiria CEO wa Exxon Mobil, Rex Tillerson
Tatizo la CEO huyo ni mahusiano yake na Russia na Rais Putin

Ikitokea Mitt kuachwa SoS, Gavana atakuwa amedhalilika sana.
Hasira hizo zitambana Trump katika seneti ambako the establishment wapo.

HACKING
Habari nyingine ni hacking kutoka Russia. Wiki hii Obama aliagiza vyombo vifanye uchunguzi

Zipo taarifa za intelligence community kuhusisha Russia na interference ya uchaguzi wa Marekani

Maseneta 4, wawili kila chama wametengeneza Bipartisan letter ya uchunguzi wa kina ufanyike
Trump na kampeni yake wanapinga suala wakisema suala halitabadili matokeo ya uchaguzi

Hapa kuna hoja mbili za kuelewa

Trump na transition wanasema hizi ni mbinu za kutaka kuondoa uhalali wa ushindi na Urais wake
Maseneta wanasema ni suala la kuchunguzwa na si kubadili matokeo kwanini nchi za kigeni ziingilie

Utata
Kwavile uchunguzi unataka kubaini kama kuna mataifa ya nje yanayoingilia uchaguzi wa Marekani, na kwavile WH na Maseneta wanasema lengo si kubadilisha matokeo, kwanini Trump hataki lifanyike?

Ikumbukwe Trump alizungumzia sana rigging na kwamba hana imani na mchakato

Iweje akiwa mshindi aone uchunguzi huo una utata na hakubaliani nao?

Tusemezane
 
Back
Top Bottom