TUJITEGEMEE
JF-Expert Member
- Nov 6, 2010
- 23,914
- 23,079
Hivi IGP anampigia salute CDF? Ninaomba jibu ili niweze kujenga hoja juu ya hotuba ya Rais alipoongea na jeshi la magereza!
Yes anampigiaa,Hivi IGP anampigia salute CDF? Ninaomba jibu ili niweze kujenga hoja juu ya hotuba ya Rais alipoongea na jeshi la magereza!
Asante sana!Yes anampigiaa,
Hujui katika masuala ya ulinzi baada ya Rais ni CDF?
Mkuu, CDF ni mkuu wa majeshi ya ulinzi yanayokusanya majeshi yote.[
Sidhani kama aliwahi kuwepo CDF aliyetoka kwenye majeshi mengine zaidi ya JWTZ. Kama ndiyo hivyo, kwa mawazo yangu, kusema mfano koplo wa JW ni sawa na wa Magereza kuna changamoto hapo. Msisitizo ulitakiwa kuwa kwenye kuheshimiana na kupendana.Halafu hii hotuba nadhani hakitakiwa kuwa public!!Raia hatukupaswa kuiona hii kitu. Hii inaathiri uaminifu wa wananchi kwa majeshi yetu. Niko tayari kukosolewa kwa maoni yangu haya.
Mkuu CDF ni Mkuu wa majeshi yote ya ulinzi. Katika majeshi hayo sio polisi wala magereza bali ni majeshi yote ya JWTZ.Mkuu, CDF ni mkuu wa majeshi ya ulinzi yanayokusanya majeshi yote.
Kwa uelewa tu ni kama ilivyo katika sekta ya afya kwamba popote, Daktari ndiye anakuwa kiongozi ingawa kuna Nurse, Pharmacist, Lab tech n.k.
Hivyo CDF kwa mafunzo na majukumu ya JWTZ anatoka huko.
Hapa haina maana wengine hawana mafunzo, la hasha, Magereza wana mafunzo yanayowiana na kazi yao kama ilivyo Polisi, Zimamoto n.k. yaani specialized
JW wanaweza kufanya majukumu ya wengine, lakini si kinyume chake
Kuhusu hoja kuwa koplo wa Magereza halingani na wa JW , kinadharia inaonekana hivyo, kikazi si hivyo wote wana hadhi sawa. Tofauti yao ni hiyo niliyokueleza katika makukumu
Kama unadhani koplo wa Magereza hana hadhi sawa na JW, vipi wa JKT?
Utambue kuwa wapo chini ya Amir Jeshi mkuu mmoja na CDF mmoja.
Huiwezekani kuwa na koplo kidogo na koplo saana
Kuhusu namna alivyoongea, nadhani tatizo ni namna anavyofikisha ujumbe na si ujumbe wenyewe
Lugha inabeba mantiki sana katika kufikisha message across the intended audience
Mfano, alipo ongelea matumizi ya wafungwa, ni kweli. Kuna wafungwa wataalam na vibarua.
Magereza wanaweza kujenga nyumba zao kwa gharama ndogo sana kwasababu wana labor
Kama wanajenga kwa maafisa nyumba binafsi, wanashindwaje kuwatumia kujenga nyumba zao?
Lakini message ya 'wamenyeke kweli' inalenga kuwapa askari fursa ya 'abuse' na hilo si sahihi
Kumfunga mtu ni kumchukulia uhuru katika mazingira magumu sana.
Hiyo ni adhabu hahitaji kubebeshwa matofali 10 kichwani ili amenyeke
Lengo la kifungo ni kumrekebisha mtu si kumuumiza.
Hili ni pamoja na kuhakikisha wafungwa mafundi wanatumika iwakitoka kujielewa na pengine kujiajiri
Wafungwa wapo wenye utaalam sana, hawa wangepewa incentive kwasababu ni cheap labor
Likewise, hakupaswa kuonyesha kuna tofauti.
Alipaswa kuonyesha usawa ili kutoleta picha tofauti kwa jamii.
Angeongea nao kama askari tu ilitosha, lakini kuwaweka katika mizani haikuwa sawa
Message yake ilikuwa nzuri tatizo ni lugha inayobeba ujumbe inakuwa na 'ukakasi' na mara nyingi kupoteza maana iliyokusudiwa
Ahsante, mkuu naomba nichangie hoja hii kwa mara nyingineMkuu CDF ni Mkuu wa majeshi yote. Katika majeshi hayo sio polisi wala magereza bali ni majeshi yote ya JWTZ.
Kumbuka kwamba ktk JWTZ kuna majeshi Manne ambayo ni Jeshi la Anga, jeshi la ardhi, jeshi la majini na JKT.
Tunapozungumzia JKT sio kwamba ni jeshi jingine tofauti na JW. JKT ni kitengo cha JW ambayo inaendesha mafunzo ya kijeshi na ukakamavu kwa ajili ya vijana ambao wanaweza kutumika katika majeshi mengine kama polisi, JW, magereza, uhamiaji na hata mgambo au makampuni ya ulinzi.
Hivyo JKT ni hawa hawa JW, na ndio maana Mkuu wa JKT anaweza teuliwa na Rais kuwa CDF. Au Mkuu wa JKT anaweza toka JW baada ya kupandishwa cheo.
Koplo wa JKT ni sawa na JW kwani wote hupata mafunzo ya Ukoplo sehemu moja.
Mnapo anza mafunzo ya kijeshi ya JW, wote hamjui mtakuww kitengo gani.
Baada ya mafunzo eidha ya uafisa au askari ndipo mnaanza kugawanywa wengine wanaenda JKT, wengine Ardhi, anga na majini.
Huko mnaenda kupata mafunzo mengine ya kijeshi kutokana na nafasi hizo.
Hivyo JKT ni kitengo cha JW kama kitengo kingine cha JW. Na unaposema JWTZ basi jua ni muunganiko wa majeshi hayo manne.
Tofauti ya JW na majeshi kama polisi na magereza ni kwamba JW yeye anafundishwa kuua tu. Hii ndio sababu JW hawawezi tumika kutuliza vurugu za maandamani na kama wakitumika eidha polisi wamezidiwa basi ikitokea wameua huwezi kumshitaki, lakini kwa polisi anaweza shitakiwa.
Mkuu Nguruvi3Ahsante, mkuu naomba nichangie hoja hii kwa mara nyingine
Kama nilivyosemaCDF ni mkuu wa majeshi yote. Hilo halina tatizo
Majeshi tuliyo nayo ni JW, Magereza, Polisi, JKT
JW ina matawi kama Anga(Air force), majini( Navy), na nchi kavu (infantry) at least kwa muundo wa commonwealth na nchi kama US zina utaratibu wao wa kutaja ingawa kwa maana ile ile
Hivyo matawi si jeshi tofauti bali sehemu ya jeshi la wananchi (JW)
Hapa ieleweke tuna JW yenye mgawanyiko wa anga, nchi kavu, majini
Matawi hayo nayo yana matawi. Kwa mfano infantry (nchi kavu) wana tawi la mizinga( artillery), wana miundo mbinu (logistic), na mbinu (tactics) kwa uchache wa kutaja ambayo si majeshi bali matawi ya tawi la infantry linalounda JW likiwa na matawi mengine ya Navy na anga
Pili, kwamba jeshi limefunzwa kuua, hiyo ni sehemu tu ya majukumu yao.
Kama ulivyosema, kuna sheria za nchi zinawasamehe wanapokuwa katika majukumu kwasababu interactions yao na civilians ni limited.
Lakini hoja ya kwamba wamefunzwa kuua ina mapungufu kwa mtazamo mpana.
Kwa wale waliowahi kupitia majeshini mtakubaliana nami kuwa jeshini kama JW kuna nidhamu ya hali ya juu ya majukumu yao,ni kimbilio la Taifa kama ilivyo sehemu zote duniani
Katika dharura ya nchi majeshi huwa tayari kuliko sehemu nyingine yoyote.
Utashangaa daraja linajengwa kwa masaa kama ilivyotokea wakati wa mvua pale msoga.
Kama ilivyokuwa Kagera wakati wa vita.
Katika uokozi wao ni namba moja na kila jambo unalofikiri
Idd Amin alivunja daraja lililoonekana kuwa tayari kujengwa kwa miezi kama si miaka. Guess what, akapokea kichapo huku daraja linajengwa, vifaa vinapita kazi inaendelea
Anga wanafanya yao, navy wapo victoria , infantry wanavusha askari, architect wana design daraja, structural Eng wapo kazini, civil eng wanatenda , madaktari wanatibu majeruhi. watu wa logistic wanaendelea na kazi n.k.
kwa muda mfupi katika mazingira magumu sana, walifanikiwa
Kwa ufupi ikitokea janga sehemu zote duniani, kitengo cha kwanza na mwisho kutumika ni jeshi.
Si kutokana na mafunzo ya 'kuua tu', bali nidhamu na utayari wakiwa na wataalam 'the best'
Hivyo jeshi liangaliwe katika mambo kadhaa, kwanza, lina wataalam waliobobea, pili, lina nidhamu ya utendaji, tatu, lina utayari wa rasilimali na rasilimali watu ambao wameandaliwa vizuri
POLITICAL STABILITY OR INSTABILITY
KAMA TAIFA TUMESIMAMA WAPI KISERA?
Tuongelee dhana ndogo sana ya kile kinachoitwa Political stability.
Dhana imechukuliwa kiurahisi kama kutokuwa na vurugu, migomo au tafrani.
Imekuwa ni rahisi viongozi kusema taifa letu lina political stability. Pengine ni kweli
Kuna kitu kinachoitwa integrity ambacho ni sehemu muhimu ya stability.
Integrity inaelezwa ni kuaminiwa kwa kile nchi au serikali inachosimamia
Integrity inaeleza tunasimiaje thamani zatu (values).
Na values hulindwa na sera(policy) tulizojiwekea. Ndiyo maana sote bila kujali itikadi zetu tunaamini binadamu wote ni sawa na wanastahili utu na heshima.
Ni kwa msingi huo, serikali yetu iliamini katika sera ya usawa, utu na heshima
Ilichukua misimamo kadhaa mingine michungu katika kulinda values zetu kama Taifa
Tulikuwa wananchama wa nchi zisizofungamana na upande wowote(NAM) ili kuwa huru kuunga mkono eneo lolote linalosimamia thamani zetu za uhuru, usawa, utu na heshima.
Tuliunga mkono harakati za ukombozi kusini hadi Magharibi. Palestina, Nigeria na kwingeneko ambapo wananchi walisimamia haki zao zinazolingana na thamani zetu
Taifa letu lilikuwa na sera bila kujali nani ataongoza kutoka wapi
Miaka ya karibuni sera za Taifa zimegeuka kuwa za vyama na kutuyumbisha
Hivi leo tuna sera ipi kuhusu uhuru, usawa, utu na heshima ya mwanadamu?
Ziara ya mfalme wa Morocco inatuweka wapi tukiiingalia Sahara , Plestina na kwingine kwenye madhila yanayofanana na hayo yayonakinzana na values zetu?
Je, bado tuna integrity katika jumuiya ya kimataifa?
Na je integrity yetu inaeleza nini kuhusu policy zetu kama Taifa na stability yetu?
Integrity yetu haiishia katika eneo hilo la Kimataifa. Hata katika local level upo wasi wasi
Awamu ya nne ilisimama kuhakikisha Watanzania popote walipo wanatoa mchango kwa Taifa.
Na kwamba uwepo wao nje iwe sehemu ya mafanikio na si usaliti.
Hilo ndilo liliunda 'idara' ya diaspora ili kuhakikisha wanachangia maendeleo ya nchi waliko
Tangazo la serikali kuhusu umilikiwa ardhi kwa diaspora limekuja na vishindo.
Kwanza, serikali ya chama kile kile haina sera na wala haiminiki. Pili kama nchi hatuna sera za Taifa
Mifano miwili awali inaeleza integrity ya serikali. Kwa mwekezaji au wawekezaji tunaowakaribisha, mifano ni mingi inatosha kuwaeleza political stability ya nchi yetu
Investors hawapendi mashaka 'uncertainty' na hali ilivyo, hata wazawa wanaona uncertainty nyingi kimataifa hadi kitaifa.
Mwekezaji ana kila sababu ya kuogopa!
Tusijidanganye kwa kauli mbiu ya political stability, tujiulize tuna integrity?
Tuna sera kama nchi?
HATUNA SERA ZA NCHI, TUNAZO SERA ZA 'WATU'
Bandiko la juu tumezungumzia political stability/instability na athari za taswira ya nchi zetu
Mataifa yaliyoendelea zipo sera za nchi, na za vyama hotofautiana utekelezaji
Kwa bahati mbaya hata sera za vyama wananchi wetu hawawezi kuzihoji
Hii imepeleka mabadiliko ya kila mara ya sera kutokana na watu na si wananchi
Hali inachanganya wananchi au wageni, inatia hasara zisizo na ulazima
Kwa mfano, suala la katiba
Hili lilikuwa takwa la wananchi lililofanywa sera za wapinzani.
Lengo lilikuwa kuboresha katiba yetu kwa kulingana na nyakati tulizo nao
Hoja ya katiba 'ikatekwa' na Rais kwa kuanzisha machakato si wananchi
Ikawa tena si ya wananchi bali takwa la kiongozi aliyekuwa madarakani
Kwa kukosa muafaka, na hoja kuporwa kutoka kwa wananchi , katiba ikawa suala la kikundi cha watu kikitaka kuamua kwa niaba ya Taifa. Tulifeli
Pesa kwa mabilioni zilitumika bila matokeo chanya.
Katika uchaguzi mkuu, katiba haikuzungumziwa kwasababu ilionekana mtego
Tusemezane
Mkuu hapa ndipo tatizo linapoonekana zaidi. Nilitegemea waziri angeanza na hilo la Mwaneromango, badala yake kaanza na diaspora. Hatuna dira au sera za kitaifa kila mtu anakuja na lake akiondoka mwingine anakuja jingine. Ndiyo yale ya elimu kwa wote, Kilimo kwanza na sasa viwanda ndani ya miaka 10Ndugu yangu Nguruvi,
Pamoja na mema yote kuhusu haki na fursa ya Watanzania waishio nje ya Nchi... aka Diaspora kuhusu umiliki wa Mali na hasa ardhi, bado Mtanzania wa Maneromango hana uhakika wa ardhi yake...
Halafu hii hotuba nadhani hakitakiwa kuwa public!!Raia hatukupaswa kuiona hii kitu. Hii inaathiri uaminifu wa wananchi kwa majeshi yetu. Niko tayari kukosolewa kwa maoni yangu haya.
Mkuu hii inaonyesha jinsi corruption ilivyofikia kiwango cha juuInfact, hotuba imenisadia kujua mambo ambayo nilikuwa siyajui.
Mfano, eti wanajeshi walikuwa wanalipia/nunua sare zao? I never thought of this?
Mkuu hii inaonyesha jinsi corruption ilivyofikia kiwango cha juu
Kwamba, Amir jeshi mkuu aliyekuwepo hakuwa na habari za askari kununua Uniform?
Kwamba, ndani ya security organs hakuna security ya kuangalia hali ya mambo
Kununua uniform ilikuwa 'deal' ambayo ni conduit ya wazee kupitisha mirija yao
Ni jambo la kushangaza sana kwasababu kuna maeneo binafsi wafanyakazi wanapewa uniform bure
Leo askari magereza walikuwa wananunua uniform! Sijui kwanini guiness book hawakuliona hili
Ingelikuwa hivyo madai yao yangekanushwa na mkuu wao pale pale.Au labda walikuwa wanapewa uniform replacement allowance? Kwa mfano, nimesoma kuwa kwa Marekani, wanajeshi wanapewa free uniforms mwaka wa kwanza wanapoingia jeshini ila baada ya hapo wanapewa allowance kila mwaka ku-replace uniform.