Dunia nzima imeona,ningeshangaa sana kama TFF ingekaa kimya

Asante Kaka kwa kunisaidia kuwaelezea hawa Watindiga(Wapenzi wa Simba) wa kizazi cha 1990s wasioijua Historia ya nchi hii, wao kazi yao ni kushangilia usajili wa kina Ngassa,Akuffor na wengineo tu uliofanikishwa na yule Mhaini...sijui hata nani alimfungulia bora angeishilia kulekule

Mhaini na Fisadi nyangumi nani afadhali?
 
Soka la bongo fitna kubwa kabisa!!wamejaa mafisadi wa soka na wanunua marefa,wachezaji ili kuboronga na kuhujumu mechi!woote wanajulikana!

Yule refa ni mpuuzi na mpumbavu...ile ni ajira yake...yeye anaitoa rehani kwa vijihela vichache (kama kweli alipewa); ama ushabiki wa kijinga...still doubting this kwakuwa aliharibu na kuvurunda kote kote!! Ona sasa katemeshwa kibarua...

Kuna mmoja alishauri katika mechi kubwa siku zijazo, atafutwe mwamuzi wa nje...kama ilivyokuwa katika pambano la masumbwi kati ya Nyilawila na Cheka...

Na hawa Tifutifu (TFF) sijui kwanini hadi wakati huu wanashindwa kusimamia suala la kupatikana waamuzi bora wa mechi Tanzania. Tuna wamiss sana akina Msafiri Mkeremi na Hafidh Ally...
 
tanzania kuna maajabu mengi mno,TFF wenyewe mpira unawashinda,kweli kazi ipo
 
Kama ilivyotarajiwa na wengi wale wachezaji wa kukodi No. 12 na No. 13 waliowawezesha Mabingwa watetezi wa Ligi kuu ya Tanzania Bara Simba S.C kutoka droo ya goli 1 - 1 na Mabingwa wa kusakata kabumbu ukanda mzima wa Africa ya Mashariki mpaka kule kwa nchi waalikwa Dar Yong Africans wameadhibiwa na Shirikisho lenye dhamana ya kuendesha mchezo huo hapa nchini kwa kuvurunda, wakati Akrama (Pichani chini) akiondolewa kabisaa kwenye Ligi Msaidizi wake Mzee wa offsides yeye amepewa onyo kali,habari kamili hii hapa:-

attachment.php

Na Prince Akbar wa Bin Zubeiry
KAMA ilivyotarajiwa na wengi, refa Mathew Akrama wa Mwanza aliyechezesha ovyo mechi ya watani wa jadi katika soka ya Tanzania, Simba na Yanga, Jumatano wiki hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ‘amekwenda na maji’.
Taarifa ya Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura imesema kwamba, Kamati ya Ligi imewaondoa marefa watatu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kutokana na kuvurunda.
Mbali na Akrama ambaye ‘Yanga hawana hamu naye’ tangu siku hiyo, wengine ni Paul Soleji wa Mwanza aliyechezesha mechi kati ya Simba na Tanzania Prisons, na mwamuzi msaidizi namba mbili kwenye mechi hiyo Mwarabu Mumbi wa Morogoro, wakati mwamuzi msaidizi namba mbili wa mechi ya Yanga na Simba, Ephrony Ndissa wa Dar es Salaam amepewa onyo.
Kamishna wa mechi namba 28 kati ya Yanga na African Lyon, Pius Mashera ameondolewa kwenye orodha ya makamishna wa ligi hiyo kwa kuchelewa kufika kwenye kikao cha maandalizi ya mechi (Pre match meeting) na uwanjani.
Vilevile Mashera kwenye ripoti yake aliwasilisha malalamiko dhidi ya msimamizi wa kituo cha Dar es Salaam, na kwa vile suala hilo ni la kinidhamu ametakiwa alipeleke kwenye Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi ya TFF.
Nayo Simba imepigwa faini ya jumla ya sh. 600,000 kwa kuchelewa kufika kwenye pre match meeting ya mchezo wao dhidi Tanzania Prisons (sh. 100,000) na kwa washabiki wake kuwatupia chupa za maji waamuzi wa mechi hiyo (500,000).
Pia Kamati ya Ligi imeagiza kuwa kwa vile suala la kipa Shaabani Kado wa Mtibwa Sugar kudaiwa kumpiga kiongozi mmoja wa Ruvu Shooting mara baada ya mechi kati ya timu hizo iliyochezwa Uwanja wa Azam Complex ni la kinidhamu lipelekwe kwenye Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi ya TFF.

wee umetumwa na wana yanga mi naona,kwa hapa hautupati ngo,mnyama yupo juu daima.
 
Yanga ni moto wa kuotea mbali, mtasingizia sana marefa mwaka huu, na bado. Kumkata simba sharubu mwaka huu ni jambo lililo wazi. Simba ni kenge blue hawazi kuifanya kitu yanga, tena mechi ijayo achezeshe Ismail Aden Rage.!
 
Marefa mnawachagua wenyewe ili wawabebe, kawabeba hambebeki sasa mlitaka achukue mpira yeye mwenyewe autumbukize kwenye kamba ndo mngeona ni refa bora, timu yenu mbovu ile si ya kulipa tano kajipangeni tena acheni kubwabwaja, Huyo Bahanuzi wenu muda wote yuko nyuma ya mabeki unategemea nini? Na kama ataendelea hivyo hivyo ataishia kufunga magoli ya penati tu lakini ya move atayasikia kwa akina Sunzu, Okwi, Ngasa na Boban.
Mkuu Masuke umewasilisha mpaka Bhaaaaaaaaass. Sio kosa lake alitumwa magoli bila ya kupewa mbinu za kiufundi, alifikiri Okwi Magoli akifunga huwa anakaa nyuma ya mabeki, akamuulize Nsajigwa na Chuji kilichowapata mwezi wa Nne mwaka huu huu mpaka wengine wamestaafishwa bila kupenda.Nafikiri kuna haja ya kulifukuza benchi nzima la ufundi la Yeboyebo FC kwa kushindwa kumfundisha Bahanuzi jinsi ya kuvunja "offside trick" za wachezaji wakimataifa kama wa Simba SC. Chezea Mnyama wewee
 
Yanga ni moto wa kuotea mbali, mtasingizia sana marefa mwaka huu, na bado. Kumkata simba sharubu mwaka huu ni jambo lililo wazi. Simba ni kenge blue hawazi kuifanya kitu yanga, tena mechi ijayo achezeshe Ismail Aden Rage.!
Si bure utakuwa umeamka muda si mrefu, kanawe uso kwanza wenzako wanajibu hoja wewe umeanza matusi. Shauri yako wenzako walianza rafu refa akawabeba kilichowatokea kawaulize akina Sufiani wenu bado wanalia.
 
Yanga ni moto wa kuotea mbali, mtasingizia sana marefa mwaka huu, na bado. Kumkata simba sharubu mwaka huu ni jambo lililo wazi. Simba ni kenge blue hawazi kuifanya kitu yanga, tena mechi ijayo achezeshe Ismail Aden Rage.!
Huo moto wa kuotea mbali wa Yanga unaonekana wapi na sisi tukaote au kwa sababu ni wa kuotea mbali utatupata huku huku, Hebu tujikumbushe msimamo wa ligi tuone huo moto wa Yanga wa kuotea mbali.
msimamo wa ligi..PNG
 
Hongera TFF kwa kumng'oa huyu Nduli refarii kibaraka mkubwa wa Gabachori kwa kuharibu mchezo kwani alishindwa kabisa kuumudu mchezo. Tatizo lake alishindwa kumkatia kidogodogo mshika kibendera wake matokeo yake Kibendera wake akafuata kanuni 17 za Soka ujinga wake kuonekana dhahiri uwanjani.
Hata hivyo sishangai leo hii Mshika Kibendera akionywa eti kisa kafuata kanuni 17 za mpira wa Soka, TFF jipangeni tena ndani yenu kumejaa Uyanga kuanzia Kamati ya Tibaigana mpaka ya Rufaa ikiongozwa na Mgongolwa. TFF tuelezeni onyo la Kibendera ni kwa kosa lipi au la kutokumuachia Bahanuzi asifunge magoli ya offside?
 
Huo moto wa kuotea mbali wa Yanga unaonekana wapi na sisi tukaote au kwa sababu ni wa kuotea mbali utatupata huku huku, Hebu tujikumbushe msimamo wa ligi tuone huo moto wa Yanga wa kuotea mbali.
View attachment 67455
Mkuu Masuke kweli moto wakuotea mbali nimeuona, yaani pamoja na makelele yote ya usajili watu wanahemea kupata nafasi ya nne! Hivi na moto wa kuotea Morogoro upo au umezimika maana naona miwa inazidi kuchanua tu. Teheteheteheteheeee
 
Yanga ni moto wa kuotea mbali, mtasingizia sana marefa mwaka huu, na bado. Kumkata simba sharubu mwaka huu ni jambo lililo wazi. Simba ni kenge blue hawazi kuifanya kitu yanga, tena mechi ijayo achezeshe Ismail Aden Rage.!
Mngeanza na Mtibwa SC kwanza halafu Simba SC wakafuatia. Kufunga magoli nane na wewe ukatundikwa sita (GD = 02) hapa naona moto wa mshumaa tu, moto wa gesi upo Simba SC wewe sisi tumetundika watu magoli kumi, tumefungwa magoli mawili tu na la penati ya kupewa moja.
 
Mambo ya ajabu sana haya mnashangilia ligi ikiwa round ya 5!!!!
 
Mambo ya ajabu sana haya mnashangilia ligi ikiwa round ya 5!!!!
Mtani vipi au wewe hujui kama "Nyota njema huonekana asubuhi" na "Biashara asubuhi" au wewe unafuata kale kamsemo "Fainali uzeeni"
 
kwa refa na mshika kibendera wanastahili kabisa, labda tusubiri na maamuzi ya kamati ya nidhamu tuone nayo itafanya nini dhidi ya wachezaji wachache walioonyesha utovu wa nidhamu uwanjani wa makusudi, kwa mfano canavaro alimkanyaga kazimoto kwa makusudi baada ya kuchezewa rafu kama picha za video zilivyoonyesha tukio ambalo halikutolewa maamuzi uwanjani, kitu ambacho kitasaidia wachezaji kuwa na nidhamu wawapo uwanjani na hata nje ya uwanja pia na si simba na yanga tu bali kwa vilabu vyote iwe ni vya ligi kuu au vinginevyo
 
Mngeanza na Mtibwa SC kwanza halafu Simba SC wakafuatia. Kufunga magoli nane na wewe ukatundikwa sita (GD = 02) hapa naona moto wa mshumaa tu, moto wa gesi upo Simba SC wewe sisi tumetundika watu magoli kumi, tumefungwa magoli mawili tu na la penati ya kupewa moja.
Karaga bao, yanga tumewashika, tena tumeshika pabaya, lazima tumkate mnyama mkia
 
Karaga bao, yanga tumewashika, tena tumeshika pabaya, lazima tumkate mnyama mkia
Naona umeishiwa na wadau pia wameliona hilo. Endelea kusema "jamani napiga njooni mniamulie' kumbe umepigwa wewe roba ya mbao halafu mchizi aliyepiga amekauka anataka mpaka aone ngama imetoka ndipo akuachie.
 
Mambo ya ajabu sana haya mnashangilia ligi ikiwa round ya 5!!!!
Unataka tushangilie ikiwa raundi ya ngapi? au tuanze kushangilia pale mtakapo lipa kisasi cha magoli matano bila au yale ya Dar mpaka Moro?

Similar Discussions

Back
Top Bottom