Duni Haji audanganya umma, TCRA wanasajili laini kieletroniki kwa kitambulisho cha taifa

hugochavez

JF-Expert Member
Mar 1, 2013
1,907
1,009
*MZEE JUMA DUNI HAJI UMEUDANGANYA UMMA KUHUSU KITAMBULISHO CHA MZANZIBAR MKAZI.*

Anaandika Abdallah Juma Makame mzanzibari halisi

Kiukweli Mzee Juma Duni Haji umekosea sana na umeudanganya umma juu ya kitambulisho cha uzanzibar mkazi kushindwa kuthaminiwa na kuwa kimekataliwa kutumika katika usajili wa line kielektroniki, hii siyo sahihi.

Ukweli ni kwamba TCRA wanasajili line za simu kwa kutumia *kitambulisho cha Taifa* ambacho kimsingi ndiyo kitambulisho kinachomtambua mtanzania, hapa inamaanisha watanzania bara na zanzibar, na vitambulisho vya Taifa vinatolewa na NIDA hapa namaanisha wazanzibar na watanzania bara kama watanzania.

Hata hivyo NIDA wana ofisi zanzibar na katika usajili huo, kitambulisho cha mzanzibar mkazi hutumika kama kigezo cha kumtambua mzanzibar.

Huu ni Mwezi mtukufu wa ramadhan mzee Duni angalau basi uwe na haya uache kuwadanganya wazanzibar kwa chuki na ubaguzi wako wa kutaka kuligawa Taifa.

Wazanzibar tunaelewa na tuko pamoja na serikali yetu chini ya Rais Magufuli.
 
Back
Top Bottom