Aliyeshtakiwa kwa kupokea rushwa ili kutoa kitambulisho cha Taifa kwa raia wa Uganda si mtumishi wa NIDA

Aug 15, 2011
30
11
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) inapenda kukakasha taarifa iliyoandikwa katika mtandao huu leo ikiwa na kichwa cha Habari kisemacho "AFISA NIDA ASHTAKIWA KWA KUPOKEA HONGO KUTOA KITAMBULISHO KWA RAIA WA UGANDA"

Tunapenda kuufahamisha Umma na watanzania wote kwa ujumla kuwa NIDA haina Mtumishi aitwaye Lilian Stanslaus katika ofisi ya Usajili wilaya ya Ilemela au mahali pengine popote.

Aidha tunatoa onyo kwa mtu yeyote atakaye bainika na kuthibitika kujifanya ni Afisa wa NIDA huku akijua fika kuwa si Mtumishi wa NIDA, hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Imetolewa na:
KITENGO CHA MAWASILIANO
MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA
 
NIDA hii wizara ya kihuni sana unaomba kitambulisho miaka 3 bado kupewa.
 
Back
Top Bottom