Dubwasha

Lumbi9

JF-Expert Member
Oct 12, 2014
8,566
11,809
Sehemu ya kwanza
Kwa Mary Robert.2010
Nayajua mengi kwakuwa nimempa kila mtu nafasi ya kuwa mwalimu wangu,,kila mtu hunifunza kwa
yale atakayo,,naheshimu kauli na mawazo ya wote kwa uzito sawa, LAKINI UELEWA NI JUU YANGU
MTANGAZAJI
Leo katika kipindi chetu, tutaendelea kusikiliza
mahojiano kati ya Patrick na mwandishi wa habari
waliowahi kuyafanya kipindi cha nyuma kabla ya
leo, tulia kwenye redio yako na kila kitu kitakujia
hapohapo ulipo, hatutakuwa na matangazo mengi
kutokana na uzito wa simulizi hii ya kusisimua
ilikuwa ni sauti ya mtangazaji wa kituo cha redio
cha SPEAK LOUD FM kilichokuwa kikirusha kipindi
cha STORY za Iam Frank, saa yangu ya mkononi ilinionyesha kuwa ilikuwa saa nne usiku na pombe
zilikuwa zimeivuruga akili yangu, lakini nilikwenda
mpaka kwenye jokofu na kuchukua Redbul kisha niliinywa haraka haraka na kurudi ili niweze
kusikiliza bila kupata chembe ya usingiziile kanda
yenye ile simulizi ilichezeshwa na sauti ya msimuliaji ilianza
kusikika.
PATRICK ANASIMULIA
".........ulifikiri nitanyamaza sio,sikutaka kufanya
yote haya ila you forced my hand(uliulazimisha
mkono wangu).."ndo sauti ya mwisho niliyoisikia katika masikio yangu ikifuatiwa na maumivu ya
kitu chenye ncha kilichoingizwa kwenye mshipa wa damu kichwani mwangu,niligundua ni sindano
baada ya kuhisi kama dawa ikisukumwa kuingia ndani ya mshipa ule, hali ya kulewa na usingizi vilianza kunisonga lakini kwa mbali niliweza kuona kama vile Mary alikuwa amezimia, nikajitahidi
kutoa sauti lakini sikuweza kabisa, wale watu sikuwaona vizuri lakini walikuwa ni zaidi ya wawili
kwakuwa nilizisikia sauti zao kwa mbali wakishauriana, sikuifahamu hata sauti moja, gari
letu lilikuwa limeharibika vibaya na ile ajali,sikumbuki ilikuwaje mpaka tukagongana na ile gari
ila nilishtuka tu na kukuta tayari ajali imetokea na wale waliokuwa kwenye ile gari ndio walioshuka na
kuja kunichoma ile sindano. Maumivu makali yaliutesa moyo wangu haswa pale nilipotaka kukumbuka hata jina langu lakini nikashindwa,,,sikukumbuka kitu chochote, niliishi maisha ya tabu
sana katika siku za ukubwa wangu, kila kitu kwenye maisha yangu kilikuwa kipya kabisa,sikumfahamu yeyote katika eneo lile. Sikukumbuka
nilipokuwa wala nilifikaje,sikufahamu chochote
kuhusu ulimwengu,kila kitu kilikuwa ni giza ndani ya maisha yangu,sikutamani kufa kwasababu
sikujua nini maana ya kuishi na nini faida ya kufa kwa wakati huo,,kwa kweli yalikuwa maisha ambayo sikuwahi kufikiri kama ningeishi. Miaka sita mbeleni nilikuja kutoka nje na ndipo nilipoona bango kubwa nje ya jengo hilo nililokuwemo bango
hilo lilisomeka Dr. ANDERSON MENTAL CLINIC,ilikuwa pia anuani chini yake iliyonijulisha kuwa
nilikuwa SUVA huko FIJI, mandhari niliyokuwepo niliipenda sana ila sikukumbuka chochote juu ya
eneo hilo,niliichukia sana hali niliyokuwa nayo wakati ule, hakuna aliyekuwa akionekana kunijali,kila mtu alikuwa busy na kazi yake.
Nilijihisi pengine nilikuwa kichaa, iweje kila mtu asinijali au kuniuliza chochote pale nilipokuwa.
Hayo yalikuwa maisha yangu kipindi cha mwanzoni mwa uzima wangu wagu wa mara ya pili, niliona watu ambao nilihisi ni tofauti sana na mimi,,,,,nilisogea mpaka mbele kwenye bustani kubwa na kutazama mbele mita 200 nikagundua pale ni
karibu kabisa na ufukwe wa bahari.
****
"hallo,,!"niliskia sauti ikiniita wakati nipo pale kwenye bustani nikageuka,alikuwa ni msichana
mwenye asili kama yangu lakini sikuwa namfahamu,,alinisogelea karibu nakuanza kunisemesha,nilielewa lugha aliyokuwa akiiongea,
niliwahi kuwa nikiiongea sehemu fulani lakini sikukumbuka ni wapi.
Patrick namshukuru sana mungu uko hai,nashukuru umerudisha fahamu zako aliongea huku akionekana kweli kuwa alikuwa akilifurahia hilo.
Sikumjua huyu dada wala sikufahamu yeye amenijuaje.
utapona kabisa na utakumbuka kila kitu,tunafanya tuwezavyo kuhakikisha kuwa unarudisha fahamu zako alizidi kusisitiza huku akifuta machozi.
wewe ni nani nilimuuliza huku nikimtazama usoni,hakika sura yake sikuijua kabisa, hata kama sikuwa na fahamu lakini sura yake ni kweli
sikuwahi kuiona hata kidogo.
Naitwa Pamela, ndiye daktari ninayemsaidia dokta Anderson katika matibabu yako, ni mimi ambaye
ndiye nakuwa na wewe muda wote kuangalia afya yako, wewe ni sababu ya mimi kuendelea kuwa hapa aliongea huku akionekana kuangalia pembeni kana kwamba alikuwa akifuta machozi.
kwanini unalia nilimuuliza huku nikimgeuza ili aniangalie.
silii, ni furaha tu kwakuwa umeamka leo kichwa changu kilikuwa kimejaa maswali mengi sana,lakini sikujua namna ya kuyauliza, kila kitu pale
kilikuwa ni michoro kwangu isiyoashiria chochote,
nilikuwa nimevurugwa akili na kila kitu kabisa,sikumfahamu yule Pamela na wala sikujua yeye ninani, sikujua anaposema nimeamka je nililala toka
lini, na kwanini kuamka kwangu kuwe ni furaha kwake, kwanini alie kwa mimi kuamka, kwanini alionyesha furaha na kusema nitapona, yeye
alikuwa nani kwangu, mimi nilikuwa na thamani gani kwake, hiyo yote ilikuwa ni jakamoyo ndani ya
moyo wangu, nilikuwa kama teja lililokuwa likihudhuria kliniki ya ukichaa.
Pamela, mimi sielewi chochote nilimuuliza huku nikilia baada ya kujitahidi sana kukumbuka lakini
ikashindikana. Hakunijibu chochote badala yake alinishika mkono na kuondoka na mimi mpaka
ndani ya ile hospitali. Tulipofika pale aliingia ndani na kutoka na daktari mmoja mzungu aliyekuja pale
na kuanza kuongea na mimi kisha Pamela alikuwa akinitafsiria.
Hellow Patrick am doctor Anderson(habari
Patrick, naitwa dokta Anderson). Alinisalimu na kunipa mkono, na mimi nilimpa mkono.
We want to discharge you, but you will be under the care of doctor Pamela, you will stay at her
place until we are sure that you can stand on your own(tunataka tukuruhusu lakini utakuwa chini ya
uangalizi wa dokta Pamela, utakaa nyumbani kwake hadi tutakapokuwa na uhakika kuwa kuwa unaweza kujitegemea) sauti ya Pamela ilisikika ikitafsiri maneno ya dokta Anderson.
Pamela dont bother to interpret, I do understand the language (Pamela usihangaike kutafsiri,
naielewa hiyo lugha), nilimuambia hayo Pamela na yeye alinyamaza kimya.
*********
Niliruhusiwa kutoka pale hospitali na sasa tuliingia kwenye gari ya dokta Pamela kuelekea kwake,
hapakuwa mbali sana na pale hospitali, muda wa dakika kumi tulikuwa tumeshafika.
karibu sana Patrick, hapa ni nyumbani kwangu,ndiko ninapoishi, na ndipo ambapo na wewe utaishi alinikaribisha huku akitabasamu na
kuruhusu vishimo vidogo kwenye mashavu yake vionekane, nilikaribia na kuketi huku nikitazama kila kona ya ile nyumba. Ilikuwa ni nyumba ndogo lakini ilikuwa ni nzuri na ilikuwa na mazingira mazuri yaliyovutia.
Unaishi na nani hapa nilimuuliza swali wakati alipokuwa akienda kuchukua kinywaji kwenye jokofu.
naishi mwenyewe, lakini kwasasa nitakuwa nikiishi na Patrick aliongea hayo na kucheka.
Sikumbuki kama niliwahi kucheka toka pale hospitali. Kwa muda mfupi niliokuwa na Pamela nilikuwa nimegundua kuwa alikuwa mtu mwenye
kupenda sana kucheka, alikuwa ni mtu mcheshi na anayependa utani muda mwingi. Nilianza maisha haya ya kuishi kwa Pamela na muda mwingi dokta Anderson alikuwa akija pale nyumbani kuniangalia.
Pamela na dokta Anderson walikuwa kama ndugu vile ingawaje Pamela alikuwa na asili tofautikidogo.
***********
Asubuhi tulivu ya desemba 1999 ilinikuta nikiwa Suva huko Fiji, ilikuwa ni miezi mitatu sasa toka
nitoke hospitali lakini mpaka wakati huo bado sikujua chochote, mbali na kumuuliza Pamela maswali mengi lakini hakuwa tayari kabisa
kunieleza chochote, siku zote historia ya maisha
yangu na sababu za kwanini sina kumbukumbu yeye hakuziona za maana.
Patrick leo tunatoka nilimsikia Pamela akinipa taarifa hiyo asubuhi wakati alipokuja kugonga chumba changu.
tunaenda wapi nilimuuliza huku nijiachanisha na shuka zito nililokuwa nimejifunika.
tunaenda Albert Park, amka ujiandae tunaondoka muda sio mrefu niliamka na kuanza kujiandaa.
***********
Safari ya kuelekea Albert Park ilianza, tulikwenda mpaka Tanoa plaza tukipitia Amy Roas na hapo
tulisimama, kisha Pamela aliniambia tushuke tuingie ndani ya lile jengo. Tuliingia mpaka ndani ya jengo lile na kwenda upande wakulia mpaka juu
kabisa ambapo tuliweza kuona mandhari yote ya
Fiji na kwambali alinionyesha nchi ya Australia.
Nikiwa pale juu nilisikia kama sauti yamsichana ikiniita na nilipogeuka nyuma sikuona mtu.
ni nini Patrick aliniuliza Pamela lakini sikuwa na la kumjibu, nilipokuwa nimegeuka sikumuona mtu
yoyote lakini kwa uhakika kabisa niliona kama kivuli cha msichana niliyehisi kumfahamu, najua
hata ningesema Pamela asingenielewa.
hamna kitu, sijui ni nini nimeona nilimueleza hayo na yeye alinifata na kunishika kichwa akiniambia
kuwa amenileta pale kwasababu japo hakunieleza ni sababu gani hiyo. Alitnitoa pale na kunipeleka
ndani zaidi kwenye chumba fulani na hapo nilianza kuhisi mapigo ya moyo yakinienda mbio.
Pamela kuna nini hapa nilimuuliza Pamela lakini hakuniambia kitu badala yake alinifunga kitambaa
usoni na kuniambia niketi, niliketi huku nikiwa na wasiwasi juu ya kilichokuwa kikitokea pale. Giza
lilikuwa limetanda kwenye macho yangu na hofu ilinifika. Nilianza kuona picha ya msichana kwa
mbali na sikujua ni nani. Alikuwa msichana mrembo mweupe ambaye nilikuwa naye sehemu kama ufukweni mwa bahari, yule msichana alikuwa
akifurahi na mimi nilikuwa nikimkumbatia kama vile tulikuwa wapenzi,,niliogopa sana kwakuwa
haikuwa kawaida, alinifungua tena kile kitambaa na kuniuliza nimeona nini lakini sikuwa na la kumjibu.
mimi ni nani Pamela? nilimuuliza huku nikiwa kama natetemeka, alinitazama machoni huku akionekana kuzuia machozi.
ukitaka kujua wewe ni nani lazima uwe makini na kile kikujiacho kwenye fikra zako aliniambia
nakuninyanyua kisha tulienda mpaka kwenye chumba kilichokuwa kulekule ndani kisha alivua nguo zake mbele yangu na kuvaa taulo na
kuelekea bafuni, akiwa bafuni nilisikia akiniita lakini
kwa uwoga nilivua nguo zangu na kuvaa taulo kisha nikamfata bafuni, nilipoingia alinikumbatia na
kuanza kunipiga mabusu mwili mzima, mihemko ya mwili wangu ilikuwa karibu kabisa na hisia zangu hivyo nilianza kulipiza mashambulizi, kila
nilipokuwa nikimshika kuna picha ya mwanamke ilikuwa ikinijia, tulitoana bafuni na kuja mpaka kitandania kisha kazi ilianza pale, Pamela alikuwa mtundu sana kitandani lakini kila alipojitahidi kunifanyia mambo flani taswira ya mwanamke
mwingine ilikuwa ikinijia, tuliendelea kusumbuana na kuchokozana hisia zetu na mwishowe
tulikutanisha maungo yetu ya uzazi, nilipokuwa katikati ya mchezo wakati Pamela akiwa juu kuongoza jahazi niliona sura ya yule msichana
tena na kushtuka ana hapo Pamela alizidisha kasi,nilikuwa kama mtoto mdogo vile jinsi ambavyo
nilikuwa nikilia na ile sura ya yule mwanamke ilikuwa ikinijia bado.
Mary,,,Mary nilijikuta nikitamka lile jina na hapo Pamela aliacha na kunishika kichwa,,kisha alikuwa
akiniangalia kwa makini.
kafanyaje aliniuliza kama vile hakuelewa ninachomaanisha, nilinyamaza kwakuwa sikujua
namna ya kuendelea kuelezea, hapo Pamela alianza tena kuushika mwili wangu na kuendelea
na shughulia yake mpaka nilipokumbuka baadhi ya vitu.
Mary ni nani Pamela nilimuuliza kisha alinyanyuka vilevile akiwa uchi na kuondoka kuelekea bafuni, alipokuwa akiondoka nilimtizama
na ile picha ilinijia tena. Nilijivuta pale kitandani na
kwenda kumfata kule bafuni, alifungua lile bomba la mvua na kunivuta kisha alinikumbatia huku maji yakitumwagikia. Nilikuwa nimetumbua macho na
yeye hakuwa anaongea zaidi ya kufungwa macho akiyaruhusu maji yazilowanishe nywele zake laini.
*****
USIKU WA SIKU HIYO.
Tulikuwa tumelala nyumbani kwa Pamela na siku hiyo ilikuwa mara ya kwanza mimi na Pamela
kufanya yote yaliyotokea mchana huo.
Mary ni nani lilikuwa swali la kwanza kumuuliza Pamela usiku ule. Alikuwa amenilalia kifuani lakini
nilipomuuliza alinyanyuka na kuketi.
Mary ni msichana uliyekuja naye Fiji miaka zaidi ya sita sasa, ni mke wako na alikaa hapa akikuuguza kwa zaidi ya miezi sita ila baadaye
aliamua kuondoka baada ya kumwambia kuwa si rahisi wewe kurudisha fahamu tena, aliondoka na
hatukujua ni wapi alikwenda, tumejaribu sana kutafuta kumbukumbu zako lakini hatukupata
alinieleza hiku akijikaza ili asilie.
kwanini sikuwa na fahamu nilimuuliza.
ulichomwa sindano ya dicomenzol, inayotumiwa kuchoma wanyama wakali ili kuwafanya watulie,
walikuchoma wakazidisha kipimo na hii ilikuwa ni baada ya wewe kupata ajali ambayo hata hivyo tunahisi ilikuwa ni ya kukusudiwa, yani kuna mtu aliitengeneza ili itokee ndo wakuchome sindano ile ambayo ilimaliza kila kitu kichwani mwako
Mary Robertnilikumbuka.
 
Ile CD yenye ile simulizi iliendelea kusikika redioni na usingizi ulikatika kabisa, nilikuwa najiuliza huyu
Mary ndiyo nani na kafanya nini. Baada ya matangazo machache yule mtangazaji wa redio alirudi hewani na kusema kuwa sasa wataweka sehemu ya pili ambayo ni mahojiano kati ya Pamela na Mtangazaji. Nilijiweka tayari kusikiliza
na kwenye ile CD ilisikika sauti ya mtangazaji ikimwambia Pamela aeleze kila kitu alichotaka kukisimulia pale.
PAMELA
Patrick alikuwa ameanza kurudisha fahamu kitu ambacho nilikuwa nikikiota siku nyingi, ingawaje kitaaluma nilikuwa daktari tena mtaalamu wa
magonjwa ya akili na ubongo na taaluma yangu hainiruhusu kukata tamaa ya kumuhudumia mgonjwa ambaye bado anapumua vizuri ila kwa Patrick ilikuwa tofauti, kuna muda nilikuwa nakata
tamaa kabisa, alipotelekezwa pale hospitali niliamua kujibebesha mzigo mzima wa jukumu la kusimamia matibabu yake japo nilipata msaada mkubwa sana toka kwa dokta Anderson na mkewe Sara.
Historia ya maisha yangu kipindi cha nyuma ilinifanya kuwa mtu mkatili sana lakini sikuwa hivyo kwa Patrick. Yeye ndiye aliyeanza kunionyesha tumaini jipya lililopotea siku nyingi na
kunifanya nianze kuwa mtu wa tofauti kabisa katika maisha yangu.Nilizaliwa na kuwa yatima miaka mingi sana
iliyopita, nilikulia kwenye kituo cha kulelea watoto yatima cha masista na huko tulifundishwa tabia njema na namna ya kuishi na kila mtu, nilipofika
kidato cha nne nilianza kujihusisha na mapenzi,sikuwa na akili vizuri, nikajiingiza kwenye mapenzi na kijana Alex ambaye na yeye alikuwa ni yatima
pia ila mara nyingi tulikuwa tukionana pale walipokuwa wanakuja kusali kanisani. Nilimpenda sana Alex na niliamini kuwa alikuwa akinipenda
pia, nikiwa kidato cha tano nilipata ujauzito na sikujua cha kufanya,nilifukuzwa pale kituoni na
baada ya kukataa kusema nani alinipa ujauzito,nisingeweza kabisa kumtaja Alex kwakuwa ningekuwa nimemuharibia mipango yake ya kimaisha. Nilikuwa tayari kuubeba ule mzigo wa mimba kwakuwa nilimtakia mema hasa nikitegemea kabisa kuwa angekuja kuwa baba wa yule mtoto, hivyo ile mimba ilibaki kuwa ya kwangu na wala Alex hakutaka kusikia, siku moja
nilikwenda kama kawaida pale ambapo huwa tunakutana na nikamweleza kuhusu ujauzito ule na aliukana kabisa akasema hajawahi kuwa na mahusiano na mimi, nilimweleza kuwa nia yangu si
kumwambia yoyote kuwa yeye ndiye aliyenibebesha ujauzito ila nia yangu ni kumtaka tu ajue kuwa kuna kiumbe chake tumboni mwangu, alikuwa
mkali sana na kuniona kama nilikuwa Malaya,siku hiyo alinipiga sana na kunisababishia maumivu makali,niliondoka na kurudi kwenye magofu yanyumba za watu nilikokuwa nikilala na mchana nilikuwa nikila mabaki ya vyakula vya wahindi. Kila
mtu aliniona kama mimi ni Malaya lakini
sikujilaumu kwakuwa nilitambua athari za nilichokuwa nafanya na Alex ila niliamua kufanya kwakuwa nampenda.
Siku tatu mbele nilianza kupata maumivu makali sana ya tumbo na baadaye nilianza kutokwa na damu mabongemabonge, sikuwa na wakumlilia
zaidi ya kumuomba mungu anisaidie, nilitokwa na damu siku mbili mfululizo huku maumivu ya tumbo yakizidi, sikuwa na dawa ya kumeza kwakuwa sikujua ni dawa gani nimeze na hata fedha ya
kununulia dawa sikujua ningeipata wapi, nilikaa nikitafuna majani ya alovera na baada ya kutokwa damu kwa muda wa siku mbili tumbo lilitulia na sikujua madhara ya kile kilichonitokea yatakuwa
wapi ila nilichofahamu ni kuwa mimba imetoka.Katika mihangaiko yangu jijini nilikutana na msichana wa umri kama wangu kwa kipindi hicho na yeye aliniambia anakwake hivyo tukakae nae na atanifundisha biashara, nilimkubalia kwakuwa sikuwa na machaguo ya kutosha na hapo alinipeleka kwake, palikuwa na chumba kimoja tu lakini kilichojaa vitu mbalimbali vya thamani,nilikaa pale siku moja lakini nilikuwa nimeshagundua kuwa alikuwa akijiuza,kuna muda
mwanaume alikuja pale na walianza kushikana mbele yangu, nilinyanyuka na kutaka kutoka lakini yule dada alinikataza na kuniambia kuwa ile ndiyo
biashara na natakiwa nijifunze, nilijizuia sana na kutaka kuondoka lakini bado maisha yale
niliyokuwa nikiishi yalikuwa ni hatari sana. Hivyo nilikubaliana na yule dada na tulianza biashara hiyo, nilifanya kwa shingo upande lakini kazi ilikuja
kunishinda pale wateja waliokuwa wakija pale walipotaka kufanya mapenzi na mimi kinyume na maumbile, nilikataa katakata na hapo yule msichana alinifukuza kwake, niliondoka na kwenda
kwenye kile kituo kuomba wanisaidie lakini walinikataa, hivyo ikabidi niingie mtaani tena,nilikutana na mzee mmoja akaniahidi atanipatia kazi nyumbani kwake na mimi nilikubaliana naye na hapo nilipata kazi ya ndani kwa huyo mzee,baada ya mwezi mmoja tu wa kazi vioja vilianza baada ya watoto wake wa kiume kuanza kunitaka,nilikataa mara nyingi lakini kuna siku wakati yule baba amesafiri tukabaki na wanae watatu wa kiume tu, siku hiyo nilitoka bafuni na kuingia chumbani kwangu, nilipovua kanga na kuanza kujifuta maji nilishtuka kuona wale vijana ndani ya
chumba changu, nikajifunika na ile kanga lakini walininyanganya na wawili walinishika kwa nguvu kisha waliniingilia kwa zamu, niliumia sana
kwakuwa walitumia nguvu nyingi sana lakini nilipanga kuja kumuambia baba yao japo waliniambia wangenifanyia kitu kibaya kama ningesema kwa baba yao. Mzee wao aliporudi nilimueleza ukweli lakini hakunielewa zaidi ya
kunifokea kuwa nimeleta umalaya wangu ndani ya nyumba yake, niliamua kunyamaza kimya na kuendelea na kazi zangu, ile nyumba hakukuwa na
mwanamke kwakuwa mke wa huyo mzee alikuwa nje ya nchi kwa masomo na hata watoto wake walikuwa ni watu ambao hawakuwa wakukaa nyumbani sana.
Wiki tatu baada ya kubakwa na wale watoto,niliamka asubuhi na kujikuta chumbani kwa yule mzee, nilikuwa nimechoka na nilishangaa nilifikaje
lakini akili yangu ilikumbuka kuwa jana usiku yule mzee alileta juice na kunipa ili ninywe, nikagundua
kuwa aliniwekea kilevi kwenye ile juice na kunibeba hadi chumbani kwake. Kilichoniliza sio yeye kuniingilia kimwili bila ridhaa yangu ila ni yeye
kuniingilia kinyume na maumbile, nililia sana lakini hakuonekana kujali;
sio sawa ulivyonifanyia nilimuambia huku nikilia lakini hakunisikiliza.
binti wewe kazi yako hapa nyumbani ndiyo hiyo,yani wewe mimi nikulipe elfu 15 kwa mwezi na nikulishe na ulale kwangu kwa kazi ya kupika,
kudeki, kufua nguo za watu wote humu ndani na kufanya usafi mwingine tu?,,ni sawa hivyo kweli?Fedha yote hiyo kwa kazi ndogo tu ya kufanya
usafi aliniambia huku akicheka.
utajisikiaje kama binti yako ndo angefanyiwa hivyo nilimuuliza huku nikimtazama.
mwanangu hawezi kuwa beki tatu, tena nyamaza kabisa usianze kunihubiria hapa, kafungashe mizigo yako uondoke maana utatuwekea sumu huku ndani, fungasha nikitoka hapa uwe nje ya hii
nyumba, chukua fedha zako hizo alinisukuma na kunipa shilingi elfu 30, nililia sana lakini sikuwa na
mahali pa kwenda, nilikwenda polisi kuripoti lakini chakushangaza mwanamke mwenzangu aliyekuwa pale ambaye ni polisi alikuwa wakwanza kunifukuza na kuniita mimi Malaya, aliyeonyesha
nia ya kunisaidia alikuwa kijana mwingine askari lakini tulishindwana baada ya yeye kunitaka kimapenzi kama rushwa. Niliamua kumuachia mungu kila kitu lakini nilimchukia kila mwanaume
duniani na nilipanga kutokuja kuolewa wala kubeba ujauzito kwakuwa kama ingetokea ningezaa mtoto wa kiume nisingempenda kabisa
 
Nakumbuka ilikuwa ni siku ya ukimwi duniani ambapo shirika la misaada la marekani lilikuwa likifanya kampeni ya kupima kwa hiari, nilikwenda
kupima ili nijue afya yangu na hapo ndipo nilikutana na dokta Anderson, nilimueleza kila kitu kuhusu maisha yangu wakati alipokuwa akinipima,
na alisema kuwa angenisaidia kurudi shule na mpaka pale ambapo ningetaka kwenda kitaaluma.
Nilirudia kidato cha nne kwa msaada wa fedha za mzee Anderson na mkewe Sara, walikuwa nje ya nchi lakini walikuwa wakinitumia fedha vizuri na
kwa wakati, nilianza kuona matumaini ya maisha tena na baada ya kumaliza kidato cha nne nilifaulu vizuri na kuchaguliwa kwenda kidato cha tano kilakala sekondari kwa mchepuo wa PCB (fizikia,
kemia na baiolojia), kidato cha sita nilifanikiwa kufaulu kwa daraja la kwanza na hapo ndipo dokta Anderson aliponichukua na kunipeleka kusoma
nchini Australia kama daktari na baadaye shahada yangu ya pili nilisomea mambo ya magonjwa ya akili, nilifanya kazi na dokta Anderson miaka yangu
yote mpaka nilipoomba uraia wa huko na kujivua uraia wa Tanzania, sikuwa na hisia na wanaume kabisa na mwaka mmoja kabla ya kumfahamu Patrick nilikuwa kwenye mahusiano na mwanamke
mwenzangu, nilikuwa msagaji lakini yote haya ni kwakuwa hisia zangu zilihama na kwenda kwa wanawake wenzangu.
Yaliyomtokea Patrick yalinikumbusha sana yaliyotokea Tanzania na hiyo ilikuwa sababu ya mimi kujitolea kumsaidia. Kwa ufupi Patrick
alirudisha hisia zangu juu ya wanaume,
mwanaume pekee niliyekuwa nikimuona kama mungu wangu ni mzee Anderson lakini wengine wote hata madaktari wenzangu niliofanya nao kazi
walinijua kuwa sikuwa nawapenda hata kidogo,wengi walijua kuwa mimi ni msagaji na walichukia tabia yangu hiyo lakini kwangu ilikuwa ni faraja na
nilijisikia vizuri sana kuwa kwenye mapenzi na mwanamke mwenzangu, nilimpenda sana na yeye alinipenda na alinipa kila nitakacho na wala
sikuhitaji mwanaume. Lakini uwepo wa Patrick pale hospitali ulinibadilisha taratibu na hata Nancy
ambaye ndiye alikuwa mpenzi wangu alianza kulalamika kuwa nimemsahau,
 
nilimueleza ukweli kuwa kwasasa sitaweza tena kuwa naye kwakuwa
nahisi nampenda mtu mwingine. Alilia lakini nilipomueleza kiundani alinielewa. Kwa miaka sita
yote Patrick akiwa kitandania kama mfu nilikuwa naye pembeni, kuna muda nililala pembeni naye usiku kucha, kuna wakati nilikuwa siendi kwangu
baada ya kazi na badala yake nilikuwa nikikaa pale chumbani kusubiri mda atakaofungua macho,nilitaka japo kuisikia sauti yake, sura yake nzuri na
ya kitoto ilinifanya nimpende,nilimuonea huruma
kwa alichotendewa lakini pia niliona nina nafasi yakumsaidia, miaka sita na mwezi mmoja ulipotimia siku hiyo ilikuwa asubuhi nikaona manesi
wakikimbizana huku na huko na dokta Anderson alikuwa akikimbia kuelekea chumba alichokuwa amelazwa Patrick, sikujua kilichoendelea ila
nilijikuta nikianza kulia kwakuwa nilidhani Patrick amefariki kwasababu jana yake usiku hali yake
haikuwa nzuri, sikuweza kwenda kule kwakuwa nilikuwa naingia kwenye chumba cha upasuaji hivyo nilijikaza na kuingia na jopo la madaktari
wengine, tulifanya upasuaji kwa masaa manne mfululizo, baada ya kutoka nilikutana na dokta Anderson aliyekuwa anaonekana akitabasamu;
Ameamka na yuko salama kabisa aliniambia huku akinifata na kunikumbatia, niliona kabisa
machozi yakinitoka.
Natumaini furaha yako itazidi Pamela na kazi kubwa kwasasa ni kuhakikisha Patrick anakuwa salama na hali yake inarudi kama mwanzo,naamini hiyo ndiyo kazi kubwa uliyokuwa nayo kwasasa binti yangu alinieleza hayo na mimi
nilipata faraja sana, dokta Anderson aliielewa furaha yangu na siku zote alinichukulia kama Semphroza ambaye ni binti yake aishiye marekani
na mumewe. Hayo ndiyo yalikuwa maisha yangu kabla ya Patrick kuamka.
*******
Mary Robert nilisikia Patrick akitaja jina la yule mwanamke aliyemtelekeza, nililia kwa furaha japo
nilijua lengo langu la kuwa na Patrick lingekuwa gumu sana kama angekuwa bado anampenda Mary. Nilifanikiwa kukaa na Mary na kuongea naye miezi michache kabla ya yeye kuondoka, alikuwa
anaonekana kama msichana wa kisasa zaidi,alikuwa ni mtu wa kuongea na simu kila saa, mtu ambaye ni msiri sana na mtu anayekwenda na mda, hakuwa muongeaji sana wala hakutaka
kukaa na mtu mda mrefu, sikuweza kujua kama anampenda kweli Patrick au la japo baada ya yeye kuondoka ndiyo nilikuja kujua kuwa hakuwa mvumilivu.
Unamkumbukaje Mary Robert nilimuuliza Patrick ambaye alionekana akiwa ameduwaa huku machozi yakimtiririka.
sikumbuki, simkumbuki Mary, sielewi kitu alizidi kulia huku akitazama mbele kama alikuwa akiona kitu, nilimshika na kumkumbatia huku na mimi
machozi yakinitoka, ilionekana kama anajitahidi sana kukumbuka lakini haikumsaidia hiyo.
Tafadhali kama unajua chochote kuhusu Mary nieleze, yeye ni nani, anafanya nini kwenye maisha yangu aliniuliza huku akilia.Nilimuacha pale na kwenda kufungua kabati kisha nilitoa boksi lenye barua na pesa ambayo Mary
aliiacha kwenye mfuko pale hospitali kabla hajaondoka bila kuaga, sikuwahi kuisoma ile barua kwa miaka yote hiyo, wala sikuwahi hata siku moja
kutumia zile pesa. Nilifungua lile boksi na kutoa ile barua na yale mabunda ya pesa nikayaweka pale
kitandani kisha nilimkabidhi ile barua na yeye akaifungua, niliona machozi yakimtoka kila alipokuwa akisoma mstari mmoja wa ile barua,sikuwa najua ni nini kimeandikwa kule ndani mpaka nilipoichukua ile barua na kuanza kuisoma.
Nilitokwa na machozi na kumgeukia Patrick.Pamela ni nini kinaendelea mbona sielewi kila kitu aliniuliza huku machozi yakiwa yameufumba
uso wake, nilimuonea huruma kwakuwa nilielewa maumivu ayapatayo kwa hilo limtokealo. Ile barua ilisomeka hivi;
mpendwa mume wangu,Nakuandikia ujumbe huu kwa uchungu na masikitiko makubwa. Najua huwezi kupona tena katika maisha yako kwani daktari amenieleza kuwa
uwezekano wa wewe kurudisha kumbukumbu zako ni mdogo sana,,nilipenda kuwa na wewe Patrick na unalijua hilo lakini sikuwahi kufikiri kuwa nitakuja
kuishi na wewe katika hali hiyo uliyokuwa nayo,,honeymoon ndo chanzo cha yote, huwezi kunikumbuka hata mimi najua,,nilikupenda sana Patrick, lakini nina malengo mengi ya kuyatimiza
kabla ya kuingia kaburin hivyo sina budi kukuacha na kwenda kuendeleza maisha huko nyumbani,,nisamehe, sina jinsi ya kufanya zaidi ya
kwenda kuwaambia nyumbani kuwa tulipata ajali kwenye boti na ulipotelea baharini,,nimeacha kiasi
cha fedha cha kutosha naamini kitakusogeza,,ikiwa hutafanikiwa kuisoma barua hii na ikitokea
kuwa umepoteza maisha basi jua kuwa ninakazi kubwa ya KUMALIZIA MENGI NILIYOANZISHA NAKUPENDA,nakupenda sana ila siwezi kuendelea kuishi na wewe hapa maana itakuwa napoteza muda. MAISHA MEMA Patrick.
Mimi Mary
Ilisomeka sehemu ya barua hiyo.
 
Sehemu ya Tatu

Kwa Mary Robert.2010
Ilikuwa inaelekea saa 5 ya usiku, ile simulizi
ilikuwa imenishika sana na sikutamani wamalize,
niliendelea kusikiliza mahojiano yale kwa makini
sana na yule msichana Pamela alikuwa anaendelea
kusimulia.

PAMELA
Niliendelea kumtazama Patrick huku nimeshikilia ile barua, alikuwa akifikiria mbali sana na sikujua
nimuanzeje kwakuwa alikuwa kwenye wakati mgumu sana.
Patrick nilimuita huku nikimshika bega.Alinigeukia na kunitazama huku machoziyakimtoka.
Usilie Patrick nipo hapa kwaajili yako nilimsogelea na kumkumbatia, haikuwa rahisi kuvumilia kumuona mtu umpendaye akilia mbele yako kwa maumivu ambayo wewe usingeyavumilia
kama ungehitajika kuyakabili.
Kwanini Mary amenifanyia hivi,sikustahili kufanyiwa hivi aliongea hayo huku akiendelea
kutoa machozi. Alikuwa tayari amesharudisha fahamu na sasa alielewa kila kitu kilichokuwa kikiendelea. Hii ilinipa faraja sana kwakuwa siku
zote nilitamani akumbuke kila kitu tena ili na mimi niwe na furaha, nilimtazama usoni na kuona jinsi gani alikuwa akimpenda Mary na alikuwa anaumia
moyoni kwa kilichotokea.

SIKU TATU MBELE
Patrick una mpango gani kwahiyo maana leo ni siku ya pili huongei chochote nilimuuliza baada ya kuchoka kumuona kila mara akikaa peke yake na
kutaka kuwa peke yake, ile hali iliniumiza sana sikuelewa wala kujua nimsaidie vipi, lakini utatuzi
pekee niliokuwa nao kwa wakati huo ni kumpenda kwa dhati na kumfanya amsahau Mary japo nilijua fika kuwa kumsahau mtu uliyempenda kwa dhati ni sawa na kujaribu kumkumbuka mtu ambaye
hujawahi kukutana naye.
sijui mpango nilionao Pamela, sijui ni nini nafikiria wala namna ya kufanya chochote aliongea hayo huku akitazama mbele kabisa ya ufukwe wa bahari.
Ulijuana wapi na Mary? ndilo swali nililomuuliza wakati akiendelea kutafakari, alinishika mkono na
kuondoka na mimi kuelekea ufukweni na tulipofika alianza kunisimulia historia yake na Mary.
Nilimjua Mary miaka miwili kabla ya kufunga nae ndoa. Tulikuwa tukiishi naye mtaa mmoja na sikumjua kwa kipindi cha udogo wake bali kipindi cha ukubwa wake. Alizaliwa pale mtaani kwetu
kule Tanzania, mimi sikuzaliwa pale, nilizaliwa sehemu nyingine lakini kwakuwa wazazi wangu walikuwa wameachana toka utoto mwangu
nililazimika kuja kuishi na baba na mama mwingine ambaye alikuwa na mtoto mmoja aitwaye Mark, kwaiyo katika familia hii tulikuwa wawili tu, mimi na mdogo wangu Mark, katika muda wote tuliokaa pale, nyumba ya kina Mary
ilikuwa ikikaliwa na mfanyakazi tu, nilielezwa kuwa mwenye nyumba ile anaishi marekani na anafanya
kazi huko, ana mtoto mmoja wa kike na mkewe nalishafariki siku nyingi nyuma. Miaka mingi baadaye walirudi yule mzee na mwanae Mary,alikuwa ni msichana mrembo sana, mrefu wa wastani, mwenye kila aina ya sifa, alikuwa ni
mtoto wa kisukuma aliyechanganyika na
mnyakyusa, mchanganyiko huo ulizalisha kitu kinachoonekana. Nilipomuona sikushtuka sana kwakuwa sikuwa na mawazo naye. Mara nyingi nilimsikia Mark akimsifu na walikuwa wakiongea
mara kwa mara kwenye simu, ni wakati huo ndipo nilikuwa nimeshahama nyumbani na kuanzisha kampuni yangu ya harusi na mapambo, iliyoitwa PATRICK WEDDING AND DECORATION COMPANY LTD, ilikuwa ni kampuni kubwa kuliko zote Tanzania kwenye mambo ya upangaji wa harusi na
upambaji. Kampuni hii ilikuwa inachukua tenda kamili za harusi, yaani mtu kama anaharusi au sherehe yoyote anakuja na kutoa fedha yote kwaajili ya sherehe na sisi tulikuwa tunatafuta ukumbi, tunahusika na kuandaa mavazi yao, sare
na kadi za waalikwa, muziki na mshereheshaji,tulikuwa tunachukua video kwenye hayo maharusi na kutoa usafiri, pia baada ya kumaliza mkataba
wa kusimamia harusi hizo ilikuwa mteja akitaka kwenda mapumizikoni basi tunaingia naye mkataba wa kumfanyia utaratibu wa kwenda na kuhakikisha usalama wake mpaka atakaporudi. Hii
ilikuwa ni kampuni kubwa sana iliyoajiri watu zaidi ya hamsini wenye fani mbalimbali, ni kampuni ya
ndoto yangu. Nilipokuwa katika shughuli zangu za kikazi nilikuja kukutana na Mary siku alipokuja ofisini
 
kwaajili ya kuomba kuonana na
mimi ili afanye mahojiano juu ya mafanikio yangu na maisha ya mapenzi, hapo ndipo niligundua kuwa Mary alikuwa akimiliki kampuni iliyokuwa
ikichapisha jarida la EXLENT MEN lilikokuwa likitoka kila mwezi na kuelezea juu ya wanaume wenye mafanikio walio chini ya umri wa miaka 35.
Alikuwa ni msichana mcheshi sana, mjanja na ambaye alijitolea maisha yake kujiimarisha na kuwa mfano wa kuigwa, alikuwa mmoja kati ya wanawake wachache ambao hawakuwa maarufu lakini walikuwa machachari na wachapakazi tena
akiwa na umri wa miaka 25 tu.

**************
karibu sana Mary ilikuwa ni siku aliyokuja rasmi kwaajili ya yale mahojiano, alikuja na timu ya
wafanyakazi wake ambao ni wapiga picha na waandishi wengine, ni mara chache saba meneja akaja kuhoji mtu badala ya waandishi waajiriwa ila
kwangu mimi alikuja kunihoji yeye mwenyewe,hivyo niliwakaribisha hadi sehemu maalumu iliyokuwa imeandaliwa kwajili ya mahojiano hayo.
Asante sana ndugu Patrick, najua mimi na wewe tunajuana ila leo nimekuja kikazi zaidi,,hahaa
aliongea huku akicheka na wakati huo wale wengine walikuwa wakifunga kamera zao na muda sio mrefu mahojiano yalianza;
kwanza nilitaka kujua juu ya mafanikio yako bwana Patrick aliniuliza swali huku akitabasamu,hapo ndiyo nilianza kugundua hisia zangu kwa Mary, japo alionekana kabisa kuwa alikuwa si
msichana mwepesi sana kukubali hisia za
mwanaume kuingilia maamuzi ya fikra zake.
mh,,baada ya kumaliza chuo kikuu ambapo nilisoma mambo ya ujasiriamali, ndiyo niliandika mradi huu wa kuanzisha kampuni, sasa zilikuwa
zikihitajika milioni 150 ilikuanzisha mradi lakini niliweza kufanikisha kupata milioni tano tu toka
kwa mzee wangu, hivyo nililazimika kuingia benki kuomba mkopo wa milioni 30 kwa kutumia kiwanja nilichopewa na mzee, baada ya kupata mkopo
nikaanza mradi wa kuku elf 3 ambao ndio ulionipa mtaji wa kuanzisha hii kampuni wakati nikimueleza hayo yeye alikuwa makini sana kunitazama usoni, niliona upendo toka kwenye sura
yake pale nilipomtazama.
uuum,,unakipato cha shilingi ngapi kwa project zako zote aliniuliza huku akicheka.
napata wastani wa milioni 40 kwa mwezi baada ya kutoa matumizi yote nilimjibu na kumtazama tena machoni na yeye aliona aibu na kutazama pembeni.
kwanini hujaoa aliniuliza huku akitabasamu.
mmh, nadhani muda bado kidogo, lakini pia wakumuoa bado sijampata, wengi wanatamani mali nilizonazo lakini mimi nahitaji mtu wa kumpenda Patrick na si mali za Patrick mahojiano
kwa siku hiyo yaliendelea kwa muda kidogo na baada ya pale tulipata chakula cha mchana na wafanyakazi wake aliokuja nao pamoja na baadhi
ya wafanyakazi wangu. Tulibadilishana namba za simu za mkononi na hapo tulianzisha urafiki wetu.
Nilimuajiri Mark kama muhasibu kwenye kampuni yangu na nilikuwa nikimlipa mshahara mara tano zaidi ya wafanyakazi wengine waliokuwa na vyeo
vinavyoendana na yeye, yote ni kumfanya yeye kama ndugu yangu awe na maisha bora, ingawaje mimi na Mark hatukuwa karibu sana au kuwa tunakaa na kuzungumza kuhusu mapenzi, bali mda
mwingi tukikaa tulikuwa tukiongelea kazi na maisha tu.
 
MIEZI MIWILI BAADA YA MAHOJIANO
Ikawa ni miezi miwili toka Mary aje kunihoji,wakati huo nilikuwa nimeshuka uwanja wa ndege nikitokea Afrika ya Kusini kwenye biashara zangu,
nikashtuka kumkuta Mary pale uwanja wa ndege akinisubiri, kilichonishangaza ni kwamba toka baada ya mahojiano nilikuwa nimeongea naye kwenye simu mara mbili tu na sikuwahi kumwambia naenda nje wala kumuambia narudi Dar hivi karibuni.
umekuja kufanya nini Mary nilimuuliza pale alipokuja na kunikumbatia.
Nimekuja kukupokea aliongea huku akicheka kama kawaida yake.
Nani kakuambia juu ya safari yangu nilimuuliza wakati tukitembea kuelekea nje, hakunijibu haraka
ila alipokea mizigo yangu na kuingiza kwenye gari yake kisha alinifungulia mlango na kuniambia niingie.
vijana wangu wale pale wamekuja kutuchukua
nilimuambia huku nikiwa nimesimama namtazama jinsi alivyokuwa akicheka.
mwambie sekretari wako aende akapande kule na huyo kijana wako mwingine, mimi leo nitakuwa dereva wako na napenda twende kwangu kwanza then nitakupeleka kwako nilimtizama na kutabasamu, sikuwa na la kusema zaidi ya
kumkubalia name niliingia kwenye gari yake tayari kwa kuondoka. Nilipofika kwake hakukuwa na mtu zaidi ya mlinzi wake, ilikuwa ni nyumba ndogo ila
yenye bustani kubwa na iliyonakshiwa vizuri sana kwa rangi za kuvutia, alikuwa na magari mawili ya
kifahari yaliyopendezesha muonekano wa ile nyumba. Tuliingia mpaka ndani na kisha aliniacha pale sebuleni huku nikishangaa jinsi alivyokuwa
amepapamba pale ndani, alirudi na kuniambia kuwa bafu liko tayari kama nataka kwenda kuoga.
hahaa sio busara kuoga nyumba ya mtoto wa kike nilimueleza huku nikicheka kama yeye alivyokuwa akicheka wakati akinieleza hayo.
mimi kwako ni zaidi ya mtoto wa kike, tafadhali nifate nikuonyeshe bafu lilipo na nguo zipo za wewe kubadilisha nilinunua kwaajili yako aliongea
hayo na hakunipa muda wa kuongea chochote,alinitazama huku akitabasamu na kuelekea kwenyenkorido na mimi nilimfata, aliingia chumbani na
kunionyesha bafu la chumba chake na nguo zilikuwa zipo pale kisha alifunga mlango na kurudi sebuleni, nilijiuliza sana nini nia ya Mary kufanya
vile.
Happy birthday Patrick niliisikia ile sauti baada ya kutoka bafuni na kwenda kwenye meza ya chakula aliyokuwa ameandaa, kiukweli sikuwa na
habari kuwa siku hiyo ilikuwa ni kumbukumbu ya siku yangu ya kuzaliwa, lakini swali lilikuwa ni je
Mary alijulia wapi siku yangu ya kuzaliwa na alifanya vile kwa nia gani.
umejuaje siku hii Mary nilimuuliza baada ya kumaliza kuzima ile mishumaa.
Nakupenda Patrick, ndiyo maana nafatilia kila linalokuhusu, natamani sana uwe mume wangu,naamini wewe utanijali na kunipenda kwakuwa
nimeona upendo kwenye macho yako aliongea hayo huku akimaanisha, niliyaamini maneno yake
kwakuwa aliyaongea kwa sauti ya ujazo wenye kumaanisha.
Mary unauhakika na unalolisema hapa?
Nakupenda pia na nina hisia na wewe toka siku ulipokuja kunihoji pale ofisini kwangu, lakini
nayajua mapenzi vizuri, si kitu cha kukikurupukia sana kama tunavyoweza kukurupukia mambo mengine nilimuuliza jambo ambalo nilikuwa na uhakika nalo kuwa jibu lake lilikuwa chanya.
nina jiweza Patrick kiuwezo na kimaishanninachofata kwako ni penzi tu aliongea huku akinishogelea na kunishika midomo yangu. Siku ile
ilikuwa ndiyo siku ya kwanza ya mapenzi yangu na Mary, nilimvisha pete ya uchumba kama miezi
mitatu baadaye na yeye ndiye alikuwa maisha yangu tena, alikuwa faraja yangu na kiongozi wa hisia zangu.
Baaya miezi sita toka nimvishe pete Mary nilisikia kuwa Mary alikuwa na mahusiano na Mark,nilishtuka lakini kwakuwa nilikuwa nina kazi nyingi
za kufanya sikutaka kufatilia kwanza lile jambo.Mary nayeye hakuwepo nchini hivyo sikuwa na namna ya kumuuliza kwa ukaribu, nilisubiri hadi siku aliporudi ndipo nilipomuuliza;
haikuwa hata ni mahusiano, ni utoto tu, mimi na Mark tulisoma shule moja ya msingi na tuliishi kipindi kirefu sana kwa ukaribu na hata sekondari
tulisoma nae, yeye ndiye aliyenitoa bikra lakini ilikuwa ni katika hali ya utoto
 
nilipofika kidato cha
tatu mama yangu alifariki na nililazimika kwenda kuishi na baba nchini marekani, niliporudi nilikuwa
na mawasiliano na Mark lakini sikuwa nampenda tena alinieleza hayo na mengine mengi lakini nikaona busara ni kumfata Mark na kumuuliza.
****
Niliondoka jioni ya siku ya jumatano na kwenda nyumbani kwa Mark, haikuwa kawaida kwa mimi kumtembelea sana nyumbani kwake mara kwa mara.
karibu bro, leo naona umepotea njia alinikaribisha huku akinitania, Mark alikuwa ni ndugu yangu wa
damu, tulizaliwa mama tofauti lakini baba yetu alikuwa mmoja lakini yeye alikuwa na tabia ya
tofauti na mimi, mimi nilikuwa muwazi sana,nikikasirishwa huwa nasema ila yeye hata umkasirishe sio rahisi sana kusema au kukuonyesha.
hapana leo nimekuja kukucheki isijekuwa ushaoa
na watoto unao huku ndani lakini husemi,,hahaa
nilimtania na kuingia ndani kisha nilikwenda kwenye jokofu na kujichukulia kinywaji.
Vipi tena bro, ni kuhusu wazee au ni nini
aliniuliza huku akiwa amesimama.
Hapana ni kitu kingine, embu keti chini
nilimuambia na yeye aliketi.
Mark nakaribia kuoa, umri unaenda na nina kila kitu, nafikiri sasa ni muda wa mimi kuoa na kuanzisha familia mapema kabla sijaishiwa nguvu
za kutafuta pesa nilimuambia hayo na kuvuta pumzi, sikujua niliielezee vipi lile swala.
Ni wazo zuri bro, na naamini Mary atakuwa mke bora kwako aliongea kwa sauti ya upole iliyojaa unyonge.
natumaini hivyo lakini kuna swala linanitatiza kidogo nilimuambia hayo huku nikimtazama usoni.
ni nini tena bro? aliniuliza huku akionekana kuhofia kitu fulani.
Ni kuhusu mahusiano yako na Mary nilimueleza hayo na kumfanya abadilishe mkao, alionekana hakuwa tayari san kuanza kuliongelea hilo lakini
sikuelewa sababu ni nini.
Bro, mimi na Mary tulikuwa wapenzi, na nadhani kwasasa hakuna linaloendela baina yetu mimi na yeye, kwahiyo wewe endelea tu alinijibu kwa kifupi
sana na alionekana alikuwa amebadilika kabisa,sikujua ilikuwaje mpaka akawa vile lakini niliyachukua maneno yake kama Baraka zake kwangu, hivyo baada ya kumsoma Mary kwa muda mrefu sasa tuliamua kuunganisha kampuni
zetu na kuwa kampuni moja, tulikuwa
tukishughulika na utoaji wa majarida na mambo ya harusi kwa pamoja, kampuni mpya iliitwa PATRIMARY GENERAL ENTERPRISES LTD, na Mary
alikuwa Meneja Masoko na Muhariri mtendaji wa Jarida, Mark alikuwa ni Muhasibu na Mkurugenzi
mtendaji, mimi nilibaki kuwa Meneja mkuu,wafanyakazi wote walibaki kama walivyokuwa na wengine tuliwapandisha cheo. Baadaye nilifunga
ndo takatifu na Mary na baadaye tulikuja mapunziko huku FIJI, yote yaliyotokea yalitokea tukiwa huku Fiji. Alielezea Patrick huku
akibubujikwa na machozi.
bado unampenda Mary nilimuuliza huku machozi yakinitoka, sikutaka aseme kuwa anampenda kwakuwa tayari mimi nilikuwa nampenda yeye.
Nampenda sana, sikuwahi kuacha kumpenda
maneno hayo yaliuchoma sana moyo wangu,
nilinyanyuka pale na kuondoka kurudi nyumbani,Patrick alibaki pale ufukweni, nilifika mbele kidogo nikasikia mlio mkubwa wa bunduki, nilishtuka na
machozi yangu yalikauka, nilipotazama nyuma niliona kwa mbali Patrick akianguka.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom