Dubai: Binti mfalme adai kushikiliwa mateka na Baba yake tangu 2018 alipojaribu kutoroka

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,516
9,317
Umoja wa Mataifa umesema utaingilia kati hatua ya mamlaka ya Milki za Kiarabu (UAE) kumshikilia bila hiari Malkia Latifa, binti ya mtawala wa Dubai.

Malkia Latifa amemlaumu baba yake kwa kumzuilia mateka Dubai tangu alipojaribu kutoroka mji huo mwaka 2018.

Katika video iliyorekodiwa kisiri na kuwasilishwa kwa BBC, Malkia Latifa amesema kuwa anahofia maisha yake.

Video hiyo imezua hisia kali kote duniani huku wito ukitolewa kwa Umoja wa Mataifa kuchunguza suala hilo.

Ofisi ya Kamishena Mkuu wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa imejibu wito huo na inaazimia kuhoji kuhusu hali ya Latifa, binti wa mtawala wa Dubai.

Msemaji wa kundi la Umoja wa mataifa linaloshughulikia masuala ya watu kuzuiiliwa bila hiari yao amesema kundi hilo litaanzisha uchunguzi baada ya video ya Malkia Latifa kuhakikiwa.

Ofisi ya Maendeleao na Mambo ya nje ya Uingereza na imeelezea hofu yake kuhusiana na kisa hicho na kuongeza kuwa japo haihusiki moja kwa moja na kesi hiyo itafuatilia kwa karibu matukio hayo.

BBC Swahili
 
Watapiga kelele tu nalo litapita, maana hawawezi kuvamia nchi kumchukua kwa nguvu huyo binti.
 
Back
Top Bottom