Dua zenu tafadhalini

Kila la kheri,mungu ni mwema atakusaidia utatotoa salama na ww na mwanao mtakua salama salimin!
 
Wandugu leo nipo safarini naelekea kilimanjaro! Kutotoa naombeni dua zenu nitotoe salama na madaktari wasigome!

Nkutakia kila la kheri katika safari yako ya kwenda kutotoa. Mungu awe pamoja nawe akujalie uweze kutotoa salama bila matatizo yoyote. Usisite kutujulisha yote yatakayoendelea
 
nimeachwa kidogo...kutotoa ndo nini mpendwa?

Pole sana Shost,
nadhani ulifikiri
KUTOTOA - Amegoma KUTOKUTOA vitu kama Sadaka , au kutokutoa malipo flani hivi.
Jibu umelipata kwenye michango ya wadau.
Kupitia hapa nimtakie mzazi mtarajiwa kila la kheri hasa ukishaingia LEBA
 
pole sana shost,
nadhani ulifikiri
kutotoa - amegoma kutokutoa vitu kama sadaka , au kutokutoa malipo flani hivi.
Jibu umelipata kwenye michango ya wadau.
Kupitia hapa nimtakie mzazi mtarajiwa kila la kheri hasa ukishaingia leba

hapo leba ndo pananiumiza kichwa kwa kweli! Mauchungu yaleeee,kweli mungu alitupa zoez kali saaana
 
Back
Top Bottom