Mnyamahodzo
JF-Expert Member
- May 23, 2008
- 1,932
- 985
Baada ya wabunge wa CCM,CUF na TLP kuwasimanga na kuwatukana wabunge wa CHADEMA na NCCR, Kikwete kuipuuza Kamati ya CHADEMA, na Serikali kukidharau kilio cha umma wa Watanganyika. Ndipo nikaenda katika uwanja wa fikra huru, nikasimama panapo jukwaa la haki nikiziegemea nguzo mbili, moja waliita USAWA na ya pili waliita UTU (wakimaanisha thamani ya utu) ambapo mbele yake palikuwa na meza ya zamani ya mvule iliyofunikwa kitambaa cha samawati kikiwa na maandishi mekundu
" Wana wa Tanganyika, wa makabila yalo changanyika,
Waliozaliwa Tanganyika, Mola ndo kawasimika,
Uhai wao kutunzwa, sii jambo la kupuuzwa"
Ndipo nikainua kichwa changu juu mawinguni na kuomba dua mbele zake Muumba nikisema,
"Ee Mwenyezi Mungu, Mola wetu, mwenye haki. Ulitufanya tukazaliwa Tanganyika si kwa matakwa yetu bali mapenzi yako. Umeliona jambo hili la Katiba namna viongozi wetu walivyotutenda kwa dhuruma na maneno ya kejeli na kutimiliza kwa kutudharau. Basi sasa, ikiwa damu ya mtanganyika yeyote itamwagika kwasababu kudai Katiba ya Haki ya Wananchi kutakakofanywa na Serikali kwa kutumia Polisi ama vyovyote, twaomba ukatulipie kisasi cha damu hiyo juu ya Rais, waziri mkuu, spika, mawaziri wa sheria, mwanasheria mkuu na wabunge wote walioruhusu udhalimu huu.
Ulipokuwa mikononi mwao walikuwa na uwezo kuuzuia bali wao walichagua kutupa kinga cha moto ktk petroli na kukitukuza kiburi chao. Kwa jinsi ileile watanganyika watakavyolia kwa kupotelewa na mzazi wao, mtoto wao ama ndugu yao na wao pia wakalie.
Ee Mola wetu, haki ina wewe, ndiwe mlipiza kisasi kwa ajili ya mnyonge. Damu hiyo ikawe juu yao.
Twaomba ukatulipie kisasi. Amina"