Dr Ulimboka

Aibu juu yao. Waliweza kumpeleka kichaa mahakamani bila hata kumhoji mhusika wa tukio Dr. Ulimboka hadi hii leo, kuna kesi hapo? Maisha ya Dr. Ulimboka kwao ni maisha ya kuku ndio maana hadi hii leo hata waliotajwa na mhusika hawajawahi hata kuulizwa. Hii ndio Tz bana.

Na sisi Wananchi tumekaa kimya wala hatunyanyui midomo yetu kuhoji maendeleo ya kesi ile, wala kutokuhojiwa kwa wahusika wakuu wa tukio lile, kama ambavyo tulipaza sauti zetu kutoa matamko ya kulaani uteswaji ule.......KIMYAAAAAA!
 
Kaka umezungumza jambo la maana kabisa wabongo ni watu wa maneno mengi vitendo sifuri tunachonga sana bila kuteki action. Nawapa Big up wakenya wako serious juzijuzi kabla ya uchanguzi wabunge walikaa bubgeni wakataka kujiongezea posho wakenya hawakubiga kelele kama vile ambavyo sisi tungefanya wao waliandamana na majeneza meusi ambayo idadi yao ilikuwa sawa na idadi ya wabunge wa kenya mwisho wa maandamano yao waliyachoma yale majeneza kama ishara ya kuwazika na walionyesha pia kwenye uchaguzi wa juzi ambapo wabunge wengi walitoswa. Hiyo ni nzuri unaonyesha unachukia jambo kwa vitendo lakini si kwa maneno tu kama tulivyo wabongo hata viongozi wetu wamesha tuzoea wanajua hawa watasema tu nayataisha ikifika wakati wa uchaguzi watatudanganya kwa peremende na tunawapa kura

Aisee umeongea point ambayo imenigusa kweli kweli kuhusu ya wabunge wa Kenya aisee!
 
Hapa niliwahi kuona uzi wa Mjumbe akidai huyu Dr. yuko pale Makerere univ. anasoma sijui kweli?

mkuu yule jamaa ni mmoja ya wapuuzi wa tiss wanatafuta taarifa ili watu wamwambie hayuko makelele ila yuko sehemu fulani
 
Ujue kuongelea hapa hakusaidii wa misri walianzia mitandaoni mpaka mtaani sasa wabongo hapa jamii forum hakutosaidia chochote,aliokuwa anatetea maslahi yao na walipigwa mkwara wa kufukuzwa kazi nao walishagawanywa makundi sasa hapo kuna nini mnategemea hapa jamii forum kama kwenye kijiwe cha kahawa kijijini tu kwani hata waliomteka nao hapa wapo na wanajifanya kusikitishwa na tukio kumbe wanataka kuangalia wana nchi wanalifuatilia vipi suala hili.Mwakyembe aliahidi kusema ya moyoni akala kona ,mwingine wa tindikali ,kimya,Lowasa kawakusanya waandishi wa habari kapigiwa simu kuhakikishiwa kuwa ataendelea kupata shavu kama ilivyokuwa awali.hawa watu wanapigana wakikoseana kwenye maslahi tu kwani hakuna mkweli hata mmoja laiti tungempata mkweli hata mmoja tungefanikiwa.
 
Hiyo video ni ya kuchongwa, kwani hata anachoelekeza lwakatare hakisikiki, huo ni uongo wa hali ya juu kabisa, hizi njama nia za serikali ya ccm na si za chadema. pili kwa nini membe hajakamatwa naye aliapa kuwa ana maadui kumi na moja wakiwemo waandishi wa habari wawili? na alisema atawamaliza mchana kweupe. chanzo Gazeti la matanzania tarehe 13. 03. 2013 la jana. Polisi waache hadaa zao za kutuhadaa.
 
kweli mara ya mwisho magazeti ya tz yalionesha kuwa yule mtuhumiwa wa utekaji,utesaji , na usafirishaji wa Dr Ulimboka kwenda msitu wa mauaji wa Pande,aligoma kula na kwenda mahakamani na ubalozi wa Kenyia ukadaiwa kuingilia kati.
Igizo hili sasa linatatanisha maana mhusika mkuu wa igizo yaani Dr ULIMBOKA hatujui alikokwenda maana press ilimsikiliza Kicheere,Learned ADVOCATE,akizungumza badili yake,Mahakama ikiwa haijamtumia kama shahidi wa Jamhuri,Gazeti lililomtaja mhusika siyo mtuhumiwa wqa utekaji,utesaji na utupwaji wa Dr ULI ,MWANAHALISI na Saed Kubenea vikiwa kifungoni.Neno moja lingetosha yaani kisa chote ni SINTOFAHAMU.
Kwa kuwa sisi tumefananishwa na mnyama pori mmoja (anayefanana katika specie na mwingine ambaye nyama yake ni veri palatable,but declared KHARAMU na TOURATI plus HOLY KORAN)kwa kuwa na kumbukumbu ndogo na usahaulifu mkubwa(partly kwa sababu maisha ni magumu hivyo sehemu kubwa ya wakati tunasaka tonge left and right) tumeachwa ROUND ABOUT!
Dawa ya hili tatizo la kugeuzwa ngiri ni KUGANGAMALA na ISSUE to its whatever conclusion!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom