Dr. Ulimboka hatukuelewi ! ! !

MARCKO

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
2,258
274
Huyu ndugu yetu alikumbwa na machungu yaliyomgusa kila mmoja wetu! Nchi nzima ilizizima, na kuamini (nakuweka msisitizo kwenye tunacho fahamu) kua vyombo vya dola ni wabaya. Tukajitolea kwa matibabu yake, hadi kufikishwa hosiptali SA ambapo hata huko tulihisi serikakali ya Tz bado ingaliweza kumfuatilia na kummalizia !. Mimi kama mimi iliniuma sana.

Tunashukuru Mungu, kwa uwezo wake kapona na karejea nchini. Watu walitoa maoni mengi mitandaoni ambayo naamini ilimfikia kua akija aibukie press conference na kuyasema yote. Hataivyo, kutokusema siku ileile hatukushangaa sana maana jamaa lazima apumzike japo kidogo! Na akusanye kumbukumbu vizuri hata kukumbuka simu yake ilipo! .

MY TAKE:
1. Huu muda uliotumia kukusanya kumbukumbu ni mrefu sana,
2. Unajaza wasiwasi.
3. Hicho unacho subiri kwanini usieleze uma?
4. Hukumbuki kua wewe ungalikwisha 'decompose' (inaniuma sana)
5. Unaumiza vichwa vya watanzania wengine wapenda haki.
6. Vikao na kamati za serikali ni vyanini tena wakati walipopanda gari kukuacha Msituni usiku walijua wamekuua?
7. Utakayo yasema hata sasahivi, bado kutakua na hojaji tofauti kisa kutokuaminika tena.
8. Kumbuka ulishasema watu waachane na familia yako , wewe ndio ufahamuye ukweli.
9. Kumbuka kuna mengi yaliyo wakumba wanao kutetea
10. Mods naombeni msichanganye hii thread na ile inayosema " polisi leo kufunguka. . . . "
 
Si unajua watz tena, mtishie kidogo, kisha mlambishe kajiasali kadogo kwisha habari yake! Atacheza kila ngoma utakayompigia. Mimi naamini kuwa kaasali na kakitisho kadogo kameshaminya haki za mamia ya watz. Si nnaijua sirikali yetu!. Uli angejua hisia zetu angeacha mchezo anaofanya. Hapo ujue anatafutiwa cheo na kazi nzuri na kajumba kanajengwa chapchap ndipo atakuja na kudai...ooh mimi ndiyo najua mchezo wote, aliyenidhuru ni yule aliyekamatwa! Nk, subirini tu mtasema nilisema
 
Huyu ndugu yetu alikumbwa na machungu yaliyomgusa kila mmoja wetu!. Nchi nzima ilizizima, na kuamini (nakuweka msisitizo kwenye tunacho fahamu) kua vyombo vya dola ni wabaya. Tukajitolea kwa matibabu yake, hadi kufikishwa hosiptali SA ambapo hata huko tulihisi serikakali ya Tz bado ingaliweza kumfuatilia na kummalizia !. Mimi kama mimi iliniuma sana. Tunashukuru mungu , kwa uwezo wake kapona na karejea nchini. Watu walitoa maoni mengi mitandaoni ambayo naamini ilimfikia kua akija aibukie press conference na kuyasema yote. Hataivyo, kutokusema siku ileile hatukushangaa sana maana jamaa lazima apumzike japo kidogo! , na akusanye kumbukumbu vizuri hata kukumbuka simu yake ilipo! . MY TAKE: 1. Huu muda uliotumia kukusanya kumbukumbu ni mrefu sana,
2. Unajaza wasiwasi.
3. Hicho unacho subiri kwanini usieleze uma?
4. Hukumbuki kua wewe ungalikwisha 'decompose' (inaniuma sana)
5. Unaumiza vichwa vya watanzania wengine wapenda haki.
6. Vikao na kamati za serikali ni vyanini tena wakati walipopanda gari kukuacha Msituni usiku walijua wamekuua?
7. Utakayo yasema hata sasahivi, bado kutakua na hojaji tofauti kisa kutokuaminika tena.
8. Kumbuka ulishasema watu waachane na familia yako , wewe ndio ufahamuye ukweli.
9. Kumbuka kuna mengi yaliyo wakumba wanao kutetea
10. Mods naombeni msichanganye hii thread na ile inayosema " polisi leo kufunguka. . . . "

Marcko,
Anza kuonyesha ujasiri wako kwa kutaja majina yako matatu na tarehe yako ya kuzaliwa. Hilo tu kwanza.
 
Huyu anajijengea uadui mkubwa na umma rather than hao anaowaogopa.namuonya UKIMYA WAKE UTASABABISHA MADHARA YA USALAMA WAKE TOKA KWA WANANCHI.hao anaowaogopa hawawezi tena kumfanya chochote ata akichezea ndevu zao.ULI UNAJITENGENEZEA BOMU BABA.
 
Wanajamvi taarifa ya Uli kwa watz bado inaandaliwa na watalaam wa kupindisha ukweli tusubiri muda ufike tutasikia 'cooked report' aibu tupu
 
Ameshapewa fungundo maana kimya Dr.Ulimboka kumbuka walikuwa na nia ya kukuangamiza umepona kwa uwezo wa Mungu ungetakiwa kufunguka na kuwaeleza watanzania waliokufanyia huo unyama.
 
huyu ameisha tulizwa subiri wammalize taratibu, imekuwa unafiki sana. Wakiwa kwenye matatizo watanzania niombeeni mwenyezi Mungu akinijalia kurudi salama nitakuja kueleza yote, wakirudi baada ya kulambishwa asali wanakuwa kimya, je mmesahau na Mwakyembe?.
 
kuna kitu gani unachotaka kusikia ambacho hujasikia? Halafu nyinyi mnaotaka aseme ni waongo na wababaishaji wakubwa na waoga. WKama kweli ninyi ni wapiganaji jitokezeni basi hadharani kama mama Kijo Bisimba, mbona mnajificha tu humu kwenye JF.

Dr. Ulimboka na kusihi tena usikubali kwendeshwa na pressure ya watu. Hakuna jipya watu wanalotaka kusikia, kila kitu ulikwisha weka wazi. Huu mfumo unaopambana nao ni mfumo HARIBIFU (Destructive System) unaongozwa na watu jamiii ya REPTILE ambao wanasumu kali ya kufisha. Huwezi kuubadili kwa press conference wala kwa maneno matupu. Watatanzania wamekuombea na Bwana Mungu kasikia maombi yao kakuponya. Kama maandiko yanenavyo " kila jambo lina wakati wake na majira yake hapa chini ya Jua".

Huu utwala wa wanamtandao, utawala uliyojengwa kwenye mfumo haribifu, unaweza kuteka nyala, kutesa na hata kuua lakini hauwezi kuteka nyala kutesa na kuuia KALENDA. Hauwezi kuzuia mawio na machweo ya Jua. Miaka mitatu iliyobakia sio milile, itapita sasa hivi tu. Tuombe uzima, watakamatwa wote waliotaka kukuua.

"How long, not long no lie can live forever" Dr Martin Luther King
 
yeye mwenyewe ajishitukia kuwa alikuwa amekosea kwanza inabidi atuombe radhi watz kwa kutuulia ndugu zetu
 
Si kesi iko mahakamani tumsikie Kova adanganye kwanza ndipo akanushwe? Madaktari wameikataa tume ya Kova, sasa Ulimboka akaseme kwa nani kama vyombo vya habari viliiuambia uma aliyoyasema kabla ila serikali kukanusha kila kitu na kutoa majumuisho hata kabla tume yenyewe haijaanza kazi zake za kuchakachua maelezo?
 
Back
Top Bottom