Dr. Ulimboka hatukuelewi ! ! !

kuna kitu gani unachotaka kusikia ambacho hujasikia? Halafu nyinyi mnaotaka aseme ni waongo na wababaishaji wakubwa na waoga. Kama kweli ninyi ni wapiganaji jitokezeni basi hadharani kama mama Kijo Bisimba, mbona mnajificha tu humu kwenye JF.

Dr. Ulimboka, na kusihi tena usikubali kwendeshwa na pressure ya watu. Hakuna jipya watu wanalotaka kusikia, kila kitu ulikwisha weka wazi. Huu mfumo unaopambana nao ni mfumo HARIBIFU (Destructive System) unaongozwa na watu jamiii ya REPTILE ambao wanasumu kali ya kufisha. Huwezi kuubadili kwa press conference wala kwa maneno matupu. Watanzania wamekuombea na Bwana Mungu kasikia maombi yao kakuponya. Kama maandiko yanenavyo " kila jambo lina wakati wake na majira yake hapa chini ya Jua".

Huu utwala wa wanamtandao, utawala uliyojengwa kwenye mfumo haribifu, unaweza kuteka nyala, kutesa na hata kuua lakini hauwezi kuteka nyala kutesa na kuiua KALENDA. Hauwezi kuzuia mawio na machweo ya Jua. Miaka mitatu iliyobakia sio milele, itapita sasa hivi tu. Tuombe uzima, watakamatwa wote waliotaka kukuua.

"How long, not long no lie can live forever" Dr Martin Luther King
 
Huyu ndugu yetu alikumbwa na machungu yaliyomgusa kila mmoja wetu!. Nchi nzima ilizizima, na kuamini (nakuweka msisitizo kwenye tunacho fahamu) kua vyombo vya dola ni wabaya. Tukajitolea kwa matibabu yake, hadi kufikishwa hosiptali SA ambapo hata huko tulihisi serikakali ya Tz bado ingaliweza kumfuatilia na kummalizia !. Mimi kama mimi iliniuma sana. Tunashukuru mungu , kwa uwezo wake kapona na karejea nchini. Watu walitoa maoni mengi mitandaoni ambayo naamini ilimfikia kua akija aibukie press conference na kuyasema yote. Hataivyo, kutokusema siku ileile hatukushangaa sana maana jamaa lazima apumzike japo kidogo! , na akusanye kumbukumbu vizuri hata kukumbuka simu yake ilipo! . MY TAKE: 1. Huu muda uliotumia kukusanya kumbukumbu ni mrefu sana,
2. Unajaza wasiwasi.
3. Hicho unacho subiri kwanini usieleze uma?
4. Hukumbuki kua wewe ungalikwisha 'decompose' (inaniuma sana)
5. Unaumiza vichwa vya watanzania wengine wapenda haki.
6. Vikao na kamati za serikali ni vyanini tena wakati walipopanda gari kukuacha Msituni usiku walijua wamekuua?
7. Utakayo yasema hata sasahivi, bado kutakua na hojaji tofauti kisa kutokuaminika tena.
8. Kumbuka ulishasema watu waachane na familia yako , wewe ndio ufahamuye ukweli.
9. Kumbuka kuna mengi yaliyo wakumba wanao kutetea
10. Mods naombeni msichanganye hii thread na ile inayosema " polisi leo kufunguka. . . . "

Unataka Ulimboka aongee nini? Je kile alichoongea akiwa Kitandani hukuiamini? Hata akiongea sasa hivi utachukua hatua gani?

Mwacheni Ulimboka apumzike.
 
Ameshapewa fungundo maana kimya Dr.Ulimboka kumbuka walikuwa na nia ya kukuangamiza umepona kwa uwezo wa Mungu ungetakiwa kufunguka na kuwaeleza watanzania waliokufanyia huo unyama.

Hii ndo njia watakayoitumia kummaliza safari hii hata kama ataenda nje ya nchi tena huko ndo rahisi. Dalili zote ukizisoma hapa chini na ukilinganisha na hali ya Dr. Mwakyembe ni perfect match

Symptoms of arsenic poisoning begin with
headaches, confusion, severe diarrhea, and
drowsiness. As the poisoning develops,
convulsions and changes in fingernail
pigmentation called leukonychia may occur. When
the poisoning becomes acute, symptoms may
include diarrhea, vomiting, blood in the urine,
cramping muscles, hair loss, stomach pain, and
more convulsions. The organs of the body that are
usually affected by arsenic poisoning are the
lungs, skin, kidneys, and liver. The final result of
arsenic poisoning is coma to
death

KOFIA na GLOVES mmepata jibu!
 
Wote mnaotaka Dr. aseme, akishasema mtafanya nini au ili mpate stori ya siku?Mangapi hadi sasa yalishasemwa na wengi lakini bado mkakipigia kura CCM na kikapata ushindi wa kishindo?Kwanza fanyieni kazi mabo ya msingi kama vile kuidai serikali huduma bora za afya na elimu kwa kufanya yafuatayo;
  1. Kuwazuia kwenda nje au hospitali binafsi kutibiwa au kuwa na daaaaktari binafsi kwa gharama zetu na badala yake watibiwe hapahapa kwenye hospitali wanazozihujumu.Ni nani anafurahi kwenda hospitali kutumia saa mbili au zaidi kumwona mganga atakayeandika dawa bila ya vipimo(kwani havipo) na kisha kukwambia ukanunue duka la dawa?Wakionja uchungu ambao sisi tumeuzoea, labda watajifunza.
  2. Kuwazuia kuwapeleka watoto wao au wao wenyewe kwenda kusoma nje au shule binafsi(international) na badala yake nao wasome kwenye mabanda yasiyo na walimu,madawati,vitabu au vifaa vya kujifunzia ambayo wao hawaachi kutufanya mazuzu kwa kutuambia wamajenga shule na kutulipisha ada kwa kutumia mabanda yao kama shule ya tabia mbaya na ngono kwa watoto wetu.
  3. Kuwazuia kutumia magari ama ya ofisi au yao ambayo wamatuibia na badala yake nao wapande daladala na vyombo vingine ambavyo siku hadi siku vinaua mamia na wao kujilipa posho kwenda kuwadhihaki wafiwa kwa kusema watachukua hatua wakati wakuchukuliwa hatua ni wao.
  4. Kuwazuia kutumia majeshi yetu kama polisi kwa maslahi yao binafsi kwani nimechoka kusikia polisi wameua raia wakati kazi yao ni kuwalinda.
  5. Kuwazuia kujipa ardhi kubwa na bora na kuiuza nchi yetu kwa wageni na raia kuwa waathirika wa miradi yao hiyo haramu.Wanataka sisi tukakae wapi?Tunywe sumu hadi lini?Mali zetu zitunufaishe lini?
Mkifanya hayo, ni jambo la maana kuliko kumtaka Ulimboka aseme kitu ambacho hakina tija. Watu makini kama Ghandhi na Martin Luther walihimiza na kuwaunganisha watu wao kupingana na mifumo dhalimu kama wetu.
Tuanze leo, kwa Tanzania bora ya kesho.
 
Ulimboka ana akili kuliko wewe na thred yako.anaendelea kupigania afya yake kwanza uchochezi badae
 
Kwani we ulimchangia shilingi ngapi katika matibabu yake zaidi ya kujificha chumbabi na komputa yako ya kizamani apo
 
Mnaharaka ya nini, mnadhan n suala la kuropoka tu kama umebanwa na...)
Kila kitu kinaandaliwa,slow but sure.
So guys,be patient...mnaharaka kama desh desh!
 
Kwani we ulimchangia shilingi ngapi katika matibabu yake zaidi ya kujificha chumbabi na komputa yako ya kizamani apo

hahahahaha,et kompyuta ya kizamani! Watu wagomvi! Lool, hata kama umechapia spellings kidogo,but well said mkuu!
 
Huyu anajijengea uadui mkubwa na umma rather than hao anaowaogopa.namuonya UKIMYA WAKE UTASABABISHA MADHARA YA USALAMA WAKE TOKA KWA WANANCHI.hao anaowaogopa hawawezi tena kumfanya chochote ata akichezea ndevu zao.ULI UNAJITENGENEZEA BOMU BABA.

hizi story za uli mnaongea nyinyi humu jf.huko kitaa hata hawakumbuki ulimboka ni nani.
 
acheni ushabiki,
alishayasema wakati akiwa ktk mazingira magumu sana aliweka wazi sasa kwa nini msitumie yale aliyoyaongea na yapo you tube?
tena basi kwa sisi tulio pitia ualimu tuna sema kuwa neno la kwanza kabisa atakalo sema mtu pindi uongeapo hilo ndilo la msingi yaliyobaki yote ni kujazia habari
hivyo basi aliyoyasema Dr Uli siku ile baada ya kuokotwa ndio ukweli wenyewe,huna haja ya kusubiri ukweli mwingine.
tuache uvivu jamani
 
Wacheni wamdai Ulimboka atekeleze hadidu rejea walizokubaliana naye kule Dodoma. Ulimboka umekula hela yao sasa unajukumu la kufanya kazi mliyokubaliana.
 
Huyu ndugu yetu alikumbwa na machungu yaliyomgusa kila mmoja wetu! Nchi nzima ilizizima, na kuamini (nakuweka msisitizo kwenye tunacho fahamu) kua vyombo vya dola ni wabaya. Tukajitolea kwa matibabu yake, hadi kufikishwa hosiptali SA ambapo hata huko tulihisi serikakali ya Tz bado ingaliweza kumfuatilia na kummalizia !. Mimi kama mimi iliniuma sana.

Tunashukuru Mungu, kwa uwezo wake kapona na karejea nchini. Watu walitoa maoni mengi mitandaoni ambayo naamini ilimfikia kua akija aibukie press conference na kuyasema yote. Hataivyo, kutokusema siku ileile hatukushangaa sana maana jamaa lazima apumzike japo kidogo! Na akusanye kumbukumbu vizuri hata kukumbuka simu yake ilipo! .

MY TAKE:
1. Huu muda uliotumia kukusanya kumbukumbu ni mrefu sana,
2. Unajaza wasiwasi.
3. Hicho unacho subiri kwanini usieleze uma?
4. Hukumbuki kua wewe ungalikwisha 'decompose' (inaniuma sana)
5. Unaumiza vichwa vya watanzania wengine wapenda haki.
6. Vikao na kamati za serikali ni vyanini tena wakati walipopanda gari kukuacha Msituni usiku walijua wamekuua?
7. Utakayo yasema hata sasahivi, bado kutakua na hojaji tofauti kisa kutokuaminika tena.
8. Kumbuka ulishasema watu waachane na familia yako , wewe ndio ufahamuye ukweli.
9. Kumbuka kuna mengi yaliyo wakumba wanao kutetea
10. Mods naombeni msichanganye hii thread na ile inayosema " polisi leo kufunguka. . . . "

Inaonyesha haraka zako huwa hazikupi matunda.....subiri ndg yangu maana haina sababu kuanza kushindana na akina Kova...ataeleza tu ipo siku.
 
Back
Top Bottom