Dr. Slaa ndio mkombozi wa watanzania 2015. Atafumua mfumo huu uliofeli miaka 50 tangu uhuru

DENYO

JF-Expert Member
Sep 14, 2010
698
57
Mpaka sasa hakuna mgombea au mtia nia anayefaa. Hawa wote waliotangaza nia ni sehemu ya watawala ambao wamesababisha ufisadi kuongezeka, umaskini kuongezeka, mafukara kuongezeka, matabaka ya wenye nacho na wasio kua nacho kuongezeka, uchumi wa nchi kuporomoka, shillingi kuporomoka na ghrama za maisha kupanda.

Kwa ufupi wote waliotangaza nia wanaongelea kushugulikia hizi kero lakini hawaongelei kufumua mfumo huu wa utawala uliosababisha matatizo yote tuliyonayo. Kila mmoja anaejitokeza anaongelea kuondoa umaskini, kukuza uchumi, kuondoa matabaka, kuondoa ufisadi na rushwa, kuboresha huduma za jamii maji, afya, elimu, makazi na kadhalika lakini hawa hawa wanasahau kua ni wao ndio wamekua sehemu ya matatizo haya yote over 50 years za uhuru, pia hakuna anaeongelea kwanini haya matatizo nini chanzo? wnakurupuka tu . Report za CAG ni ufisadi kila mwaka, wengine waliuza nyumba za serikali, wengine wamejiuzulu kwa matuhuma kama escrow, richmond, epa etc etc

Tunahitaji mtia nia atakayeongea kufumua mfumo mzima wa utawala na kuchora mstari kwenye baadhi ya masuala kama rushwa na ufisadi. Mtu huyu hawezi hata kidogo kutoka ndani ya ccm kwa sababu ndani ya ccm ukisema kufumua mfumo wa utawala unatafuta shida au uadui, kama unabisha nenda kamuulize mzee Warioba.

Kwa maoni yangu ninaamini mtu ambae anaweza kututoa hapa tulipo ni Dr Slaa tu. Hawa wengine ni porojo na kutafuta kuendelea kufanya yaleyale miaka nenda rudi, hakuna anaeweza kufumua mfumo huu wa utawala uliotufikisha katika dimbwi hili la umaskini na ufisadi uliokithiri, hakuna anaeweza kuichukua rasimu ya pili ya katiba ya mzee Warioba na kuisimamia, hakuna ndani ya hawa waliotangaza na ndani ya ccm.

Tatizo letu limeanzia kwenye mfumo. Jana katika kipindi cha siasa za siasa Dr RYOBA alimwambia Nape kwamba rushwa inaendelea kuwepo na itaendelea kuwepo mpaka tutakapopata serikali makini itakayosema basi. Mambo yote yamekwama kwa sababu ya mfumo wa utawala uliopo. Kuna mgombea mmoja Sumaye i think kidogo na kwa mbali aligusia kuunda mahakama ya kushugulikia rushwa na ufisadi na kuanzisha chombo maalum cha uchunguzi wa wala rushwa na ufisadi, meaning PCCB wamefeli na DPP hapo alikua anagusa mfumo tata uliopo sasa. Lakni hataweza akiwa ndani ya ccm. Kwa ufupi ni wakati muafaka watanzania tuamuke kuchagua kiongozi atakaefumua mfumo ulichemuka na kufeli kuleta mabadiliko for 50 years. DR SLAA IS MY CHOICE
 
Unalipwa shilingi ngapi kwa siku...kwa kila ujinga unaopost hapa?
Njaa+viroba ni shida...
 
Japokuwa kule ccm simkubali yyte ila hapo ukawa huyo Mzee simkubali hata kidogo, sijawahi kuona tofauti yake na ccm, Huyu Mzee ni kizazi cha ccm bado kabisa tabia kibao za ccm anazo,
Wizi, ufisadi, visasi, hapo ukawa sijaona zaidi Mbatia
 
Huyo ni mkombozi kwenu huko huku tz ni mganga njaa na mwizi wa ruzuku za chama chake

mtu aliyefeli atazungumziaje mfumo ulio feli??.. wewe toka umemjua huyo mzee Slaa unadhani amefanikiwa kwenye nini?? kuanzia ngazi ya familia, dini hadi kugombea urais???... Failure huyo kikongwe!!
 
Nachokijua ni ki,oja tu; Peke yake Dr. Slaa hana uwezo ila kwa team inayomfuata, kweli anafaa kuwaongoza walete mabadiliko makubwa Tz.
CCM hakuna hata mmoja mpaka pale watakapoondoka na kukaa nje ya lichama hilo. Huwezi ogea ndani ya dimbwa la tope ujisifu kuwa umetakata. Atakaye endelea kua ccm kamwe hawezi kukemea rushwa na ufisadi. Come out and stay away from them. Tukuonee mbali nao useme, nipo hapa nataka kusafisha uovu huu usisikike tena.
Naamini Dr. Slaa akichaguliwa, hata huko ccm atatwaa wachapa kazi pia kama UKAWA wakiisha. Namkubali
 
mtu aliyefeli atazungumziaje mfumo ulio feli??.. wewe toka umemjua huyo mzee Slaa unadhani amefanikiwa kwenye nini?? kuanzia ngazi ya familia, dini hadi kugombea urais???... Failure huyo kikongwe!!
Dr Slaa ndie anao uwezo wa kufumua mfumo huu uliotusababishia ufisadi, umaskini, huduma mbovu Za jamiii
 
Unalipwa shilingi ngapi kwa siku...kwa kila ujinga unaopost hapa?
Njaa+viroba ni shida...

Dr Slaa anawatoa kamasi, huu mfumo umefikia mwisho kabisa. Unahitaji mtu mwenye uwezo wa kufumuafumua ili kuondokana na Haya Majanga Ya ufisadi, ujinga, umaskini na maradhi
 
Dr. Slaa akiingia ikulu mafisadi watafute nchi yao.

Watanzania wanatarajia kuingia nchi ya ahadi, matumaini yao kwa Dr. Slaa
 
Umeandika ukweli mtupu.Dr Slaa ana viwango vyote vya kuwa Rais wa Tanzania.
 
mkuu hayo si maoni yako tu , watanzania nchi nzima wanajua kwamba rushwa na ufisadi ndio vinavyokwamisha kila kitu nchi hii , wanasema anahitajika mtu makini kabisa na asiyemung'unya maneno wala kufumba macho , wote kwa pamoja wamemteua Dr Slaa kujaza nafasi hiyo .
 
Inatakiwa akili ya juu zaidi kutatua matatizo ya watanzania kwani akili za ccm zaku tembea na wanyama kutumia jembe na nyundo zimeshidwa Dr wa ukweli sio waku gushi kama kikwete sory jamani kikwete.
 
wasomi dunia nzima tumefahamu kwamba hata siku moja matatizo hayawezi kutatuliwa na akili zilezile zilizoyaleta , inahitajika akili kubwa .
 
mkuu hayo si maoni yako tu , watanzania nchi nzima wanajua kwamba rushwa na ufisadi ndio vinavyokwamisha kila kitu nchi hii , wanasema anahitajika mtu makini kabisa na asiyemung'unya maneno wala kufumba macho , wote kwa pamoja wamemteua Dr Slaa kujaza nafasi hiyo .

Aliyeshuhudia mapokezi ya Dr Slaa Sumbawanga anaweza kushuhudia haya usemayo.Aliitetemesha Sumbawanga kwa takriban saa 6 shughuli zote zilisimama!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom