Dr Slaa na wabunge wawili wakamatwa

Haiwezekani hata kwani kama kosa lilikuwa maandamano kwanini polisi walikuwepo kwenye mkutano???:A S 13:
 
badala ya kumkamata al adawi yeye anakamata wapambanaji... ya misri na tunisia yanamnukia
 
Sasa hapo ikitokea vurugu watasema mwanzilishi ni Chadema au Polisi? Kweli Kikwete haoni mbali, atajutia hatua yake hii ya kuwasumbua viongozi wa umma wa watanzania, yeye ni rais wa NEC na TISS, lakini Dr. Slaa ni rais ambaye yuko kwenye mioyo ya watanzania, shauriyake Kikwete kwa kitakachofuta baada ya hapa, asije akasema hakuonywa.
 
"kwani kumkamata Dr Slaa ndio kutashusha bei ya bidhaa?Kutapunguza Ugumu wa maisha?"

Hapo ndio wale waliokuwa wanauliza "maandamano ndio yanabadilisha mabo..." wanatakiwa kujibu.

Moja ya vitu vinavyozungumzwa sana na vichwa vyenye PhD za ukweli kwenye hii mikutano na maandamano ni mfumuko wa bei unaoathiri bei za bidhaa ikiwemo sukari. Our most hopeless government ever imecopy hilo na kuanza kulifanyia kazi blindly kwenye sukari peke yake na kusahau bidhaa zingine. Anyway angalau watu watakunywa chai though bila vitafunwa.So hata ukiwa mtupu kiasi gani unao uwezo wa kutueleza kama maandamano yanabadilisha mambo au hapana. Tafakari usikukurupuke!
 
Serikali ya CCM inaingia kichwakichwa katika kukabiliana na hili la maandamano. Wao hawajui kuwa wananchi wanasubiri kuona viongozi wanaowatetea wanabughuziwa ili moto ulipuke. Hakuna yeyote hapa mwenye uwezo wa kupambana na nguvu ya umma ikilipuka, kashindwa Gaddafi na midege yake itakuwa sie? Tumeshuhudia kila mahala CDM walipofanya maandamano yamekuwa ya amani ya hali ya juu ni ujumbe tu unaokuwa mzito. Sasa uchokozi wa nini?
 
kazi ipo mwaka huu! Watakamata wangapi? Mie mwenyewe nimeandamanisha watu hapa mtaani kwangu, kujadili maisha magumu na kupanda kwa gharama za maisha. Waje watukamate.
 
Sasa wanaamini slaa ni kikwazo kwao.
Hata wakimkamata lakini bado wana mapinduzi wengine wataongeza munkari na mapambano yanaendelea.
 
Serikali ya CCM inaingia kichwakichwa katika kukabiliana na hili la maandamano. Wao hawajui kuwa wananchi wanasubiri kuona viongozi wanaowatetea wanabughuziwa ili moto ulipuke. Hakuna yeyote hapa mwenye uwezo wa kupambana na nguvu ya umma ikilipuka, kashindwa Gaddafi na midege yake itakuwa sie? Tumeshuhudia kila mahala CDM walipofanya maandamano yamekuwa ya amani ya hali ya juu ni ujumbe tu unaokuwa mzito. Sasa uchokozi wa nini?

Hayo maandamano ya Shinyanga ni Trailer tu na yamewatia tumbo joto,sasa yanakuja maandamano ya mafuriko kushinikiza Dr aachiwe...
Deal with the current situation and not arresting people...poor leadership!
I hate police wanaotumikishwa kihovyo hovyo huku wanalipwa kiduchu
 
badala ya kumkamata al adawi yeye anakamata wapambanaji... ya misri na tunisia yanamnukia

Inkoskaz, nakubaliana nawe kwamba ya Misri na Tunisia yanamnukia J.K. Endelea na mazoezi yako, yanayonichekesha sana, ili uwe fit zaidi kuingia ktk maandamano.
 
hizi taarifa zinakera sana...je polisi hawana kazi nyingine?
wakamate basi na watu wanaokusanyika makanisani na misikitini
wakamate watu wanaokusanyika uwanja wa taifa kwenye mechi mbalimbali maana wanasingizia mikusanyiko inaleta uvunjifu wa amani
hata humu JF waje watukamate maana tunajadili hayohayo
 
Well done ! amani ya nchi lazima ilindwe kwa gharama zozote !

Kumkamata Dr. Slaa ndio kulinda amani ya nchi??? Kwani ilikua inaporwa? Mwanza, Musoma na Shinyanga walikofanya mikutano, ni wapi amani ilivurugwa?? Serikali ndio inataka kuvuruga amani sasa.
 
unasema cha ajabu polisi walikuwepo wewe umesahau presdent alifungua hoteli pale arusha na kesho yake Tanroad wakaibomoa kwa kusema imejengwa ndani ya barabara nchi hii imeshikwa na vilaza
wanahojiwa na polisi kwa kuendesha mkutano jana. Cha ajabu jeshi la polisi lilikuwepo wakati wa mkutano kutoa ulinzi. Radio one
 
Habari za uhakika kutoka kwa diwani hapa kahama ni kwamba alipokuwa anapita kahama kuelekea Bukoba walimkamata kwa makosa haya:

1. Kufanya mkutano Malampaka bila kibali
2. Kwamba ametoa maneno ya uchochezi kwenye mkutano wa Maswa
3. Kwamba kuna nyaraka za siri wanazitafuta, wanahisi yeye anazo- hapo alikataa kukaguliwa

Magari mengi ya CHADEMA yalionekana kituoni na wananchi wakanusa kwamba Dr. amekamatwa wakaanza kusogea kituo cha polisi,

Wamemwachia na ameendelea na safari yake kwenda Bukoba muda mrefu.

Polisi wanasema ilikuwa ni mahojiano tu!!
 
wanahojiwa na polisi kwa kuendesha mkutano jana. Cha ajabu jeshi la polisi lilikuwepo wakati wa mkutano kutoa ulinzi. Radio one

Nyie Chadema kuweni wakweli Banaaa.

Si msema wanahojiwa kutokana na kauli zao walizozitoa katika mikutano yao zenye kuashiria uvunjifu wa amani na uchochezi.

na ikibainika Nguvu za Doula lazima ziwaangukie kwa kishindo kikubwa sana mpaka wajute kuzaliwa nchi hii.
 
Kinachotakiwa ni kuzikamata na kuziweka ndani fikra za Watz waliochoshwa na maisha magumu. Ikiwa ni pamoja na ukosefu wa huduma muhimu. Kibaya zaidi ajira zote muhimu wamepewa wageni kwa baraka za Wizara husika
 
Habari za uhakika kutoka kwa diwani hapa kahama ni kwamba alipokuwa anapita kahama kuelekea Bukoba walimkamata kwa makosa haya:

1. Kufanya mkutano Malampaka bila kibali
2. Kwamba ametoa maneno ya uchochezi kwenye mkutano wa Maswa
3.kwamba kuna nyaraka za siri wanazitafuta, wanahisi yeye anazo- hapo alikataa kukaguliwa

Magari mengi ya CHADEMA yalionekana kituoni na wananchi wakanusa kwamba Dr. amekamatwa wakaanza kusogea kituo cha polisi,

Wamemwachia na ameendelea na safari yake kwenda Bukoba muda mrefu.

Polisi wanasema ilikuwa ni mahojiano tu!!

taratibu..wanataka kupunguza kasi yake..
wakati mwengine anakula trip nje ya nchi mwenzake an address matatizo ya mwananchi wa kawaida na kuhamasisha serikali itatue matatizo.
 
Nyie Chadema kuweni wakweli Banaaa.

Si msema wanahojiwa kutokana na kauli zao walizozitoa katika mikutano yao zenye kuashiria uvunjifu wa amani na uchochezi.

na ikibainika Nguvu za Doula lazima ziwaangukie kwa kishindo kikubwa sana mpaka wajute kuzaliwa nchi hii.

Mwambie Mkwere afanye kazi yake si aliiomba mwenyewe kwani sisi tulimlazimisha? Sisi tunahitaji majibu kwenye masuala ya msingi yeye analeta hoja za juu kwa juu - sisi wananchi ndiyo waajiri wake na lazima ariport kwetu, tunaweza kutengua uteuzi tukiamua. Hata kama ni kweli kumshikiria DR. wala hakutasaidia lolote.

Miaka 50 ya uhuru hata umeme na maji vitu basic kabisa hakuna - sasa mnakusanya kodi zetu za nini kama hamuwezi kutupatia basic needs?

Na wewe HM Hafif acha ushabiki wa kizamani.
 
Back
Top Bottom