Dr Slaa na wabunge wawili wakamatwa

fangfangjt

JF-Expert Member
Apr 25, 2008
571
139
wanahojiwa na polisi kwa kuendesha mkutano jana. Cha ajabu jeshi la polisi lilikuwepo wakati wa mkutano kutoa ulinzi. Radio one

UPDATE: baada ya kuhojiwa kwa muda na polisi Kahama, Dr Slaa na wabunge wawili wa CHADEMA waachiwa hadi upelelezi utakapo kamilika. Wanaelekea kagera. RADIO1 STEREO.
 
Sasa nimeamini kwamba hata humu jamvini kuna watoto wa jk
 
Kupitia itv,nimeona maandishi yakisema Dr Slaa akamatwa kahama,please wadau tujuzeni kwa kina nini kinajiri kwa kina
 
hata wafanyaje hawawezi shindana na nguvu ya umma,walichakachua wenyewe sasa yamewarudi
 
Alilolisema JK linatimia, kwamba wao kama serikali wako makini, watahakikisha amani haivunjiki, kaacha maagizo wakamatwe wakati yeye hayupo. Atasababisha machafuko, timing sio nzuri. watu waliohamasika kuandamana wanaweza kuhamasika kumfuata Slaa, kitakachotokea JK anakijua.
 
ndio agizo aliloacha kikwete? watu wamesema ameondoka na kuacha kishindo!
 
Alilolisema JK linatimia, kwamba wao kama serikali wako makini, watahakikisha amani haivunjiki, kaacha maagizo wakamatwe wakati yeye hayupo. Atasababisha machafuko, timing sio nzuri. watu waliohamasika kuandamana wanaweza kuhamasika kumfuata Slaa, kitakachotokea JK anakijua.

ndio maagizo aliyowaachia TISS wakati anaenda France...
apambane na kero sio mtu!
 
Yangu macho hapo ni kuzidi kumuongezea umaarufu na kukubalika Dr. wa ukweli. Nimeamini wajinga ndio waliwao
 
amekamatwa kwa lipi? maana hata Arusha alikamatwa!
Nafikiri sasa wametia mafuta kwenye moto uliokuwa umekosa nguvu. Tusubiri tuone nini kitatokea. Lakini ningekuwa mimi ni Kikwete katu nisingemkamata Slaa.
 
mbona tupo kama wakimbizi ndani ya nchi yetu kwann lkn?jk iko siku ataibeba hii nchi kwa kichwa!
 
kwani kumkamata Dr Slaa ndio kutashusha bei ya bidhaa?Kutapunguza Ugumu wa maisha?

Hajajifunza kwa wenzake wa Africa ya Kaskazini?Tatizo la viongozi wetu wanapelekewa taarifa za kupikwa wao wanakurupuka kutoa maamuzi
 
What the hell!Kinachoonekana ni kuwaharibia ratiba ya Kagera kwa Kagasheki.Polisi wanaonekana wamekumbushwa kazi yao ya kusababisha ghasia.Kwa mujibu wa mtoa habari Erasto Tumbo kupitia redio one,Kama saa moja na nusu iliyopita wakati msafara ukijiandaa kuvamia kagera Dr.Slaa aliitwa kituoni na mpaka sasa bado anahojiwa pamoja na wabunge wawili Chiku Abwao na Rahel Mashishanga.Mliopo eneo la tukio endeleeni kutujuza humu jamvini.
 
wanasema Chadema hawa kua na kibali cha kuendesha mkutano.

Hapa naomba kueleweshwa kidogo hivi wanapaswa kuomba kibali ama wanatakiwa kutoa taarifa polisi kwamba watafanya mkutano wa hadhara ili wapewe ulinzi pale watakapohitaji? Ushauri wangu kwa JK, fanya kazi uliyoahidi ya kuboresha maisha ya watanzania kwa kuacha kucheka na ufisadi ilihali wananchi/maboss wako wanaangamia kwa vifo vya kipuuzi kabisa na hali ya maisha ngumu isiyoelezeka. Haya mengine unaendelea kujidhalilisha tu wewe baba.
 
Kupitia itv,nimeona maandishi yakisema Dr Slaa akamatwa kahama,please wadau tujuzeni kwa kina nini kinajiri kwa kina

kahama hakuwepo aliyekuwepo ni mbowe inasemekana slaa alikuwa maswa
 
"kwani kumkamata Dr Slaa ndio kutashusha bei ya bidhaa?Kutapunguza Ugumu wa maisha?"

Hapo ndio wale waliokuwa wanauliza "maandamano ndio yanabadilisha mabo..." wanatakiwa kujibu.
 
surprising, Just a minute kabla Regia kutoa ratiba ya Kagera tunaona Slaa amekamatwa
 
Back
Top Bottom