Dr. Slaa makampuni yasiyorejesha pesa za EPA hadharani

Makampuni yachota yatakavyo Yamo pia Deep Green, Tangold WIZI wa mabilioni ya
shilingi katika Benki
Kuu ya Tanzania (BoT)
ulifanywa kwa baraka
za serikali,
MwanaHALISI limegundua. Nyaraka za benki na
Hazina ambazo nakala zake zimeifikia gazeti hili zinaonyesha ushirika
usiokuwa wa kawaida katika kuwezesha
uchotaji wa fedha za umma. Ushirika huo unahusisha makampuni ya Tangold
Limited, Deep Green Finance Company na benki
ya Nedbank ya Afrika Kusini. Kwa mfano, kile ambacho BoT inaonyesha
kuwa ni hati za dhamana zilizouzwa kwa
kampuni ya Tangold Limited, kimegundulika
kuwa ni “hewa.” Nyaraka zinaonyesha kuwa mwaka 2005
Tangold ilinunua hati za dhamana za Sh. 50
bilioni, lakini taarifa kutoka ndani ya BoT na
Hazina zinaeleza kinyume chake. Kwa mujibu wa taarifa Na. 001/2005 ya BoT,
Tangold Limited ilinunua na kupewa hati ya
dhamana yenye thamani ya Sh. 25 bilioni, tarehe
1 Mei 2005. Hii ilikuwa Siku Kuu ya Wafanyakazi
(Mei Dei) ambayo huwa ni siku ya mapumziko
kwa ofisi zote za serikali. Vilevile kwa taarifa Na. 002/2005 ya BoT,
Tangold ilinunua na kupewa hati ya dhamana ya
thamani ya Sh. 25 bilioni, tarehe hiyohiyo. Kufuatana na masharti ya mkataba, Tangold
ilipaswa kulipwa na serikali riba ya asilimia 10
kila mwaka, kwa mikataba yote miwili kwa
kipindi cha miaka 10 hadi mwaka 2015. Lakini kumbukumbu za BoT ambazo ni nadra
sana kuonekana hata kwa wakaguzi
zinaonyesha kuwa hakukuwa na mnada wala
tangazo la serikali la kuuza dhamana ambako
Tangold ilinunua dhamana hizo. “Kwa utaratibu, dhamana za serikali
hutangazwa rasmi kwa umma kupitia Gazeti la
Serikali (Official Government Gazette) au hata
kwenye vyombo vingine vya habari,” ameeleza
ofisa mwandamizi wa BoT. “Nakwambia kama kungekuwa na hati ya
dhamana ambayo imenunuliwa na Tangold,
ingetangazwa na kujulikana kwa umma.
Haikuwepo,” amefafanua ofisa huyo. Mbali na gazeti la serikali na vyombo vya habari,
matangazo huweza pia kutolewa kupitia tovuti
ya BoT ambayo ni www.bot-tz.org ambako
imethibitishwa kwamba hakukuwa na
matangazo kuhusu uuzaji dhamana hizo,
ameeleza. Kauli hizo na ukweli wa nyaraka
vinathibitishwa na hali halisi ya Tangold kama
ilivyoonyeshwa kwenye akaunti yake iliyoko
mjini Port Luis, Mauritius. Taarifa ya akaunti ya Tangold ya tarehe 31 Julai
2005 inaonyesha kiwa Tangold ilikuwa na
amana ya kiasi cha dola za Marekani 996.75 tu. Tangold ilipofungua akaunti yake Na. 04413136
katika benki ya Federal Trust mjini Port Louis,
tarehe 31 Desemba 2004, iliweka dola 2,455.00.
Kiasi hicho hakikuongezeka hadi 31 Julai 2005. Aidha, hata kwenye akaunti yake nchini
Tanzania, katika benki ya NBC, makao makuu,
haikuwa na fedha za kununulia dhamana za
serikali. Fedha za kwanza kuingia akaunti ya Tangold
hapa nchini zilikuwa Sh. 1.5 bilioni na ilikuwa 1
Agosti 2005. Fedha hizo zilitoka BoT na
haikuelezwa ni kwa kazi ipi. Siku hiyo hiyo zilihamishwa Sh. 1.5 bilioni
kwenda kampuni ya Deep Green kutoka BoT
vilevile kwa kazi ambayo haijaweza
kugundulika. Tangold ni moja ya makampuni yenye utata
katika miliki na usajili wake. Wakati
inaonyeshwa ilisajiliwa Mauritius na baadaye
kufungua tawi Tanzania, serikali ilieleza
bungeni kuwa ni kampuni yake kwa asilimia
100. Kwa mujibu wa taarifa zilizopo kwa Wakala wa
Usajili wa Makampuni (BRELA), wakurugenzi wa
Tangold ni pamoja na Daudi Ballali, Gray Mgonja,
Andrew Chenge, Patrick Rutabanzibwa na
Vincent Mrisho. Nayo Deep Green inaonyesha ilisajiliwa
Tanzania mwaka 2005 na kwamba anwani
yake ya usajili ni IMMA House, Kiwanja Na. 357
Barabara ya Umoja wa mataifa, Upanga Dar es
Salaam. IMMA ni kampuni ya mawakili Protase
Ishengoma, Aloysius Mujulizi, Lawrance Masha
na Sadock Magai ya Dar es Salaam. Hivi sasa
Mujulizi ni jaji wa mahakama kuu na Masha ni
waziri wa mambo ya ndani. Gazeti hili liliwahi kufichua ukwapuaji wa Sh. 8
bilioni kutoka BoT uliofanywa na Deep Green,
kati ya Septemba na Desemba 2005
(MwanaHALISI Na. 087). Haikuelezwa pia
zilikuwa kwa shughuli ipi. Katika hali isiyo ya kawaida, Tangold
inayodaiwa kuwa kampuni ya serikali, iliingia
mkataba na Deep Green ambayo ni ya binafsi
ambao uliipa Deep Green haki zote za mikataba
yake na BoT na serikali. Nyaraka za Tangold zinaiagiza serikali na BoT
kutii mikataba yake na bila swali, na gavana
Ballali na Katibu Mkuu Hazina Gray Mgonja
wanakubaliana kutii. Kwa mfano vifungu Na. 3 na 4(e) vya mkataba
wa Tangold na Deep Green, vinafanya Tangold,
ambayo inadaiwa kuwa mali ya serikali, kukosa
kabisa maamuzi katika mkataba. Hili linajidhirisha katika barua Na. PST/GEN/2005
ya 25 Mei 2005 kutoka Hazina kwenda Deep
Green ikikubali masharti ya kutobadili lolote
katika mikaba ya makampuni hayo. Kwa mfano, BoT ilikubali kuwasilisha malipo
yoyote, pamoja na kile kinachoitwa riba kwa
dhamana hewa, katika akaunti Na.
011103024840 katika NBC makao makuu na
akaunti nyingine ambazo Deep Green itaagiza. “Tutalipa bila masharti yoyote kwetu, fedha
zote zinazohitajika katika akaunti Na.
011103024840 au kama itakavyoelekezwa na
Deep Green,” ilisema barua ya serikali. Barua hiyo ina saini ya “mwenye mamlaka ya
kusaini kwa niaba ya serikali” – Authorised
Signatory for and on behalf of the government
of the United Republic of Tanzania na nakala
kupelekwa Tangold. Ni hali hii ambayo inafanya wafuatiliaji wa
masuala ya utawala wa fedha BoT kuwa na
mawazo kuwa Deep Green ama ni ya
Watanzania au wana ubia ndani yake. Kufuatia serikali kujifunga kulipa katika akaunti
za Deep Green, gavana Daudi Ballali aliagiza
malipo ya Sh. 1, 546,778,770.92 (1.6 bilioni)
yafanywe kwenye akaunti ya Tangold Na.
011103024840 iliyoko NBC makao makuu. Katika maelekezo kwenye karatasi isiyo na
tarehe wala saini (maofisa BoT
wamethibitisha), Ballali anasema dhamana
tayari imejikusanyia riba tangu 1 Mei 2005. Mkanganyiko hapa ni kwamba Tangold
haikuwa na fedha kwenye akaunti zake ndani
na nje ya nchi. Ilikuwa haijasajiliwa Tanzania. Aidha, siku inayotajwa kuwa Tangold tayari ina
limbikizo la riba, ni siku hiyohiyo
inayoonyeshwa kuwa ndipo kampuni hiyo
ilifunga mkataba wa kununua dhamana! Bila kujali kuwa Tangold haina dhamana,
haijasajiliwa, haijawa na lundo la riba, wala
fedha kwenye akaunti zake, gavana Ballali
anaagiza kuwa fedha zinazobaki, zipelekwe
akaunti Na. 011103024852. Tangold, Deep Green na benki ya Nedbank
wanatumia karatasi na anwani zilezile za mitaa
na jengo mjini Sandton, Afrika Kusini nakupitia
msemaji mmoja aliyetajwa kuwa Wayne
Khoury katika Nedbank. Gazeti lilijitahidi kumpata Bw. Khoury kwa
baruapepe yake ili kujua uhusiano wake na
taarifa za malipo. Hata hivyo hadi tunakwenda
mitamboni baruapepe ilikuwa haijajibiwa. Simu
yake haikujibu. Nedbank, kwa mujibu wa uchunguzi wa
MwanaHALISI, ilitumika pia kupitisha malipo
kwa ajili ya kampuni ya Meremeta, moja ya
makampuni yanayodaiwa kukwapua mabilioni
ya shilingi kutoka BoT na serikalini. Wiki iliyopita, gazeti hili liliripoti ukosefu wa
kanuni za utoaji fedha katika akaunti ya EPA;
udhaifu katika utendaji na wizi wa nyaraka za
BoT. Imefahamika kuwa gavana Ballali alikuwa
akimwagiza meneja wa tawi la NBC makao
maku, P.J. Mapunda kulipa mabilioni ya shilingi
kwa Deep Green, Tangold na Meremeta. Mwandishi alipotaka kupata maoni ya Bw.
Mapunda kuhusu madai hayo, aliambiwa na
maofisa wa NBC kuwa kuwa ameishafariki. Gavana Ballali alifariki Mei mwaka jana katika
mazingira yaliyoacha maswali mengi; baada ya
serikali kuficha alipo kwa kipindi kirefu.
 
Huyu Slaa hana mambo mengine ya msingi ya kufanya? Anachoona TZ hii ni ufisadi na EPA tu?
Ni muda muafaka kwake kubadilika, tunataka kusikia mambo mapya kutoka kwake, siyo haya ambayo yameshaota sugu masikioni mwetu!!

Rejao = FaizaFozy.

Mkisikia ufisadi na EPA mnakimbilia kusema hakuna kipya? Hilo ndiyo jipya na wala halichakai. Kama ufisadi hutaki kuusikia basi uuache. Unategemea kitu gani cha msingi uambiwe wakati wananchi wengine wa Tanzania wakihangaikia maisha lakini wengine wanajikusanyia fedha za nchi bila kuzifanyia kazi.

Kutokana na majina yenu (FaizaFoxy na Rejao) hatutegemee kutopata zaidi ya mnachotoa kutoka katika hazina zenu. Jitihada hizo tunazitambua katika kutetea ufisadi ingawa hatujui kwa malengo yepi.
 
Tunaambiwa hadharani kisha mnaogopa kutaja? Dr. Mwenyewe aliyataja, kisha gazeti lenu la TzDaima linaogopa kusema tuwaeleweje?

Dr. kaweka hadharani, wahariri wameamua kutoyaweka hadharani kwa sababu na hoja za maadili ya kiuandishi, huo ndio utaratibu wa kuandika habari kwenye vyombo vya habari, hoja ya kutoweka wazi majina hayo wakishaifanyia kazi hapana shaka utapata orodha ya majina hayo.
 
Tunaambiwa hadharani kisha mnaogopa kutaja? Dr. Mwenyewe aliyataja, kisha gazeti lenu la TzDaima linaogopa kusema tuwaeleweje?

Mkuu kakalende,

Lakini orodha yote si ipo? na mheshimiwa Dr Slaa akisema kwamba kampuni ambazo hadi sasa zimerudisha pesa hizo zile zote zinazobakia ni kwamba zimegoma kurudisha pesa hiyo.

Kampuni zote zinazomilikiwa na Lukaza na Maregesi ambazo ni zaidi ya nne hazimo kwenye orodha ya wale walorudisha pesa hiyo.

Pia kampuni za Noble Azania Investiment ambayo inajulikana inamilikiwa na nani nayo haijarudisha pesa hiyo ingawa pia inaushirikano na kampuni na Mibare Farms Ltd hizi kampuni zote ni za akina Jeehtu Patel na bwana Mehta.

Hawa jamaa akina Mehta pia wanamiliki Bina Resorts Ltd, Venus Hotels Ltd, Ndovu Soaps Ltd, Bencon Ltd na Ocean Side Ltd.

Kwahio utaona kwamba wakti pesa hii inachotwa pale BOT pia kulikuwa na harakati za kuzitawanya pesa hizi katika maeneo mbalimbali mithili ya watu wanaofanya "money laundering" ili kuvuruga utambuzi kwa intelligence officers na wengine wenye interest ya kujua kinachoendelea.

Sasa Dr Slaa amerudi kuuliza kuhusu uchunguzi unaoendelea na ameambiwa kwamba kuzishughulikia kampuni hizi ni kazi nzito na ndio maana inabidi awakumbushe watanzania na sio kwamba hiyo ni opportunity bali ni wake up call.

Sisi watanzania tunatakiwa tuwe tunakumbushana kila wakti hasa kwenye mambo kama haya kwani ukisahau basi wale wahusika wanaendelea kufurahi ukizingatia kwamba kule Geneva ambako ndipo inashukiwa baadhi ya pesa imetunzwa itakuwa ni kazi kubwa kuipata.
 
Tunashukuru kwa taarifa nzuri sana ila tunaomba uwe wazi hapa:

(Hata hivyo, alizitaja kampuni 13 ambazo zimegoma kurejesha fedha hizo (majina tunayo) na kwamba hazijalipa jumla ya fedha zote zinazokisiwa kufikia sh bilioni 50.)
Zilizobaki ndio zilizotumika kwenye kampeni na Magamba mmesahau t shirt za kijani na kofia kila kijiji
 
Makampuni yachota yatakavyo Yamo pia Deep Green, Tangold WIZI wa mabilioni ya shilingi katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ulifanywa kwa baraka za serikali, MwanaHALISI limegundua. Nyaraka za benki na Hazina ambazo nakala zake zimeifikia gazeti hili zinaonyesha ushirika usiokuwa wa kawaida katika kuwezesha uchotaji wa fedha za umma. Ushirika huo unahusisha makampuni ya Tangold Limited, Deep Green Finance Company na benki ya Nedbank ya Afrika Kusini. Kwa mfano, kile ambacho BoT inaonyesha kuwa ni hati za dhamana zilizouzwa kwa kampuni ya Tangold Limited, kimegundulika kuwa ni "hewa." Nyaraka zinaonyesha kuwa mwaka 2005 Tangold ilinunua hati za dhamana za Sh. 50 bilioni, lakini taarifa kutoka ndani ya BoT na Hazina zinaeleza kinyume chake. Kwa mujibu wa taarifa Na. 001/2005 ya BoT, Tangold Limited ilinunua na kupewa hati ya dhamana yenye thamani ya Sh. 25 bilioni, tarehe 1 Mei 2005. Hii ilikuwa Siku Kuu ya Wafanyakazi (Mei Dei) ambayo huwa ni siku ya mapumziko kwa ofisi zote za serikali. Vilevile kwa taarifa Na. 002/2005 ya BoT, Tangold ilinunua na kupewa hati ya dhamana ya thamani ya Sh. 25 bilioni, tarehe hiyohiyo. Kufuatana na masharti ya mkataba, Tangold ilipaswa kulipwa na serikali riba ya asilimia 10 kila mwaka, kwa mikataba yote miwili kwa kipindi cha miaka 10 hadi mwaka 2015.

Lakini kumbukumbu za BoT ambazo ni nadra
sana kuonekana hata kwa wakaguzi zinaonyesha kuwa hakukuwa na mnada wala tangazo la serikali la kuuza dhamana ambako Tangold ilinunua dhamana hizo. "Kwa utaratibu, dhamana za serikali hutangazwa rasmi kwa umma kupitia Gazeti la Serikali (Official Government Gazette) au hata kwenye vyombo vingine vya habari," ameeleza ofisa mwandamizi wa BoT. "Nakwambia kama kungekuwa na hati ya dhamana ambayo imenunuliwa na Tangold, ingetangazwa na kujulikana kwa umma. Haikuwepo," amefafanua ofisa huyo. Mbali na gazeti la serikali na vyombo vya habari, matangazo huweza pia kutolewa kupitia tovuti ya BoT ambayo ni www.bot-tz.org ambako imethibitishwa kwamba hakukuwa na matangazo kuhusu uuzaji dhamana hizo, ameeleza. Kauli hizo na ukweli wa nyaraka vinathibitishwa na hali halisi ya Tangold kama ilivyoonyeshwa kwenye akaunti yake iliyoko mjini Port Luis, Mauritius. Taarifa ya akaunti ya Tangold ya tarehe 31 Julai 2005 inaonyesha kiwa Tangold ilikuwa na amana ya kiasi cha dola za Marekani 996.75 tu. Tangold ilipofungua akaunti yake Na. 04413136 katika benki ya Federal Trust mjini Port Louis, tarehe 31 Desemba 2004, iliweka dola 2,455.00. Kiasi hicho hakikuongezeka hadi 31 Julai 2005. Aidha, hata kwenye akaunti yake nchini Tanzania, katika benki ya NBC, makao makuu, haikuwa na fedha za kununulia dhamana za serikali. Fedha za kwanza kuingia akaunti ya Tangold hapa nchini zilikuwa Sh. 1.5 bilioni na ilikuwa 1 Agosti 2005. Fedha hizo zilitoka BoT na haikuelezwa ni kwa kazi ipi. Siku hiyo hiyo zilihamishwa Sh. 1.5 bilioni kwenda kampuni ya Deep Green kutoka BoT vilevile kwa kazi ambayo haijaweza kugundulika.

Tangold ni moja ya makampuni yenye utata
katika miliki na usajili wake. Wakati inaonyeshwa ilisajiliwa Mauritius na baadaye kufungua tawi Tanzania, serikali ilieleza bungeni kuwa ni kampuni yake kwa asilimia 100. Kwa mujibu wa taarifa zilizopo kwa Wakala wa Usajili wa Makampuni (BRELA), wakurugenzi wa Tangold ni pamoja na Daudi Ballali, Gray Mgonja, Andrew Chenge, Patrick Rutabanzibwa na Vincent Mrisho. Nayo Deep Green inaonyesha ilisajiliwa Tanzania mwaka 2005 na kwamba anwani yake ya usajili ni IMMA House, Kiwanja Na. 357 Barabara ya Umoja wa mataifa, Upanga Dar es Salaam. IMMA ni kampuni ya mawakili Protase Ishengoma, Aloysius Mujulizi, Lawrance Masha na Sadock Magai ya Dar es Salaam.

Hivi sasa
Mujulizi ni jaji wa mahakama kuu na Masha ni waziri wa mambo ya ndani. Gazeti hili liliwahi kufichua ukwapuaji wa Sh. 8 bilioni kutoka BoT uliofanywa na Deep Green, kati ya Septemba na Desemba 2005 (MwanaHALISI Na. 087). Haikuelezwa pia zilikuwa kwa shughuli ipi. Katika hali isiyo ya kawaida, Tangold inayodaiwa kuwa kampuni ya serikali, iliingia mkataba na Deep Green ambayo ni ya binafsi ambao uliipa Deep Green haki zote za mikataba yake na BoT na serikali. Nyaraka za Tangold zinaiagiza serikali na BoT kutii mikataba yake na bila swali, na gavana Ballali na Katibu Mkuu Hazina Gray Mgonja wanakubaliana kutii. Kwa mfano vifungu Na. 3 na 4(e) vya mkataba wa Tangold na Deep Green, vinafanya Tangold, ambayo inadaiwa kuwa mali ya serikali, kukosa kabisa maamuzi katika mkataba. Hili linajidhirisha katika barua Na. PST/GEN/2005 ya 25 Mei 2005 kutoka Hazina kwenda Deep Green ikikubali masharti ya kutobadili lolote katika mikaba ya makampuni hayo. Kwa mfano, BoT ilikubali kuwasilisha malipo yoyote, pamoja na kile kinachoitwa riba kwa dhamana hewa, katika akaunti Na. 011103024840 katika NBC makao makuu na akaunti nyingine ambazo Deep Green itaagiza. "Tutalipa bila masharti yoyote kwetu, fedha zote zinazohitajika katika akaunti Na. 011103024840 au kama itakavyoelekezwa na Deep Green," ilisema barua ya serikali.

Barua hiyo ina saini ya "mwenye mamlaka ya
kusaini kwa niaba ya serikali" – Authorised Signatory for and on behalf of the government of the United Republic of Tanzania na nakala kupelekwa Tangold. Ni hali hii ambayo inafanya wafuatiliaji wa masuala ya utawala wa fedha BoT kuwa na mawazo kuwa Deep Green ama ni ya Watanzania au wana ubia ndani yake. Kufuatia serikali kujifunga kulipa katika akaunti za Deep Green, gavana Daudi Ballali aliagiza malipo ya Sh. 1, 546,778,770.92 (1.6 bilioni) yafanywe kwenye akaunti ya Tangold Na. 011103024840 iliyoko NBC makao makuu. Katika maelekezo kwenye karatasi isiyo na tarehe wala saini (maofisa BoT wamethibitisha), Ballali anasema dhamana tayari imejikusanyia riba tangu 1 Mei 2005.

Mkanganyiko hapa ni kwamba Tangold
haikuwa na fedha kwenye akaunti zake ndani na nje ya nchi. Ilikuwa haijasajiliwa Tanzania. Aidha, siku inayotajwa kuwa Tangold tayari ina limbikizo la riba, ni siku hiyohiyo inayoonyeshwa kuwa ndipo kampuni hiyo ilifunga mkataba wa kununua dhamana! Bila kujali kuwa Tangold haina dhamana, haijasajiliwa, haijawa na lundo la riba, wala
fedha kwenye akaunti zake, gavana Ballali anaagiza kuwa fedha zinazobaki, zipelekwe akaunti Na. 011103024852. Tangold, Deep Green na benki ya Nedbank wanatumia karatasi na anwani zilezile za mitaa na jengo mjini Sandton, Afrika Kusini nakupitia msemaji mmoja aliyetajwa kuwa Wayne Khoury katika Nedbank.

Gazeti lilijitahidi kumpata Bw. Khoury kwa
baruapepe yake ili kujua uhusiano wake na taarifa za malipo. Hata hivyo hadi tunakwenda mitamboni baruapepe ilikuwa haijajibiwa. Simu yake haikujibu. Nedbank, kwa mujibu wa uchunguzi wa MwanaHALISI, ilitumika pia kupitisha malipo kwa ajili ya kampuni ya Meremeta, moja ya makampuni yanayodaiwa kukwapua mabilioni ya shilingi kutoka BoT na serikalini. Wiki iliyopita, gazeti hili liliripoti ukosefu wa kanuni za utoaji fedha katika akaunti ya EPA; udhaifu katika utendaji na wizi wa nyaraka za BoT.

Imefahamika kuwa gavana Ballali alikuwa
akimwagiza meneja wa tawi la NBC makao maku, P.J. Mapunda kulipa mabilioni ya shilingi kwa Deep Green, Tangold na Meremeta. Mwandishi alipotaka kupata maoni ya Bw. Mapunda kuhusu madai hayo, aliambiwa na maofisa wa NBC kuwa kuwa ameishafariki. Gavana Ballali alifariki Mei mwaka jana katika mazingira yaliyoacha maswali mengi; baada ya serikali kuficha alipo kwa kipindi kirefu.

Asante kutupa donzoo hizi zioizopita kupata ufafanuzi zaidi
 
Taarifa za fadhaha kama hizi kwa serkali yetu inakuwa kama ni donda ndugu maana WEZI WA EPA ndio wanoendesha uchumi wetu
muda ukifika watakoma tu.Wako wapi akina GADDAFI
 
Slaa kweli ni "opportunist" kwani anajuwa kabisa kuwa hili jambo linashughulikiwa na Serikali na Takukuru na anajuwa kabisa kuwa karibu litatangazwa, anawahi aonekane yeye ndio kaliibuwa. Amma kweli mfa maji haishi kutapatapa.

fikiria zaidi,pengine anafahamu na ndio maana ametoa takwimu ili isitokee serekali ikapindisha ukweli kama kawaida yake...sometimes fikiria zaidi achana na unazi usio na tija
 
Huyu Slaa hana mambo mengine ya msingi ya kufanya? Anachoona TZ hii ni ufisadi na EPA tu?
Ni muda muafaka kwake kubadilika, tunataka kusikia mambo mapya kutoka kwake, siyo haya ambayo yameshaota sugu masikioni mwetu!!

Mnataka kusikia ufisadi mpya! Ufisadi wa EPA mmeumaliza? Kwa mwenye akili, Mafisadi kupewa grace period kurudisha pesa waloiba ni aibu. Ok, grace period imeisha Mafisadi wamegoma kulipa mbona Rais kimya? Serikali kimya? Dk Slaa naye akae kimya?
Uwe mzalendo
 
Mnataka kusikia ufisadi mpya! Ufisadi wa EPA mmeumaliza? Kwa mwenye akili, Mafisadi kupewa grace period kurudisha pesa waloiba ni aibu. Ok, grace period imeisha Mafisadi wamegoma kulipa mbona Rais kimya? Serikali kimya? Dk Slaa naye akae kimya?
Uwe mzalendo
Soma post ya FF utaelewa zaidi. Raisi wetu katumia njia ya busara kuhakikisha fedha zinarudishwa, hakukurupuka kuwachukulia hatua cuz angefanya hivyo hata hizo zilizorudishwa zisingepatikana.

Still hili suala linafanyiwa kazi na serikali. Slaa hakuwa na sababu ya kurudia rudia kitu ambacho kimeshafanyiwa kazi. Aje na mambo mapya. Aache kulia lia kila siku.
 
Rejao = FaizaFozy.

Mkisikia ufisadi na EPA mnakimbilia kusema hakuna kipya? Hilo ndiyo jipya na wala halichakai. Kama ufisadi hutaki kuusikia basi uuache. Unategemea kitu gani cha msingi uambiwe wakati wananchi wengine wa Tanzania wakihangaikia maisha lakini wengine wanajikusanyia fedha za nchi bila kuzifanyia kazi.

Kutokana na majina yenu (FaizaFoxy na Rejao) hatutegemee kutopata zaidi ya mnachotoa kutoka katika hazina zenu. Jitihada hizo tunazitambua katika kutetea ufisadi ingawa hatujui kwa malengo yepi.
Hii ni name calling. Kasome vizuri sheria za JF
 
Huyu Slaa hana mambo mengine ya msingi ya kufanya? Anachoona TZ hii ni ufisadi na EPA tu?
Ni muda muafaka kwake kubadilika, tunataka kusikia mambo mapya kutoka kwake, siyo haya ambayo yameshaota sugu masikioni mwetu!!

We unataka afanyeje?mbona majibwa yenu hayabadiliki?viva chadema,viva slaa dr wa ukweli
 
Tatizo kubwa la msingi hapa ni kwamba serikali haiwezi kuwashtaki wale wote walohusika na wizi huo wa kalamu kwani walikuwa makini sana na walisaini makaratasi yote kati yao na serikali ikiwakilishwa na bwana Mkono na mikataba hiyo haijashiba sana kisheria hivyo kufanya kazi ya kufungua mashitaka iwe ngumu.

Wale dagaa ambao walipatikana walirudisha pesa hiyo ambayo inafikiriwa kwamba ni kama bilioni 60 hivi lakini pia inawezekana pesa hiyo haiukuingia kwenye akaunti hiyo bali kuishia mifukoni mwa watu.

Kwahio wale wanasheria wote wa aina ya kina Mkono walijua kwamba wanafanya ulaghai katika kutayarisha mikataba hiyo na kama ni hivyo je IMF wameshindwaje kugundua hilo maana hiyo ni "scandal" ingine kubwa tu tosha kutoirudisha CCM madarakani.

Kuna "lack of skills" kubwa kwa wanasheria wetu katika kutayarisha na kuandika mikataba hii ambayo ni sawa na ile ya madini ambapo kwa makusudi kabisa kwa interest yao mbele ya nchi wanahujumu watanzania.

Ukiishaona mende mmoja anazungukazunguka sebuleni basi ujue atakuwa anatokea sehemu za mafichoni hasa kwenye makabati jikoni na kwingine kwahio unaita watu wa "fumigation". Ni watu wanaotumia njia hii kuharibua mazaliano ya wadudu, kuzuia ukuaji wa eneo la mazaliano, kulinda dhidi ya ujio wa wadudu wapya na kuhifadhi muundo uliopo uwe makabati au mbao.

Sasa serikali inashindwa kukomboa pesa yote ilioibiwa na pia inashindwa kuwafikisha wahusika wote mbele ya vyombo vya sheria je tupime vipi?

Kwahio njia pekee ya kufanya kwa sasa- lete "fumigation".
 
Huyu Slaa hana mambo mengine ya msingi ya kufanya? Anachoona TZ hii ni ufisadi na EPA tu?
Ni muda muafaka kwake kubadilika, tunataka kusikia mambo mapya kutoka kwake, siyo haya ambayo yameshaota sugu masikioni mwetu!!

hana ubunifu..ataje basi hizo kampuni .13 ama anagwaya nini?
 
Soma post ya FF utaelewa zaidi. Raisi wetu katumia njia ya busara kuhakikisha fedha zinarudishwa, hakukurupuka kuwachukulia hatua cuz angefanya hivyo hata hizo zilizorudishwa zisingepatikana.

Still hili suala linafanyiwa kazi na serikali. Slaa hakuwa na sababu ya kurudia rudia kitu ambacho kimeshafanyiwa kazi. Aje na mambo mapya. Aache kulia lia kila siku.
Mkuu sheria ya Uhujumu uchumi inamweka mtu hatiani na ikidhihirika (mahakama) anataifishwa mali zake ... Hizo fedha zisingerudi vipi?..
 
Faiza foxy na Rejao nyinyi ni sehemu ya mafisadi japo yawezakana mliambulia kanga,kofia na T-shirt,na inavyoonekana hata aibu hamna kama magamba yalivyoshindikana kuvulika,hivi kweli mnadhani kuna kitu kingine cha kuzungumzia kama sio ufisadi na rushwa ambazo CCM na serikali yake imeshindwa kuzishughulikia na kutupatia ufumbuzi?hivi inaonekana hata ile basic mths hamkusoma,kiasi gani cha pesa kilipote na kinaendela kupotea kutokana na ufisadi unafanywa na viongozi waandamizi wa serikali ya CCM- Magamba?hivi mnashindwa kuona kwamba pesa hizo zina gusa miradi ya maendeleo ambayo imeshindwa kutekelezeka kutoka na fedha nyingi kukwapuliwa na mafisadi?kwa pesa hizo kama zingelikuwa zinaelekezwa kwenye miradi ya maendeleo,eg kujenga Zahanati,kunua madawa,miradi ya shule eg kununua madawati ,pembejeo etc,hivi kuna watoto wangapi hadi leo hawana madawati?hawana maji ya kunawa pindi wanapotoka kujisaidia au ya kutumia wawapo toilet,mnajua hayo?na kama hamjui semeni tuwatajie shule hata zilizoko hapa DAR mkajionee,leo mnasema Dr Slaa abadilishe cha kuongea eti hilo la ufisadi limekuwa sugu,eti mmelichoka hivi nyie faizafoxy,Rejao na wenye akili finyu kam zenu mnadhani hilo la ufisadi na Rushwa zingine zinazoendelea ndani ya serikali ya CCM ni suala la fashion kwamba hii imepitwa na wakati?mkiach kushabikia ufisadi,mkiacha rushwa na Dr Slaa na watu wengine wanaouchukia ufisadi wataacha kuzungumzia lakini kama hamuachi na wala hamtarudisha fedha hizo nasi hatunyamaza kamwe.mnatia aibu japo hatuwajui kwa sura,lakini ni wazi kwamba akili zenu zina malyenge,ni vipofu wa fikra,ni walafi wa utajiri tena wenye madhambi,MLAANIWE DAIMA KAMA MTAENDELEA KUKEMEA WATU WANAOPINGA NA KUHOJI UFISADI UNAOFANYWA NA CCM NA SERIKALI YAKE,NAAMINI MUNGU YUPO UPANDE WETU,MIJITU GANI NYIE MSIEONA JAPO MNA MACHO,JUZI TU AIBU YA WIZI WA KINA JAIRO BADO MNAPATA NGUVU YA KUMKEMEA DR SLAA ANAPOZUNGUMZIA UFISADI,NAOMBA ISITOKEE NIKAWAJUA NYIE
 
Soma post ya FF utaelewa zaidi. Raisi wetu katumia njia ya busara kuhakikisha fedha zinarudishwa, hakukurupuka kuwachukulia hatua cuz angefanya hivyo hata hizo zilizorudishwa zisingepatikana.

Still hili suala linafanyiwa kazi na serikali. Slaa hakuwa na sababu ya kurudia rudia kitu ambacho kimeshafanyiwa kazi. Aje na mambo mapya. Aache kulia lia kila siku.

Mkuu Rejao,

Hili suala linafanyiwa kazi hadi lini?
 
Mkuu sheria ya Uhujumu uchumi inamweka mtu hatiani na ikidhihirika (mahakama) anataifishwa mali zake ... Hizo fedha zisingerudi vipi?..
Hebu mkuu isome vizuri sheria ya kuhujumu uchumi iliyofanyiwa marekebisho mwaka 1983, chini ya kifungu cha sheria namba 16 cha mwaka 1979 uniambie haya makampuni yatashtakiwa kwa criteria zipi.
 
Mkuu Rejao,

Hili suala linafanyiwa kazi hadi lini?
Muulize Slaa, yeye anazo statistics za kampuni ambazo tayari zimesharejesha fedha. Almost 90% ya fedha zote tayari zimesharejeshwa. Huko ndiko kufanyiwa kazi kwa hili swala.
 
Soma post ya FF ... Raisi wetu katumia njia ya busara kuhakikisha fedha zinarudishwa,... angefanya hivyo hata hizo zilizorudishwa zisingepatikana.
Still hili suala linafanyiwa kazi na serikali. Slaa...Aje na mambo mapya. Aache kulia lia kila siku.
Linafanyiwa kazi miaka mingapi? Deadline ilikuwa lini? Miaka kadhaa imepita bado linafanyiwa kazi. Suala la Gr
een Finance na TANGOLD litafanyiwa kazi lini? Unataka kashfa mpya zipi? Mbona zimeshaibuliwa au hadi aibue Slaa?
 
Back
Top Bottom