Dr. Slaa Kulipwa maslahi kama mbunge anastahili?

Naomba tutambue ya kuwepo kwa viwango wa mishahara kutokana na kazi anayoifanya mtu, Dr Slaa alipinga mshahara huo katika level ya UBUNGE ambapo sehemu kubwa ya kazi zake ni eneo la jimbo na si kwa level ya KATIBU MKUU wa chama ambapo anahitaji kutumika nchi nzima hivyo kazi zake zimeongezeka zaidi. KATIBU MKUU wa chama kikuu cha upinzani level yake ni sawa na waziri mkuu!!
 
Milion 7 ni pesa ndogo sana kwanza Dr Slaa anampa Kikwete changamoto jinsi ya kuiongoza serikali na asingekuwa anafanya mikutano, midahalo, Kikwete asigeweza kuiendesha serikal angekuwa anatabasamu tu.

Kwa hiyo Rizwan amshukuru sana Dr Slaa anampa babake shavu pamoja na nyie mnaomkandia, yani wengine mna maudhi natamani mngekuwa karibu niwazabe vibao, vitu vingine havihitaji uwe na degree kuelewa.

Big up to Dr Slaa, na kama chama kitakosa pesa ya kukulipa mkuu usisite kutuambia sisi wadau wadogo tuchange vijisenti vyetu.
 
Mkuu Mlengo wa Kati, ni lazima kutofautisha hoja zinazoelekeza katika kujenga misingi ya utoaji wa mishahara kwa ulingano (equitable rewards system) na malipo anayopata mtu kama mshahara.

Kwa nilivyomuelewa Slaa wakati ule akiwa mbunge kuhusu malipo ya wabunge, ni ulingano uliokuwepo/uliopo kati ya anacholipwa mbunge na wafanyakazi wengine wa serikali.

Dr Slaa alifafanua katika maelezo yake niliyoyasikia sehemu mbalimbali za nchi kwa kuuliza maswali kama inakuaje daktari analipwa kiasi ambacho hakifiki hata milioni na mwalimu kiasi kisichofika hata laki tano wakati mbunge anachukua Mamilioni.

Hoja yake ilikua katika kuangalia utaratibu uliopo wa kutoa malipo na usivyokuwa wa haki au kwa maneno mengine ulivyokuwa wa upendeleo kwa wanasiasa.

Kuhusu kiasi anacholipwa yeye DR Slaa kwa uelewa wangu ni kidogo ukilinganishwa na anacholipwa Mtendaji mkuu wa Kampuni nyingi na taasisi hapa nchini.mfano PPF, NSSF,TRA. Mabenki n.k.

Kwa msingi huo sioni mantiki katika hoja yako ya kuhusianisha hoja ya Slaa kutetea malipo linganifu na anacholipwa yeye kama mtendaji mkuu katika chama cha siasa.
 
We Kifo cha mende kuwa na ADABU!! Hivi kwa kazi anayoifanya na wadhifa alionao unashangaa kuona analipwa ml 7.5? Au umetumwa nini!!! Ushindwe na ulegee!
 
Ndg wana JF, Kwanza niwapongeze kwa mwendelezo wa uwazi unaoendelea hapa ndani ingawa si mara zote tunaweza zungumza lugha mmoja.After all si lazima tukubaliane kwa kila jambo ila tunaweza kutokubaliana na kufikia mwaafaka.

Kuhusu la mshahara nisingependa tunavyotukanana au kutumia lugha isiyo na tija. Mtoa mada aliuliza swali aliloona linahitaji majibu kwa mtazamo wake na hao wachache aliowawakilisha humu. Kama wengine tunaona ni wazo potofu au halina msingi tunaachana nayo bila ya lugha mbaya.

Kwa mtazamo wangu tu, Dr.Slaa deserve the mentioned figure na ukitazama na mchango wake kwa Taifa hili tangu akiwa bungeni hakuna shaka
kupewa huo mchahara. Actually Serikali ndo lapaswa kumpa na si chama.

Rejea alivyopigania haki za wanyonge kule bungeni, alivyoibua hoja za ufisadi mpaka leo hii hawathubutu kujitoa hadharani kama walivyoimbiwa na Mpoto.

Haya ni baadhi tu ya mafanikio ya Dr kwa Taifa hili kuliko hata kina Mzee Yusuph waliotumia nguvu na rasilimali za chama kusafisha kisichosafishika

Nawakilisha
 
Wewe umelipwa bei gani kwa kazi ya kukaa na laptop siku nzima kuwachafua wapiganaji wa ukweli?.....fuatilia mikutano ya saa huko kusini, balaa mnalo 2015.
Kwa akili za CHADEMA Mgombea atakua Dr Slaa 2015 ambaye hadi sasa kamshahara kamemkimbiza hapa JF! Mtapata 28 percent tehehetehetehee!
 
Ndg wana JF, Kwanza niwapongeze kwa mwendelezo wa uwazi unaoendelea hapa ndani ingawa si mara zote tunaweza zungumza lugha mmoja.After all si lazima tukubaliane kwa kila jambo ila tunaweza kutokubaliana na kufikia mwaafaka. Kuhusu la mshahara nisingependa tunavyotukanana au kutumia lugha isiyo na tija. Mtoa mada aliuliza swali aliloona linahitaji majibu kwa mtazamo wake na hao wachache aliowawakilisha humu. Kama wengine tunaona ni wazo potofu au halina msingi tunaachana nayo bila ya lugha mbaya.
Kwa mtazamo wangu tu, Dr.Slaa deserve the mentioned figure na ukitazama na mchango wake kwa Taifa hili tangu akiwa bungeni hakuna shaka kupewa huo mchahara. Actually Serikali ndo lapaswa kumpa na si chama. Rejea alivyopigania haki za wanyonge kule bungeni, alivyoibua hoja za ufisadi mpaka leo hii hawathubutu kujitoa hadharani kama walivyoimbiwa na Mpoto. Haya ni baadhi tu ya mafanikio ya Dr kwa Taifa hili kuliko hata kina Mzee Yusuph waliotumia nguvu na rasilimali za chama kusafisha kisichosafishika
nawakilisha

Jana ulimalizia kunywa bia gani vile? ndio una amka sasa?
 
Naomba tutambue ya kuwepo kwa viwango wa mishahara kutokana na kazi anayoifanya mtu, Dr Slaa alipinga mshahara huo katika level ya UBUNGE ambapo sehemu kubwa ya kazi zake ni eneo la jimbo na si kwa level ya KATIBU MKUU wa chama ambapo anahitaji kutumika nchi nzima hivyo kazi zake zimeongezeka zaidi. KATIBU MKUU wa chama kikuu cha upinzani level yake ni sawa na waziri mkuu!!

Aise mbona hujaenda Kibosho siku nyingi?
 
Mkuu Mlengo wa Kati, ni lazima kutofautisha hoja zinazoelekeza katika kujenga misingi ya utoaji wa mishahara kwa ulingano (equitable rewards system) na malipo anayopata mtu kama mshahara. Kwa nilivyomuelewa Slaa wakati ule akiwa mbunge kuhusu malipo ya wabunge, ni ulingano uliokuwepo/uliopo kati ya anacholipwa mbunge na wafanyakazi wengine wa serikali. Dr Slaa alifafanua katika maelezo yake niliyoyasikia sehemu mbalimbali za nchi kwa kuuliza maswali kama inakuaje daktari analipwa kiasi ambacho hakifiki hata milioni na mwalimu kiasi kisichofika hata laki tano wakati mbunge anachukua Mamilioni. Hoja yake ilikua katika kuangalia utaratibu uliopo wa kutoa malipo na usivyokuwa wa haki au kwa maneno mengine ulivyokuwa wa upendeleo kwa wanasiasa.
Kuhusu kiasi anacholipwa yeye DR Slaa kwa uelewa wangu ni kidogo ukilinganishwa na anacholipwa Mtendaji mkuu wa Kampuni nyingi na taasisi hapa nchini.mfano PPF, NSSF,TRA.Mabenki n.k. Kwa msingi huo sioni mantiki katika hoja yako ya kuhusianisha hoja ya Slaa kutetea malipo linganifu na anacholipwa yeye kama mtendaji mkuu katika chama cha siasa.

Unajua Chadema inapata kiasi gani kwa mwezi kutoka Ruzuku ? Chadema ni kampuni inayo tengeneza faida kama unavyolinganisha na PPF,NSSF,TRA,na mabenki! Chadema sio chama tajiri bado kipo chini kinahitaji kukua kimapata! Lakini Slaa ameamua kula kuku na mayai halafu anataka kuendelea kupata kuku!!!
 
Ilka jk ndiye anastahili kupora nyumba za watu..........?
Maana kapora nyuma mikocheni mtaa wa Ursino.......upi ufisadi? kama mna akili kweli?
 
wewe ni shemeji yake makamba?

Haaaaaaaaaa haaaaaaaaaaaaaaa haaaaaaaaaaaaaa!!!!! Shemegiiiii!! Onga mshi.
Jamani kweli wana jamii sometimes wanakuwa wamechoka. Hii thread uatafikiri comedy bwana!! Mtu just an auditor wa benki fulani anapata mshahara 10 mil wewe huyu anaetumikia umma wa watanzania unataka alipwe shs ngapi jamani?! Mbona unashangaza, ndio pamoja na umaskini tulionao lakini jamaa kazi yake ni ngumu inayoweza kugharimu hata maisha yake halafu akirudi nyumbani awe na maisha duni, mmhhh sina zaidi.
 
Hili la Mshahara wa Dr. mbona lilikwisha tolewa ufafanuzi, wala halipwi zote hizo kama mshahara. Hizo ni pamoja na posho ya pango la nyumba, posho ya mafuta na matengenezo ya gari nk. Analipwa kidogo kuliko Mkama.

Kama posho ya chai kwa mkubwa wa Manispaa ya Moshi ilikuwa ni mamilioni kadhaa iweje kwa mashahara wa Dr. Slaa! Anyway kuchangia post zenu za kipuuzi ni kuwapandisha chati, jiandaeni 2015 maana hapo ndo mtakapojua kuwa "nguvu ya umma" inashinda "nguvu ya ufisadi"
 
Lazima apewe 7.5 ni mzee wa totos na unajua tena bongo kuweka kimada ni gharama kubwa kuliko kuendesha chama.

Kwa kuwa mmetumwa kujakuleta ukakasi jF mimi naanza kuwauliza maswali ya msingi kutokana na hoja zenu

Hivi
1. Dr-Dr Kikwete (Phd za kupewa) totos wangapi? Hujui soma thread Kikwete: Black and White.
2. Ustaadhi Mzee Makamba anavimada wangapi?
3. Kapiteni/kapateni Chiligati anatotos ngapi?
4. Mshari Chenge anatotos ngapi?
5. Dogo Ridhiwan anatotos wangapi?
6. Dogozela Nape "naye" anatotos ngapi?
Nimewauliza wangapi[/] nikimaanisha kupata idadi, msije na pumba.

Nambari one, totos zake zinaigharimu nchi hii kwa kiasi gani? Ukianzia safari za ndege, hoteli, ulinzi, nk
 
crap crap crap.

Dr W.P.Slaa alikua ni mtu mahili sana kuvinjari hapa JF kabla suala la kulipwa mshahara mkubwa ambao awali aliulalamikia kuwa ni mkubwa sana akiwa Bungeni na sababu yake kubwa ilikua ni hela nyingi sana kwa Wabunge kupewa kiasi hicho! Lakini baada ya kuacha Ubunge na kufanya kile anacho kiita kuwa ni makubaliano ya kuwa alipwe kama Mbunge yameacha maswali mengi kwa Wazalendo wa tanzania na Kushindwa kumuelewa Dr Slaa kama kweli ni Mzalendo au Mwanasiasa maslahi!
Wadau wengi hapa JF wamekua wakitaka kauli ya Slaa mwenyewe juu ya Suala hilo la Mshahara anaolipwa lakini kiu yao kubwa ikiwa kwanini alipinga mshahara huo akiwa bungeni lakini katoka bungeni anataka alipwe kama wabunge wanavyolipwa!
Dr Slaa pamoja na kulipwa kiasi hicho na Chadema bado anaiibia serikali kwani Mshahara huo haukatwi kodi hata kidogo! Aidha ikumbukwe kua mfanyakazi wa ngazi ya Chini Chadema makao makuu analipwa Shilingi 150,000 kabla ya kukatwa kodi hivyo take home yake ni 123,000 kwa mwezi akiwa mkazi wa dar es salaam na ana familia!
My take: Wanasiasa hujulikana huluka zao kwa kurekodi kauli zao na vitendo vyao! Kwa hili ni doa ambalo Dr Slaa hakulipima mazara yake! Dr Slaa kama ilivyokuwa desturi yako hapa JF tunaomba popote ulipo utoe ufafanuzi wa Mkanganyiko huu wa wewe kupinga kiasi hicho wabunge wasilipwe na baadae wewe mwenyewe tena kushinikiza ulipwe kiasi hichohicho na Chadema wakati ukijua kipatao cha Chadema kilivyo,pia kwa jambo hili una sababu za msingi za kutokuitwa Fisadi! Huu ni Ufisadi ndani ya CHADEMA!
 
Hii thread imenipa fursa ya kuelezea jambo moja. Naamini sio Dr (PhD) Slaa pekee ameacha kujivinjari humu jamvini kwa kuchangia mada. Wapo wengi sana. Na ninaamin ni baada ya jukwaa kuvamiwa na watu wasio na fikra na wanaosukumwa na waliowatuma halafu wanaleta mada za kipuuzi kama hii. Tena zinarudia rudia kila siku. Nadhan wanavinjari lakini hawawezi kuzungumzia jambo ambalo lilishatolewa ufafanuzi maana ni kupoteza muda! Leteni mada mpya za kujenga utamwona.
 
Back
Top Bottom