ntogwisangu said:Ni vizuri kafanya hivyo!
Sijalisoma bado la yaelekea anajibu kwa kuonyesha postive achievements za CHADEMA na hilo ni kosa!
Mayage kasema chama kina nafasi wafanye zaidi ya walivyofanya sasa! Sasa inaonekana watu hawapendi kukosolewa, hili nalo ni mapungufu ya kiuongozi! Ndo maana Dr Slaa naye hafai kuwa kiongozi wa nchii hii!
Haya ni maoni yangu kama mwana CHADEMA, unafiki kwangu hauna nafasi!!!
nafasi ya chama kufanya zaidi hutolewa na wananchi na chama hakina uwezo wa kuinyakua. Kama umekiri kuwa kwa kiasi fulani wamefanikiwa na unaamini wanahitajika kufanya zaidi, suala sahihi la wewe kufanya ni kuunga mkono yale yaliyofikiwa ili ridhaa ya wananchi ipatikane, wapewe dola na waweze kufanya hiyo zaidi unayoitaka.
Kuna tofauti kubwa kati ya kukosoa na kuponda. Usipoijua hiyo tofauti utagombana na mama mkwe wako. mayage ameconclude kwenye makala yake kuwa solution ni kuanzishwa chama kingine, huu ni ukosoaji? yawezekana huna nia mbaya ktk comments zako, lkn yaelekea huna akili pia. ni nini unachohitaji wewe kama mwananchi, siasa za kubwabwaja majukwaani na kusubiri uchaguzi au chama kilicho active wakati wote kikiwatumikia wananchi?
uanaharakati ndio hasa msingi wa mabadiliko chanya ktk mataifa ya kidemokrasia. Ndio njia ya kupata haki toka kwa watawala dhalimu. Shida yetu watanzania ni uoga wa mabadiliko. Badilika kimtazamo, acha uoga na unga mkono harakati hizi za chadema. Tanzania haitakuwa huru kwa uwakilishi wa wabunge wanaoorodhesha msululu wa matatizo ya majimbo yao halafu wamalizie kwa 'naunga hoja mkono kwa 100%'.
Na kama shida yako ni yale yanayohubiriwa majukwaani na chadema, labda nikuulize: ulitaka wajadili nini zaidi ya yale yanayotukwamisha tusiendelee?
Kuna kingine kinachotukwamisha zaidi ya ufisadi, mikataba mibovu, wizi wa rasilimali, uwajibikaji mdogo, kujuana na kufumbiana macho tunapokosea?
ni vyema wananchi tukaaacha upuuzi, hizi nguvu za kuisakama chadema tungeielekeza kwenye kuisakama serikali iwachukulie hatua wanaotufilisi. Kama tutagoma kushiriki harakati na kukaa tusubiri kuanzishwa kwa chama kitakacholeta maajabu kwa kukaa ofisini na kukomesha mabaya haya, basi hatutakuwa na tofauti na mayage anayewaza kwa kutumia tumbo.
Wako ktk kupinga mambo ya kijinga na ukosoaji usio na mashiko,
shizukan
Haya ni maoni yangu kama mwana CHADEMA, unafiki kwangu hauna nafasi!!!
ntogwisangu, umeanza lini kuwa mwanachadema? Acha kutudanganya mkuu, ninakufahamu vema sana na harakati zako zote za ccm. Sitaki tu kusema kwa mifano nisije nikaambiwa name calling, lakini si vizuri kujivika ngozi ya kondoo wakati wewe ni mbwa mwitu.
Nyie CHADEMA ni watu gani msiotaka kukosolewa???? Mayage katika makala yake aliwakosoa na kuwataka mfanye vizuri zaidi lakini mmeigeuza makala yake kuwa ugomvi kana kwamba amewatukana matusi ya nguoni. Ni nyie mnaolalamika hali ya nchi kwa sasa na kuhoji kama kweli Rais ana washauri. Nyie mnaukataa ushauri wa Mayage, je huyo Padri wenu aliyeasi akiingia Ikulu atamsikiliza nani?
nimesoma nimechoka kweli!!!!!!!ruksa ulichonacho kuhusu mimi kiweke!!!!!!!!hunijui sikujui!!!that"s all!!!!majina yetu haya tabora,shinyanga,mwanza na hata mkoa mpya geita!!!
Sasa wewekama ni mwana CHADEMA kwanini usiende kwenye chama ukaeleza haya matakwa yako kuliko kulalama hapa JF?
Huyu Mayage Mayage ndio nani? Sijawahi kumsikia au kumsoma popote. Kama kuna mtu ana profile yake atumwagie hapa ili tuone kama ana sifa za kutosha kubishana na Dr wa ukweli.
Mayange S Mayange yupo sahihi kwenye ili..
Mayange S Mayange yupo sahihi kwenye ili..
Lini CHADEMA wataacha kulalamika hovyo!!!!!!!!!!!!!!!
Hebu ainisha hapa matokeo mabaya ya Mbowe ktk chama kama mwenyekiti kwa kiasi cha wewe kusema sio mtu sahihi wa kwenda naye 2015. Una uhakika hauna kaudugu na Hamad Rashid kweli? coz mnafanana kimtazamo sana.huo na wewe upotoshaji!!yawezekana kweli sina akili!!lakin kama ni ya darasani nina uhakika mkubwa hiyo ninayo!!tena wa 100%labda kwa vile wanasema zipo za darasani na za mtaani pengine huo upande wa pili nikawa sina!!!sijapinga yafanywayo!!!ninachokisema kwamba mapendekezo aliyotoa mayage yana tija!!ni ya kufuatwa!!!ukosoaji wake ni chama kujitizama tu!!!ila mimi nikaja na hoja nyingine nikasema kwamba tuna golden chance sasa katika siasa za nchi hii!!ila nikasema mwenyekiti wetu tangu ahachiwe na mh mtei,sasa yatosha ang'atuke!!maana si mtu sahihi wa kwenda naye 2015!!!na nikatoa baadhi ya sababu!!!!ni hayo tu!!!!na kwangu mjadala umefungwa!!!!