Mohamedi Mtoi
R I P
- Dec 11, 2010
- 3,321
- 6,328
Leo katibu mkuu wa CHADEMA Dr Willbroad Slaa amefanya mkutano mkubwa wa hadhara jimbo la Momba mkoani Mbeya.
Mkutano huo umetanguliwa na shughuli za mchana kutwa za kukagua zoezi la uandikishaji daftari la kudumu la wapiga kura kwa mfumo wa BVR kwenye maeneo mbalimbali ya jimbo hilo ambapo zoezi la uandikishaji linaendelea.
Hamasa ilikuwa kubwa na watu wengi waliojitokeza kwenye vituo mbalimbali na kujiandikisha hasa baada ratiba ya ziara hiyo kutangazwa kwenye vijiji na vitongoji mbalimbali wilayani hapo.
Kwenye mkutano mkubwa wa hadhara Dr Slaa aliwaambia wakazi wa Mbozi kuwa huu ni wakati muhimu sana kwao kwa kuhakikisha wanachuja kauli za wagombea mbalimbali watakao waomba ridhaa ili kuwachagua kushika nafasi mbalimbali.
Aliwatahadhirisha na kundi la wagombea walioanza kutangaza nia kwa kutoa kauli za hadaa wakati wamekuwa viongozi waandamizi wa serikali ambayo imeshindwa kuwaletea watanzania maisha bora kama ilivyo ahidi miaka 5 iliyopita.
Amewaambia huu sio wakati wa kusikia kauli za hadaa kuhusu matumaini bali niwakati wa Watanzania kupata kiongozi atakaye waletea watanzania uhakika wa kupata huduma mbalimbali za kijamii.
Amesema huu ni wakati wa vijana wa kitanzania kuwa na uhakika wa kusoma elimu ya juu wakiwa na uhakika wa mikopo na kuwa na uhakika wa kupata ajira mara baada ya kumaliza elimu kwenye vyuo mbalimbali. Amesema hii haipaswi kuwa safari ya matumaini kwa kina mama wanao kwenda kujifungua kwenye mahospitali bali ni wakati wa kina mama kwenda kwenye huduma za afya wakiwa na uhakika kuwa watapata dawa, vitanda na watarudi nyumbani salama mara baada ya kujifungua na kuendelea na maisha yao tofauti na ilivyo sasa ambapo ujauzito umekuwa kama jaribio la kifo kwa kina mama.
Alieleza utajiri wa raslimali ambazo Tanzania imebarikiwa lakini bado hazija wanufaisha watanzania kama ilivyopaswa kuwa. Amewahimiza wakazi wa Mbozi kuhakikisha wana tunza kadi zao za mpiga kura ili wafanye maamuzi sahihi kwenye uchaguzi mkuu ujao kwa kuachana na chama ambacho kimendelea kuwaacha watanzania wengi wakiishi kwenye lindi la umaskini wakiwa hawana hata uhakika wa kupata mlo au kujenga nyumba bora za kuishi.
Naomba kuwasilisha japo kwa kifupi kilicho jiri Momba.