Dr. Slaa Afuatiliwa na watu wasiojulikana kutoka Iringa hadi Dar Es Salaam

Dr. Wa ukweli usife moyo kwani penye mafanikio hapakosi changamoto kama hizi na mwisho wake mafanikio yatakuwepo mfano mzuri ni NELSON MANDELA wakati akipigania uhuru wa south afrika

mandela hakuwa muongo na mzushi kama dokta ni makosa makubwa dokta kumfananisha na mandela.
 
Ili nimuone Dr anaakili timamu
1. Athibitishe hiyo namba ya gari sisi tuko tayari kufuatilia na kutaja gari ni ya nani.
2. Abandike hiyo picha ya gari iliyo pigwa. Na kama picha imechakachuliwa tutaielewa ninazo tools.

La sivyo huyu mzee atakuwa anazeeka vibaya.
 
samahani Dr.W.Slaa tunaomba utuwekee hiyo picha mlio piga tuione. tunaweza kulitambua. mia
 
Last edited by a moderator:
Spinning at the highest order.

Hivi wewe kwa akili zako kama kweli kuna watu wanataka kuwadhuru viongozi wa CHADEMA watahangaika kwa jinsi unavyoelezea hapa.

Siyo kila jambo ni siasa siasa siasa. Siku hizi mwanasiasa hata akikumbana na vibaka anadai wanasiasa wanamfanyizia.

Jifunzeni kutokuwa wepesi wa kupata majibu kabla ya uchunguzi makini.

Cha kushangaza hao hao watu wa usalama mnaowatuhumu kwa matukio mbali mbali yanayowahusu, ndiyo hao hao mnaotueleza mlienda kulipoti tukio.

Yaani umeamua kuja na ID mahususi kwa ajiri ya SPINNING za kiulinzi.

Kweli tutasikia mengi.

kwa TISS ya sasa kwa jinsi wasivyo na akili haya yanawezekana. kwani dr ulimboka ilikuwaje?
 
Spinning at the highest order.

Hivi wewe kwa akili zako kama kweli kuna watu wanataka kuwadhuru viongozi wa CHADEMA watahangaika kwa jinsi unavyoelezea hapa.

Siyo kila jambo ni siasa siasa siasa. Siku hizi mwanasiasa hata akikumbana na vibaka anadai wanasiasa wanamfanyizia.

Jifunzeni kutokuwa wepesi wa kupata majibu kabla ya uchunguzi makini.

Cha kushangaza hao hao watu wa usalama mnaowatuhumu kwa matukio mbali mbali yanayowahusu, ndiyo hao hao mnaotueleza mlienda kulipoti tukio.

Yaani umeamua kuja na ID mahususi kwa ajiri ya SPINNING za kiulinzi.

Kweli tutasikia mengi.
Mkuu hawa jamaa wanatafuta attention kwa gharama zote sasa,
Usishangae kesho ukisikia mbunge wa chadema anatoa show ya bolingo kariakoo ili aandikwe magazetini.
Haya mambo ya magari kukufuata au kuongozana nayo katika safari ni jambo la kawaida , wakati mwingine hutokea tu kwani wengine wakiwa kwenye safari ndefu hupenda kuongozana na magari mengine ili wasichoke na pia kuwa na back up kama wakipatwa na lolote barabarani, mimi pia huwa napenda kufuata gari ambalo naliona linaenda safari ndefu kama yangu kama kampani.
Na pia ni kawaida kwa binadamu kuhisi anafuatwa hasa pale anapokuwa mtu maarufu kama Dr.
Mbona mimi nilipotoka kwa Dr kuna magari mawili yalinifuata sana mpaka nikaamua kusimama na kuwapiga mkwara wakasepa? Dr si ana walinzi? kwa nini mlinzi asifyatue moja ya juu ili jamaa wasepe? Unajuje kama hao sio vibaka waliokuwa wanataka kuwapora hela walizochangisha kwenye mikutano?
 
Ili nimuone Dr anaakili timamu
1. Athibitishe hiyo namba ya gari sisi tuko tayari kufuatilia na kutaja gari ni ya nani.
2. Abandike hiyo picha ya gari iliyo pigwa. Na kama picha imechakachuliwa tutaielewa ninazo tools.

La sivyo huyu mzee atakuwa anazeeka vibaya.
Mkuu si unajua usiposikika ndio unakuwa umekwisha kisiasa ?
Inabidi ufanye lolote lakini sio kama anavyofanya lema ili uonekane upo, hiyo ndio siasa ya chadema
 
Mkuu si unajua usiposikika ndio unakuwa umekwisha kisiasa ?
Inabidi ufanye lolote lakini sio kama anavyofanya lema ili uonekane upo, hiyo ndio siasa ya chadema
Hawa jamaa wanadhani wanaogea na watu ambao hamnazo.
Hivi kweli wewe inakujia akilini. Mzee mzima unakua muongo.
Na Mzee Slaa anatoa maelezo ya kitoto kabisa. Hivi anatuona sisi kama nini huyu mzee?
Asipo thibitisha basi huyu mzee kila kitu atakacho ongea nitajua tu akili zake zimeanza kuliwa nauzee
 
Wanasema hilo gari limewafuata kwa muda mrefu sana na waliweza kulitambua kila wakikutana nalo.
Hata kama hawajalipiga picha basi watupatie usajili wa hilo gari/ namba zake
Kama hawana mimi naweza kuwapatia namba ya gari la polisi moja
STG 8915 TOYOTA LANDCRUISER
Kama hiyo haitoshi naweza kuwapatia nyingine nyingi tu ninazikumbuka nilipokuwa polisi au kuna lile la usalama wa taifa namba T500 SER nalo ni li landcruiser ila sijui kama rangi zinafanana
 
Hao ni CCMTISS. Kudos Jack Zoka and Ramadhani Ighondu, the nation is watching everything you do...

Waliomfuatilia wanajulikana na sababu zinajulikana. Amezaa na mke wa mtu mkuu, kwa hiyo ni lazima ashughulikiwe. Sio kila kitu eti TISS wakati mitaani mnabeba wake za watu.
 
hivi ni mimi pekeyangu ninayehisi kuwa tangu Video ya Lwakatare itolewe, CHADEMA wamekuwa wakihangaika namna ya kuifunika na kuonesha kuwa mbaya ni serikali na vyombo vyake vya dola?? mana tangu kutoka kwa video ile, tuhuma dhidi ya serikali na vyombo vyake vimezidi maradufu, haya, lilipokuja bunge ndo kabisa, wakaweka tuhuma zao hadi kwenye hotuba ambazo zilistahili kulenga kuikosoa serikali katika kushindwa ama kuchelewa kuleta maendeleo ya nchi..badala yake zikaongelea tuhuma dhidi ya usalama, na kupigwa ama kutishiwa kuuwa kwa viongozi wa CDM?? hivi ni mimi pekee ninayeona kuwa hadi leo CDM imeshindwa kutoa neno ama skendo inayoweza fumba macho na ufahamu wa vijana wachache wa kitanzania ambao bado tuna uwezo wa kufikiri na kuamua tofauti na wale vijana waliokuwa brainwashed na kuamini kila neno linalotoka midomoni mwa viongozi wa CDM na kuwa tayari kutetea maneno hayo hata kwa uhai wao bila ya kufahamu ukweli wake??
Dr. W slaa, najua juzi tu CDM imetangaza kuwa wewe ndiye mgombea wa Urais 2015, hivi ukishinda, utahudhuria sherehe yoyote ya kitaifa?? hivi utafuta vyombo vyote vya ulinzi na usalama na kuweka watu wako?? hivi utafanya kazi na nani ambaye bado hujamtukana?? au hao vijana wako wanaovaa makoti makubwa meusi na miwani meusi ndiyo watakuwa wanausalama wako?? kwa akili yako, do u think its that simple?? au nawewe umekuwa brainwashed na wazungu??
 
Pre empting approach in solving difficult problems. Watuambie detailde information kuhusu kumvamia mama yake zitto..nyie ni wa maana wengine takataka
 
Mkuu hawa jamaa wanatafuta attention kwa gharama zote sasa,
Usishangae kesho ukisikia mbunge wa chadema anatoa show ya bolingo kariakoo ili aandikwe magazetini.
Haya mambo ya magari kukufuata au kuongozana nayo katika safari ni jambo la kawaida , wakati mwingine hutokea tu kwani wengine wakiwa kwenye safari ndefu hupenda kuongozana na magari mengine ili wasichoke na pia kuwa na back up kama wakipatwa na lolote barabarani, mimi pia huwa napenda kufuata gari ambalo naliona linaenda safari ndefu kama yangu kama kampani.
Na pia ni kawaida kwa binadamu kuhisi anafuatwa hasa pale anapokuwa mtu maarufu kama Dr.
Mbona mimi nilipotoka kwa Dr kuna magari mawili yalinifuata sana mpaka nikaamua kusimama na kuwapiga mkwara wakasepa? Dr si ana walinzi? kwa nini mlinzi asifyatue moja ya juu ili jamaa wasepe? Unajuje kama hao sio vibaka waliokuwa wanataka kuwapora hela walizochangisha kwenye mikutano?
...Attention mbona mnatupa bure tu wenyewe? mfano MULONGO wenu wa Arusha ameieneza CDM kwa kasi sana siku mbili hizi hadi raha. Na kanda zitatengenezwa 3000 kuwaonyesha watanzania waamue nani ana hatia kati ya RC na Lema. Unajua pamoja na ubaya wenu Mungu ameamua kuwatumia ninyininyi kuwazindua watanzania.
 
Msikubali kulaghaiwa na Dr. Slaa.

Note kuwa hajataja namba ya gari. Hii ni kujaribu kujiweka mbali na responsibility za huu uzushi.

Hii simulizi ni sawa Dar Express lifike Arusha halafu waseme Scandnavia lilikuwa linatufuata!

Weka picha ya gari hapa tulione.

Mkuu Zemarcopolo post yako ina thibitisha ya kuwa kuitetea CCM na Serikali yake lazima uwe tahira; Watu wenye uwezo finyu wa kufikiria kama wewe na shindwa ni waweke katika kundi gani. Mwanzoni mmeanza kumshambulia mleta mada kwa madai ya kuwa hizo ni porojo kwa sababu yeye siye verified user, imefikia mahali ambapo Moderator ameamua kuufunga huu mjadala kwa madai ya kuwa ni lazima tupate mtu mwenye credibility kutoka kwenye uongozi wa chama cha Ukombozi aweze kuthibitisha hayo madai. Dr. Slaa amejitokea na kueleza wazi bila kupepesa macho, kama kawaida yenu misukule mmegeuka tena na kuibuka na hoja ya kipuuzi ya kudai picha ya ghari; Je tuwaeleweje ?

Kwa taarifa yenu Tunampenda sana, tunamthamini, tunamheshimu, tunamwamini na tunamwombea Dr.Slaa usiku na mchana ili mwenyezi Mungu amuepushe na hila zenu chafu zilizo ghubikwa na ufedhuli.
 
Spinning at the highest order.

Hivi wewe kwa akili zako kama kweli kuna watu wanataka kuwadhuru viongozi wa CHADEMA watahangaika kwa jinsi unavyoelezea hapa.

Siyo kila jambo ni siasa siasa siasa. Siku hizi mwanasiasa hata akikumbana na vibaka anadai wanasiasa wanamfanyizia.

Jifunzeni kutokuwa wepesi wa kupata majibu kabla ya uchunguzi makini.

Cha kushangaza hao hao watu wa usalama mnaowatuhumu kwa matukio mbali mbali yanayowahusu, ndiyo hao hao mnaotueleza mlienda kulipoti tukio.

Yaani umeamua kuja na ID mahususi kwa ajiri ya SPINNING za kiulinzi.

Kweli tutasikia mengi.

Mkuu si kila police ni saidi mwema au kila TISS ni igondu. Mendine wanakerwa na uovu wa mabosi wao lakini hawana la kufanya kwakua wakubwa wameshika mpini ila wakipata nafasi wanadhibiti uovu ulioko ngazi za juu
 
Sijui nilikua naota au ni kweli, nakumbuka (kama nilikua naota sijui) Mzee Wassira alisema Bungeni kua Usalama wa Taifa hawawezi kumtesa Absalom Kibanda kwasababu sio kitisho kwa serikali labda Dr. Slaa au Mbowe, kama ni ndoto labda ndio inataka kutimia (kumbe ndoto zingine hua kweli) kama haikua ndoto may be we have to start connecting the dots here.
 
WanaJF,

Mimi Dr Slaa ambaye kwa siku 4 nimekuwa na ziara ya mkoa wa Iringa,Mbeya na Njombe nilikuwa narudi Dar jana baada ya kulala Iringa mjini kutokea Njombe.

Tukio linaloelezwa ni la kweli na nimelishuhudia mwenyewe. nimeingia kwa jina langu na ID yangu ili kuondoa dhana ya Spinning.
Namshukuru sana aliyetoa Taarifa, na kuliwasilisha kama ilivyotokea bila kuongeza wala kupunguza kitu.

Tuliondoka Iringa majira ya saa 3.30 hivi. Kwa mwanzo hatukutambua kitu, ila mara ya kwanza tuliona gari hilo likitupita kwa kasi km kama 20 hivi baada ya kupita junction ya Ipogolo. Tuliona kawaida. katika hatua hiyo tulijua ni wasafiri wenzetu. baadaye tukawa tunawapita, wanatupita kasi na kupotea, lakini baada ya muda tunawakuta na kutupisha. hatukustuka sana, japo kuanzia Ilula tukaanza kuulizana.

Mlima Kitonga wakatipita kwa kasi sana japo mbele yetu kulikuwa na semitrela kama 4 zikiteremka pole pole sana na nabasi 2 kwenye kona moja basi lililpkuwa mbele yetu kikakwaruzwa na lori lililokuwa lunapanda. Tukachukua tahadhari sana.

Tulipovuka daraja la Mtp Ruaha tukalikuta Lcruiser hiyo imesimama pembeni lakini abiria wake wote walikuwa ndani. tulipolikaribia likaondoka kwa kasi. kidogo tulistuka. sisi tukaamua makusudi kusimama na kununua vitunguu. Tulipofika Mikumi mjini tukalikuta tena likienda taratibu. kuanzia hapo tukawa makini sana hasa kwenye kona na au vichaka vikubwa. kimsingi tukajiweka kwenye hali ya tahadhari kubwa.

Moro tuliingia Petrol Station nao pia wakaingia nyuma yetu lakini hawakujaza mafuta. Punda wakaondoka direction ya Dodoma. Ikumbukwe sisi tumetoka Njombe tumetangaza tunaenda Kongwa ,Jimbo la Ndugai. mimi nikakapata dharura nikapaswa kurudi Dar. hivyo baada ya mufuta tukafuata direction ya Dar. Punde likatokeza tena na kutupita. Tukalipita kidogo kabla ya Chalinze. Baada ya Chalinze hatukuliona tena mpaka tulipolikuta Junction ya Tamko limepaka. mata nyibgine huwa natumia hiyo junction badala ya kuingia Jijini. Na kweli driver akapiga indicator nyingie hapo. nikaagiza tuelekee jijini Dar. ndipo ghafla nao wakaingia barabarani nyuma ya gari langu kabisa. ndipp nikaagiza afisa wangu apande juu ya gari letu -roof top na kulipga picha. kuona hivyo ghafla likatoka pembeni na kupaki. sisi tukaendelea, ndipo mbele kidogo tukakuta askari walioko zamu yao ya kawaida wakatusimamisha na tukawapa taarifa ya halu hiyo.

Sasa katika mazingira hayo kuna mtu bado anafikiria ni spinning anaweza kuamini hivyo hatuwezi kumlazimisha.

Natumaini nimefafanua ya kupotosha. Nawashukuru wote waliotupa pole. Tunaanza na Mungu tunabaki na Mungu. Hatumwogopi Binadamu na mapambano ya ukombozo hayatakoma kwa vitisho vya aiina hiyo, ndiyo kwanza vinatupa ari na mori.

Too Low!
 
Wanasema hilo gari limewafuata kwa muda mrefu sana na waliweza kulitambua kila wakikutana nalo.
Hata kama hawajalipiga picha basi watupatie usajili wa hilo gari/ namba zake
Kama hawana mimi naweza kuwapatia namba ya gari la polisi moja
STG 8915 TOYOTA LANDCRUISER
Kama hiyo haitoshi naweza kuwapatia nyingine nyingi tu ninazikumbuka nilipokuwa polisi au kuna lile la usalama wa taifa namba T500 SER nalo ni li landcruiser ila sijui kama rangi zinafanana
hivi una akili timamu kweli?Namba ya gari si imewekwa hapo juu?
 
Back
Top Bottom