Mkuu,
Huko peke yako mie binafsi nilikuwa impressed sana nilipomuona Mke wa rais wa zanzibar akienda kufuturu na wananchi wa kawaida vijijini na sio kuwaita watu wamfuate ikulu. Hata hivyo tusubiri bado mapema sana.
Hata hivyo CUF nao wanastahiki kupongezwa sana kwani wana ushiriki mkubwa katika haya mafanikio. Tunawaombea kila la kheri na sie Tanganyika tupate vigezo vya kuleta mageuzi kwetu.
Mkuu, tueleweshane zaidi huo ustahiki ulivyo kwa CUF hapo penye wino mwekundu.
kazi na kula hapana shida bwana,good job DAKTARI.Duh! Kazi nzuri Dr Shein kama ndiyo hali halisi ya Zanzibar unastahili pongezi. Inawezekana ni matunda ya kufanya kazi na mtu kama Mkapa, sasa la kuangalia akiweza kuhifadhi pesa nyingi asije geuka kama Mkapa
hapo nilipo bold,mzanzibar aongoze kwake,tanganyika kuna watu wake,hatuwezi kuongozwa na mzanzibar karne,thos edays za wao kuongoza huku ziliisha,na hawa wachache waliopo kwenye uongozi huku tanganyika watakuja kwisha kabsa,hawana nafasi tena hukuDr shein ni rais wa zanzibar ambaye wengi wetu tulikuwa tunamfahamu kama mzee wa mikasi. Nimekuwa namfuatilia kwa karibu utendaji wake tangu ashike madaraka. Sasa hivi wamefikia miezi sita tangu serikali anayoiongoza ashike hatamu na kwa utendaji wake na performance ni wa kuigwa. Nimefanya tathmini haya yafuatayo:-
Aliposhika madaraka motto ya uongozi wake ni Zanzibar yenye maendeleo na kujitegemea.
Vitu alivyovifanya hadi sasa tangu awe kiongozi wa nchi:-
a. Ameweza kutengeneza motto ya serikali ni kuhakikisha wizara za zanzibar zinakuwa na mipango sahihi na kutekelezeka.
b. Amepunguza matumizi ya viongozi wa juu wa serikali pamoja na safari zisizo na muhimu na kuongeza mishahara ya wafanyakazi wa chini kwa zaidi ya asilimia 100.
c. Zanzibar ina current account surplus na imekuwa inaongezeka kila mwezi kuonyesha kukuwa kwa exports kuliko imports in the country.
d. GDP ya zanzibar inakuwa kwa kasi na ndio inachangia kwa kukua kwa sekta ya uzalishaji (production and trade) Tanzania.
e. Hospitali kuu ya mnazi mmoja inafanyiwa ukarabati mkubwa jambo ambalo hospitali hii ilitelekezwa kitambo.
f. Ameweza kuwakamata wafanyabiashara wakuu wa madawa ya kulevya zanzibar na wako mbio kufikishwa mahakamani.
g. Airport kuu ya unguja inaanza kujengwa kufikia hadhi ya kimataifa (jambo lilikuwa hekaya za kufikirika zamani) na wameanza mchakato wa kuanza kujenga airport kubwa pemba.
h. Zanzibar wako mbioni kuanzisha shirika lao la ndege.
i. Amepandisha bei ya karafuu kutoka shillingi 3,000 hadi Tshs 20,000 (na hivyo kutatua tatizo la umaskini kwa upande mwengine kwani ni zao la karafuu ni uti wa mgongo wa zanzibar na serikali ililitupa mgongo na matokeo Kenya wametajirika na wengine wameamua kuacha kulima karafuu na kufanya biashara na vijana wengine kuwa hawana kazi) baada ya kupanda bei vijana wengi wameamua kurudi shamba kuanza kulima tena karafuu.
Hayo ni machache ninayo fahamu ila binafsi nampa pongezi Dr Shein wewe ni kiongozi makini na tunasikia mwadilifu mmungu akupe nguvu uendelee na umakini huo huo uwasaidie wazanzibar kwa walikuwa maskini mno!!! Tunatamani uje kutuongoza na sie Tanganyika kwani tumekosa mwelekeo kwa sasa!!!!
SMZ yaondoa muswada wa mafao ya viongozi | Send to a friend |
Saturday, 22 October 2011 09:32 |
0digg Talib Ussi, Zanzibar BARAZA la Wakilishi Zanzibar (BLW) limeukataa muswada wa sheria uliohusu maslahi na mafao ya viongozi wakuu wa nchi akiwamo rais na makamu wake baada ya kustaafu. Mwenyekiti wa Kamati ya Viongozi wa Kitaifa katika Baraza la Wakilishi, Hamza Hassan Juma, alisema wameitaka wizara husika kufanyia marekebisho vipengele ambavyo wajumbe waliviona vina kasoro kubwa. Hamza alisema siyo vyema kuangalia maslahi ya vingozi bila kuangalia hali ya uchumi wa nchi hasa kutokana na gharama kubwa zinazohitajika kwenye muswada huo. Kwa upande wake, Spika wa Baraza la Wakilishi, Pandu Ameir kificho, alisema wajumbe wengi wameona ni bora kuwekwa vipaumbele kwenye masuala ya uchumi na mambo yanaohusu jamii kuondoa umaskini. "Suala hili lingali linaleta mgawanyiko kidogo kwenye jamii, ndiyo maana wajumbe wakaona ni vyema kuliweka kando kwanza na kwenda kulitafakari upya kwa maslahi ya taifa," alisema Kificho na kuongeza: "Muswada huo umeondolewa kutokana na kuwapo kasoro nyingi na hata upande wa tafsiri yake katika vifungu vingi havifahamiki." Katika muswada huo ulikuwa unampa rais uwezo kupokea mshahara wake wote baada ya kustaafu na pindi anapofariki, mkewe angepokea pencheni kama mshahara wa rais aliyopo madarakani.Kwa upande wa makamu wa rais, kama akifariki mkewe angepokea kwa muda wa miaka mitatu mshahara sawa na aliokuwa akipokea mume wake akiwa madarakani. Pia, spika akistaafu angelipwa kiinua mgongo kwa asilimia 50 mshahara wake aliokuwa akilipwa akiwa madarakani. Kuondolewa kwa mswada huo ni kuzima hasira za wananchi kutokana na kudai kuwa Serikali inatoa kipaumbele kwa viongozi, ilhali wananchi wanaendelea kuwa maskini wa kutupwa. |
wetu wa bara ana Ph.D za kupewa yeye wa visiwani kasomea tofauti kubwa haswa
Pamoja na Ufisadi, nadhani ni bora pia sifa japo kidogo zikamuendea Mkapa aliyemuibua kwenye jukwaa kuu. At that time wengi tulimuona ni mgeni sana kwenye siasa na hatukuwahi kumsikia kabla.
Pia Karume aliweka mipango mizuri ambayo Dr. Shein anaitekeleza now maana alikuwa anajiandaa kuwa raisi wa muungano baada ya kustaafu Zanzibar. Aliyeharibu mpango huo ni Mkapa baada ya kuona kuwa Zanzibar haitatawalika kama Bilal ataachwa mtaani.
Ah...nchi yenye ukubwa kama wilaya nadhani hata Lusinde anaweza kuiendesha. Hivi ile ripoti ya tume iliyochunguza kuzama kwa ile meli iliyoua wazanzibari wengi imefanyiwa kazi au ndiyo hivyo tena viongozi(including Shein) wapowapo tu kama majoka ya kibisa kwenye hii issue?Hayo ndio matunda ya Serikali ya umoja wa kitaifa. Kwani wakti wa malumbano umekwisha sasa wanajenga nchi.
Hongera Dr Alli Moh'd Shein