Dr Peter Dalaly Kafumu apata ajali

Kuchasoni Kuchawangu

JF-Expert Member
Aug 21, 2012
603
340
Habari za kuaminika nimezipata sasa hivi kuwa Dr Kafumu amelazwa hapa Hospitali ya Nkinga mission baada ya kupata ajali wakati akitokea Tabora kukata rufaa ya kupinga hukumu ya kuvuliwa ubunge.Ameumia vibaya sehemu za kichwani. Habari nimepewa na doctor mmoja ambaye yupo karibu nami.Nitawajulisha zaidi.
 
Habari za uhakika na zimethibitishwa na Mwigulu Nchemba mbele ya mkutano wa hadhara Nkinga leo jioni.

Kuwa Dr Dalaly Kafumu amepata ajali mbaya maeneo ya kijiji cha Mwisi, amelazwa hapa Nkinga hospital ameumia kichwani.

Nchemba amehusisha ajali hiyo na imani za kishirikina kuwa ni uchawi wa Cdm uliosababisha ajali hiyo.

-------
Kutoka kwa Kigwangalla:

Dr. Dalaly Kafumu amepata ajali ya kupinduka na gari akielekea kwenye kijiji kimoja kilichopo kata ya Mwisi ambako alikuwa anaelekea kushiriki mazishi ya Mama mmoja maarufu. Ajali hiyo ilitokea jana ambapo gari ilipoteza uelekeo kutokana na hitilafu ya barabara na hivyo kuvutwa, kugonga gema na kupinduka mara moja na gari kukaa matairi juu.

Gari iko nyang'anyang'a huwezi amini kama kuna mtu ametoka salama, lakini tunavyoongea hapa Dr. Kafumu na kijana wake ambaye alikuwa akiendesha walitoka salama. Dk. Alibanwa na Airbags na walilazimika ili kumtoa kuvunja mavyuma kwa shooka na kumkuta amezimia na alizinduka baada ya muda kidogo, pia alikuwa na bruises zilizokuwa zinavuja damu sana kichwani na alilazwa hospitali ya Nkinga na asbh hii atapewa ruhusa arudi nyumbani.

Amekuwa jimboni humo toka Jumatatu akifanya ziara ya kukamilisha miradi ya maendeleo aliyoianzisha, pia kuwaondoa mashaka wananchi kuwa hatowatelekeza kwa kuwa ametolewa Ubunge, na kwamba bado yuko nao pamoja tu.
 
Huyu jamaa Mwigulu Mchemba ni wa aina gani huyu mtu lile domo lake kubwa linaropoka tu kila leo,huyu jamaa ni mshirikina sana na hawa ndio wanaouwa vikongwe kule kwao huyu t..i...g....o kwao si ndo Singitaa atakuwa na laana ya kuua vikongwe so ile damu ndio inamtafuta na bado we shall see
 
haa haa haaa


Udini na ukabila vimeshindikana .... sasa wamehamia kwa sangoma
 
Chadema again what for nyinyi CCM? Sasa hapo wamehusika na nini?Huwa mnawatafuta CHADEMA sana naona maana kila kitu ni CHADEMA na why sio CUF au TLP??
 
hiyo ni ishara kuwa apumzike siasa si mpango wa mungu, nimeambiwa alikuwa anatoka kukata rufaa ya kesi kutenguliwa ubunge, mungu akisema no ukilazimisha matokeo ndio huwa haya ya ajali mbaya!
 
oi Siasa hizi hadi za kutabiliana Vifo? naona CCM Wamehamia kwenye Imani za Kishirikina alizoanzisha jk na Marehemu Sheikh Yahya....
 
Watanzania tumefikia pabaya mpaka tunapoteza ubinadamu wetu suala la ajali linaweza kumtokea yoyote, pole sana Dr Kafumu.
 
Back
Top Bottom