Francis12
JF-Expert Member
- Sep 30, 2016
- 7,533
- 22,276
- Thread starter
- #21
Kwani amemrudisha Lipumba ofisini na kumtangaza kama Mwenyekiti halaliwa CUF ni nani?
Hongera Dr.
Kila mtu ameona na kusikia
Msajili alipaswa kumkemea Prof. Lipumba kwa ubabe na vuruvu alizofanya na kuharibu mkutano wa CUF.Ameonekana wazi akisamama na kutetea uvunjifu wa amani na mtu aliyesababisha wakina mama kupigwa na kudhalilishwa huku mali za ukumbi zikiharibiwa na viti vikivunjwa na watu kupigwa hovyo.
Hata kama Prof. Lipumba alikua na haki basi angeenda mahakamani na sio kutumia vijana kujichukulia sjeria mikononi.
Msajili anaufundisha nini umma wa watamzania kuhusu umuhimu wa kuzitumia mahakama kudai haki badala ya kufanya vurugu na ubabe kama alivyofanya Lipumba na mabaunsa wake.
Msajili wa vyama hakusimama kama juji zaidi ya kuegemea upande mmoja bila kujua kuwa hata kiongozi wa nchi kwa mfano akiamua kujiuzulu mwenyewe halafu ghafla akachukua baadhi ya majenerali wa jeshi waliokua marafiki zake na kutangaza kuridi basi atakua ameiweka nchi hiyo kwenye hali ya vurugu kwani unapojiuzulu unawafanya wanachama wengine kuwa kwenye nafasi ya kujiandaa kisaikolojia kupata nafasi iliyoachwa wazi.
Lipumba alipaswa ajiweke pembeni ili baadae achukue form tena ya kugombea kama mwanachama mwingine na akikosa kura basi akae pembeni na sio kulazimisha kurudi kama vile mtu aliyekua amesafiri.
Katiba ilikaa kimya mana hakuna mtu aliyetegemea kuona kiongozi mwenye akili timamu akijiuzulu yeye mwenyewe kwa hiyari halafu anakuja tena kusema ametengua barua yake.
Suala la kutengua linajadiliwa na kukubaliwa au kukataliwa na sio lazima likubaliwe.