Dr. Kimei: Hatua ya Serikali kuhamishia akaunti zake BoT, itasaidia kupunguza mfumuko wa bei

Anaunga tu mkono,mbona hatuweki wazi jinsi watakavopwaya kwa kukosa hizi hela
 
Yaani kwa lugha rahisi ni kwamba Serikali ilikuwa na akaunti mbalimbali kupitia mashirika yake Katika benki hzi za biashara mf.Crdb,NBC na NMB.Sasa kila ambapo serikali ilikuwa inapungukiwa hela kwenye mipango yake ilikuwa inakopa kutoka kwenye haya mabenki kupitia hati za dhamana na fungano(Treasury Bills & Bonds) na kulipa pamoja na riba.Tupo hapo??Sasa nini kulikuwa kinatokea??...Mf.Uweke kwangu elfu 10,halafu baada ya siku 3 uje unikope Elfu 8 sasa mimi ninachofanya ni nakukopesha na riba..mf 10%,ili unilipe 8800.Lakini ulichokopa ni kiasi ambacho nimekuwekea,ki mantiki ni umekopa hela yako tena na riba.Serikali ilikuwa inakopa hela yake yenyewe na kisha kuzilipa hizi benki na riba.Hiki ndicho JPM anachopigana nacho.Benki hizi zina kama Bil550/- sasa zikienda BoT shida za serikali nyingi zitazungushwa na hizi hela kuliko kukopa kwenye mabenki hela zake yenyewe.Kikubwa kutokana na kukosa fedha hizi Mabenki haya yatarudi kutafuta wateja mitaani pamoja na kushusha viwango vya riba ili wananchi wakope na wao wapate faida.
Natumai picha mmepata wakuu.
Hapa kidogo nimeelewa ila naomba nikuulize hizo zikishawekwa zitazungushwa vipi wakati bot hawafanyi biashara?
 
Sawa.Kama kukopa hata angekopa hyo elfu10 bado angenilipa elfu11 jumla na riba ya 10%.Kwa hiyo ningetengeneza elfu 1 kwa kumkopesha hela yake mwenyewe.Ndo sasa Serikali imeamua kuacha huo utaratibu,wanataka elfu 10 yao waichukue moja kwa moja wakae nayo wakiihitaji hawaji kukopa tena.
Hapo vipi??
hapa napata jibu kidogo ila hizi hela za serikali si zilikuwa zinashungushwa kwenye mabenk mwisho wa siku na wao wanapata riba kidogo kutoka kwenye haya mabenk mfano kwenye fixed account au inakuwaje maana ninachokiona BOT hawafanyi biashara hiyo hela itazarishwa vipi?
 
na utaathiri kipato cha hao wajanja wajanja,..i can tell walikuwa wanaziweka kwenye fixed deposit bila permission ya hazina...
Hata mimi nakunbali kwamba baadhi ya bank na WAJANJA wataumia na mfumo huu, ila kwenye soko kutaondoa ubaguzi maana vihela vidogo vitahitajika sana bank tofauti na mfumo wa sasa wa kubagua wateja wadogo, hivyo huenda rate za kufix zikapungua lakini pia nina wasiwassi na uwezo wa kukopesha wa hizi banks kama utaongezeka au!!
 
Ngoja tuone itavyokuwa vyovyote vile lazima kuna watu wataumia kwa njia moja ama nyingine, na pia wapo watu watafaidika
 
Inamaana Dr. Kimei alikuwa anajua kwamba serikali ilikuwa inapigwa na hizi bank na alikuwa kala ganzi tu? Wasi wasi wangu ni huduma kwa wateja manake hizi account zilipelekwa ktk mambenki ili kurahisisha huduma za kulipa kodi sasa ambacho sijakipata vyema ni uwekezaji wa kufungua branches ktk ofisi za TRA itakuwa vipi. BOT haina staff wengi na branches za kutosha isijekuwa tunarudishwa mambo ya kuweka jiwe katika foleni.

Dr. Kimei kweli hapa amesaza mpaka mwenyewe anasema basi manake wakati mwingine watu wanaweka hata msuri.
Mkuu hilo la malipo wala usiwe na wasiwasi wala haitohitaji wewe kwenda BOT kulipa kodi... mbona tayari mfumo ulibadilishwa tangu mwishoni mwa mwaka jana kodi yote inalipwa kupitia mabenki lakini inaenda moja kwa moja BOT? Walianzisha mfumo unaitwa Tax Bank ambapo benki zote zimewekewa hiyo system na software mteja yeyote analipia benki yoyote lakini pesa haibaki baenki inaenda BOT direct
 
Huyu jamaa anamyemelea beno ndulu.

Aliitaka sana hii nafasi toka enzi za kikwete. Haingii akilini kwamba bank yake ndio victim no 2 kwa hii move then yeye awe wa kwanza kuipongeza serikali kwa hili.
 
Naiona CRDB ikianza kudumaa, ila kabla ya kufika huko namuona Kimea akijifanya kuachia ngazi.
Soko letu liko tofauti sana.....unaweza kuamini baada ya serikali kutangaza kuondoa fedha zake ktk mabenki CRDB ikiwa mnufaika mkubwa lakini matokeo yake share za CRDB sokoni zinapanda!!!!!!!!
 
Hapa kidogo nimeelewa ila naomba nikuulize hizo zikishawekwa zitazungushwa vipi wakati bot hawafanyi biashara?
Ndo hapo patamu sasa kwa sababu BoT ni regulatory tu yaani ni Benki ya Usimamizi siyo benki ya kibiashara kabisa.Kwa hiyo kukusanya fedha hizi na kuziacha zikae tu ni kuondoa huo mzunguko wa pesa kwenye soko na kuzi dampu.Nadharia nyingine ni kuwa BoT itanunua Bonds (hati fungano) za kimataifa (kama ilivyokuwa kwenye skendo ya Stanbic) na hivyo kusababisha hitaji kubwa la dola sababu itatumia Tsh hizi kununulia dola hizo ili ikawekeze huko.
 
Hii
Kila kitu kikikosekana huwa kinaathiri kingine....Magari ya mikopo yakikosekana LIFT zitakosekana, watu wa dalalada wataongezeka hivyo kupelekea kuwa na msongamano wa abiria vituoni....Mtajazwa katika daladala hadi katika buti...sababu watu wamekosa hela za kununua magari yao binafsi
...
Ufinyu wa barabara ndio unaosababisha foleni..karne hizi si zakuwa na barabara moja...

hiyo argument niliyobold ni haina mashiko. kwenye uchumi, kubana matumizi ni policy yenye dhumuni la kurekbisha mzunguko wa fedha na mwenendo wa uchumi kwa ujumla, kama kuna sababu nzuri ya kufanya hivyo.
Anyway, kila policy (hata ya kutokubana matumizi) ina prons and cons. Always kuna gainers na loosers, hakuna policy ya kumnufaisha kila mtu. La muhimu ni what we gain (society yote kwa ujumla) kutokana na policy tunayoimplement. Swala la mtu/ kikundi cha watu kuloose hakisababishi tusi-implemnent policy especially kama ina faida kwa jamii yetu kwa ujumla wake.

Ulitakiwa tu kujazia nyama hiyo argument yako ya pili kuhusu ufinyu wa barabara. Barabara ziongezwe na public transport ziboreshwe, probably kwa kuwa na miradi ya mabasi yaendayo kasi. Mfano serikali ikiamua kuinvest kwenye ujenzi wa barabara/ reli tayari ni expansionary policy through increasing of government expenditure. So wakati ina-contract kwa kuwabana commercial banks inapoondoa accounts zake huko, at the same time inaweza kuwa ina-expand kwa kuinvest kwenye constructions kama hizo za barabara na sehemu nyingine.

Kuongezeka kwa magari binafsi hakutatui taizo la jam. Ushawahi kujiuliza kwa nini majiji kama london ukiingia na gari city centre unapigwa fine kubwa. Ili kupunguza foreni na kuencourage watu watumie public transport
 
Baadhi ya mashirika ya umma yalikuwa yakiwekeza pesa zao za ziada kwenye "fixed deposits" hivyo mabenki ya biashara yalikuwa yanapata faida kwa kupata pesa za kukopesha wateja wake toka kwa haya mashirika ya umma. Uamuzi wa serikali utaathiri haya mabenki kwa kiasi kikubwa tofauti na maelezo ya Dr Kimei
Mimi mwenyewe sielewi hapa moja jumlisha moja ngapi...
Yani benki biashara ishuke afu wapunguze riba tena kuwa attract high risk borrowers ...watu wa pato la chini...
Kama sielewi...anyways labda kwa kuwa sijui accounting...mimi naona kama wakiparamia soko la chini kwa riba ndogondio watafunga virago
 
Ndo hapo patamu sasa kwa sababu BoT ni regulatory tu yaani ni Benki ya Usimamizi siyo benki ya kibiashara kabisa.Kwa hiyo kukusanya fedha hizi na kuziacha zikae tu ni kuondoa huo mzunguko wa pesa kwenye soko na kuzi dampu.Nadharia nyingine ni kuwa BoT itanunua Bonds (hati fungano) za kimataifa (kama ilivyokuwa kwenye skendo ya Stanbic) na hivyo kusababisha hitaji kubwa la dola sababu itatumia Tsh hizi kununulia dola hizo ili ikawekeze huko.
Mi nashauri BoT iakopeshe tu (kwa jinsi yoyote) hasa watumishi ...
Maana kumkopa mtumishi una uhakika wa malipo...tungeondokana na mikopo kandamizi ya mabenki at the same time serikali inge make profit ambayo haya mabenki yamekuwa yakiinyonya...
Mbona benki zakopesha wafanya kazi wake kwa riba ndogo????serikali ifanye the same badala ya kurundika tu pesa zisizozaa...
 
Yaani kwa lugha rahisi ni kwamba Serikali ilikuwa na akaunti mbalimbali kupitia mashirika yake Katika benki hzi za biashara mf.Crdb,NBC na NMB.Sasa kila ambapo serikali ilikuwa inapungukiwa hela kwenye mipango yake ilikuwa inakopa kutoka kwenye haya mabenki kupitia hati za dhamana na fungano(Treasury Bills & Bonds) na kulipa pamoja na riba.Tupo hapo??Sasa nini kulikuwa kinatokea??...Mf.Uweke kwangu elfu 10,halafu baada ya siku 3 uje unikope Elfu 8 sasa mimi ninachofanya ni nakukopesha na riba..mf 10%,ili unilipe 8800.Lakini ulichokopa ni kiasi ambacho nimekuwekea,ki mantiki ni umekopa hela yako tena na riba.Serikali ilikuwa inakopa hela yake yenyewe na kisha kuzilipa hizi benki na riba.Hiki ndicho JPM anachopigana nacho.Benki hizi zina kama Bil550/- sasa zikienda BoT shida za serikali nyingi zitazungushwa na hizi hela kuliko kukopa kwenye mabenki hela zake yenyewe.Kikubwa kutokana na kukosa fedha hizi Mabenki haya yatarudi kutafuta wateja mitaani pamoja na kushusha viwango vya riba ili wananchi wakope na wao wapate faida.
Natumai picha mmepata wakuu.
 
Hii

hiyo argument niliyobold ni haina mashiko. kwenye uchumi, kubana matumizi ni policy yenye dhumuni la kurekbisha mzunguko wa fedha na mwenendo wa uchumi kwa ujumla, kama kuna sababu nzuri ya kufanya hivyo.
Anyway, kila policy (hata ya kutokubana matumizi) ina prons and cons. Always kuna gainers na loosers, hakuna policy ya kumnufaisha kila mtu. La muhimu ni what we gain (society yote kwa ujumla) kutokana na policy tunayoimplement. Swala la mtu/ kikundi cha watu kuloose hakisababishi tusi-implemnent policy especially kama ina faida kwa jamii yetu kwa ujumla wake.

Ulitakiwa tu kujazia nyama hiyo argument yako ya pili kuhusu ufinyu wa barabara. Barabara ziongezwe na public transport ziboreshwe, probably kwa kuwa na miradi ya mabasi yaendayo kasi. Mfano serikali ikiamua kuinvest kwenye ujenzi wa barabara/ reli tayari ni expansionary policy through increasing of government expenditure. So wakati ina-contract kwa kuwabana commercial banks inapoondoa accounts zake huko, at the same time inaweza kuwa ina-expand kwa kuinvest kwenye constructions kama hizo za barabara na sehemu nyingine.

Kuongezeka kwa magari binafsi hakutatui taizo la jam. Ushawahi kujiuliza kwa nini majiji kama london ukiingia na gari city centre unapigwa fine kubwa. Ili kupunguza foreni na kuencourage watu watumie public transport
Asante kwa kumpa somo huyo jamaa
 
Mi nashauri BoT iakopeshe tu (kwa jinsi yoyote) hasa watumishi ...
Maana kumkopa mtumishi una uhakika wa malipo...tungeondokana na mikopo kandamizi ya mabenki at the same time serikali inge make profit ambayo haya mabenki yamekuwa yakiinyonya...
Mbona benki zakopesha wafanya kazi wake kwa riba ndogo????serikali ifanye the same badala ya kurundika tu pesa zisizozaa...
Yess..Nayo pointi hiyo kwa kuwa taarifa isiyo rasmi ni kuwa BoT itaingilia kati na kukopesha mabenki kwa riba ndogo ya iliyopo sokoni ili kuzinusuru pale zinapokuwa na tatizo la fedha yaani Short liquidity. So tunategemea kwamba kwa sababu BoT itashusha riba basi na Benki hizi zitashusha riba zake ili kukopesha watu wengi zaidi.
 
Back
Top Bottom