Dr Harrison Mwakyembe atua Tabora kwa gari moshi leo

Tuzo yake ni hiyo kukabidhiwa wizara dogo hilo?

Kumbe kukabidhiwa WIZARA NI TUZO!!!! Ndio maana eti........ eeh!! Watu wanafaidika kutokana na "tuzo", sio wanawajibika.
Hapa ndipo hoja zinazosemwa siku nyingi kuwa "jk anatoa vyeo kama tuzo/zawadi kwa anaowapa" ZIMETHIBITISHWA na RIZ. ​That's why I like magamba's portofolio.
Sasa inabidi zipunguzwe hizo wizara ili "tuzo zipungue" kwakuwa zinafilisi nchi.
 
MZALENDO WA UKWELI, WAKO NA WENGINE LAKINI NADHANI UOGA WAO NDIO UNAOWAFANYA WASHINDWE KUKUNJUA MAKUCHA YAO...Kikubwa hapa ni namna gani tutaweza kuifanya nchi yetu kupiga hatua katika uchumi haswa ktk huu ushindani wa soko huria la A.Mashariki, kiukweli kama tukiweza kuitumia reli kama kitega uchumi kwa kusafirisha bidhaa toka pwani mpk nchi kavu haswa hizi nchi za Rwanda, Burundi, Uganda, DRC na Zambia hakika RELI ni kitega uchumi kizuri hakuna mfano wake. Mwakyembe hongera umejaribu lakini kaza buti kwani wako walionyumba yako nao wanapita mlemle unamopita wewe ili kuharibu lakini kweli itabakia kuwa kweli maisha. Shime kwa wale wote wenye dhamana serikalini kutumia nafasi zao ktk kuifanya Tz kuwa mfano wa kuigwa kwa kufufua zilivyokufa, WAZIRI WA VIWANDA inawezekana General Tyre kurudi mahala pake, Inawezekana UFI, MWATEX, KILITEX, MBEYATEX n.k kufufuliwa.
Leo wanapiga kelele suala la vijana na ajira kuwa ni bomu linalosubiri kulipuka ni kweli na hili litatuletea shida mbeleni kwani ajira zitakuwa kwa watu special yaani kama huna mjomba au refa itakuwa ngumu kupata ajira na hili litaletelezea chuki miongoni mwetu. Mfano. Mtoto wako wewe Mtz mwenye maisha ya kawaida amefanikiwa kusoma hizi shule zetu za kawaida au umejitahidi umempeleka kwenye hizi za grade ya kati na akafika Chuo Kikuu, kule wakakutana na mtoto wa Kigogo flani serikalini na wakawa intake moja na bahati nzuri wakamaliza wote, huyu wa kigogo flani hakai hata kusubiria matokeo yeye ajira nje nje tena hiyo nafasi anayopewa haijawai kutangazwa kama iko wazi, lakini kwa Mtz wa kawaida hata kama umechangamkia matangazo ya ajira kwa kuomba ajira atajikuta anasota hakuna mfano, hapa nini nataka kusema, kutakuwa na chuki kati ya walionacho na wasionacho na ndipo tulipo sasa watz na gepu hili linazidi kupaa, madhara yake hakika Mungu ndiye ajuae...Tuangalie na vyema wale wenye nia ya kurudisha nyuma harakati zinazofanywe na wale waliojitoa mhanga juu ya taifa hili katika kukuza uchumi vyema tukaanza kuwaweka wao pembeni ili tuwe salama huko tuendako.


Tz nakupenda kwa moyo wangu wote.
Mtazamo tu.
 
Dr hawazii kufa kwa afya yake bali anawaza kufa kwa taifa lake.

Hawezi kukosa mapungufu lakini Tungekuwa na akina mwakyembe japo 7 tu jamii yetu ingeanza kunyooka kwa awamu polepole.
 
Mwakyembe ataendelea kuwa Waziri hata baada ya Magamba kuondoka 2015.Tena anafaa kuwa waziri MKUU.

Umenena mkuu,

jamaa anafaa sana kuwa Waziri Mkuu kusimamia maagizo ya rais, sera za chama chake na utendaji wa Mawaziri.
 
Nilimsikia majuzi kwenye TV akiwa mwanza alipowasha moto kwa tanroad na halimashauri akawapa siku mbili kumpisha mkandarasi anayepanua uwanja wa ndege mwanza.

Alisema wanacheza na fedha zetu endapo mkandarasi ataamua kuomba fidia kwa kucheleweshwa na vikao vya tanroad na Halmashauri visivyotoa maamuzi.

Akasema wasipofanya hivyo ataagiza mkandarasi kutengeneza njia ya muda karibu na uwanja huo na kubomoa njia ya lami ya magari ili ujenzi uanze kwani fedha ipo tayari.
 
Dr Mwakyembe amepanda daladala mbovu dar es salaam kufuatilia ukweli na sasa treni mbovu kujua kulikoni. Kuongoza kwa matendo ni silaha muhimu sana katika uongozi na uwajibikaji wa kweli.
 
Safi sana Dr wa ukweli piga kazi.

Safi sana Dr.Harrison Mwakihembe kwa kufanya kazi kwa juhudi,kwani viongozi wa CCM wangekuwa wachapakazi kama wewe na kuweka ufisadi pembeni tusingekua na haja ya kuichukia CCM!!

Mhe Mwakyembe ni jembe kweli kweli ila yuko mahali pabaya, naomba tafadhari huyu mtu aongezewe ulinzi aweze kufanya kazi bila wasi wasi!!!


Tumpongezenni kwa pamoja , huu si upepo naamini ana nia nzuri

Samaki Fresh ukimuweka katika Tenga lenye Samaki waliooza, ujue wote wataoza tu.

Mwakyembe yupo katika Tenga bovu wenzie wote wameoza hivyo naye tunamuona ni walewale tu!!!!!!!!

Hata ukimuosha vipi samaki anayegusana na waliyeoza atanuka uvundo du.



MIZAMBWA
NABII MTARAJWA!!!
 
Samaki Fresh ukimuweka katika Tenga lenye Samaki waliooza, ujue wote wataoza tu.

Mwakyembe yupo katika Tenga bovu wenzie wote wameoza hivyo naye tunamuona ni walewale tu!!!!!!!!

Hata ukimuosha vipi samaki anayegusana na waliyeoza atanuka uvundo du.



MIZAMBWA
NABII MTARAJWA!!!

kama dk. mwakyembe angekuwa na upuuzi puuzi na ufisadi fisadi tungeshajua siku nyingi. jamaa ni clean. na kikubwa zaid ni kutanguliza maslah ya nchi mbele.
 
hongera Mwakyembe sio kukaa tua ofisini na kuletewa taarifa za uongo.
 
Back
Top Bottom