DPP amwondolea hati ya kuzuia dhamana bosi wa zamani wa Rahco na wenzake wawili

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP), Sylvester Mwakitalu amemuondolea hati ya kuzuia dhamana aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa kampuni hodhi ya rasilimali za reli Tanzania (Rahco), Benhardard Tito.

Mbali na Tito, hati hiyo pia imeondolewa kwa wenzake wawili ambao ni mwanasheria wa zamani wa kampuni hiyo, Emmanuel Massawe na mwakilishi wa kampuni ya Rothschild (South Africa) Proprietary Limited, Kanji Mwinyijuma.

Watatu hao walikuwa wanakabiliwa na mashtaka nane likiwemo la kuisababishia Serikali hasara ya dola 527, 540 za Marekani sawa na Sh1.2 bilioni.

Dhamana ya washtakiwa hao ilizuiwa na DPP wa zamani, Biswalo Mganga kwa kuwasilisha hati ya kuzuia dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mwaka 2016.

Chanzo: Mwananchi
 
Mwananchi wanatuchanganyia habari
1623847026150.png
 
Watatu hao walikuwa wanakabiliwa na mashtaka nane likiwemo la kuisababishia Serikali hasara ya dola 527, 540 za Marekani sawa na Sh1.2 bilioni.

Chanzo: Mwananchi
Walikuwa ? Hawakabiliwi tena ? Au wanapata dhamana na tunaendelea kuchunguza mbivu na mbichi ?
 
afadhali sana wapate dhamana
iwe hivo pia kwa wengine na hatau zaidi zichukuliwe makosa yote yawe na dhamana
 
Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP), Sylvester Mwakitalu amemuondolea hati ya kuzuia dhamana aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa kampuni hodhi ya rasilimali za reli Tanzania (Rahco), Benhardard Tito.

Mbali na Tito, hati hiyo pia imeondolewa kwa wenzake wawili ambao ni mwanasheria wa zamani wa kampuni hiyo, Emmanuel Massawe na mwakilishi wa kampuni ya Rothschild (South Africa) Proprietary Limited, Kanji Mwinyijuma.

Watatu hao walikuwa wanakabiliwa na mashtaka nane likiwemo la kuisababishia Serikali hasara ya dola 527, 540 za Marekani sawa na Sh1.2 bilioni.

Dhamana ya washtakiwa hao ilizuiwa na DPP wa zamani, Biswalo Mganga kwa kuwasilisha hati ya kuzuia dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mwaka 2016.

Chanzo: Mwananchi
mi naonaga hakunaga dpp independent kila anaeingia hakutakua na mzuri anayejitegemea, kila maamuzi ya dpp yana favor kada flani hivi na kutofurahisha nyingine, reason being ni kua kila dpp anafuata maelekezo ya boss wake na do & dont's hakuna cha ziada. asanteni
 
either kesi ziende haraka ijulikana watu wana hatia wafungwe au hawana hatia waachiwe, kuliko kumuweka mtu mahabusu 10yrs nenda rudi kila siku mahakamani halafu at the end unamsikia mtu anasema haoni haja ya kuendelea na kesi, Pumbavu kabisa...
 
Kama huna ushahidi, kwanini umkamate mtu? halafu utuambie ushahidi haujakamilika?.. issue hapa ni kuimalisha vyombo vya uchunguzi viendeshe kazi kisasa na viwe na uwezo wa kuchunguza kitalaam bila uonevu then vikishakamilisha uchunguzi ndio vinamkamata mtu...
 
Hii ndiyo raha ya kuachia mihimili ifanye kazi wa weledi siyo kwa kufuata magufuli anatakaje
Kweli mkuu, bora wazito waachiwe kama hivi. Haina tija kuwashikilia wazito wakati wanaopaswa kuwepo mahabusu/gerezani ni akina sie kajamba nani!
 
Back
Top Bottom