DOWANS yatikisa UDSM; Wanafunzi kuandamana leo...

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Na Tumaini Makene

SAKATA la kashfa ya kampuni tata ya Dowans ambayo inatakiwa kulipwa sh. bilioni 94 jana lilitikisa katika mdahalo wa wasomi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ambako lilielezwa kuwa ni 'sehemu ndogo ya familia kubwa ya ufisadi' unaoendelea nchini ambayo kama haitachukuliwa hatua stahili, itahatarisha amani na utulivu nchini.

Ilielezwa kuwa kashfa hiyo ni dalili ya tatizo kubwa katika sekta mbalimbali ikihusisha mikataba ya kilaghai, huku ikiathiri maendeleo ya nchi kisiasa na kiuchumi, kiasi ambacho viongozi wameshindwa kutumikia umma wa Watanzania, badala yake wanatumikia maslahi binafsi.

Kashfa zingine zilizotajwa kukuhusishwa katika hicho kinachoitwa 'familia ya ufisadi' zilikuwa ni pamoja na ununuzi wa rada, mikataba ya IPTL, ubinafsishaji wa mali za umma, matatizo ya ardhi ambapo wawekezaji wamekuwa na sauti kubwa kuliko wananchi wa maeneo husika, ukitajawa mgogoro wa wakulima na wawekezaji huko Babati.

Hayo yalisemwa jana katika mdahalo juu ya sakata la Dowans, ulioitishwa na Chama cha Wanataaluma UDSM (UDASA), ambapo pia ilitolewa njia mbadala ya kutatua matatizo kama ya Dowans kwa kutaifisha mali za wahusika.

Akiwasilisha maada yake juu ya sakata la Dowans katika mlengo wa Sayansi ya Siasa, Bw. Bashiru Ally ambaye pia ni mhadhiri wa idara hiyo UDSM, alisema kuwa kashfa hiyo ni sehemu ya familia kubwa ya ufisadi inayoendelea kuitafuna nchi katika nyanja ya uchumi na siasa, kiasi cha kupandisha hasira za makundi mbalimbali ya watu katika jamii.

Kwa upande wake, Dkt. Adolf Mkenda aliwasilisha mada yake kwa mlengo wa uchumi, alisema kuwa soko huria haliwezi kuwa sababu ya kulaumiwa pale kashfa kama hizo zinazonuka makosa ya jinai kama rushwa, zinapotokea, bali hiyo ni dalili ya watumishi wa umma wakishirikiana na wale wa sekta binafsi kujinufaisha wao.

Akiwasilisha mada yake kwa mlengo wa kisheria, kwa kutoa historia ya Dowans, kuanzia Richmond, mpaka hukumu ya kesi ya ICC, Bw. Jesse James kutoka Shule Kuu ya Sheria Chuo Kikuu Dar es Salaam, alisema kuwa mkataba ulioifikisha nchi katika sakata la Dowans hauna tofauti na ile iliyokuwa ikisainiwa na machifu wajinga, wakati wa enzi za kuingia ukoloni (Chifu Mangungo wa Msovero).

Kwa upande wake, mwanasheria na mwanaharakati Bw. Tundu Lissu alisema kuwa wanasheria waliowakilisha upande wa serikali wakati wa uendeshaji kesi, hawakuzungumza dalili za uwepo wa rushwa katika sakata zima la Dowans, kuanzia katika Kampuni ya Richimond, suala ambalo lingeweza kusababisha ICC isisikilize kesi hiyo, kwa mujibu wa mikataba ya kimataifa.

Wakati huo huo Majira limepata habari ya kuwepo kwa maandalizi ya maandamano ya amani ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam ambapo moja ya hoja zitakuwa ni kudai ongezeko la fedha za kujikimu kutoka sh. 5,000 ya sasa mpaka sh. 10,000.

Habari kutoka vyanzo mbalimbali zilisema kuwa hoja nyingine ambayo imewasukuma kuandaa maandamano hayo ni kupinga tamko la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) la kutaka kuvunjwa kwa Uongozi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kwa madai kuwa umeshindwa kuwahudumia wanafunzi inavyotakiwa.

Alisema kuwa tatizo la mikopo na migomo ya wanafunzi vyuo vikuu ni mfumo wa uanzishwaji wa bodi yenyewe unaotokana na serikali kushindwa kusimamia na kuiwezesha vya kutosha pamoja na uzembe wa uongozi wa baadhi ya vyuo na Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), hasa katika kuwasilisha taarifa za wanafunzi mapema.
 
Panapofuka moshi panaficha moto...............................It is a question of time before this government resigns.........................
 
Wanachuo wana haki ya kuandamana na kudai ongezeko la pesa ya kujikimu kutokana na kupanda kwa garama za maisha zinazoongezeka kila siku. Kiasi cha sh. 5000 kwa siku kilianza kulipwa mwaka 2007 na leo miaka 4 imepita. Ukijaribu kuangalia ongezeko la bei ya bidhaa mbalimbali utagundua kwamba ile sh. 5000 ya wakati ule haitoshi tena. Lakini sababu nyingine ya kudai ongezeko hilo ni uwepo wa pesa za kutosha serikalini (rejea pesa zilizoandaliwa kuilipa kampuni ya dowans). Mada ya kupinga tamko la UVCCM pia ina uzito wa kipekee kwa sababu uvccm wanataka kutumia bodi ya mikopo kwa manufaa ya CCM ya kisiasa na si vinginevyo.
 
:sick::sick::sick::sick:UVCCM ni wahuni tu, hawana lolote zaidi ya kutafuta kuungwa mkono na wanafunzi wa vyuo vikuu! UVCCM imegundua kuwa imepoteza wanachama wengi vyuoni na hawana mvuto kabisa kwa wanafunzi, hivyo wanatafuta njia ya kuwarubuni wanafunzi wawarudie tena! Kwa wasomi wa sasa, UVCCM imechemsha, itafute wanachama wapya huko vijijini na sio kwa wanafunzi wa vyuo vikuu!!!!!!!!!!!!:sick::sick::sick::sick::sick:
 
Hakika UVCCM wamepotea njia ,njia sahihi kwao ni kumrudia MUNGU ili awainue kwa wakati wake na waache kuwa Vibaraka.Tanzania ya leo siyo ya miaka 5 iliopita ,ni ya tofauti kinadharia na kivitendo pia.Sauti ya Umma ndo mhimili mkuu katika kuwatetea wanyonge ambao ndo wengi katika Taifa LETU.Peoplezzzzzzzzzzzzzzz powerrrrrrrrrrrrrr
 
Go udsm soldarity forever kwa kuwa nyinyi ni watu pekee ambao mnaweza amsha morali ya wananchi and because your intellectual mind is solution kwenye haya matatizo .
We need changes na changes zinaletwa na wasomi kwa kweli tumekuwa nyuma sana sisi kwenye hii jamii ya kitanzania yenye mambumbu wengi inabidi tuwaangazie ndugu zetu walio gizani
remember those days 2006/07 tulipokuwa tunagomea kwa fedha ya meals and acomodation kutoka 3500/= mpaka 5000/= it is remains kwa miaka minne yote niliyo kaa hapo mlimani regardless of mfumuko wa bei na serikali imekaa kimya it is time now tuamke maisha yamekuwa magumu .
Soldarity forever udsm is place where changes begin
 
kautaratibu kameanzia Tunisia, Egypt, Sudan kaanza taratibu. sijui katampitia mu7, harafu January 24 kanaingia Rocky city hadi bongo. Peoplesssssssssssssss Powerrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr.
 
kautaratibu kameanzia Tunisia, Egypt, Sudan kaanza taratibu. sijui katampitia mu7, harafu January 24 kanaingia Rocky city hadi bongo. Peoplesssssssssssssss Powerrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr.

kabaisa, njooni huku kwa mu7 aka raisi wa maisha afu tuzame home tuwakeshee mafisadi na broda wao wasepe...
huu wimbo wa mafisadi tushaujua na hapa mpaka kieleweke, hao SISIEM wanafanya remix tu ili tusahau:roll:
 
UVCCM mlango upo wazi, acheni kufungwa na wazee! kwa nini mjitese ivo? tunajua mlijiunga uko kwa lengo zuri, sasa hamen pi mkiwa bado safi la sivyo tutawatapika kam baba yenu! karibuni mjiunge na nguvu ya umma kumpiga vita mwonevu wetu. Jiskieni amani kuwa na vijana wenye busara na akili timamu wa CHADEMA, ivi kwa akili yenu kweli mnaona huyo baba yenu anatufaa hata sisi? yani nawaona km vile hamna amani wala furaha tena! sasa ya nini kujitesa kiasi hicho choteeeeeeeee!!! NJONI KWETU NINYO MLIOGUNDUA UOVU NA UDHAIFU WA BABA YENU NASI TUTAWAPOKEA!
 
Ni vita ya wanafunzi na polisi UDSM Send to a friend Friday, 04 February 2011 21:47 0diggsdigg

WALITAKA KWENDA IKULU KUMUONA JK, VURUGU ZASABABISHA MWANAFUNZI KUJIFUNGUA MTOTO MFU
Waandishi Wetu
POLISI mkoani Dar es Salaam jana walilazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi, maji ya kuwasha na risasi kuwakabili wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU) ambao walikuwa wakijibu mapigo kwa kuwarushia mawe polisi hao.

Wanafunzi hao walikuwa wakifanya maandamano kuelekea Ikulu, wakishinikiza nyongeza ya fedha ya posho wanayopewa na Serikali kutoka Sh5,000 hadi Sh10,000 kwa siku.

Mapambano hayo yaliyodumu kwa zaidi ya saa moja, maandalizi yake yalianza kusukwa kuanzia saa moja asubuhi jana kwenye Hosteli za Mabibo na ilipofika saa mbili asubuhi, wanafunzi walikuwa wamefika UDSM sehemu ya Mlimani.

Wakiwa katika safari ya kuelekea Ikulu, walipita Chuo Kikuu cha Ardhi kuwashawishi wanafunzi wajiunge nao ili kujenga nguvu zaidi wakisema wanataka wakamuone Rais Jakaya Kikwete, kwani ndiye mwenye uwezo wa kuamuru waongezewe posho yao ya kila siku ili ilingane na hali halisi ya maisha ya sasa.

Wakati harakati hizo zikiendelea, polisi walikuwa wamepata taarifa na wakawa wamejipanga eneo la Savei, tayari kuyasambaratisha maandamano hayo.

Katika maandamano hayo, wanafunzi walikuwa wamebeba mabango kadhaa yakiwa na ujumbe tofauti unaoshutumu Serikali kwa mambo mbalimbali, huku pia wakiimba nyimbo zinazosisitiza wapatiwe fedha zinazotolewa kwa kampuni ya Dowans ili wakabiliane na maisha magumu kutokana na fedha kidogo wanazopewa za kujikimu.

Nyimbo nyingine zilikuwa zikiwashutumu viongozi serikalini ambao wanajihusisha na ubadhilifu wa fedha huku wakiwa wamesomeshwa bure katika enzi za Serikali ya Awamu ya Kwanza.

Wakalinganisha mazingira hayo ya elimu ya bure kwa vigogo hao kwenye awamu hiyo ya kwanza na mateso ya mazingira magumu wanayoyapata sasa huku wao wakiendelea kujilimbikizia mali na kuwabana kiasi kwamba wanashindwa kusoma.

"Kama siyo juhudi zako Nyerere mafisadi wangesoma wapi?" waliimba moja ya kibwagizo kwenye nyimbo zao, wakati wa maandamano.

Wakati wakiendelea na maandamano hayo, walikuwa wanazuia magari ya Serikali, yenye namba za STK kupita barabarani kwa kuwaamuru madereva kubadili njia.

"Hawa ndio mafisadi wenyewe. Kama hutaki kugeuza gari tutakushughulikia. Mnanunua magari ya kifisadi sisi tunakufa njaa, ipo siku tutagawana fedha yetu hiyo," mmoja wa wanafunzi hao alimueleza dereva wa gari la serikali huku akiungwa mkono na wenzake ambao walizomea na kutukana.

Mapambano na Polisi

Maandamano yalipofika eneo la Savei yalikutana na kundi la polisi likiwa limetanda pamoja na magari madogo nane na magari ya maji ya kuwasha yalikuwa mawili.

Askari hao walikuwa wakikagua mabasi yote ya daladala yaliyokuwa yanatoka Barabara ya Savei kuingia Sam Njoma kwa kuwashusha chini vijana wote waliowahisi ni wanafunzi wa UDSM.

Hatimaye msururu mkubwa wa maandamano ya wanafunzi hao ilikumbana na askari hao na wakawa wanaamriwa kurudi na kutawanyika, lakini yao waliwatia moyo wenzao, wakisema "twendeni, hawawezi kutufanya kitu."

Polisi walipoona wanafunzi wanawajia kwa kasi bila woga wala kujali amri yao wala vifaa kama vile bunduki, mabomu ya machozi na maji ya kuwasha, waliamua kurudi nyuma kuwakimbia.

Kuona hivyo, wanafunzi hao walionekana kuwa na nguvu zaidi kwa kusonga mbele, huku wengine wakizomea ndipo askari mmoja aliporushia bomu la kutoa machozi.

Baadhi ya wanafunzi walisita kuendelea, lakini walipovurumishiwa mengine, walikimbia huku wawili wakianguka papo hapo na kukamatwa na kuwekwa kwenye gari la polisi.

Mabomu hayo yaliwafanya wanafunzi kukimbia kurudi walikotoka na wengine kutawanyika kuelekea kwenye baadhi ya nyumba na vichaka katika eneo hilo.

Kukimbia huko kuliwafanya wanafunzi hao kujipanga upya japokuwa si kwa wingi kama ilivyokuwa awali ambapo baadhi waliamua kufunga njia kwa kupanga mawe makubwa barabarani mbele ya Chuo cha Ardhi.

Katika eneo hilo, waliweka ngome yao wakisema liwe liwalo hawatakubali askari yoyote avuke, huku wakijikusanya katika kundi kubwa zaidi na kuimba nyimbo za kushutumu Serikali na wakati huo huo askari walikuwa wakisogea polepole kuwafuata.

Askari hao wakiongozwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela wakiwa wanawasogelea, wanafunzi nao wakijiandaa kwa kubeba mawe ya kuwarushia kama njia ya kukabiliana nao.

Kuona hivyo, askari hao waliwavurumishia maji ya kuwasha na kupiga hewani risasi za moto ili kuwatawanya, lakini wao waliwajibu kwa kuwarushia mawe.

Baada ya kupambana kwa muda mrefu, gari moja la kumwaga maji ya kuwasha liliishiwa maji na wanafunzi hao wakatumia nafasi hayo kuongeza kasi ya kuwarumisha mawe polisi.

Baada ya muda mfupi, gari lingine la maji ya kuwasha liliwasili ili kuongeza nguvu, lakini wanafunzi walionekana kuwa na nguvu ya kukabiliana nao kiasi cha kuwafanya askari kurudi nyuma.

Hali hiyo iliwafanya polisi kuamua kuongeza vikosi vingine vya askari ambapo walikuja na kasi kubwa zaidi ya kurusha mabomu mengi ya kutoa machozi ambapo baadhi yalielekezwa kwenye Chuo Cha Ardhi na kuwafanya wanafunzi waliokuwepo kuanza kukimbia hovyo.

Hali hiyo iliwatawanya kabisa wanafunzi hao na kusalimu amri ya kufanya maandamano kuelekea Ikulu ambayo ipo karibu kilomita zaidi ya 10 kutoka eneo la Mwenge.

Kauli ya RPC Kenyela

Kamanda Kenyela alisema walivunja maandamano hayo kwa sababu waandamanaji hawakufuata taratibu zinazotakiwa, za kuwa na kibali.

Alielezea kuwa hali hiyo wasingeweza kuiruhusu kwa sababu ingeweza kuhatarisha amani katika makazi ya watu na mali zao.

Alisema Jeshi la Polisi lilipata taarifa za kiintelijensia kwamba wataandamana hadi Ikulu.

"Tulipata taarifa za kiintelijensia kwamba wataandamana hadi Ikulu jambo ambalo ni kinyume na taratibu za nchi pia hata amani isingekuwepo katika makazi ya watu kwa hiyo tutaimarisha ulinzi wa kutosha kuhakikisha hakuna mwanafunzi anayetoka maeneo ya chuo," alionya Kenyela.

Kenyela alisema kuwa wanafunzi hao wanatakiwa kuzungumza na uongozi wa chuo ili kupata namna ya kumaliza matatizo yao kuliko kufanya maandamano yasio na kibali.

Mwanafunzi ajifungua, mtoto afa
Wanafunzi watatu kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM), wamejeruhiwa vibaya na kulazwa hosptalini huku mmoja wao akijifungua mtoto mfu, kutokana na vurugu hizo.

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Yunus Mgaya aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa katika vurugu zilizotokea juzi, mwanafunzi mmoja aliyekuwa mjamzito, aliumia na hatimaye kujifungua mtoto ambaye hata hivyo alikuwa tayari amefariki.

Alisema baada ya tukio hilo, mwanafunzi huyo alipelekwa katika Kituo cha Afya kilichoko katika hosptalini chuoni hapo, kupatiwa matibabu na kwamba hadi jana alikuwa bado amelazwa.

"Katika vurugu za leo (jana) zilizohusisha wanafunzi hao na polisi, wanafunzi wawili wameumia, mmoja baada ya kukatwa na kitu chenye ncha kali na amekimbizwa katika Hosptali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi. Mwanafunzi mwingine, alianguka na kuumia sehemu ya usoni na kushonwa katika kituo chetu,"alisema Mgaya.

Alisema katika vurugu za jana, baadhi ya wanafunzi walikamatwa na polisi na kupelekwa kituoni kwa kosa la kufanya maandamano yasiyo rasimi na kusababisha vurugu huku taarifa za kipolisi zikionyesha kuwa wanafunzi waliokamatwa ni zaidi ya arobaini.

Akisimulia tukio hilo, Mgaya alisema maandamano ambayo jana yaliwalazimu polisi kutumia nguvu kuyatawanya, yalianza juzi mchana chuoni hapo.

Alisema kuwa, siku ya kwanza ya maandamano kikundi kidogo cha wanafunzi kilikutana eneo liitwalo ‘Revolution Square' na kuanza kuhamashisha wanafunzi wengine kuandamama kwa lengo la kuishinikiza Serikali kuongeza fedha za kujikimu kutoka Sh5000 hadi Sh10,000.

Alisema kikundi hicho baada ya kushindwa kuafikiana na wanafunzi wengine kiliondoka na kwenda ‘Cafeteria' namba moja na namba mbili na kufanya fujo kwa kupiga kelele na kuwapiga wenzao waliokuwa wakila chakula, kuvunja vyombo na kuchukua soda zilizokuwamo ndani na kunywa.

"Walipotoka hapo walikwenda kwenye madarasa ya ‘Arts' (sanaa), huko walifanya vurugu kwa kuwafukuza wenzao waliokuwa wakisoma pamoja na walimu, wakiwatisha kwa kutumia fimbo,"alisema Mgaya.
Alisema baada ya hapo wanafunzi hao walielekea kampas ya uhandisi kwa lengo la kushawishi wanafunzi wa huko wawaunge mkono katika jitahada zao.

Kwa mujibu wa Mgaya, baada ya ushawishi wao kutofanikiwa, wanafunzi hao walifanya vurugu baina yao na wanafunzi wa huko na kusababisha uharibifu wa mali katika eneo la kantini iliyokopo eneo hilo.

Alisema mara baada ya vurugu hizo, wanafunzi hao walifunga safari kuelekea Ubungo Plaza kwa lengo la kumuona Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na kumkabidhi madai yao.

Alisema kabla ya kufika Ubungo, wanafunzi hao walipata taarifa za waziri mkuu kutokuwapo Ubungo Plaza, ndipo walisimama na kuanza kushambulia magari yaliyotumika kubeba wanafunzi wa chuo hicho.

Akizungumza madai ya wanafunzi ambayo pia alikiri kuwa ni ya msingi.

Profesa Mgaya alisema tayari kuna taarifa za kuaminika kuwa upo mkakati wa kuangalia uwezekano wa kuongeza fedha hizo, ambao uko katika hatua za mwisho.

"Ni dhahiri kwamba tangu kiwango hicho kipandishwe mwaka 2007/2008, gharama halisi za maisha vyuoni zimepanda.

Hivyo basi kuna taarifa za kuaminika kwamba kupitia Bodi ya Mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya Juu, mchakato kubaini gharama halisi za maisha umeshakamilika na majadiliano yanaendelea kati ya bodi hiyo na wawakilishi wa Serikali za wanafunzi katika vyuo mbalimbali ili maamuzi stahiki yafanyike,"alisema Mgaya.

Mgaya alisema baada ya kufikiwa kwa makubaliano hayo, ongezeko hilo litaingizwa kwenye bajeti na kuanza kutolewa kwa wanafunzi wote vyuoni na kwamba hali hiyo itasaidia kupunguza matatizo ya wanafunzi.

"Kwa mantiki hiyo, hakuna sababu ya wanafunzi kusababisha vurugu na hali ya uvunjifu wa amani vyuoni, kwa kisingizio cha kudai mabadiliko ya viwango vya fedha za kujikimu,"alisema Mgaya.

Wanafunzi wakamatwa
POLISI jijini Dar es Salaam imewakamata wanafunzi 42 wa UDSM na ARU kwa tuhuma za kufanya maandamano kuelekea Ikulu bila kibali.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam, Suleiman Kova aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa awali wanafunzi waliokamatwa walikuwa 60, lakini baadaye walichujwa na kubakia 42.

"Mchujo bado unaendelea ili kuwabaini waliohusika kuyaandaa maandamano hayo waliyosema kuwa yana lengo la kushinikiza kuongezwa fedha za kujikimu.

Kova alisema wanafunzi hao walikamatwa baada ya kutoka nje ya maeneo ya vyuo vyao na kujiandaa kuanza maandamano hayo ya kuelekea Ikulu.

Alisema walikamatwa kutokana na maandamano hayo kutokuwa halali kwa kuwa hayakuwa na baraka za polisi, chuo wala uongozi wa serikali ya wanafunzi.

"Kuna baadhi ya wanafunzi wamekula njama, ndiyo walioshinikiza maandamao hayo. Hii inatokana na baadhi yao kuonekana wakiwalazimisha wanafunzi wengine kuandamana bila hata ridhaa yao,'' alisema Kova.

Lakini Kamanda Kova alieleza kuwa polisi imefanikiwa kuzuia maandamano hayo kabla hayajafika katikati ya jiji ambako yangeweza kuleta uvunjifu wa amani na kusababisha msongamano mkubwa wa magari.

Awali habari zilizolifikia gazeti hili zimeeleza kuwa maandamano hayo yalianza asubuhi baada ya wanafunzi wanaoishi Hosteli ya Mabibo kuandamana na kwenda kuungana na wenzao wanaoishi katika mabweni ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam kisha kuwafuata wengine wa chuo cha Ardhi.

Kwa mujibu wa habari hizo, polisi pia lilikamata mabango manane yaliyokuwa yamebebwa na waandamaji hao yenye maneno mbalimbali ya kushinikiza madai yao hayo.

"Pia tumekamata rundo la mawe makubwa na madogo ambayo yalikuwa na lengo la kuwapiga askari na makubwa yalilenga kuzuia magari barabarani," alisema Kamanda Kova.

Habari hii imeandaliwa na Gedius Rwiza, Geofrey Nyang'ro na Festo Polea

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites

Comments

0 #6 KANIALE 2011-02-05 06:28 Matatizo ya wanafunzi ni kioo cha jinsi nchi yetu ilipofikia baada ya wale tuliowapa dhamana ya kutuongoza kusahau wajibu wao kwetu na kugeuka kuwa wala nchi. Ni wanafunzi wa Chuo Kikuu, Ni Dowans,Ni EPA, Ni vichanga mwanayamala, Ni uoza wa shule za sekondari za Kata, Ni matatizo ya umeme nchi nzima, ni matatizo ya maji nchi nzima,ni kupanda kwa gharama za maisha kila kukicha.Ni dhihaka ya viongozi kwa kutoa majibu ya kejeli na mengi mengineyo.

Watanzania amkeni tumieni kura zenu vizuri. Ghiliba na uongo vimefikia kikomo. Na leo hii si jana. DUMISHA AMANI lakini tumia uwezo na haki yako kuleta mabadiliko. INAWEZEKANA. Hakuna Chama wala kikundi chenye hati miliki ya kuongoza taifa hili.
MUNGU IBARIKI TANZANIA. MUNGU WAFUMBUE MACHO WATANZANIA.

Quote

-2 #5 gombera 2011-02-05 04:45 Imefika wakati serikali ijipange kujua inatoka wapi na inkwenda wapi vinginevyo amani itapotea Tanzania kumbuka zamani chuo kilikuwa kimoja hivyo ilikuwa rahisi kukidhibiti sasa hivi vipo vingi chonde serikali.
Quote

-2 #4 john 2011-02-05 04:43 nashangaa sana wazili wa ulinzi yupo kimya kukemea tabia mbaya ya kutumia nguvu na silaha za moto kwa wanafunzi wasio na hata njiti ya jiberiti kuwarushia, hawa polisi wenyewe wengi wao ni wale waliofeli mtihani wa kidato cha nne hawajui maisha ya chuo yalivyo wanaboa sana kuzuia maandamano...
Quote

-1 #3 MPARE WA UPARE 2011-02-05 02:56 Haileti maana kwa wanafunzi na watu wengine wa mtaani, eti pesa za kuwalipa wanafunzi hazipo mpaka majadiliano na ziingizwe kwenye bajeti wakati za kuwalipa matapeli kama DOWANS zipo tayari wakati hata kwenye bajeti hazipo.
Mwanafunzi na msomi wa Chuo Kikuu hawezi kuelewa ukimwambia eti serikali haina pesa wakati huo una uharaka sana kulipa kundi la matapeli wachache wa Dowans.
Sijui hii serikali yatupeleka wapi, hivi wanafikiri watu ni [NENO BAYA] bado? Hatutaki yaliyotokea Tunisia na yanayoendelea Misri na nchi zingine za Kiarabu yafike kwetu.Lakini kama hamtatenda haki na kuendelea kufisadisha wachache kwa kunyonya wengi msishangae yakitokea hapa kwetu.
MUNGU IBARIKI TANZANIA

Quote

-1 #2 Mkalimoto 2011-02-05 01:36 ACHENI WAANDAMANE KWA NINI MNAWAZUI NYIE POLISI. IPO SIKU NANYI MTAANDAMANA MAANA HUYU BWANA WENU MNAEMTETEA NA KUMLINDA HAMNAZO
Quote

-1 #1 Mzalendo 2011-02-05 01:09 Tunakoelekea ni kubaya sana,serikali ijaribu kuondoa matatizo haya.Kama watu wanadai haki wanapewa,Je kwa nini wasipewe kabla ya kufanya hivyo.Imekuwa ni rahisi kulipa matapeli wa dowans na kuwaacha wanafunzi wa Tanzania na wananchi kwa ujumla tena agizo linatolewa na wazito,hawajali elimu ndio maana wanataka elimu ya sasa iishie elimu ya kata kwa kugawa 4 na 0 ili [NENO BAYA] wawe wengi.Inaonekana watanzania wamechoka nchi yao ambayo wanapotaka haki yao wanapigwa kama mbwa.Serikali na chama tawala wajue kinachotokea Misri kimetokana na watu kuchoka.Tanzania ina ela lakini zinakuwa za wachache wanaofanya nchi kama shamba la bibi.Sasa hakuna kisicho na mwisho wajue hivyo kwamba siku ipo maana hata Mungu ameona watanzania wakiteseka na kuteswa.
Quote

Ni vita ya wanafunzi na polisi UDSM Send to a friend Friday, 04 February 2011 21:47 0diggsdigg

WALITAKA KWENDA IKULU KUMUONA JK, VURUGU ZASABABISHA MWANAFUNZI KUJIFUNGUA MTOTO MFU
Waandishi Wetu
POLISI mkoani Dar es Salaam jana walilazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi, maji ya kuwasha na risasi kuwakabili wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU) ambao walikuwa wakijibu mapigo kwa kuwarushia mawe polisi hao.

Wanafunzi hao walikuwa wakifanya maandamano kuelekea Ikulu, wakishinikiza nyongeza ya fedha ya posho wanayopewa na Serikali kutoka Sh5,000 hadi Sh10,000 kwa siku.

Mapambano hayo yaliyodumu kwa zaidi ya saa moja, maandalizi yake yalianza kusukwa kuanzia saa moja asubuhi jana kwenye Hosteli za Mabibo na ilipofika saa mbili asubuhi, wanafunzi walikuwa wamefika UDSM sehemu ya Mlimani.

Wakiwa katika safari ya kuelekea Ikulu, walipita Chuo Kikuu cha Ardhi kuwashawishi wanafunzi wajiunge nao ili kujenga nguvu zaidi wakisema wanataka wakamuone Rais Jakaya Kikwete, kwani ndiye mwenye uwezo wa kuamuru waongezewe posho yao ya kila siku ili ilingane na hali halisi ya maisha ya sasa.

Wakati harakati hizo zikiendelea, polisi walikuwa wamepata taarifa na wakawa wamejipanga eneo la Savei, tayari kuyasambaratisha maandamano hayo.

Katika maandamano hayo, wanafunzi walikuwa wamebeba mabango kadhaa yakiwa na ujumbe tofauti unaoshutumu Serikali kwa mambo mbalimbali, huku pia wakiimba nyimbo zinazosisitiza wapatiwe fedha zinazotolewa kwa kampuni ya Dowans ili wakabiliane na maisha magumu kutokana na fedha kidogo wanazopewa za kujikimu.

Nyimbo nyingine zilikuwa zikiwashutumu viongozi serikalini ambao wanajihusisha na ubadhilifu wa fedha huku wakiwa wamesomeshwa bure katika enzi za Serikali ya Awamu ya Kwanza.

Wakalinganisha mazingira hayo ya elimu ya bure kwa vigogo hao kwenye awamu hiyo ya kwanza na mateso ya mazingira magumu wanayoyapata sasa huku wao wakiendelea kujilimbikizia mali na kuwabana kiasi kwamba wanashindwa kusoma.

"Kama siyo juhudi zako Nyerere mafisadi wangesoma wapi?" waliimba moja ya kibwagizo kwenye nyimbo zao, wakati wa maandamano.

Wakati wakiendelea na maandamano hayo, walikuwa wanazuia magari ya Serikali, yenye namba za STK kupita barabarani kwa kuwaamuru madereva kubadili njia.

"Hawa ndio mafisadi wenyewe. Kama hutaki kugeuza gari tutakushughulikia. Mnanunua magari ya kifisadi sisi tunakufa njaa, ipo siku tutagawana fedha yetu hiyo," mmoja wa wanafunzi hao alimueleza dereva wa gari la serikali huku akiungwa mkono na wenzake ambao walizomea na kutukana.

Mapambano na Polisi

Maandamano yalipofika eneo la Savei yalikutana na kundi la polisi likiwa limetanda pamoja na magari madogo nane na magari ya maji ya kuwasha yalikuwa mawili.

Askari hao walikuwa wakikagua mabasi yote ya daladala yaliyokuwa yanatoka Barabara ya Savei kuingia Sam Njoma kwa kuwashusha chini vijana wote waliowahisi ni wanafunzi wa UDSM.

Hatimaye msururu mkubwa wa maandamano ya wanafunzi hao ilikumbana na askari hao na wakawa wanaamriwa kurudi na kutawanyika, lakini yao waliwatia moyo wenzao, wakisema "twendeni, hawawezi kutufanya kitu."

Polisi walipoona wanafunzi wanawajia kwa kasi bila woga wala kujali amri yao wala vifaa kama vile bunduki, mabomu ya machozi na maji ya kuwasha, waliamua kurudi nyuma kuwakimbia.

Kuona hivyo, wanafunzi hao walionekana kuwa na nguvu zaidi kwa kusonga mbele, huku wengine wakizomea ndipo askari mmoja aliporushia bomu la kutoa machozi.

Baadhi ya wanafunzi walisita kuendelea, lakini walipovurumishiwa mengine, walikimbia huku wawili wakianguka papo hapo na kukamatwa na kuwekwa kwenye gari la polisi.

Mabomu hayo yaliwafanya wanafunzi kukimbia kurudi walikotoka na wengine kutawanyika kuelekea kwenye baadhi ya nyumba na vichaka katika eneo hilo.

Kukimbia huko kuliwafanya wanafunzi hao kujipanga upya japokuwa si kwa wingi kama ilivyokuwa awali ambapo baadhi waliamua kufunga njia kwa kupanga mawe makubwa barabarani mbele ya Chuo cha Ardhi.

Katika eneo hilo, waliweka ngome yao wakisema liwe liwalo hawatakubali askari yoyote avuke, huku wakijikusanya katika kundi kubwa zaidi na kuimba nyimbo za kushutumu Serikali na wakati huo huo askari walikuwa wakisogea polepole kuwafuata.

Askari hao wakiongozwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela wakiwa wanawasogelea, wanafunzi nao wakijiandaa kwa kubeba mawe ya kuwarushia kama njia ya kukabiliana nao.

Kuona hivyo, askari hao waliwavurumishia maji ya kuwasha na kupiga hewani risasi za moto ili kuwatawanya, lakini wao waliwajibu kwa kuwarushia mawe.

Baada ya kupambana kwa muda mrefu, gari moja la kumwaga maji ya kuwasha liliishiwa maji na wanafunzi hao wakatumia nafasi hayo kuongeza kasi ya kuwarumisha mawe polisi.

Baada ya muda mfupi, gari lingine la maji ya kuwasha liliwasili ili kuongeza nguvu, lakini wanafunzi walionekana kuwa na nguvu ya kukabiliana nao kiasi cha kuwafanya askari kurudi nyuma.

Hali hiyo iliwafanya polisi kuamua kuongeza vikosi vingine vya askari ambapo walikuja na kasi kubwa zaidi ya kurusha mabomu mengi ya kutoa machozi ambapo baadhi yalielekezwa kwenye Chuo Cha Ardhi na kuwafanya wanafunzi waliokuwepo kuanza kukimbia hovyo.

Hali hiyo iliwatawanya kabisa wanafunzi hao na kusalimu amri ya kufanya maandamano kuelekea Ikulu ambayo ipo karibu kilomita zaidi ya 10 kutoka eneo la Mwenge.

Kauli ya RPC Kenyela

Kamanda Kenyela alisema walivunja maandamano hayo kwa sababu waandamanaji hawakufuata taratibu zinazotakiwa, za kuwa na kibali.

Alielezea kuwa hali hiyo wasingeweza kuiruhusu kwa sababu ingeweza kuhatarisha amani katika makazi ya watu na mali zao.

Alisema Jeshi la Polisi lilipata taarifa za kiintelijensia kwamba wataandamana hadi Ikulu.

"Tulipata taarifa za kiintelijensia kwamba wataandamana hadi Ikulu jambo ambalo ni kinyume na taratibu za nchi pia hata amani isingekuwepo katika makazi ya watu kwa hiyo tutaimarisha ulinzi wa kutosha kuhakikisha hakuna mwanafunzi anayetoka maeneo ya chuo," alionya Kenyela.

Kenyela alisema kuwa wanafunzi hao wanatakiwa kuzungumza na uongozi wa chuo ili kupata namna ya kumaliza matatizo yao kuliko kufanya maandamano yasio na kibali.

Mwanafunzi ajifungua, mtoto afa
Wanafunzi watatu kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM), wamejeruhiwa vibaya na kulazwa hosptalini huku mmoja wao akijifungua mtoto mfu, kutokana na vurugu hizo.

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Yunus Mgaya aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa katika vurugu zilizotokea juzi, mwanafunzi mmoja aliyekuwa mjamzito, aliumia na hatimaye kujifungua mtoto ambaye hata hivyo alikuwa tayari amefariki.

Alisema baada ya tukio hilo, mwanafunzi huyo alipelekwa katika Kituo cha Afya kilichoko katika hosptalini chuoni hapo, kupatiwa matibabu na kwamba hadi jana alikuwa bado amelazwa.

“Katika vurugu za leo (jana) zilizohusisha wanafunzi hao na polisi, wanafunzi wawili wameumia, mmoja baada ya kukatwa na kitu chenye ncha kali na amekimbizwa katika Hosptali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi. Mwanafunzi mwingine, alianguka na kuumia sehemu ya usoni na kushonwa katika kituo chetu,”alisema Mgaya.

Alisema katika vurugu za jana, baadhi ya wanafunzi walikamatwa na polisi na kupelekwa kituoni kwa kosa la kufanya maandamano yasiyo rasimi na kusababisha vurugu huku taarifa za kipolisi zikionyesha kuwa wanafunzi waliokamatwa ni zaidi ya arobaini.

Akisimulia tukio hilo, Mgaya alisema maandamano ambayo jana yaliwalazimu polisi kutumia nguvu kuyatawanya, yalianza juzi mchana chuoni hapo.

Alisema kuwa, siku ya kwanza ya maandamano kikundi kidogo cha wanafunzi kilikutana eneo liitwalo ‘Revolution Square’ na kuanza kuhamashisha wanafunzi wengine kuandamama kwa lengo la kuishinikiza Serikali kuongeza fedha za kujikimu kutoka Sh5000 hadi Sh10,000.

Alisema kikundi hicho baada ya kushindwa kuafikiana na wanafunzi wengine kiliondoka na kwenda ‘Cafeteria’ namba moja na namba mbili na kufanya fujo kwa kupiga kelele na kuwapiga wenzao waliokuwa wakila chakula, kuvunja vyombo na kuchukua soda zilizokuwamo ndani na kunywa.

“Walipotoka hapo walikwenda kwenye madarasa ya ‘Arts’ (sanaa), huko walifanya vurugu kwa kuwafukuza wenzao waliokuwa wakisoma pamoja na walimu, wakiwatisha kwa kutumia fimbo,”alisema Mgaya.
Alisema baada ya hapo wanafunzi hao walielekea kampas ya uhandisi kwa lengo la kushawishi wanafunzi wa huko wawaunge mkono katika jitahada zao.

Kwa mujibu wa Mgaya, baada ya ushawishi wao kutofanikiwa, wanafunzi hao walifanya vurugu baina yao na wanafunzi wa huko na kusababisha uharibifu wa mali katika eneo la kantini iliyokopo eneo hilo.

Alisema mara baada ya vurugu hizo, wanafunzi hao walifunga safari kuelekea Ubungo Plaza kwa lengo la kumuona Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na kumkabidhi madai yao.

Alisema kabla ya kufika Ubungo, wanafunzi hao walipata taarifa za waziri mkuu kutokuwapo Ubungo Plaza, ndipo walisimama na kuanza kushambulia magari yaliyotumika kubeba wanafunzi wa chuo hicho.

Akizungumza madai ya wanafunzi ambayo pia alikiri kuwa ni ya msingi.

Profesa Mgaya alisema tayari kuna taarifa za kuaminika kuwa upo mkakati wa kuangalia uwezekano wa kuongeza fedha hizo, ambao uko katika hatua za mwisho.

“Ni dhahiri kwamba tangu kiwango hicho kipandishwe mwaka 2007/2008, gharama halisi za maisha vyuoni zimepanda.

Hivyo basi kuna taarifa za kuaminika kwamba kupitia Bodi ya Mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya Juu, mchakato kubaini gharama halisi za maisha umeshakamilika na majadiliano yanaendelea kati ya bodi hiyo na wawakilishi wa Serikali za wanafunzi katika vyuo mbalimbali ili maamuzi stahiki yafanyike,”alisema Mgaya.

Mgaya alisema baada ya kufikiwa kwa makubaliano hayo, ongezeko hilo litaingizwa kwenye bajeti na kuanza kutolewa kwa wanafunzi wote vyuoni na kwamba hali hiyo itasaidia kupunguza matatizo ya wanafunzi.

“Kwa mantiki hiyo, hakuna sababu ya wanafunzi kusababisha vurugu na hali ya uvunjifu wa amani vyuoni, kwa kisingizio cha kudai mabadiliko ya viwango vya fedha za kujikimu,”alisema Mgaya.

Wanafunzi wakamatwa
POLISI jijini Dar es Salaam imewakamata wanafunzi 42 wa UDSM na ARU kwa tuhuma za kufanya maandamano kuelekea Ikulu bila kibali.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam, Suleiman Kova aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa awali wanafunzi waliokamatwa walikuwa 60, lakini baadaye walichujwa na kubakia 42.

"Mchujo bado unaendelea ili kuwabaini waliohusika kuyaandaa maandamano hayo waliyosema kuwa yana lengo la kushinikiza kuongezwa fedha za kujikimu.

Kova alisema wanafunzi hao walikamatwa baada ya kutoka nje ya maeneo ya vyuo vyao na kujiandaa kuanza maandamano hayo ya kuelekea Ikulu.

Alisema walikamatwa kutokana na maandamano hayo kutokuwa halali kwa kuwa hayakuwa na baraka za polisi, chuo wala uongozi wa serikali ya wanafunzi.

“Kuna baadhi ya wanafunzi wamekula njama, ndiyo walioshinikiza maandamao hayo. Hii inatokana na baadhi yao kuonekana wakiwalazimisha wanafunzi wengine kuandamana bila hata ridhaa yao,’’ alisema Kova.

Lakini Kamanda Kova alieleza kuwa polisi imefanikiwa kuzuia maandamano hayo kabla hayajafika katikati ya jiji ambako yangeweza kuleta uvunjifu wa amani na kusababisha msongamano mkubwa wa magari.

Awali habari zilizolifikia gazeti hili zimeeleza kuwa maandamano hayo yalianza asubuhi baada ya wanafunzi wanaoishi Hosteli ya Mabibo kuandamana na kwenda kuungana na wenzao wanaoishi katika mabweni ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam kisha kuwafuata wengine wa chuo cha Ardhi.

Kwa mujibu wa habari hizo, polisi pia lilikamata mabango manane yaliyokuwa yamebebwa na waandamaji hao yenye maneno mbalimbali ya kushinikiza madai yao hayo.

"Pia tumekamata rundo la mawe makubwa na madogo ambayo yalikuwa na lengo la kuwapiga askari na makubwa yalilenga kuzuia magari barabarani," alisema Kamanda Kova.

Habari hii imeandaliwa na Gedius Rwiza, Geofrey Nyang'ro na Festo Polea

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites

Comments

0 #6 KANIALE 2011-02-05 06:28 Matatizo ya wanafunzi ni kioo cha jinsi nchi yetu ilipofikia baada ya wale tuliowapa dhamana ya kutuongoza kusahau wajibu wao kwetu na kugeuka kuwa wala nchi. Ni wanafunzi wa Chuo Kikuu, Ni Dowans,Ni EPA, Ni vichanga mwanayamala, Ni uoza wa shule za sekondari za Kata, Ni matatizo ya umeme nchi nzima, ni matatizo ya maji nchi nzima,ni kupanda kwa gharama za maisha kila kukicha.Ni dhihaka ya viongozi kwa kutoa majibu ya kejeli na mengi mengineyo.

Watanzania amkeni tumieni kura zenu vizuri. Ghiliba na uongo vimefikia kikomo. Na leo hii si jana. DUMISHA AMANI lakini tumia uwezo na haki yako kuleta mabadiliko. INAWEZEKANA. Hakuna Chama wala kikundi chenye hati miliki ya kuongoza taifa hili.
MUNGU IBARIKI TANZANIA. MUNGU WAFUMBUE MACHO WATANZANIA.

Quote

-2 #5 gombera 2011-02-05 04:45 Imefika wakati serikali ijipange kujua inatoka wapi na inkwenda wapi vinginevyo amani itapotea Tanzania kumbuka zamani chuo kilikuwa kimoja hivyo ilikuwa rahisi kukidhibiti sasa hivi vipo vingi chonde serikali.
Quote

-2 #4 john 2011-02-05 04:43 nashangaa sana wazili wa ulinzi yupo kimya kukemea tabia mbaya ya kutumia nguvu na silaha za moto kwa wanafunzi wasio na hata njiti ya jiberiti kuwarushia, hawa polisi wenyewe wengi wao ni wale waliofeli mtihani wa kidato cha nne hawajui maisha ya chuo yalivyo wanaboa sana kuzuia maandamano...
Quote

-1 #3 MPARE WA UPARE 2011-02-05 02:56 Haileti maana kwa wanafunzi na watu wengine wa mtaani, eti pesa za kuwalipa wanafunzi hazipo mpaka majadiliano na ziingizwe kwenye bajeti wakati za kuwalipa matapeli kama DOWANS zipo tayari wakati hata kwenye bajeti hazipo.
Mwanafunzi na msomi wa Chuo Kikuu hawezi kuelewa ukimwambia eti serikali haina pesa wakati huo una uharaka sana kulipa kundi la matapeli wachache wa Dowans.
Sijui hii serikali yatupeleka wapi, hivi wanafikiri watu ni [NENO BAYA] bado? Hatutaki yaliyotokea Tunisia na yanayoendelea Misri na nchi zingine za Kiarabu yafike kwetu.Lakini kama hamtatenda haki na kuendelea kufisadisha wachache kwa kunyonya wengi msishangae yakitokea hapa kwetu.
MUNGU IBARIKI TANZANIA

Quote

-1 #2 Mkalimoto 2011-02-05 01:36 ACHENI WAANDAMANE KWA NINI MNAWAZUI NYIE POLISI. IPO SIKU NANYI MTAANDAMANA MAANA HUYU BWANA WENU MNAEMTETEA NA KUMLINDA HAMNAZO
Quote

-1 #1 Mzalendo 2011-02-05 01:09 Tunakoelekea ni kubaya sana,serikali ijaribu kuondoa matatizo haya.Kama watu wanadai haki wanapewa,Je kwa nini wasipewe kabla ya kufanya hivyo.Imekuwa ni rahisi kulipa matapeli wa dowans na kuwaacha wanafunzi wa Tanzania na wananchi kwa ujumla tena agizo linatolewa na wazito,hawajali elimu ndio maana wanataka elimu ya sasa iishie elimu ya kata kwa kugawa 4 na 0 ili [NENO BAYA] wawe wengi.Inaonekana watanzania wamechoka nchi yao ambayo wanapotaka haki yao wanapigwa kama mbwa.Serikali na chama tawala wajue kinachotokea Misri kimetokana na watu kuchoka.Tanzania ina ela lakini zinakuwa za wachache wanaofanya nchi kama shamba la bibi.Sasa hakuna kisicho na mwisho wajue hivyo kwamba siku ipo maana hata Mungu ameona watanzania wakiteseka na kuteswa.
Quote
 
Vita Chuo Kikuu Dar
• Mabomu ya machozi, mawe, maji vyatumika

na Janet Josiah na Violet Tillya

amka2.gif
POLISI wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) jana walilazimika kutumia mabomu ya machozi, maji ya kuwasha na virungu kuwazuia mamia ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na wale wa Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU) waliokuwa wakiandamana kuelekea Ikulu.
Ili kuwazuia wanafunzi hao, FFU walilazimika kuweka vizuizi kuanzia katika Barabara za Sam Nujoma, Survey na wengine wakatanda katika maeneo ya katikati ya jiji yaliyo karibu na ofisi ya Rais Ikulu.
Mapambano kati ya wanafunzi hao ambao walikuwa wakirusha mawe na FFU waliokuwa wakitumia mabomu ya mchozi na magari yenye maji ya kuwasha, yalianzia mbele ya geti la kuingia Mlimani City kwenye Barabara ya Survey na katika mageti mengine ya kuingia chuoni hapo (UDSM) na Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU).
Hali hiyo ilidumu kwa takriban saa nne huku askari hao wakiimarisha ulinzi katika viunga vyote vya maeneo ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kusababisha shughuli mbalimbali kusimama kwa muda, ikiwamo magari ya abiria na mengineyo kushindwa kuingia.
FFU kwa kushirikiana na askari wengine wa jeshi hilo walikuwa wakiyazuia maandamano ya wanafunzi wa vyuo vikuu hivyo ambao walikuwa wakielekea Ikulu kumwona Rais Jakaya Kikwete ili kumweleza dai lao la kuongezewa fedha za kujikimu kutoka sh 5,000 wanazolipwa sasa hadi kufikia sh 10,000.
Gazeti hili lilishuhudia gari za polisi aina ya Land Rover Defender zipatazo nane zikiwa zimewabeba wanafunzi waliokamatwa katika maandamano hayo.
Hata hivyo, baada ya saa kadhaa, askari hao walifanikiwa kuzima maandamano hayo ambayo hayakuweza kufika popote na kusababisha wanafunzi waishie kukaa vikundi wakiwapigia kelele na kuwalaani FFU ambao walikuwepo chuoni hapo kuimarisha ulinzi.
Wakati wote wanafunzi hao walionekana wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe tofauti yakisomeka, ‘Hatuwezi kukubali Dowans walipwe huku sisi tukiteseka.' ‘Vitu vimepanda hivyo tuongezewe fedha, ninyi mlisoma kwa raha'.
Hali hiyo ilimlazimu Naibu Makamu Mkuu wa UDSM, (Utawala na Fedha) Profesa Yunus Mgaya kuwaita waandishi wa habari kuzungumzia suala hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari chuoni hapo, alisema vurugu zimesababisha baadhi ya wanafunzi kuumia na wengine kupata madhara mengine ya kiafya.
Profesa Mgaya alisema vurugu hizo pia zilisababisha mwanafunzi mmoja wa kike aliyekuwa akisoma shahada ya uzamili ambaye alikuwa mjamzito aumie na kujifungua mtoto aliyekwishafariki na yeye (mama) kulazwa katika Hospitali ya Hurbert Kairuki.
Alisema wanafunzi wengine wawili waliumia ambapo mmoja aliumia usoni na kulazimika kushonwa nyuzi katika kituo cha afya chuoni hapo na mwingine kukatwa na kitu chenye ncha kali wakati akikimbia kujihami na polisi na alipelekwa Hospitali ya Taifa (Muhimbili).
Hata hivyo, Profesa Mgaya hakuwa tayari kutaja majina ya majeruhi kwa madai kuwa hajapelekewa majina zaidi ya kueleza kuwa ni wanafunzi wa mwaka wa kwanza.
Akizungumzia dai kuu la wanafunzi la kutaka kupatiwa shilingi 10,000 na serikali, Profesa Mgaya alisema chuo kinazo taarifa za kuaminika kwamba kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, mchakato wa kubaini gharama halisi za maisha vyuoni umekwishakamilika na majadiliano yanaendelea.
Alisema mchakato wa kuongezewa malipo hayo ulifanyika hivi karibuni na kwamba utaratibu huo umekuwa ukifanyika mara kwa mara baina ya serikali za wanafunzi, wizara pamoja wahusika na elimu ya juu.
"Mabadikiko ya fedha za kujikimu yalikuwa kama yafuatayo, hadi kufikia mwaka wa masomo 2005/06 wanafunzi wa vyuo vya juu walilipwa shilingi 2,500, mwaka 2006/2007 zilipanda na kuwa shilingi 3,500 na mwaka 2008/09 hadi sasa zilipanda tena na kuwa 5,000, je tatizo la kufanya vurugu linatoka wapi? Alihoji Profesa Mgaya.
Katika hilo alisema hakuna sababu yoyote ya wanafunzi kusababisha vurugu na hali ya uvunjifu amani vyuoni kwa kisingizio cha kudai mabadiliko ya viwango vya fedha za kujikimu.
Wakati huo huo Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam liliitisha mkutano na waandishi wa habari na kutoa taarifa kuwa linawashikilia na kuwahoji wanafunzi 42, wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na wa Chuo Kikuu cha Ardhi kwa kosa la kufanya maandamano bila kibali kinyume cha taratibu za jeshi hilo.
Jeshi hilo lilisema kuwa baadhi ya wanafunzi wa vyuo hivyo walikula njama za siri na kupanga kufanya maandamano hayo jana majira ya asubuhi kutoka chuoni hapo kwenda Ikulu jambo ambalo lingesababisha uvunjifu wa amani.
Akitoa taarifa hizo jana Kamanda wa Kanda Maalumu, Suleiman Kova, alisema kuwa jeshi hilo lilifanikiwa kuwatawanya wanafunzi hao kwa kutumia nguvu za wastani kwa kutumia maji ya kuwasha na mabomu ya machozi ambapo hakuna polisi wala mwanafunzi aliyeumia katika tukio hilo.
Kamanda Kova alisema kuwa wanafunzi hao ambao walikuwa wanakaribia 200 tayari walikuwa wamefanikiwa kutoka nje ya uzio wa vyuo huku wakiwa wamebeba mawe makubwa ya kuzuia magari na mawe madogo ya kuwapiga polisi lakini hawakuweza kufanikiwa kufanya hivyo kutokana na jeshi hilo kuwahi kuwadhibiti.
"Sisi kama Jeshi la Polisi tulipata taarifa za kiintelejensia kutoka kwa wasamaria wema ambao ni wanafunzi ndani ya vyuo vyao, hivyo tulijipanga," alisema Kova.
Alisema awali walikuwa wamewashikilia wanafunzi wapatao 60, mara baada ya kufanya mchujo mkali waliwabakisha 42 ambao nao wanaendelea kuwahoji na kuwachuja pia, na kati yao watakaobainika kuwa chanzo cha kuanzisha maandamano hayo watachukuliwa hatua za kinidhamu.
Hata hivyo, Kamanda Kova aliwataka wanafunzi wa vyuo vikuu nchini kuacha kufanya migomo bila kufuata taratibu zote badala yake watulie na kuendelea na masomo yao kwa faida yao ya baadaye na vizazi vijavyo.
Alisema jeshi hilo tayari limeshaongea na uongozi wa ngazi za juu na kuambiwa kuwa suala lao tayari linatafutiwa ufumbuzi na linazungumzika.
 
02_11_463ktn.jpg
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) waliokuwa wakiandamana na kukabiliana na askari Polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU). Hata hivyo, baadhi ya watu walitilia shaka kijana aliye kulia kama naye kweli ni mwanachuo. (Na Mpigapicha Wetu).
 
h.sep7.gif

Serikali mnataka ya Misri yafanywe na wanafunzi?

ban_tahariri.jpg

amka2.gif
JUZI na jana wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu nchini walifanya maandamano waliyodai ni ya amani wakitaka kwenda ofisi ya Wizara ya Elimu, kutoa malalamiko yao kuhusu madai mbalimbali.
Mgomo huo umetokana na wanafunzi hao kudai kuwa wamechoshwa na ubabaishaji unaofanywa na serikali juu ya utoaji wa fedha za mikopo kwa wanafunzi.
Kwa mujibu wa madai yao, wanafunzi hao ambao ndiyo viongozi wa taifa la kesho wanadai kuongezewa fedha ya kujikimu kutoka shilingi 5,000 kiasi cha awali hadi kufikia 10,000 kwa siku kutokana na kupanda kwa gharama za maisha.
Kadhalika wanafunzi wengine ambao ni wa Chuo Kikuu cha Tumaini wao wanataka ada ipunguzwe kutoka sh milioni tatu hadi sh mil 1.5.
Mwezi mmoja uliopita, wanafunzi wa Kitivo cha Elimu, Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), na Kitivo cha Sayansi, chuo hicho hicho, nao waligoma na kufanya maandamano kwa madai hayo hayo, kiasi cha kulazimisha Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) kuingilia kati.
Mgomo uliofanywa jana jijini Dar es Salaam, sambamba na maandamano ya amani ulisababisha kwa masaa kadhaa eneo la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kugeuka eneo la vita baada ya askari kutumia mabomu na maji ya kuwasha kuwatawanya wanafunzi hao.
Licha ya kuzalisha wataalamu ambao ni tegemeo kwa maendeleo ya taifa, UDSM miaka iliyopita kilikuwa na sifa lukuki, ukiachilia mbali uzuri wa majengo yake, kilikuwa na sifa ya amani, utulivu, uongozi bora na sifa nyingine kubwa ya kudahili wanafunzi wengi zaidi kuliko vyuo vingine.
Sifa hizo sasa zimetiwa doa na migomo na maandamano ya mara kwa mara ya wanafunzi ambao wanadai kuwa madai yao hayo ni ya muda mrefu.
Kwa mantiki hiyo basi madai hayo ya wanafunzi ni ya msingi na yangeweza kushughulikiwa bila kusababisha vurugu zilizotokea, ikiwamo kuwajeruhi, kuharibu mali n.k.
Lakini hoja ya wanafunzi kwamba madai yao hayo ni ya muda mrefu ni dhahiri kwamba serikali imeshindwa kuwajibika si tu kwa wanafunzi hao, bali pia katika vyuo vikuu vingine nchini ambavyo vimekuwa na malalamiko yanayofanana na hayo.
Tunasema serikali imeshindwa kuwajibika kwa sababu tangu wanafunzi wa UDSM, UDOM, Kitivo cha Sayansi walipogoma takriban mwezi mmoja sasa, hakuna ufumbuzi wa kudumu uliopatikana.
Awali tulidhani kwamba njia pekee nzuri ya kutatua mgogoro huo ni pande zote mbili kukubali kurudi katika meza ya mazungumzo.
Lakini njia hiyo inaonekana kushindikana kutokana na mipango dhaifu ya serikali na wanafunzi wameliona hilo na ndio maana wakaona hakuna njia nyingine ya kufikisha kilio chao zaidi ya kuandamana.
Yaliyotokea UDSM si jambo jipya kwani tumeshuhudia yakitokea katika vyuo vingine nchini, lakini mpaka leo viongozi wa serikali bado wameshindwa kujifunza jinsi ya kushughulikia changamoto za wanafunzi kwa amani na mbinu shirikishi kuepusha vurugu na bila kusababisha maafa mengine.
Kinachoonekana ni kwamba viongozi wetu hawana ujuzi mwingine wa kushughulikia matatizo ya wanafunzi, zaidi ya kulitumia Jeshi la Polisi ambalo mwisho wa siku husababisha maafa na kuharibu mantiki ya suala zima.
Tusome alama za nyakati kwenye nchi zenye migogoro ya kisiasa na wanafunzi hivi sasa, matatizo kama haya mara nyingi ndiyo huchangia kwa kiasi kikubwa kutokea kwa uvunjifu wa amani na vurugu nchi nzima.
Misri na nchi nyingine zilianza machafuko kwenye migogoro midogomidogo kama hii ya wanafunzi; Je, serikali inataka ya nchi za Misri, Tunisia na zingine yafanywe na wanafunzi hawa?
Tanzania Daima tunasema hatupendi wanafunzi wafikie katika hali ya kuhatarisha amani ya nchi katika kipindi hiki ambacho nchi imetoka kwenye uchaguzi, kwani juhudi zaidi zinahitajika katika kuwaletea maendeleo wananchi badala ya kutumia nguvu nyingi kuwadhibiti wanafunzi hao bila sababu za msingi.
 
Migomo isipotafutiwa ufumbuzi itaigharimu nchi
ban.mtazamo.jpg

Haji Kalili

amka2.gif
MIGOMO ya wafanyakazi wa taasisi mbalimbali duniani imekuwa ni njia mbadala baada ya mazungumzo ya kutafuta muafaka kushindikana baina yao na waajiri wao.
Hivi karibuni kumeibuka wimbi la migomo kutoka kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu nchini na sababu kubwa ni ucheleweshaji wa mikopo kutoka kwa bodi husika.
Kimtazamo migomo siyo mizuri na ina athari kubwa hasa kiuchumi.
Hebu fikiria kama ule mgomo uliokuwa umeitishwa na Shirikosho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) kama ungefanyika ulivyokuwa umepangwa nini kingetokea?
Taifa lilikuwa linakabiliwa na ugeni mkubwa wa Jukwaa la Kiuchumi la Dunia (WEF) uliokuwa ukifanyika kwa mara ya kwanza katika Ukanda wa Maziwa Makuu, ni wazi taifa lingekumbwa na aibu kubwa ambayo ingetugharimu na kutoaminika mbele ya jumuia za kimataifa.
Hili wimbi la migomo kutoka vyuo vya elimu ya juu kimsingi inatokana na kukosekana kwa mawasiliano baina ya Tume ya Elimu ya Vyuo Vikuu (TCU), Bodi ya Mikopo na Vyuo husika.
Ni hivi majuzi tu wanafunzi wa chuo kikuu kimoja mkoani Iringa waligoma baada ya kukosa mikopo kama walivyokuwa wameahidiwa.
Mkuu wa chuo hicho alipobanwa alijitetea kwa kusema kozi wanayochukua ambayo ni ya ualimu haitambuliwi na Bodi ya Mikopo.
Hapa binafsi najiuliza maswali na kukosa majibu yake. Wanafunzi wale ni nani alihusika katika kuwadahili? Nani aliwapa nafasi ya kujiunga na chuo kile?
Kama walipitishwa na kuonekana wana sifa ya kusoma shahada ya ualimu na Tume ya Vyuo Vikuu, iweje leo Bodi ya Mikopo ikatae kuwapa mikopo? Naamini lipo tatizo la kukosekana kwa mawasiliano baina yao.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT), Dk. Charles Kitima, alisema katika uzinduzi wa Chuo Kikuu Kishiriki tawi la Tabora kwamba migomo hiyo ya wanafunzi inasababishwa na ukiritimba wa viongozi wa Bodi ya Mikopo ambao fedha zilizotengwa kwa ajili ya kuwakopesha wanafunzi, wamekuwa wakizifanya kama zao binafsi.
Hapa nchini historia inatukumbusha kwamba katika karne ya 18 vyama vya mwanzo vya wafanyakazi viliundwa kadri uzalishaji wa bidhaa ulivyokuwa ukiongezeka, vikijulikana kama ‘Trade Clubs' katika kupambana na uonevu sehemu za kazi.
Moshi mjini mwaka 1927 wafanyakazi na madereva waliunda chama chao cha wafanyakazi ili kupigania haki zao na baadaye mwaka 1932 wakoloni waliruhusu kuundwa kwa vyama vya wafanyakazi lakini kwa masharti viwe vya burudani hasa baada ya saa za kazi.
Kipato ndiyo madai ya msingi ya wafanyakazi duniani kote, mazingira bora na muda wa mfanyakazi kuwa kazini.
Baada ya Azimio la Arusha kuzikwa, hivi sasa wafanyakazi wameangukia kwenye mikono ya matajiri na mabepari ambao sasa wamejipachika jina la wawekezaji.
Wafanyakazi ndio walipakodi, mishahara ni midogo lakini bado inakatwa kodi. Hili bado linapiganiwa na vyama mbalimbali vya wafanyakazi.
Serikalini na sekta binafsi wote katika hili hakuna wa kukwepa. Mzigo wa lawama unaangukia katika sekta zote mbili.
Serikali inalalamikiwa kwa kukumbatia wawekezaji na kusahau kundi kubwa la wazawa ambao ni wafanyakazi wa kada ya chini, kati na wenye vipato duni.
Wawekezaji wameachwa huru mno na kujifanyia mambo wanavyotaka. Wafanyakazi wanataka wawekezaji waheshimu sheria za kazi pamoja na usalama mahali pa kazi
Ipo haja ya kumaliza ukiritimba wa Bodi ya Mikopo kwa shutuma hizi zinazoelekezwa kwake kwa kuwakutanisha na Tume ya Vyuo vya Elimu ya Juu nchini na wakuu wa vyuo vikuu wakaketi pamoja, wajadili matatizo ya msingi na kumaliza kabisa tofauti zao.

Hizi taasisi tatu muhimu kwa mustakabali wa elimu ya juu nchini zikiachwa ziendelee kila moja kufanya kazi kivyake athari zake zitakuja kuigharimu serikali na tutashuhudia yaliyotokea Tunisia na Misri.
Serikali inaonekana kuogopa migomo ya wafanyakazi ambao idadi yao ni ndogo na ni rahisi kudhibitiwa kama ikiamua.
Yanayotokea hivi sasa Tunisia na Misri ni matokeo ya kutojali na kuheshimu misingi ya haki za binadamu.
Hizi mbwenbwe za kizamani "Tanzania ni kisiwa cha amani" zimeshapitwa na wakati na iko haja ya kuanza kuwajibika kwa uwazi na kwa dhati kabisa.
Athari za migomo inayoendelea hivi leo itakuwa kubwa hapo mbeleni kama isipodhibitiwa na kumalizwa leo.
Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.

h.sep3.gif

Tuwasiliane 0717 321 444
kalilihaji@gmail.com
 
Back
Top Bottom