Double Standards za Ikulu kumtetea Ombeni Sefue

Mmmm hapa kazi hipo jpm unakibarua sana kusafisha nchi hii mm naona cha muhimu nikukaza sara aisee
 
Ikulu imetoa press release kumtetea Katibu Mkuu ombeni sefue ambaye anakabiliwa na tuhuma za rushwa na kampuni ya ujenzi ya kichina ya CRJE

Cha ajabu ni kuwa utetezi wao umekuwa one sided. Iweje wao wanamtetea Ombeni sefue lakini wengine haijawatetea?

Ina maana kuwa kwenye hizi tuhuma za majipu kuna sheria nyingine kwa wafanyakazi wa serikali na kuna nyingine ya Ombeni Sefue?

Hizi double standards tulidhani zitaondoka kipindi hiki cha awamu 5 lakini bado tuko kule kule zama za zamani za impunity.

Kwa utetezi wa leo wa Ikulu ina maana wanasema kuwa watuhumiwa wengine wako GUILTY lakini sefue ni SAFI?

Wameona taabu gani kutoa statement ambayo ni impartial na isiyoegemea upande wowote?

Ahhh nimesahau, usikute statment imeandikwa na huyo huyo sefue.

Once again, tuko kwenye zama za ANIMAL FARM ya George Orwell , wanyama wengine ni bora kuliko wengine
 
Double Standard utaijua hapo itakapofika muda wa gazeti la Dira kumuangukia na kuomba radhi kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
 
magufuli kwishney, wizara aliokuwepo ya ujenzi haigusi akigusa mwenyewe kaisha aibu!
 
Waliotoa utetezi huo ni Idara ya Habari Maelezo, na sio Ikulu kama ulivyoeleza. Kimsingi ktk utetezi huo wamekanusha kwa Hoja zenye mantiki tuhuma zilizoandikwa kwenye gazeti husika dhidi ya Balozi Sefue.
Kwahivyo kama wewe mleta mada hujaridhishwa na utetezi huo, wasilisha ushahidi wa tuhuma za Sefue kwenye mamlaka zilizoainishwa kwenye taarifa husika..
Mbona kwa wengine huwa hawahitaji ushahidi?
 
Huijua hata Idara ya Habari Maelezo? Taarifa za Ikulu hutolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu (kwa sasa Kaimu). Idara ya Habari Maelezo Mkurugenzi wake Asah Mwambene. Huoni tofauti kati ya Ikulu na Idara ya Habari Maelezo?
Idara ya Habari Maelezo inahusikaje na mambo personal ya sefue maana ametuhumiwa yy binafsi kwa kutumia cheo chake labda kama ndio sielewi
 
Hivi Fisadi Lowassa anatumbuliwa lini? Au ni siasa za kuchafuana kama ilivyokuwa kwa Salim Ahmed Salim?
 
Waliotoa utetezi huo ni Idara ya Habari Maelezo, na sio Ikulu kama ulivyoeleza. Kimsingi ktk utetezi huo wamekanusha kwa Hoja zenye mantiki tuhuma zilizoandikwa kwenye gazeti husika dhidi ya Balozi Sefue.
Kwahivyo kama wewe mleta mada hujaridhishwa na utetezi huo, wasilisha ushahidi wa tuhuma za Sefue kwenye mamlaka zilizoainishwa kwenye taarifa husika..

Uzuri wangu mimi sina upande wala chama, nataka haki tu. Nilisema naamini hata gazeti lililoandika si wajina, wana sababu na si kukurupuka na kusema wafungiwe. Kama wamekurupuka baada ya ushahidi na wafungiwe. Lakini kama wana ushahidi ndio wakati wa kuutoa na Ombeni achukuliwe hatua haraka. Lakini najua kwa hujuma zilivyo nyingi hapa nchini na ni akina Ombeni na Kikwete walikuwa madarakani hatua hazikuchukuliwa hadi kaingia Magufuli, sishngai hata siku moja.
 
Pamoja na matakataka yote ya mkwere na sefue akiwa katibu hivi inawezekana kweli sefue akawa cleean! kabisa hana kimeo hata kimoja uongozi wa mkwere? nawaza tu
 
Na mimi nilifikiri kama alivyofanyiwa Classmate wangu Dr wa Ligula na Kassimu Majaliwa na kwa Ombeni itakuwa hivyohivyo,maana msela wangu jana kaaibishwa tu kwa "malalamiko" ya ndugu wa mgonjwa,akasimamishwa mbele za watu na mbele ya camera bila kupewa muda.Sasa huyu Ombeni katolewa kabisa kwenye gazeti,ambalo Magufuli alisema waandike tu maana yeye anasoma sana magazeti na anafanyia kazi habari za magazeti.Sasa Gazeti la DIRA limesema ili lisomwe naona wanalionya,nafikiri likisema gazeti la Jamuhuri ndio watachukua hatua
Wanyama wote ni sawa,lakini si wanyama wote ni sawasawa
 
Idara ya Habari Maelezo inahusikaje na mambo personal ya sefue maana ametuhumiwa yy binafsi kwa kutumia cheo chake labda kama ndio sielewi
Wengine wakituhumiwa tu wanasimamishwa kazi "ili kupisha uchunguzi!" Sasa kwa nini Sefue naye asipishe uchunguzi?
 
"ALL animals are equal but some animals are more equal than others" George Orwell
 
Ikulu imetoa press release kumtetea Katibu Mkuu ombeni sefue ambaye anakabiliwa na tuhuma za rushwa na kampuni ya ujenzi ya kichina ya CRJE

Cha ajabu ni kuwa utetezi wao umekuwa one sided. Iweje wao wanamtetea Ombeni sefue lakini wengine haijawatetea?

Ina maana kuwa kwenye hizi tuhuma za majipu kuna sheria nyingine kwa wafanyakazi wa serikali na kuna nyingine ya Ombeni Sefue?

Hizi double standards tulidhani zitaondoka kipindi hiki cha awamu 5 lakini bado tuko kule kule zama za zamani za impunity.

Kwa utetezi wa leo wa Ikulu ina maana wanasema kuwa watuhumiwa wengine wako GUILTY lakini sefue ni SAFI?

Wameona taabu gani kutoa statement ambayo ni impartial na isiyoegemea upande wowote?

Ahhh nimesahau, usikute statment imeandikwa na huyo huyo sefue.

Once again, tuko kwenye zama za ANIMAL FARM ya George Orwell , wanyama wengine ni bora kuliko wengine

Ilipatwa kusemwa na mtu mmoja mashuhuri sikumbuki ni nani kuwa "All people are equal but some are more equal than others" kwa anayejua vema nitashukuru akinisahihisha
 
Si ajitetee Mwenyewe? Hizo ni Dalili za Double Standard kweli
sio dalili ,mkuu bali ni double standard waziwazi kwasababu tumeshuhudia baadhi ya wakuu wa mashirika ya umma wamefukuzwa kazi kwa tuhuma tu au tetesi ambazo hazijathibitishwa lakini kwahili la sefue nahisi litalindwa kwelikweli ikiwezekana hata kwa sheria ya makosa ya mtandao kuwasilence critics...haya majipu wanatumbuliwa watu ili kuwatoa kwenye nafac zao na kuwaweka wanaowapenda wao..isingekua kuwa hivyo hawa wanaotumbuliwa wangepelekwa mahakamani kwanza huko ndo wakaonekane kama wana hatia na kama hawana warudi kwenye nafac zao za kazi..
 
Back
Top Bottom