Doto Biteko kapelekwa Wizara ya Nishati kipindi cha Mgao wa umeme, achunge yasimkute ya Lowassa

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
890
4,138
Kumpeleka Ndugu yetu Biteko pale Nishati na kumwondoa Makamba kipindi ambacho Makamba amevurunda siyo picha nzuri kwa mwanetu huyu.

Sisi watu wa kanda ya ziwa tunazungumza na miungu yetu mvua inyeshe shetani asipate nafasi yakumwaibisha Mwanetu.

Hizi royal family za Pwani si familia nzuri sana kushirikiana nao; wana sura ya ubaguzi na wanapenda sana kusifiwa bila kufanya kazi. Walimpeleka mtoto wao pale wakitegemea hali ya umeme itakuwa nzuri lakini project zake zote zikashindwa kuzaa matunda.

Nani anakumbuka ile project ya mitungi ya gesi; leo hii ipo wapi? Pale kwenye gesi ilikuwa promo ya Taifa gesi. Nani anakumbuka mavikao ya mabilioni yaliyopewa jina la tathimini ambayo tulisomewa ripoti Lukuki....leo miradi inasua sua na mgao umeanza.

Doto achukulie hi kama changamoto na aombe mvua inyeshe la sivyo atageuzwa Lowassa wa pili.
 
Kazi ya Kiongozi ni kutatua au kwenda kwenye raha kusiko na Changamoto? Sukuma gang mbona mna matatizo sana?
 
Back
Top Bottom