Dogo kichwa dafu - Mwalimu ana chuki na mimi.

MAMMAMIA

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
3,811
1,604
Dogo alifeli mtihani na karibu abakishwe darasa lile kam si baba yake kwenda kumwomba mwalimu ampe mwanawe fursa nyengine. Mwalimu alikubali.

Siku ya mtihani wa marudio, dogo alifanya mtihani na matokeo yakawa yale yale - alifeli.

Baba alihamaki sana. Alipomwuliza mwanawe kwa nini alifeli na alipewa fursa ya kurudia mtihani.

"Mwalimu anachuki na mimi. Nimefeli kwa sababu amenipa mtihani ule ule niliofeli kabla. Kama sio hivyo, kwa nini akanitolea mtihani ambao tayari nilikwisha feli."
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom