Dodoma: Yaliyojiri Mkutano Mkuu maalum wa CCM, mabadiliko yamepitishwa, Arfi na Machali wahamia CCM

Makada wa chama cha magamba mliopo huko naomba mmwambie Polepole aache kurusharusha mikono wakati akiongea...ndo uongeaji gani huo kurusharusha mikono kama dictator Mussolini

Anarushaje mikono? Weka kavideo au kapicha unachokiongelea kionekane mubashara then ombi lako litafanyiwa kazi.
 
Habarini wanajamvi wakubwa shkamooni na wadogo marahaba. Samahani nimejikuta nawasha tv hapa nikakuta mkutano wa ccm unaoendelea huko dodoma nimekuta ndio ma balozi wanatambulishwa .nikakumbuka kuna kipindi Kinana katibu wa ccm alimualika balozi wa china kwenye mkutano wa ccm ilileta vita sana watu waka mcomplain yule balozi kwamba hakufanya sawa.
Sasa basi naomba niulize hv hawa mabalozi ambao wapo dodoma sa hii kwenye mkutano wa ccm je ni sahii wao kuwapo hapo au sio sahii ?? Maana wale ni mabalozi wanao wakilisha nchi zao hapa kwetu inakaaje hii? Je vyama vingine vya upinzani wanaruhusiwa kuwaalika hao mabalozi kwenye mikutano yao au hawaruhusiwi? naomba kujibiwa ,cko hapa kichama au nini nimesema tu niulize ili nieleweshwe. Asanteni.
 
Wapinzani juimarisheni , mujenge upinzani wenye nguvu.Hiki ndio kipindi cha kumngoa goliati.kwani mungu anakwenda kuvunja,vunja nguvu zake ili kuisafisha njia ya kwenda ikulu.
 


Habari waungwana,

Leo habari kubwa ni mkutano mkuu 'Maalum' wa chama cha mapinduzi ambao cheche zake zilianza jana kwa makada kadhaa kupewa adhabu ikiwemo kuondolewa chamani. Tuwe sote pamoja nikujuze yanayojiri katika mkutano mkuu maalum wa chama cha mapinduzi.
=======

Akizungumza mbunge wa Nzega, Hussein Bashe amegoma kuzungumzia yeye kushikiliwa na polisi hapo jana na kusema suala hilo kamuachia katibu mkuu wa chama hicho, Abdurahman Kinana. Alipoulizwa kama ana hofu ya kutimuliwa chamani, amedai hana hofu hiyo kwani hayo mambo hufanyika kwa utaratibu.

Katibu wa uenezi wa chama cha mapinduzi, Humphrey Polepole amesema CCM inatarajia kujenga chuo kikuu kwa ajili ya kufundisha makada wa chama hicho.

Kinachoendelea kwa sasa ni utambulisho wa wageni mbalimbali waliohudhuria hasa mabalozi wa nchi mbalimbali waliofanikiwa kufika katika mkutano huo, pia mwakilishi wa msajili wa vyama vya siasa nchi.

Pia wametambulishwa wadhamini wa chama cha mapinduzi, wake za wake wa viongozi ikiwemo Karume, Kawawa, Ali Juma, Salma Kikwete na wake wa viongozi wa sasa ikiwemo Mary Majaliwa, Mwanamwema Shein, Janet Magufuli.

Yupo pia Pandu Kificho, Anna Makinda, manaibu makatibu wakuu wastaafu.

Mbona Kikwete ameshangiliwa sana zaidi ya wote walio tamburishwa...kuna tatizo apo..
 
Back
Top Bottom