DODOMA: Saed Kubenea(Mb) augua ghafla, akimbizwa hospitali

Kupewa taarifa tuu kaugua ghafla furaha iliyowakumba haina mfano. Mashetani utawajua tuu, wao kwao kitu kibaya kwa mwingine ndio sherehe kwao. Nadhani mkisikia gari limeanguka na abiria 30 wamekufa kati yao 20 ni wanachama wa Chadema mnaandaa pati
 
Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea, ameugua ghafla na kupumzishwa Hospitali mjini Dodoma leo
==============

By Sharon Sauwa, Mwananchi

Dodoma. Mbunge wa Ubungo(Chadema), Saed Kubenea ameugua ghafla na kupumzishwa katika zahanati ya Bunge.

Katibu wa wabunge wa Chadema, David Silinde amesema leo Alhamisi jioni kuwa mbunge huyo alikwenda katika zahanati hiyo baada ya kujisikia vibaya.

“Alijisikia kukosa nguvu akaenda katika zahanati hiyo, amepumzishwa na sasa hivi ndio anasema ni simu yake ya kwanza kuongea nayo tangu apumzishwe. Ndio kwanza amekaribia kumalizia dripu,” amesema Silinde.

Hata hivyo waandishi wa habari walipofika katika zahanati hiyo hawakuruhusiwa kumuona na badala yake wauguzi walisema amepumzika.

Daktari wa zahanati ya Bunge, Dk Noel Solomoni amethibitisha kupumzishwa kwa mbunge huyo tangu saa 10 jioni leo.

Hata hivyo, hakuwa tayari kueleza zaidi kama alifikishwa ama alikwenda mwenyewe katika zahanati hiyo iliyopo ndani ya Bunge.

Chanzo : Mwananchi
Pole sana Mh. Kubenea. Tuwe wapole, sote duniani hapa tunapita, muda wa kulumbana eti mara hamuiamini serikali ni utoto, tujikite na issue za kulijenga taifa letu. Tunakutakia uponaji wa haraka Mh.
 
Irikusudi kureta maendereo ya chama cha mapinduzi. Askari wanajua cha kufanya hadi richama retu risiwe na mpinzani wara yeyote wa kureta fyokofyoko.
 
Au Albadri inayosomwa imeanza kazi?
ikianza kazi wa kwanza atakuwa Le mutuz na boss wake ambao wametima watu kwenda kuwasaka hao watu wanaotaka kusoma Albadri waache kuisoma kwani wanahofia kupotea Duniani.
 
Spika apunguze vitisho.
Sasa kaamua kutembea na bakora kama alivyofanya kule jimboni kwake Spika ndungai tokea Mtukufu amtishe kumpora Uanachama wa CCM anekuwa muoga na Mwehu sana
 
Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea, ameugua ghafla na kupumzishwa Hospitali mjini Dodoma leo

==============

By Sharon Sauwa, Mwananchi

Dodoma. Mbunge wa Ubungo(Chadema), Saed Kubenea ameugua ghafla na kupumzishwa katika zahanati ya Bunge.

Katibu wa wabunge wa Chadema, David Silinde amesema leo Alhamisi jioni kuwa mbunge huyo alikwenda katika zahanati hiyo baada ya kujisikia vibaya.

“Alijisikia kukosa nguvu akaenda katika zahanati hiyo, amepumzishwa na sasa hivi ndio anasema ni simu yake ya kwanza kuongea nayo tangu apumzishwe. Ndio kwanza amekaribia kumalizia dripu,” amesema Silinde.

Hata hivyo waandishi wa habari walipofika katika zahanati hiyo hawakuruhusiwa kumuona na badala yake wauguzi walisema amepumzika.

Daktari wa zahanati ya Bunge, Dk Noel Solomoni amethibitisha kupumzishwa kwa mbunge huyo tangu saa 10 jioni leo.

Hata hivyo, hakuwa tayari kueleza zaidi kama alifikishwa ama alikwenda mwenyewe katika zahanati hiyo iliyopo ndani ya Bunge.

Chanzo : Mwananchi
labda kuna harufu mbaya kaivuta....
 
Yani sasa likitokea sintofahamu yeyote, kuna MUTU pale magogoni atahusishwa.
Sijui kwanini
 
Back
Top Bottom